CHADEMA imefanya nini kustahili dhamana ya Uongozi wa Taifa?

Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu mifano yangu ipo karibu sana na reality ya MIAFRIKA. Tunazo mila na desturi zetu ambazo hutengeneza matendo yetu kwa ujumla, hivyo mifano yangu mara nyingi ipo karibu na Mtanzania yaani mambo ambayo ni rahisi kwetu sote kuyatazama pasipo kutumia taalama..Kisha usije fikiria kabisa mfano huu unahusiana na mambo ya ngono kwani mume hachaguliwi kwa sababu ya ngono ila uwezo wa kusimamia mamlaka ya mume ndani ya nyumba...hii ndio maana ya mfano wangu.
Na pengine yawezekana hapa ndipo tunapotofautiana, wakati mimi nazungumzia uwezo wa Chadema (msera) kuongoza kama baba mwenye nyumba na ndipo wewe umeweka Doubt zako, kumbe mwenzangu unakitazama chama hiki kama Mtalimbo umelala - unataka ushahidi kuonyesha kama Chadema kawahi kuwa na hata Girlfriend! Duh..Hee heee heee -makubwa haya!

Mkuu usinielewe vibaya mifano huo hauna maana wewe ni mwanamke asiyejua akitakacho, hapana najua fika unajua ukitakacho na ndio maana umekuwa mstari wa mbele ktk mapambano haya isipokuwa mfano wangu unalenga kuonyesha kwamba wewe mzito ku make decision based on factors ambazo zinakutaka wewe na sii chama kuziwakilisha. Kwa hiyo ni wewe unayetakiwa kukubali kuolewa na huyu Chadema kwa mategemeo kwamba nyumba yenu mtaijenga nyote na sii kutegemea Chadema (mume) alichowahi kujenga kiwe ndio factor kubwa.

Je, Sii kweli wapo watu wamekaa ktk ndoa pasipo kujali maslahi yao?..Je, sii kweli watu wa aina hiyo hututupeleka kufikiria kwamba hawaoni kuna maisha zaidi ya kuwa chini ya mume huyo, wengine hata husingizia watoto kama sababu lakini ukweli ni kwamba matatizo wanayo wenyewe..

Mkuu wangu CCM ni abusive kwako, na kama utaendelea kuwatazama kina Chadema na CUF kwa kipimo cha uwezo wake basi wewe hutafuti changes ila unataka kumbadilisha huyu mume CCM characters zake kwa kuwakosoa.. Jambo ambalo unafanya makosa kabisa kwani mtu yeyote abusive siku zote ukimkosoa ndio kwanza unazidisha hasira zake.

Walisema hivi kwa kila Mageuzi yoyote.. Hakuna chama cha Upinzani kilichoweza kujijenga pasipo watu wake.Chama Chadema sii chama kama wewe na wengine wote mtasimama nje kama watazamaji ukifikiri dhamana ya usafiri wetu wameichukua Chadema kwa gharama ya Ujamaa..Ni wewe, mimi na wengine wote tutakao kiwezesha chama chochote kile kiweze kuongoza nchi kama ilivyotokea Iran, Poland, Cuba, South Africa, Kenya na kwingineko kote.

Na ndio maana mara zote michango yetu iwe kwa CCM ama Chadema inatakiwa iwe ile ya kuziba nyufa, kufanya ukarabati ama kujenga upya kwani vyama hivi vitakuwepo hata baada yetu. Chadema au TTTP ni vyama, sii Mbowe wala Rev. Kishoka wanaotazamwa..kwani tukifanya hivyo tutashindwa kabisa kuelewa nini maana haswa ya kuwa na Demokrasia.
 
.

Walisema hivi kwa kila Mageuzi yoyote.. Hakuna chama cha Upinzani kilichoweza kujijenga pasipo watu wake.Chama Chadema sii chama kama wewe na wengine wote mtasimama nje kama watazamaji ukifikiri dhamana ya usafiri wetu wameichukua Chadema kwa gharama ya Ujamaa..Ni wewe, mimi na wengine wote tutakao kiwezesha chama chochote kile kiweze kuongoza nchi kama ilivyotokea Iran, Poland, Cuba, South Africa, Kenya na kwingineko kote.

.

Mkandara ndugu yangu, nadhani tunkosea maada hii, ishu si kuwa watu hawataki changes,ishu ni kuwa hivi vyama viko tayari kwa kiasi gani kuleta hizo changes.

Haya kila siku kuna vurugu kwenye hivyo vyama, wanafukuzana, mambo ya fedha hayako wazi, yet wasiwe questioned.

Kuna watu wanataka wagombee uongozi wananyimwa! kuna watu wanataka kutoa fedha wanasita!

Kama mimi mwanamke mkuu, ninaona kuna mwanaume anapiga wake zake wote aliowataliki, na kila aliyemtaliki ana alama, huyu kilema, huyu chongo, then bado akija kunitongoza niende tu!

I believe these are challenges that Chadema needs to face.NAtaka washike nchi, nimechoka na CCM. They need to be smart than they are now!

msipowaambia ukweli mnawadanganya
 
Waberoya,
Haswaa mkuu wangu maneno yako msumari na ndicho mimi najiuliza zaidi kila siku ya Mungu..Lakini pamoja na yote haya hukunisoma vizuri kuwa Ugonvi wa Chadema ni ungonvi wa ndugu yaani wanalambana makofi kwa sababu ya mirathi, mali au hata ardhi..Wanachohitaji ni ushauri mzuri, mwamuzi wa haki katika mapato na mwenye hekima ambao ndugu hawa watamsikiliza na kumwamini..
Hivyo maamuzi ya kwamba familia nzima haifai kutokana na ugonvi wao kuyaweka ktk maswala ya ndoa sidhani kama vinahusiana.
CCM, wao wanaweza kumaliza matatizo ya kifamilia ndani ya vikao vyao, ni utaratibu tofauti sana na Chadema lakini wanaokuja umia ni wake na watoto wa kizazi chao (wananchi) wakati Chadema hata kumpata mke imekuwa shida.. Ndio maana nimekusanya mawazo ya watu hapa na kupata hofu ya wananchi kuhusiana na uwezo wa Chadema kuongoza kutokana na udogo wake, experience yake na mengineyo ambayo hayahusiani kabisa na kumchambua Msera anayetafuta mke.
 
Mkandara ndugu yangu, nadhani tunkosea maada hii, ishu si kuwa watu hawataki changes,ishu ni kuwa hivi vyama viko tayari kwa kiasi gani kuleta hizo changes....


I believe these are challenges that Chadema needs to face.NAtaka washike nchi, nimechoka na CCM. They need to be smart than they are now!

msipowaambia ukweli mnawadanganya

Waberoya, mimi nafikiri Watanzania na sio vyama vya upinzani ndivyo vinatakiwa kuwa smarter than they are right now. Habari za ugomvi na mafarakano unayoyazungumzia yanayotokea kwenye vyama vya upinzani kwa kiasi kikubwa yanachochewa na vyombo vya habari. Na vyombo hivi tunajua wanaovimiliki ni wakina nani. Wengi wao wana political ambitions. Kuna magazeti na stesheni za redio zimeanzishwa mwaka huu purposely kwa ajili ya uchaguzi wa 2010. 2005 ilikuwa hivyohivyo yakaja magazeti lukuki baada ya uchaguzi yakapotea. Hivyo propaganda za kupakana matope zimeanza.

Haya kila siku kuna vurugu kwenye hivyo vyama, wanafukuzana, mambo ya fedha hayako wazi, yet wasiwe questioned.

CHADEMA hamna mtu aliyefukuzwa. Dk Slaa amemwondoa Kafulila kwenye sekretariat kwa kufuata kanuni za chama. Ameeleza kwenye vyombo vya habari kwanini amefikia uamuzi huo. Ni vema tukajadili sababu alizozitoa Dk Slaa za kumvua uongozi Kafulila na sio kung'ang'ania kwanini amefukuzwa wakati hamna aliyefukuzwa.


Kuna watu wanataka wagombee uongozi wananyimwa! kuna watu wanataka kutoa fedha wanasita!

Kama mimi mwanamke mkuu, ninaona kuna mwanaume anapiga wake zake wote aliowataliki, na kila aliyemtaliki ana alama, huyu kilema, huyu chongo, then bado akija kunitongoza niende tu!

CHADEMA hamna mtu aliyenyimwa kugombea uongozi. Zitto alishauriwa na wazee wa chama aondoe jina lake kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa uenyekiti na yeye akakubali kuliondoa. Hajawahi kusema popote pale kwamba alinyimwa. Na hii sio mara ya kwanza kwa mgombea kuombwa kuondoa jina kwenye uchaguzi ndani ya chama. Mwaka 2004 Shaibu Akwilombe alipochaguliwa kuwa naibu katibu mkuu mgombea mwezie aliombwa aondoe jina lake baada ya kuonekana kampeni zinaelekea pabaya.

Usikubali kusikia majirani na wapambe nuksi wakikuambia yule alipigwa akaondoka na kilema, ah na yule mwingine chongo, nenda mwenyewe ukahakikishe. Pengine hao watoa habari wanakuonea wivu wanataka watongozwe wao. Hivyo tunatakiwa tuwe wabunifu zaidi kujua kuwa hizi habari tunazoambiwa ni za kweli au ni watu wanajipanga kwa ajili 2010. Yes indeed, We need to be smarter.
.
 
Wapo wanaoamini kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ndiyo chama mbadala cha kisiasa chenye uwezo wa kushika hatamu ya Uongozi kwa kuunda serikali. Wenye imani hii wanaamini kabisa kuwa CCM imeshindwa kabisa na hivyo ni lazima iondolewe madarakani ili chama kinginge "kipewe nafasi" ya kuliongoza Taifa letu kuelekea kule tunakotaka.

Tukilinganisha uwezo wa watu, raslimali, historia na mwelekeo kati ya CCM na Chadema chama cha CCM kinaicha Chadema kwa mbali sana. Linapokuja swali la mahusiano ndani ya vyama hivyo ni wazi kuwa vyama hivyo vyote havina tofauti sana katika kusababisha migogoro ya ndani, kutumia michakato ya ndani kushughulikia matatizo yao na vile vile kuendesha propaganda dhidi ya kingine.

Hata hivyo tunapoelekea katika Uchaguzi Mkuu ujayo na tukiamua kupima rekodi ya Chadema kwa miaka hii karibu 15 iliyopita tunalazimika kujiuliza kama kweli Chadema ndicho chama kinachoweza kweli kuliongoza Taifa letu. Na tukiiangalia historia hiyo kwa ukaribu wa miaka hii minne iliyopita tunalazimika kujiuliza kama Chadema kimefanya mambo yoyote, kuonesha uongozi katika jambo lolote au kwa namna yoyote ile kuamsha Watanzania katika kujiletea mabadiliko kiasi cha kuweza kustahili mapenzi, imani, na ufuasi wa watu wengi sasa hivi.

Je, yawezekana watu wanaokimbilia Chadema sasa hivi au wanaoiamini Chadema wanafanya hivyo si kwa sababu ya mapenzi yao kwa Chadema ilivyo bali kutokana na chuki yao kwa CCM na utawala wake wa mfumo wa kifisadi kwa miaka 45 iliyopita?

Je, yawezekana katika kutoridhika huku watu wamefumbia mapungufu makubwa ya kimuundo, kiitikadi, kichama na kimwelekeo ya Chadema ambayo yanaweza kujitokeza kwa nguvu kubwa endapo chama hicho kitashika madaraka ya nchi na hivyo kuturudisha kwenye "madudu" yale yale ya CCM?

Je, yawezekana kwa kuweka imani pofu (blind faith) kwa kundi la watu ambao wamejithibitisha mara kadhaa kuwa hawajamudu fani na sanaa ya siasa na kuwa ni jopo la watu wenye mtazamo wa kisomi zaidi (elitist) kuliko wa kimwamko wa mabadiliko wanajiandaa kwa kukatishwa tamaa?

Je, yawezekana ndio sababu bado wasomi wengi na watu wengi katika taifa letu bado wanaikumbatia CCM na kuikubali kwa sababu tayari wanajua madudu yake (zimwi likujualo) na hawako tayari bado kuweka imani yao kwa chama hiki au kingine chochote cha upinzani?

Je, yawezekana uongozi wa Chadema ulivyo sasa hasa mvutano wa kipuuzi kati ya Freeman Mbowe na Zitto Kabwe ni kikwazo kikubwa zaidi kwa kumuamsha jitu huyu aliyelala (this sleeping giant) kiasio kwamba hawa wawili peke yao kinyume na inavyochukuliwa ndio kikwazo kikubwa zaidi kwa Chadema kupiga ile hatua ya lazima mbele? Je, itakuwa bora kama hawa wawili wakaachilia nafasi za juu za uongozi wa Chama ili kukipa chama ule msukumo unahojitajika?

Katika kutafuta majawabu ya maswali haya siyo vyema kwa kweli kuendelea kuikumbatia CCM na madudu yake na kujaribu kuiokoa kwani ndio njia ya haraka ya kuleta mabadiliko ya haraka kuliko kukumbatia upinzani ulivyo sasa?
Ni maoni yako MM....Kwa jinsi nionavyo mimi..Chadema imefanya mambo makubwa sana.Mfano VITA DHIDI YA UFISADI,Ikumbukwe kwamba Chadema ndio waanzilishii wa mapambano dhidi ya ufisadi nchini ambao umepelekea kuwajibika kwa baadhi ya viongozi wakubwa serikalini...ni mafanikio ya kujivunia..Pili kwa majimbo yaliyo chini ya chadema baadhi ya kero kwa wananchi zimepungua mfano kodi ndogondogo,uboreshwaji wa huduma kwa jamii(Karatu).
Lakini MM tambua kwamba Chadema Haikushika DOLA hivyo usitaraji ifanye mambo makubwa sana..Haya hiyo CCM karibu nusu karne sasa imefanya nini.....???
Mi nafikiri suala la migogoro ndani ya chama ni jambo la kawaida na inaonesha kukomaa kwa chama..mfano ANC(kilipitia katika migogoro mikubwa),CCM migogoro bado inaendelea,Hivyo migigoro ndani ya chama ni kawaida,Pia viongozi wasiofuata Miiko na Maadili ya Chama kamwe hawawezi kuvumilika katika chama chochot kile.
Ni imani yangu kuwa hata MM unafahamu kuwa Chadema ni chama chenye katiba bora kabisa ambayo inaonesha dira ya maendeleo ya nchi hii..
 
Tuwape nchi CHADEMA then tuone watafanya nini after 5 years, wakiboronga kama JK then tutawauliza wamefanya nini.
majaribio hayo ni mabaya sana;
katika hali hii kweli tunataka kuwapa dhamana ya maisha ya watu takribani milioni 40? Not in my watch.

hapana.. CCM isibaki madarakani kwa sababu inastahili! Lakini tusiwapandishe watu wengine madarakani pasipokustahili.. maanake ni kuwa kwa yeyote anayetaka kuja juu yetu we have to set the bar very high not very low.. Hivyo, siyo kuiondoa CCM for the sake of kuindoa CCM.. we have learned in Kenya.. we have to remove the ruling party kwa sababu we got something better!.. Na njia pekee ya kupata "better" ni kuhakikisha tunawapitisha kwenye tanuru ya moto kwanza...

Mwanakijiji,
Nakubaliana na wewe kabisaa. Haya ni maendeleo mazuri sana kutoka kwako kuacha kukiangalia CHADEMA katika mtazamo wa kiushabiki bali kuwa tayari kukikosoa. Constructive critisim zitakapofanyiwa kazi, CHADEMA itajengeka. Ila sasa utegemee matusi ya nguoni, kwani ustaarabu uliopo wa wapenzi wa CHADEMA ni kuwa ukisema lolote ambalo sio la kuisifia CHADEMA, basi wewe ndio unakuwa mchawi. Kwa hiyo usishangae unapoanza kuitwa a 'SHE'.

Ukweli ni kuwa kwa hali ya kibinafsi iliyopo ndani ya CHADEMA, Mtanzania yeyote mwenye akili na uchungu na nchi yake atakuwa radhi kuwapa CCM waendelee kutawala kuliko kumpa nchi Mbowe, Mtei au hata Dr. Slaa wa sasa.

Kama marehemu Wangwe alionekana kichaa, sasa hawa wengine wanaokuja na kelele zile zile za Wangwe nao ndio kusema wameambukizwa?

Let's be realy, it is our country that we should be fighting for and not personalities or parties.
 
CHADEMA wajipange upya hasa uongozi wa juu. Pia wapunguze "umiliki" wa chama unaoonekana wazi ni wa watu fulani. CHADEMA imilikiwe au ionekane inamilikiwa na WANACHAMA wote.

  1. Unapoona kiongozi anang'ang'ania madarakani hata ikibidi kufukuza wenzake, inabidi ujiulize je ana nia gani na chama?
  2. Unapoona hao wanaoitwa wafadhili wa chama wanang'ang'ania kuwa na watoto wao kama viongozi wa juu chamani, hapo inabidi ujiulize wanapigania nchi au familia zao?
  3. Unapoona hao wafadhili wanachangia pesa kwa ajili ya chaguzi zao/ndugu zao, halafu wanarudi kinyume-kinyume kukidai chama kutoka kwenye ruzuku, jiulize je wanakisaidia chama au wanakitumia tu chama kujijengea maslahi bila kukisaidia?
  4. Unapoona chama kinaongozwa na kihiyo halafu wasomi nao wanapotaka kuingia madarakani wanafukuzwa, basi ujue kuwa, huu ni mradi binafsi uliofichika.
Ukweli ni kuwa CHADEMA chini ya Mbowe, Mzee Mtei na Slaa, haiwezi kuwavuta watu wa kuiingiza ikulu. Watabakia na wale-wale wanaoimba zidumu fikra za Mtei/Mhowe huku wapiga kura wakijirudia CCM. Wake up people!!
 
Babu yangu, Mimi binafsi tumechoshwa na vyama hivi ambavyo kutokana na katika na taratibu za kuiga toka CCM ni yale yale na watu wale wale. sasa kuna haja hata ya kutokuwa na chama chochote kile kama ulivyo wewe mzee wangu
 

Ukweli ni kuwa CHADEMA chini ya Mbowe, Mzee Mtei na Slaa, haiwezi kuwavuta watu wa kuiingiza ikulu. Watabakia na wale-wale wanaoimba zidumu fikra za Mtei/Mhowe huku wapiga kura wakijirudia CCM. Wake up people!!


Ukweli gani huo wakati umekosa mipira ya kumhoji Mbowe?

Chicken ... qckshaaaccck .....ackhasdfaxckkl ...... qwekckeeee
 
Mag3..

- Kuanzisha shule ya sekondari ya kuchukua wanafunzi na yenye kutoa elimu bora. Wazazi bila kujali itikadi zao wangepeleka watoto wao kwenye shule hiyo kama ingeonekana kufanya vizuri zaidi kuliko zile za "wazazi" za CCM!

- Kuanzisha Kliniki au Hospitali kwenye maeneo kadhaa ya nchi aidha kwa mchango wao wenyewe au kwa kuandika project ya mradi na kuhakikisha kuwa taasisi hiyo inatoa huduma inayoshinda na kliniki au hospitali za serikali au binafsi. Watu wangeona Chadema in action. Hilo halihitaji kuwa madarakani.
r u serious mkjj?? you r way off the mark...
hii sio kazi ya upinzani kabisa
kazi ya upinzani ni kuhakikisha wananchi wanapata hizi huduma
upinzani haumiliki kodi ni ccm ndio wanachukua kodi yako na kuitumia wanavyotaka wao, upinzani wanatakiwa wakueleze alternative ya wao jinsi
watakavyotumia kodi yako na jinsi ccm wanavyo tumia vibaya ya kwako.

hata kama chadema au cuf watakuwa mafisadi zaidi ya ccm, ni mara mia mabadiliko ya tokee, hii itasaidia waTZ kuamka kwenye usingizi mzito
 
hapana.. CCM isibaki madarakani kwa sababu inastahili! Lakini tusiwapandishe watu wengine madarakani pasipokustahili.. maanake ni kuwa kwa yeyote anayetaka kuja juu yetu we have to set the bar very high not very low.. Hivyo, siyo kuiondoa CCM for the sake of kuindoa CCM.. we have learned in Kenya.. we have to remove the ruling party kwa sababu we got something better!.. Na njia pekee ya kupata "better" ni kuhakikisha tunawapitisha kwenye tanuru ya moto kwanza...
Mkuu hapa hata mimi nakubaliana nao lakini usije wapitisha Chadema ktk Tanuri la Pizza wakati unataka kuoka Mikate.. hutapata jibu.

Mkuu mimi nakubaliana nawe baadhi ya sehemu muhimu sana ambazo zinakitazama Chadema kama chama, sera zake, mrengo wake lakini hizi habari za wamefanya nini wakati Wabunge wake wanajitolea sehemu za mapato yao kwa wananchi wao lakini haihesabiki ila kwa Ujenzi wa shule na Zahanati ambazo unafahamu fika KISIASA ni jukumu la chama Tawala kulingana na mfumo wetu.

Amini maneno yangu ikiwa Chama chochote kitaheshimika kwa hayo basi utakuwa umehalalisha maneno ya Pinda kwamba maendeleo ya Kigoma yanapelekwa na CCM. Na ujenzi wa shule na Zahanati zote nchini, hao wabunge wa Chadema hawastahili sifa hata ya kupitisha badget ya matuzi hayo. Mkuu wangu hatuna madaraka mikoani ama serikali ya majimbo kiasi kwamba unaweza pima vyama hivi vimewawezesha vipi wananchi wake. Kifupi ni sawa na kupima maisha ya Mkimbizi akiwa Ulaya kambini kawasaiidia kiasi gani wananchi wa kwao. Bungeni ni kambi ya wakimbizi (economic refugees) wanakimbia ukweli wa maisha huku nje..
Mimi naamini hatuwezi kuona mabadiliko yoyote tokea Katiba, kusimamisha sheria, Uzalishaji, Ukusanyaji ushuru, Utekelezaji na Uwajibikaji pasipo kuchukua madaraka toka CCM. na kipimo pekee cha chama kinachoweza kufanya hivyo ni sera na vipaumbele vyake kwa mahusiano ya vitu hivyo..Hapo ndipo unaweza kupima mabadiliko, na ndivyo vyama vyote duniani hupimwa..
 
Mkandara ndugu yangu, nadhani tunkosea maada hii, ishu si kuwa watu hawataki changes,ishu ni kuwa hivi vyama viko tayari kwa kiasi gani kuleta hizo changes.

Haya kila siku kuna vurugu kwenye hivyo vyama, wanafukuzana, mambo ya fedha hayako wazi, yet wasiwe questioned.

Kuna watu wanataka wagombee uongozi wananyimwa! kuna watu wanataka kutoa fedha wanasita!

Kama mimi mwanamke mkuu, ninaona kuna mwanaume anapiga wake zake wote aliowataliki, na kila aliyemtaliki ana alama, huyu kilema, huyu chongo, then bado akija kunitongoza niende tu!

I believe these are challenges that Chadema needs to face.NAtaka washike nchi, nimechoka na CCM. They need to be smart than they are now!

msipowaambia ukweli mnawadanganya

hivi ile issue ambayo serikali inaandaa sheria yake na iliyokuwa discussed humu kuhusu mgongano wa kimaslahi kati ya biashara na siasa kwa viongozi wetu, CHADEMA wanaifahamu? au hawahusiki nayo? maana chadema wana tatizo la mda mrefu katika matumizi ya pesa hasa ya ruzuku. isije kuwa inazungushwa kwanza kwenye biashara:)
 
Ha ha haaa! Hakika mitanzania ndivyo tulivyo.

Mawazo ya kwamba CUF, CHADEMA, UDP, DP, NCCR wafanye hivi ndipo wapewe madaraka ya kuongoza nchi, ni upotoshaji wa hali ya juu. Naweza kusema ni mawazo yatokanayo na akili zilizodumaa.

Mimi ninachoangalia ni je, chama kilicho madarakani kimetekeleza yale kilichotuahidi? Kama ni jibu ni hapana; na labda wameharibu zaidi, basi chama hicho kifukuzwe toka ikulu. Mambo mengine haya ni kupotezeana muda, na jaribio la kulinda CCM ibakie madarakani kwa kuorodhesha kasoro nyingi za upinzani. Chama chochote kinachokaa ikulu na kushindwa kutimiza ahadi, kinafukuzwa kwa njia ya kura. Maboresho na kutimiza ahadi kutakuja kwa namna hiyo.

Sasa hivi inajulikana wazi tuna ombwe la uongozi, wakati CCM ipo madarakani. Mnataka ushahidi gani tena kwamba CCM haistahili kuwa ikulu baada ya uchaguzi ujao?

Wabongo bwana! Tunasikitisha.
 
Nimeona nirudi na kuendelea kujiuliza swali hili kwa kadiri siku zinavyoendelea. Yawezekana tumaini likatahayarisha?
 
Ukweli ni kwamba hatuna chama wala mtu tunachoweza/ tunayeweza kumpa dhamana ya uongozi. Not if we want to be critical.

And even if we don't want to be critical, static, mathematical, logical, bado hatuna chama wala mtu.

Kwa sababu gani? System yetu hairuhusu meritocracy. Wanaojulikana hawafai, wanaofaa hawajulikani. Na hatuna guarantee kwamba hata hao wanaofaa na kutojulikana leo wakipewa madaraka hawatabadilika, kwani Lord Acton alisema power corrupt and absolute power corrupt absolutely. Na bado hatujakomaa kuondoa absolute power mikononi mwa watu angalau kisheria, seuze kiutendaji.

Cha kufanya ni kuangalia nani atakuwa afadhali. Kuumizwa na mafisadi tunaowajua wa CCM au kuchukua a gamble with CHADEMA.

Halafu swala lingine CHADEMA ZNZ mbona iko kama haiko? Ina maana hawautaki muungano au vipi? Maana ZNZ mimi nasikia CCM na CUF tu. Kama hawautaki muungano si jambo baya kwangu, lakini tuambiane mapema, wengine tuna usongo wa kuja kupiga kura mwaka huu, and whoever it is going to be, it is not going to be CCM.
 
Nimeona nirudi na kuendelea kujiuliza swali hili kwa kadiri siku zinavyoendelea. Yawezekana tumaini likatahayarisha?

Unaonekana una moyo wa kishujaa kuendelea kujiuliza! mimi sina hata nguvu ya kujiuliza! tumaini linalochanganya watu ni lile unaona kabisa lipo, ikitokea bahati mbaya! angalia hii clip ya mtu anayetumainiwa kufunga magoli just 30s.

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=6zXpmGmRDTE&feature=related[/ame]

Tumaini unalolisema halikuwepo tangu mwanzo, watu wamecreate ideology lionekane lipo, likikosekana watu hao hao hawastuki wanasema -tulijua!!!
 
Nimeona nirudi na kuendelea kujiuliza swali hili kwa kadiri siku zinavyoendelea. Yawezekana tumaini likatahayarisha?

Kwa uongozi upi wa mbowe na Slaa...embu uliza kwenye department zao less than 10 people wanatenda haki na usawa? wanawakubali kwelikweli

Afadhali ya CUF kuliko hao CHADEMA sioni kama kuna watu nyuma yao, kwasababu wao wenyewe hawaonyeshi wako kwa ajili ya watu wenyewe

Mabadiliko yataanzia Zanzibar yataletwa na CUF na CUF bara inaweza kuleta mabadiliko zaidi kwa status quo

Chadema ondoa hiyo mizigo unayoitwa mbowe na slaa wekeni watu wengine mnaweza kuleta cha maana has kifikra.

Btwn. Baregu vipi hagombee tena? he has my vote.
 
Pamoja na Uchache wao Bungeni lakini Jitihada walizoonesha naamini wakiwa kama 40% Bungeni basi mambo yalitokea last week yasingetokea
 
CHADEMA imefanya mengi tu kustahili kupewa dola.Hivi kwani CCM walipopewa nchi toka kwa mkoloni walikuwa wamefanya nini?unakumbuka maneno ya Mwl wakati anadai uhuru?alisema kwamba mkoloni ameshindwa kuuondoa maadui watatu(Ujinga,Umasikini na Maradhi) hivyo walitaka wapewe nchi ili waondoe hawa maadui.Je hawa maadui hatunao tena?mabya zaidi wameongeza na adui mwingine Ufisadi..Watch steps za CHADEMA utagundua kuwa wanastahili kupewa nchi.
 
Pamoja na Uchache wao Bungeni lakini Jitihada walizoonesha naamini wakiwa kama 40% Bungeni basi mambo yalitokea last week yasingetokea

This is complacent! is not supposed to be a standard, ni kama una mtoto yuko dara la watu 40, masomo yote kapata zero, isipokuwa math kapata 80% unasema , no problem you are doing good!

Tunajadili ili wafikie asilimia 100% , maana wapinzani kuwa wengi bungeni ni uamuzi wao kama wanataka au hawataki, na kinachoonekana hawataki kuwa wengi bungeni!!

Kumbuka silaha ya CCM ni kuwa , (nyie semeni), hii mbaya sana kama tunakuwa wasemaji sana hili hali hakuna linalofanyika!

Ok, ku nalist of shame ilitangazwa miaka 5 iliyopita, and what happened

waliokata tamaa kabisa wanasema sio kazi ya chadema kuwapeleka mahakamani! au kufanya lolote lile baada ya kutangaza!

wasiotaka malumbano wanasema Yes walijitahidi kwa kufanya hivyo

sisi wengine tunasema wameshindwa kabisa wala hawakujua wanafanya nini!

wanaopenda comparison wanasema Chadema=Msemakweli(aliyetoa list yake ya vihiyo)

wasiotaka siasa kabisa wanasema walitakiwa kuandamana, hao watu warudishe mali zetu, na kuandamana huku kungeendana na wapinzani hawa kwenda segerea n.k(ambako hakuna anayejua gharama za upinzani ni kubwa)

Tusipokaa chini na ku-evaluate kama ambavyo MKJJ anavyosema gharama za mageuzi , basi tukubali kuwa CCM waendelee lutawala na ikifikia hapa nitaitisha maandamo yangu kuwa

kuwa...

kuwa...

vyama hivi visipate ruzuku yoyote!! kumbukeni ni kodi yetu ile!

Yaani kila failure ina sababu na kila sababu ina kakisifa fulani kamefichwa ndani ili ku-reinforce failure!!we dont want to reach the perfection of 90% , we want to stay in 5% with a lots of excuses!
 
Back
Top Bottom