CHADEMA imekonga mioyo ya Watanzania

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
CHADEMA imekonga mioyo ya Watanzania
ban.mtazamo.jpg

Barnabas Lugwisha​

HAKUNA ubishi kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetokea kuwa kipenzi cha wananchi, maana mioyo ya Watanzania wengi imevutiwa na umakini wa viongozi wa chama hicho.
Ukitaka kuhakikisha hilo, rejea siku ile ya kutangazwa kwa matokeo ya awali ya kura za udiwani, ubunge na urais kwa kuyaangalia matokeo kwenye kata za vigogo ambazo baadhi yake ni Oysterbay, Masaki na Mbezi Beach.
Huko ni kwa waliofaidi matunda ya nchi hii na hata kufikia hatua ya kugawana nyumba za serikali. Lakini wote hao wameungana na walalahoi kwa kuipa kura CHADEMA.
Binafsi nasema, vigogo walioiunga mkono CHADEMA, hongereni sana kwani kwa mara ya kwanza mioyo yetu imeunganishwa na sera makini za CHADEMA.
Hata hivyo kwa bahati mbaya, kule kwetu Kiwalani, ndani ya Jimbo la Segerea alikoshinda Dk. Makongoro Mahanga, kura zetu zilipotea.
Katika vituo 37 tulikotumbukiza kura zetu, ilikuwa ni hasara tupu, kwani ofisa mtendaji wetu (jina tunalihifadhi), alitutangazia kuwa kura zetu zimepotea. Tulinyamaza kwa kuwa viongozi wetu walituasa tudumishe amani.
Mpendazoe umo mioyoni mwetu kwa kuwa tulikupa kura zetu, ila wajanja wamezichakachua. Inshallah siku moja utatinga mjengoni!
Turejee kwenye mada, Je, chama hiki kimekuwa mwandani wetu kirahisi? Jibu ni hapana:
Hadi kukonga nyonyo za Watanzania viongozi wakuu wa chama hiki wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, walihenyeka, wamezunguka huku na kule, kuanzia Mwanza hadi Mtwara, kote huko wamekuwa wakitoa elimu ya uraia sanjari na sera za chama chao.
Nakumbuka ni katikati ya mwaka 2003 nikiwa mwandishi wa gazeti la Mtanzania na The African, naambiwa na mabosi wangu niambatane na CHADEMA katika ziara ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, niliambatana na Waheshimiwa mzee Philemon Ndesamburo, Freeman Mbowe, Dk. Willibrod Slaa na Grace Kiwelu, ambao wote hao walikuwa ni wabunge katika majimbo, Kiwelu alikuwa ni Mbunge wa Viti Maalumu.
Narejea nyuma kutokana na mafanikio makubwa sana ambayo chama hicho kimeyapata achilia mbali uchakachuaji wa hali ya juu wa kura za chama hicho uliotokea kufuatia uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni.
Katika ziara hiyo ambayo ilikuwa ni ya kukitangaza chama na kutoa elimu ya uraia nilijifunza mengi na nikiyaakisi kwa sasa unatimia msemo wa ‘ukitaka cha uvunguni sharti uiname.'
Tulifika Iringa, Mbeya na kwingineko, leo ni mabadiliko makubwa ambayo nimeyaona kutoka kitambo, CHADEMA imepata mbunge Iringa mjini ambako kulikuwa na wana CCM watiifu mno.
Jambo lililonishanganza ni kwamba katika ziara hiyo, eneo hilo lilikuwa gumu kwa chama hicho, kiasi cha kuwakatisha tamaa viongozi wa CHADEMA katika mikutano yao ya Iringa mjini.
Mathalani, Iringa mjini, ulifanyika mkutano wa hadhara maeneo ya stendi pale, jina la uwanja silikumbuki, katika mkutano huo wananchi wengi walijitokeza lakini cha ajabu kila walipokuwa wakisalimiwa na kiongozi aliye hutubia kwa kauli mbiu ya CHADEMA, wananchi hao walikuwa kimya ama waliitikia kwa mashaka, ni dhahiri walionyesha utii kwa chama tawala.
"People's power, People's Power, People's Power (kimya)." "Aisee hawa watu ni wagumu sana," alisikika akisema mzee Ndesamburo aliyekuwa akiwasalimia wananchi hao.
Aisee hawa watu ni wagumu sana, kumbe mzee huyu hakugundua kwamba miaka saba baadaye chama chake kitaaminika kiasi cha kupata mbunge katikati ya watu hao wagumu.
Narejea nyuma kidogo kwa sababu ninapenda niwakumbushe Watanzania wenzagu kwamba maisha unavyoyapanga na unavyotaka yawe ndivyo yanavyokuwa.
Hakuna muujiza katika maisha kwamba utapata maziwa na asali bila kufanya kazi, haiwezekani! Viongozi hawa wa CHADEMA wamemenyeka sana, walitembea nchi nzima kwa gharama zao kuwaelewesha Watanzania sera za chama hicho, kuna walio waona wanapoteza muda, lakini kuna waliowaona kama wakombozi wa baadaye wa taifa hili.
Kuna mahali tulipita katika ziara hiyo tukielekea Tarafa ya Makongorosi, nje kidogo ya Jiji la Mbeya, eneo tajiri kwa madini ya dhahabu, lakini lililotopea katika lindi la umaskini.
Nakumbuka ilinibidi kupanda juu ya mti ili nipate mtandao wa simu.
Tukiwa njiani kuelekea eneo hilo, tulikutana na bibi mmoja wa makamo, Mbowe alimuuliza maswali mbalimbali, moja ya maswali hayo nalikumbuka, lilikuwa ni jina la rais wa Tanzania kwa wakati huo (2003).
"Jina la rais ni Nyerere (alikuwa ni Rais Mkapa), alijibu bibi huyo." Mbowe alitikisa kichwa na kusema, ‘kazi ipo.'
Kazi ipo, kwani mbali na kuwaeleza ukweli juu ya umuhimu wa mabadiliko, imekichukua chama hicho takiriban miaka 18 tangu kuanzishwa kwake kukubalika, hasa kwa Watanzania, na kuwa chama kikubwa rasmi cha upinzani ndani ya mioyo ya Watanzania.
Tukirejea Iringa na Mbeya, sehemu ambayo kila mara baada ya mikutano ya elimu kwa umma viongozi wa CHADEMA walikuwa wakiitwa polisi na kukumbushwa kuzingatia mambo fulani fulani, ilimradi tu kuwabana, leo hii imekuwa ni vituo vikuu vya upinzani katika njia kuu hiyo ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Leo hii ni faraja kubwa sana kutambua kwamba nguvu, rasilimali na elimu ya uraia waliyoitoa viongozi hawa wa CHADEMA havikupotea bure.
Havikupotea bure, kwa sababu ilihitaji ujasiri wa hali ya juu kujitolea kusafiri nchi nzima katika safari zilizopewa majina mbalimbali kama ‘Operesheni Sangara' ilimradi kuwaelezea Watanzania umuhimu wa mabadiliko katika taifa letu.
Dk. Slaa alitumia muda mwingi kuwaelezea namna ambavyo wana Karatu wanafaidi matunda ya jasho lao, kwa maana ya maendeleo, baada ya kuichagua CHADEMA na hatimaye kuunda halmashauri. Zilikuwa ni hadithi nyingi za kuwaomba Watanzania wabadilike.
Leo hii, Watanzania wameusikia mwangwi kutoka Karatu, Moshi, Kigoma, Mbeya, Iringa, Mwanza na Arusha.
Source Tanzania daima.
 
Na mimi kwa sababu hizo hapo juu mwaka jana niliamua kwa moyo wangu kuwa nahitaji kuwa mwanachama wa Chadema. Nilipewa kadi yangu tarehe 22.11.2009 na Mh Freeman Mbowe. Nafurahia sana kuwa Mwana wa Chadema.
Nakumbuka niliwahi kupata kadi ya CCM mwaka 1982 nikiwa JKT maana ilikuwa ni lazima na wakati huo tulikuwa na mfumo wa chama kimoja. Sikukipenda chama cha mapinduzi kabisa hata wakati ule maana kilikuwa ni chama cha kibabe kilichotunyima fursa ya maamuzi binafsi, lakini sikuwa na option.
Kisha nilipomaliza JKT sijui hata kadi yenyewe ya CCM ilipitia njia gani. Hata hivyo niliendelea kujiweka mbali na chama hiki cha CCM kadri nilivyoendelea kuzeeka. Ulipoanza mfumo wa vyama vingi nilikuwa bado siipendi CCM lakini pia sikuwa nataka kujiunga na chama chochote bila kujua kipi hasa ni chama kinachonifaa. Sikutaka kukurupuka. Hii ilinifanya kwa miaka yote hiyo kuendelea kuvipima vyama na kuona kipi hasa ni chama kiko serious na kinadhamira ya kweli kumkomboa mtanzania? Miaka kama minane iliyopita nilianza kuvutiwa na sera na uongozi imara na thabiti usioyumba wa Chadema. Hata hivyo sikuwa mwepesi kujiunga na chama hiki. Na, mwaka jana nilipokutana na Mbowe nililazimika kuweka rehani mapenzi yangu kwa Chadema. Nimekitumikia kwa nguvu sana wakati wa uchaguzi huu na nafurahi nimeona matunda yake.
Yaliyo mbele yangu kwa sasa ni kujitolea kwangu tena kuijenga Chadema kwa nafasi ndogo niliyonayo. Najua mchango wangu hautajulikana kwa wakubwa wa chama lakini I feel proud kwamba nitauona na kuufurahia mimi mwenyewe binafsi. Nimewashauri na wanangu kwamba hakuna mkombozi wao kisiasa zaidi ya Chadema na nafurahi familia yangu Yaani mama yangu ambaye alikuwa mkereketwa mkubwa wa CCM na wadogo zangu na wana wao ( wale wa kike walioolewa hata waume zao) na sasa mke na watoto wangu wanne, wote tuko Chadema. Haya ni mafanikio makubwa.
 
Na mimi kwa sababu hizo hapo juu mwaka jana niliamua kwa moyo wangu kuwa nahitai kuwa mwanachama wa Chadema. Nilipewa kadi yangu tarehe 22.11.2009 na Mh Freeman Mbowe. Nafurahia sana kuwa Mwana wa Chadema.
Nakumbuka niliwahi kupata kadi ya CCM mwaka 1982 nikiwa JKT maana ilikuwa ni lazima na wakati huo tulikuwa na mfumo wa chama kimoja. Sikukipenda chama cha mapinduzi kabisa hata wakati ule maana kilikuwa ni chama cha kibabe kilichotunyima fursa ya maamuzi binafsi, lakini sikuwa na option.
Kisha nilipomaliza JKT sijui hata kadi yenyewe ya CCM ilipitia njia gani. Hata hivyo niliendelea kujiweka mbali na chama hiki cha CCM kadri nilivyoendelea kuzeeka. Ulipoanza mfumo wa vyama vingi nilikuwa bado siipendi CCM lakini pia sikuwa nataka kujiunga na chama chochote bila kujua kipi hasa ni chama kinachonifaa. Sikutaka kukurupuka. Hii ilinifanya kwa miaka yote hiyo kuendelea kuvipima vyama na kuona kipi hasa ni chama kiko serious na kinadhamira ya kweli kumkomboa mtanzania? Miaka kama minane iliyopita nilianza kuvutiwa na sera na uongozi imara na thabiti usioyumba wa Chadema. Hata hivyo sikuwa mwepesi kujiunga na chama hiki. Hata hivyo, mwaka jana nilipokutana na Mbowe nililazimika kuweka rehani mapenzi yangu kwa Chadema. Nimekitumikia kwa nguvu sana wakati wa uchaguzi huu na nafurahi nimeona matunda yake.

Asante Kaa la Moto
 
Hata mie nilipewa kadi ya CCM nikiwa Ruvu JKT, lakini nilipotoka kule mwaka 1995 sikumbuki niliiacha wapi. Mimi na familia yangu chadema dam. Mwaka huu nimefanya jitihada kubwa ya kuhakikisha chadema wanashinda udiwani kwenye kata yangu. Kijana aliyegombea nilimwomba mimi ili agombee japo ndiyo kamaliza shule. Nilimpigia kampeni mpaka kashinda kata, na hata mbunge wangu ni chadema.

Japo ushindi wa chadema uliathiri ajira yangu, kwa kuwa nilikuwa nafanya kazi kwenye kampuni ambayo ilimpa JK helicopta, ( nilipewa demotion kwa kitendo cha kupiga kampeni ya chadema), sijaathirika kisaikolojia kutokana na kujiamini kwangu. Hata hivyo Mungu ni Mwema, kwani tarehe ya kesho pakikucha salama nimeitwa kufanya kazi sehemu nyingine ambapo nitakuwa nalipwa ujira mara 3 ya ule niliokuwa nalipwa.

CHADEMA NA MIMI MIMI NA CHADEMA MPAKA TUINGIE IKULU.
 
Hayo ndiyo mapambano mwenzangu. Usijali. Mandela hakufikia rekodi aliyonayo kirahisi. Leo is a hero.
Mungu atakuwa nawe. Asante kwa uaminifu wako na kushiriki mapambano!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom