CHADEMA imekiri kufadhiliwa kutoka nje ya nchi katika shughuli zake za kujijengea uwezo

Status
Not open for further replies.
Mahakama haitaongelea MAANA ya kuchukua pesa toka nje , itajiridhisha kama KWELI CDM imechukua pesa toka nje.
Hivyo ni vitu viwili tofauti kisheria.
Uwe unaelewa mambo Nape ailichokisema kuhusu madhumuni ya pesa ndicho kinaleta kesi sio kuchukua kutoka nje!.
 
Mbona serikali inafadhiliwa 40% kwenye budget yake kila mwaka! na wanaoenda kuomba msaada ni viongozi wa s/kali ya CCM.Waseme wazi masharti wanayopewa huko ughaibuni ili tuchujue jinsi ya kuwasaidia isije ikawa wanavurugwa ili kupata misaada

Kwa hiyo unaharalisha wizi wa serikali ili CDM nao waibe. Mkuu, mbona sikuelewi hata kidogo.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekiri kufadhiliwa kutoka nje ya nchi katika shughuli zake za kujijengea uwezo.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt Willibrod Slaa alisema hayo jana katika semina iliyoshirikisha baadhi ya viongozi wa chama hicho na wageni kutoka shirika la Chama cha Kikristo cha Ujerumani (CDU) la Konrad Adenauer Stiftung (KAS).

Kwa mujibu wa Dkt. Slaa, CHADEMA na KAS, wamekuwa na ushirikiano wa karibu kwa miaka sita sasa na ushirikiano huo umelenga zaidi kukuza demokrasia nchini.

Dkt. Slaa alidai kuwa CHADEMA ni chama chenye uwazi kwa kila mtu na katika uhusiano wao na KAS, hakiletewi fedha moja kwa moja kwa ajili ya operesheni au maandamano, ila kujijenga kiuwezo.

“Kwa sasa kumekuwa na propaganda zinazoenezwa kwamba CHADEMA wanapata mabilioni ya fedha kutoka kwa wafadhili, hii si kweli, ila wanatujengea uwezo na si kutufadhili kampeni. Napenda kusema propaganda za aina hii zimepitwa na wakati na wote watakaozifanya tutawafungulia kesi,” alisema Dkt. Slaa.

“Wanaosema kwamba CHADEMA wanapokea mabilioni nao wanashirikiana na mashirika ya aina hiyo yenye mrengo mmoja na ni utamaduni duniani kote, vyama vyenye mrengo mmoja kushirikiana, hivyo hii dhana isipotoshwe,” alidai.

Pamoja na kusema kuwa KAS haitoi fedha moja kwa moja kwa CHADEMA kwa ajili ya maandamano na kampeni, lakini Dkt. Slaa alidai kuwa shirika hilo huwasaidia wastani wa Sh milioni 60 kwa mwaka kwa ajili ya machapisho na kutoa elimu.

Pia alisema kipo chama cha Uholanzi ambacho hakukitaja jina, lakini akakiri kuwa huwafadhili Sh milioni 20 kulingana na idadi ya wabunge walio bungeni.

Pamoja na kusema kuwa ni kawaida kwa vyama vya mrengo mmoja kusaidiana duniani, Dkt. Slaa alisema chama hicho cha Uholanzi kinachowasaidia, pia hufadhili CCM fedha zaidi ya zinazopelekwa CHADEMA kutokana na chama hicho tawala kuwa na idadi kubwa ya wabunge.

Nape ashitakiwa

Dkt. Slaa alidai kwamba kwa kuanzia wameamua kumshitaki Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

Kwa mujibu wa madai ya Dkt. Slaa, tayari CHADEMA imefungua kesi namba 186 ya mwaka 2012, katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi Nape, ambaye anadaiwa alitamka CHADEMA kufadhiliwa kutoka nje.

Dkt. Slaa alidai kuwa kesi hiyo itakapokuwa ikiendelea, wataongeza watu wengine walioeneza kauli hiyo.

Semina ya KAS

Akizungumzia semina ya kujenga uwezo iliyotolewa jana kwa makada wa CHADEMA, Dkt. Slaa alisema imelenga kuangalia wanavyoweza kuleta uchumi wa soko utakaoshirikisha watu walio katika ngazi za juu na chini.

Lengo la kushirikisha watu hao wa tabaka mbalimbali kwa mujibu wa Dkt. Slaa, ni ili raslimali za nchi zitumike kwa faida ya Watanzania wote ambapo pia mgeni kutoka KAS ambaye alipata kuwa Naibu Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Klaus-Jurgen Hedrich atatoa mada.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alisema ili uchumi uwe endelevu, lazima wananchi wapewe haki na kuruhusu sekta binafsi kusimamia uchumi na si rahisi kusimamia uchumi kwa sera za kijamaa.

via HabariLeo

Source: wavuti - wavuti




My VIEWS!
Kila mtanzania anaefuatilia siasa za Tanzania anamfahamu ndugu NAPE NNAUYE tangu alipokua UVCCM na hatimae ukuu wa wilaya. Mabadiliko yake hasa alipokua mkuu wa wilaya ilibidi mtambue kua kelele alizokua akipiga UVCCM ilikua ni kutokana na kutaka kutimiza ndoto flani aliokua nayo, na pindi alipoona mwanga (Baada ya kua m/wilaya) mtazamo ukaanza kuota kutu. Hii ni kwa kua anajaribu kuonyesha ukweli ulio nyuma ya pazia tangu enzi za waliomlea (CCM).

Kukimbizana na mtu kama huyu mahakamani ni kupoteza muda kwani mi ninamfahamu kama mtu wa maneno mengi hasa linapokuja suala la FEAR OF THE UNKNOWN.......
CHADEMA endelezeni kile mnachoamini kitatutoa katika hali hii tuliyonayo na Watanzania wataamua katika sanduku la KURA katika chaguzi, CCM sera ni ileile iliyomtoa Rostam katika siasa(MAJI TAKA) japo si muumini wa kigezo hiki.

we jamaa ni mbunifu.jina lako na ulichokiandika vanafanana.ila bahati yko hautonani humu ingekua umeshaaga sayari leo.ila hongera kwa kutuletea cdm mapovu day.
 
Imagine CUF ikiri kupokea misaada kutoka chama kimoja cha Kiislamu IRAN! JF pasingekalika na magezeti yao pia! Mungu hawafich wanafiki! Wadini wakubwa nyie!
mkuu hawa waG niwanafiki wakutupwa. usiwaone wanakuchekea machoni yaliyo nyoyoni zao ungeyajua ungekimbia kama si kupaa kwa kasi. sisi tuko tofauti sana nao. in short we are so open, lakini wenzetu ni tofauti sana kama hujui.
 
Kwa uelewa wangu finyu,MAANA ya kuchukua pesa inakuja BAADA ya kuchukua pesa hizo.
Kipi kinakuja kwanza?
Inamaana unaongelea kitu ambacho hukijui?. Kamuulize Nape mwenyewe alisema nini mimi nikikuambia utasema nakudanganya!.
 
Inamaana unaongelea kitu ambacho hukijui?. Kamuulize Nape mwenyewe alisema nini mimi nikikuambia utasema nakudanganya!.

Ndiyo maana nasema Dr kachanganyikiwa kwa sababu
  • kakubali kuwa kachukua pesa toka nje(as if that is not bad enough)
  • anasema pesa hiyo ni ya kujenga uwezo(whatever that means)
Kwa kifupi, its an admission of guilt hata kabla kesi haijaongelewa kwa kila anachoshitaki.

Sijui vyama vikianza kuomba omba pesa toka nje -kwa ajili ya kujenga uwezo-Tanzania itakuwa inafadhiliwa hata kwenye siasa zake.
Kitu kile kile ambacho CDM inakipigia kelele na kupinga majukwaani, niambie mkuu mnafiki yu wapi?

Mimi nikianzisha chama na nikawaalika wachina kukiendesha kwa ajili hawana gharama natumaini utanipata madhara yake yatakuwaje.
 
Sasa nyie argument yenu ni kuwa kama CCM anafanya basi kwanini na nyie msifanye. Kama ni hivyo ni ukombozi gani mtauleta, CCM mnasema wameuza nchi kwa wafadhili sasa na nyie mnafanya nini? TZ hakuna mkombozi wa kweli wanasiasa wote ni wizi tu,hakuna cha CCM wala CDM.

Nikisoma koment kama hii napata picha jinsi gani vijana wetu wanahitaji elimu ya maarifa! Tatizo ni nini? Ni mitaala ya elimu ama uvivu wa kujisomea? Mbaya zaidi,mhariri wa gazeti la serikali anaposhindwa kusahihisha maneno ya kishabiki ktk gazeti lake! Ingekua Uhuru/Mzalendo nisingechangia chochote!
 
[/B]

Mwandishi ametoa source ya habari hii. lakini wasomaji wengi wamaishia kusoma habari hii nusu nusu.
Katika source ya habari hii, Dr. Slaa aliendelea kusema kuwa Chadema, CCM na Cuf wote wanashirikiana na mashirika fulani ya huko Ujerumani.
Ila watu kwa uvivu wa kusoma na kwa kukurupuka kwa mvuto wa udini, wameanza kutoa comments za ajabu sana.
Kama Chadema inashrikiana na mashirika ya Ujerumani, na inabandikwa udini, sasa CCM na CUF nazo zitabandikwa nini ??
Kwa mijibu waDr. Slaa, "...CCM inashirikiana na FES, CUF inashirikiana na FNF zote za Ujerumani..."

Sasa hebu tuone yaho mashirika mengine yaliyotajwa hapo.

1. Tuanze na FES ambayo CCM inashirikiana nayo:
The Friedrich Ebert Foundation (German: Friedrich-Ebert-Stiftung; Abbreviation: FES) is a German political foundation associated with the Social Democratic Party of Germany (SPD), yet independent of it. Established in 1925 as the political legacy of Friedrich Ebert, Germany's first Democratically elected President, it is the largest and oldest of the German party-associated foundations. It is headquartered in Bonn and Berlin, and has offices and projects in over 100 countries. It is Germany's oldest organisation to promote democracy, political education, and promote students of outstanding intellectual abilities and personality. The current President of the FES is Peter Struck.

2. Tuje kwa FNF ambayo CUF inashirikiana nayo:
The Friedrich Naumann Foundation (German: Friedrich-Naumann-Stiftung für die Freiheit) (FNF) is a German foundation for liberal politics, related to the Free Democratic Party. Established in 1958 by Theodor Heuss, the first president of the Federal Republic of Germany, it promotes individual freedom and liberalism.
The Foundation follows the ideals of the Protestant theologian, Friedrich Naumann. At the beginning of the last century, Naumann was a leading German liberal thinker and politician. He resolutely backed the idea of civic education. Naumann believed that a functioning democracy needs politically informed and educated citizens.

Hao SPD wanaoshirikiana na CCM ndio wanaounga mkono sana ndoa za jinsia moja.
Halafu, hao FNF wanaoshirikiana na CUF, sera zao zinafuata maadili ya kikristo ya mwanzilishi wao Pastor Friedrich Naumann.



  • Sasa kwa msingi huu hapo juu, tunaweza kusema nini kuhusu CCM na CUF ??
  • Kwamba CCM wanaunga mkono ushoga, na CUF wapo kidini zaidi ndani ya Ukristo ???


tatizo jina la chama na sera zake zimelenga kundi fulani! chama chenyewe kinaitwa Chama cha Kikristo cha Ujerumani (CDU) .... JINA LA CHAMA LINABEBA LENGO ZIMA LA HIKO CHAMA AU KAULI MBIU YAO! . no wonder chadema ni anti muslims
 
My VIEWS!
Kukimbizana na mtu kama huyu mahakamani ni kupoteza muda kwani mi ninamfahamu kama mtu wa maneno mengi hasa linapokuja suala la FEAR OF THE UNKNOWN.......

Views zako ni nzuri ila ni nje ya hoja.

Hoja 1. Chanzo au gazeti lililoandika ni Habari Leo. Ni la kupuuza maana kwao sumu ni sukari na sukari kwao ni sumu.

Hoja 2. "CDM yakiri" ni tafsri iliyokengeuka yenye lengo la kupotosha maana halisi. CDM inasemekana kupokea "mabilion toka kwa serikali zilizoahidiwa (na CDM) kuja kujinufaisha na rasilmal ya nchi waingiapo madarakani". Gazeti letu halizungumzii hilo.

Hoja 3. Kumuunganisha Nape kwenye uzi ni dhahiri ndilo lengo la gazeti kwa ajili ya kujenga mazingira ya kumsafisha. Ni upuuzi kwa sababu suala limeshatua kwenye mahakama ambapo pumba na mchele vitapembuliwa.

Mimi binafsi nilikwisha sitisha kusoma gazeti hili hadi hapo litakapo anza kutuandikia taarifa sahihi za kitaifa kuhusu maendeleo na vita dhidi ya dhuluma mbali mbali zikiwemo za watawala.
 
Ndiyo maana nasema Dr kachanganyikiwa kwa sababu
  • kakubali kuwa kachukua pesa toka nje(as if that is not bad enough)
  • anasema pesa hiyo ni ya kujenga uwezo(whatever that means)
Kwa kifupi, its an admission of guilt hata kabla kesi haijaongelewa kwa kila anachoshitaki.

Sijui vyama vikianza kuomba omba pesa toka nje -kwa ajili ya kujenga uwezo-Tanzania itakuwa inafadhiliwa hata kwenye siasa zake.
Kitu kile kile ambacho CDM inakipigia kelele na kupinga majukwaani, niambie mkuu mnafiki yu wapi?

Mimi nikianzisha chama na nikawaalika wachina kukiendesha kwa ajili hawana gharama natumaini utanipata madhara yake yatakuwaje.
Maliza moja sijakuuliza kauli za Dr. Slaa leta kauli ya Nape inayolalamikiwa, kama hujui alisema nini acha kuleta soga.
 
Nape umeshinda kesi mapema mwambie wakili wako haya maneno ya Dokta Slaa ndiyo ushahidi tosha. Ninavyowajua CDM watasema hawana imani na mahakama.
 
inaelekea waislamu wengi mnaogopa sana ukristo? Na kwanini wakristo wengi hawaogopi uislamu?

Maana watu mkiona neno ukristo tu mnaanza kutokwa povu.
mkuu upo dunia gani? sisi tumeishi na ukristo kwa miaka mingi, serikali ya nyerere ilikuwa ya kikristo kupitia mgongo wa ujamaa (na nndo maana hata haikufanikiwa kama wenzetu china kwani ilikuwa inawapendelea wakristo waziwazi), vatican ipo pale magogoni, lakini miaka yote tupo poa. sasa hebu angalieni suala la OIC lilipozungumzwa jinsi mlivyowaoga. jiulize oic ipo mpaka kenya, s. africa, uganda, uingereza na nchi nyingi zenye wakristo wengi. SWALI JE WAKRISTO WA TANZANIA MNAOGOPA NINI? kwa mantiki hiyo,nani kati ya waislam na wakristo wanawaogopa wenzao?
 
Mbona mnapenda propaganda za udini?

Imagine CUF ikiri kupokea misaada kutoka chama kimoja cha Kiislamu IRAN! JF pasingekalika na magezeti yao pia! Mungu hawafich wanafiki! Wadini wakubwa nyie!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom