CHADEMA imefanya nini kustahili dhamana ya Uongozi wa Taifa?

CCM na Chadema hawa wote ni dugu moja.. Udhaifu umeshajitokeza ndani ya Chadema hawana jipya mambo yatakuwa yale yale.. Mimi nadhani iwepo CCM #1 na CCM#2 kieleweke.. wale wote wanaoipenda nchi yao basi wawe CCM#2(wanachama safi wasio na tamaa ambao wananchi wanawafahamu kwa dhati hata wakisimama tutasema naaam!! kweli mpo kwa ajili yetu lakini wawe wametoka CCM#1(chama tawala). Vyama vya upinzani hawana jipya ni malumbano na migogoro isiyoisha. Baada ya hapo tutawaomba CCM #1 wajiunge na Chadema kiwe chama kimoja sasa wao wawe wapinzani. Kwa mtazamo wangu
 
Mag3..

- Kuanzisha shule ya sekondari ya kuchukua wanafunzi na yenye kutoa elimu bora. Wazazi bila kujali itikadi zao wangepeleka watoto wao kwenye shule hiyo kama ingeonekana kufanya vizuri zaidi kuliko zile za "wazazi" za CCM!

- Kuanzisha Kliniki au Hospitali kwenye maeneo kadhaa ya nchi aidha kwa mchango wao wenyewe au kwa kuandika project ya mradi na kuhakikisha kuwa taasisi hiyo inatoa huduma inayoshinda na kliniki au hospitali za serikali au binafsi. Watu wangeona Chadema in action. Hilo halihitaji kuwa madarakani.

- Kuanzisha mipango ya usafishaji mji, mitaro n.k JIjini Dar au programu ambayo itatofautisha CCM na CHadema kwenye suala la usafi wa mji. Sidhani kama hili linahitaji kuwa madarakani kuweza kulifanya.

- Kutoa elimu ya uraia au kuanzisha programu ya elimu ya demokrasia kwenye matawi yao na kuwaalika wananchi kuja kusikiliza au kujifunza bure. Hata kutoa Warsha au Semina kwa wananchi au wanaotaka juu ya Uongozi, Demokrasia n.k na watu wakajiandikisha kuja kushiriki kwa ada kiasi na hilo likawa chanzo cha mapato. Hapa wangeweza kuwa na Idara ya Elimu ya Demokrasia ambao wangekuwa wanapita kutoa semina kikanda, kimkoa au kiwilaya! - halihitaji kuwa madarakani..

Ninayo mengi kweli.. ambayo naamini mahali penye uongozi mzuri wangeweza kabisa kuyafanya. So far, wanasubiri kuingia madarakani ili waweze kufanya! I don't think so, ndugu yangu.

Duh! Mkjj, hapa umeua, umemaliza kabisa

1. Haya yote uliyoonyesha hapo juu si tu yataipa chadema indicator ya viongozi wazuri, bali watakuwa karibu na wananchi na hivyo kupelekea kupata kura

Hivi sasa chadema; Haina viongozi 'critical thinkers ambao wako tayari kucheza na kununua every opportunity ya makosa ya CCM' mfano juzi Sofia simba ametokota, nilitegemea angalau chadema watoe mabango na picha kubwa ya SS akisema hakuna msafi CCM! lakini wapi!

Tumeshawahi kuchangia hapa kuwa Cahdema kikwe chama cha wananchi, kwa mfano ishu ya ruzuku inawalevya sana , lakini katika ruzuku hiyo mkatoa laki 5 na kununua madaftari ya sh. 50 na kugawa kwa wanafunzi kwenye baaadhi ya shule, hilo goal tosha sana kisiasa

Hayo yote aliyosema MKJJ hapo juu ni moja ya nji rahisi ya kuwafikia wananchi kuliko helkopta! wakifanya hivyo miaka kama 3-5, baadae utashangaa root ya chadema iko imara sana. Hii ndiyo Obama anasema tulipita kwenye nyumba tukaomba dola 5, 10 kupata fedha ya kampeni! Angalieni na igeni Vodacom foundations-hawachezi wale! Tigo na zain wanakuja na kila style, lakini wapi Voda wako juu, ona Tigo nao wanavyotoa misaada. Hii ishu MKJJ awafundishe??

Kutofanya hayo kunaleta impression ya kuwa hivi vyama vimekaa ki-NGO zaidi, hata kama hamko ki-NGO. Chama ambacho viongozi wana hakika ya kula kwa mwezi na wala hawafanyi jambo lolote kwa jamii, ni ishara tosha kuwa hawana lengo la kuiondoa CCM. Au wanataka waiondoe CCM kwa huruma ya wananchi kitu ambacho si kizuri

Kenya mfano mazuri wapinzani wameingia serikalini , hwataki kutoka! LOL!

Issue za uchaguzi ndani ya chadema hivi karibuni,maneno yasiyoeleweka ya akina Mtei, udikteta wa Mbowe na kuburuzwa kwa slaa , vinatupa wasiwasi hata kama tunaipenda chadema.

MKJJ nimefurahi umeongelea swala la 'KUPITISHWA KWENYE TANURU' kila mwenye mawazo ya kuwapitisha wapinzani kwenye tanuru ana lengo zuri na nchi yetu. CCM wameshajifia, wameishathibitika wameshindwa, ila anayekuja lazima tuamini ataweza! kuna watu humu wanakipenda Chadema hata maswali ya msingi kama haya hawajiulizi mpaka unafikia point na kusema, hivi hawa jamaa ni mbumbumbu, wajinga, wapumbavu, wana lao jambo? hizi challenge watu wanazo-zipose ndiyo njia nzuri ya Chadema kubadilika.

Hayo aliyoshauri MKJJ yatakifanya chadema kupendwa, just imagine mtoto wa mkulima anaandikia kwenye daftari alilopewa na chadema! just imagine mama mjamzito kwenye zahanati fulani alilalia kitanda cha chadema, akamweleza mtoto wake jinsi alivyozaliwa.Jamani chadema ingekuwa midomoni na mioyoni mwa watu.

Chama hiki kikiwa cha wananchi wote, kiasi ambacho kila mtu anakuwa na matumaini ya kuwa na kupata uongozi kwa demokrasia kwa namna anavyotaka alitumikie taifa, basi mmewapata watu. Hii ishu ya juzi ya kuibaka demokrasia waziwazi nachelea kusema imewarudisha wengi nyuma

Ubishi andikeni humu, teteni, semeni vibaya, ila ukweli ndiyo huu, lazima mmpite kwenye tanuru, na tanuru hili si JF ninyi ni mashahidi wa jinsi mnavyopigiwa kura. kuwabadili watu ni kazi , Chadema haiitajiki kuwa na doa

Kulaumu CCM wanawaua wapinzani ni utoto, hata nyie mngefanya hivyo hivyo, you need extra brain to overcome those issues.

Zitto ukipitia hapa hizi ni challenge, mkianza sasa 2015 nchi yenu hii, mwakani hadithi ni ile ile , I am pretty sure about that

Asante MKJJ
 
Good point Mkandara,

Kama Chadema inaweza kujiendesha kama chama, na malengo ya chama cha siasa ni kushika nchi kwa mujibu wa katiba, Basi Chadema chaweza kuongoza nchi.

kama; You meant if? what if is not if, will you change your mind?

kama; You meant as?

Inabidi tujue definition ya chama na uendeshwaji wake.
 
Waboreya,
Mkuu wangu pengine huelewi tofauti ya chama cha Siasa na NGO.. Ikiwa Chadema watayafanya hayo basi hawatakuwa na tofauti kabisa na NGO..Kisha basi Chadema hata majimbo wanayoongoza ni vigumu sana kufikiria kwamba Chadema wanaweza jenga Zahanati kirahisi pasipo greenlight toka CCM. Ni rahisi kwa NGo kufanya hivyo kuliko Chadema au CUF..

Mkuu wangu kitu kimoja ni lazima tukikubali. Kutokana na mfumo wa uchaguzi, Utawala na mengineyo mengi tu, CUF,Chadema, TLP na sijui TTTP wote hawa hakuna hata mmoja wao anaweza kuongoza nchi chini ya mfumo uliopo.. Kazi iliyopo sasa hivi ni kuwasha joto la kifira tu hadi siku au miaka ambayo watakuja generation inayotambua umuhimu wa mabadiliko kwa vitendo. Sisi tuendelee kulonga tu maanake ndi kilichobakia.. hatuna ari ya kufanya mabadiliko.
Lakini tukizungumzia uwezo inachekesha kwani - No doubt Kikwete atapita mwaka 2010 pasipo uwezo vile vile... sasa sielewi mnazungumzia uwezo wa kitu gani haswa.
 
Mkuu wasipofanya hayo wasahau kushika nchi, nimesema kwa faida yao na huu ni ushauri tu, kama kuna njia nyingine ya wao ku wa-win watu basi ni vizuri.Mkuu hata msiba ukitokea chadema washindwe hata kutoa rambirambi ya sh.50 eti kwa sababu siyo NGO?

Mkandara, mwaka 1995-CCM walipata 61% kura ya urais
2000-CCM walipata kura 71%
2005-CCM walipata 80%
2010-CCM-???
Kumbuka maendeleo ya internet , redio, tv Tulijua lazima miaka kadiri inavyoongezeka basi CCM watakosa kura.

Otherwise tufanyeje, Chadema lina gazeti lake, redio n.k?? si kuna

Hilo joto unalolisema inategema sana na hali ya watu, nchi hii watu wamechoka maneno.

By the way, hayo hapo juu aliyoyasema MKJJ siyo kwa sababu ni chama tu, hata watu kwenye mitaa tunatakiwa kufanya, siyo kutegemea serikali! ni ustaarabu mpya.

Unafikiri wafanye nini ili waingie mioyoni mwa watu, operation sangara?

Mfano; nikiongelea kwenye church point of view, watu wanaookoka kwenye mikutano mikubwa kama ya jangwani ni wachache sana kulinganisha na wale wanaookoka, kutokana na kuwa inspired na kitu fulani kama ukarimu, kuangalia wagonjwa, n.k these make people to get connected to you, uchaguzi mwakani mtu hana haja ya kusikiliza sera za chadema! anawajua chadema in and out, ataenda kuipa kura yake chadema, siyo kwa sababu amewasikia jangwani au ameona helkopta la! kwa sababu anawajua!

Mwisho na ambalo ni masikitiko sana kwangu; umesema hakuna atakayeongoza kutokana na mfumo uliopo upi? tatizo letu ni kuwa tuna katiba mbovu na tume ya uchaguzi isiyo huru 'kenya-kenya' .Katiba yetu inatakiwa ibadilishwe ili kusuit vyama vyote, kwa mfano tukiwa na serikali ya umoja wa kitaifa ni best, kila mmoja anashika serikali kulingana na asilimia ya kura

Cha ajabu mkandara swala la katiba ni history, vyama vya siasa vinaenda kwenye uchaguzi wakijua fika kuna tatizo la katiba na tume ya uchaguzi, wakishindwa utasikia kelele nyingi.

Kwa nini sasa wasipiganie hayo, badala hata ya kuwaza uchaguzi NCHI SIYO YA CCM HII, TUNATAKIWA KUJENGA MISINGI MIPYA KWA VIZAZI VYOTE kama kweli vyama vya upinzani lengo lao ni kujenga taifa jipya , basi ilitakiwa waanze na katiba na tume ya uchaguzi, LAKINI WAPI MWAKANI WANAINGIA KWENYE UCHAGUZI WAKIJUA WATASHINDWA! NA KUONEWA HURUMA KWENYE VITI VYA UBUNGE! YES kwani tume yao? kwani watafanya nini, kuna wa kuingia msituni nchi hii? Tarime JK ndiyo alisema wapeni ubunge hao!!!

KWA NINI NISIAMINI KUWA VYAMA VYA UPINZANI VIKO KWA AJILI YA MALENGO YAO BINAFSI NA SI KWA TAIFA HILI?

Mkandara hupo?

Kesho nao wakipata kura(assume) basi tume ya uchaguzi itakuwa yao na mabadiliko ya katiba hawatayafanya kwani yatakuwa yakiwafavour wao!!!! na yeyote mwingine atakayetaka kuja basi atapata kikwazo hiki hiki

Their first priority ana only one ni kubadili katiba na tume ya uchaguzi, wangeng'ang'ania hayo hata kukataa kuingia kwenye uchaguzi tungejua hawa wana nia bora , lakini kwa sasa mmmh!!! I doubt
 
Mkuu Mwanakijiji asalaam aleikum

Kabla ya Kuuliza CHADEMA imefanya nini, nadhani tungeuliza kwanza CHADEMA kama chama cha Upinzani kilipaswa kufanya nini, namaanisha tujue kama CHADEMA kikiwa kama chama cha Upinzani kimetimiza majukumu yake!

Vinginevyo Swali lako litakuwa ni contradictory kidogo kwa maana halijatofautisha majukumu ya CHADEMA kama opposition party na majukumu ya CHADEMA kama kingekuwa ni ruling party.

CHADEMA kama opposition party nadhani kimejaribu sana kuisimamia Serikali na katika miaka mitano iliyopita tumeona namna wabunge wachache wa CHADEMA walivyoweza kuilzimisah Serikali kuamka kutoka katika usingzi mzito
nakuunga mkono.
Atuambie majukumu ya chadema kama chama cha upinzani.watuambie na nguvu zao kiuchumi rasilimali watu ili tujue wameshindwa nini.
 
majaribio hayo ni mabaya sana;

katika hali hii kweli tunataka kuwapa dhamana ya maisha ya watu takribani milioni 40? Not in my watch.

Hapa mwanakijiji unajivika utukufu ambao huna. Kwamba majaribio ni mabaya sana according to whom? watu wasingekuwa wanajaribu bila shaka huko uliko usingeweza kufika maana haiwezekani kutembea kwa miguu. Halafu kudai not on your watch; who do you think you are?

hapana.. CCM isibaki madarakani kwa sababu inastahili! Lakini tusiwapandishe watu wengine madarakani pasipokustahili.. maanake ni kuwa kwa yeyote anayetaka kuja juu yetu we have to set the bar very high not very low.. Hivyo, siyo kuiondoa CCM for the sake of kuindoa CCM.. we have learned in Kenya.. we have to remove the ruling party kwa sababu we got something better!.. Na njia pekee ya kupata "better" ni kuhakikisha tunawapitisha kwenye tanuru ya moto kwanza...
Contradiction after contradiction. Unawezaje kusema CCM wameshindwa halafu unawalinganisha na ambao hujawapa nafasi? Kwa nini lazima ulinganishe na Kenya na siyo Ghana. Jibu ni malice!

Mzee mwanakijiji,
Mkuu wangu kama ungekuwa mwanamke basi hadi leo usingekuwa na Mume na kama ungekuwa naye bila shaka angekuwa abusive kwako..
Nasema hivi kwa sababu, ni Wadanganyika wengi wenye mawazo kama yako na ndio maana tunaburuzwa na CCM kwa sababu hatuoni mwanaume zaidi ya CCM. Maisha yetu yanaishia na CCM..Cases za namna hiyo tunaziona kila siku na hujiuliza hivi kuna watu wengine wanapenda kiasi hicho jamani.. unakubali hakufai lakini hutaki kumwacha!
Mkandara kwa vijimifano huwezekani. Your posts are a joy to read.

Mkuu wasipofanya hayo wasahau kushika nchi, nimesema kwa faida yao na huu ni ushauri tu, kama kuna njia nyingine ya wao ku wa-win watu basi ni vizuri.Mkuu hata msiba ukitokea chadema washindwe hata kutoa rambirambi ya sh.50 eti kwa sababu siyo NGO??
ukisikia mifano mifu ndio kama huu wa kwako

Mkandara, mwaka 1995-CCM walipata 61% kura ya urais
2000-CCM walipata kura 71%
2005-CCM walipata 80%
2010-CCM-???
Kumbuka maendeleo ya internet , redio, tv Tulijua lazima miaka kadiri inavyoongezeka basi CCM watakosa kura.
wanaweza kupata hata asilimia 1,ooo,oooo lakini je zimepatikana vipi? Ni watu kama wewe wanaohesabu namba bila hata kujua hizo namaba zimepatikana vipi ndio wanaosumbuliwa na hizo namba.

Otherwise tufanyeje, Chadema lina gazeti lake, redio n.k?? si kuna

Hilo joto unalolisema inategema sana na hali ya watu, nchi hii watu wamechoka maneno.

By the way, hayo hapo juu aliyoyasema MKJJ siyo kwa sababu ni chama tu, hata watu kwenye mitaa tunatakiwa kufanya, siyo kutegemea serikali! ni ustaarabu mpya.
Ustaarabu wa wapi? Ukiniambia matumizi ya kodi zetu ni yapi ndio naweza kukubaliana na haya mawazo ya kifisadi.

Unafikiri wafanye nini ili waingie mioyoni mwa watu, operation sangara??
Wewe unaonaje

Mfano; nikiongelea kwenye church point of view, watu wanaookoka kwenye mikutano mikubwa kama ya jangwani ni wachache sana kulinganisha na wale wanaookoka, kutokana na kuwa inspired na kitu fulani kama ukarimu, kuangalia wagonjwa, n.k these make people to get connected to you, uchaguzi mwakani mtu hana haja ya kusikiliza sera za chadema! anawajua chadema in and out, ataenda kuipa kura yake chadema, siyo kwa sababu amewasikia jangwani au ameona helkopta la! kwa sababu anawajua!
Sasa mtu ataokokaje kama hajamsikia mtu wa kumhubiria kuhusu wokovu?

Mwisho na ambalo ni masikitiko sana kwangu; umesema hakuna atakayeongoza kutokana na mfumo uliopo upi? tatizo letu ni kuwa tuna katiba mbovu na tume ya uchaguzi isiyo huru 'kenya-kenya' .Katiba yetu inatakiwa ibadilishwe ili kusuit vyama vyote, kwa mfano tukiwa na serikali ya umoja wa kitaifa ni best, kila mmoja anashika serikali kulingana na asilimia ya kura.
Kesho nao wakipata kura(assume) basi tume ya uchaguzi itakuwa yao na mabadiliko ya katiba hawatayafanya kwani yatakuwa yakiwafavour wao!!!! na yeyote mwingine atakayetaka kuja basi atapata kikwazo hiki hiki

Their first priority ana only one ni kubadili katiba na tume ya uchaguzi, wangeng'ang'ania hayo hata kukataa kuingia kwenye uchaguzi tungejua hawa wana nia bora , lakini kwa sasa mmmh!!! I doubt

Cha ajabu mkandara swala la katiba ni history, vyama vya siasa vinaenda kwenye uchaguzi wakijua fika kuna tatizo la katiba na tume ya uchaguzi, wakishindwa utasikia kelele nyingi.
Unajua tatizo ni katiba halafu ung'ang'ana kuwalaumu upinzani amakweli wewe mtu wa ajabu kwelikweli. Kwani hawajwahi kuilalamikia hiyo katiba? acha uzandiki wako

Kwa nini sasa wasipiganie hayo, badala hata ya kuwaza uchaguzi NCHI SIYO YA CCM HII, TUNATAKIWA KUJENGA MISINGI MIPYA KWA VIZAZI VYOTE kama kweli vyama vya upinzani lengo lao ni kujenga taifa jipya , basi ilitakiwa waanze na katiba na tume ya uchaguzi, LAKINI WAPI MWAKANI WANAINGIA KWENYE UCHAGUZI WAKIJUA WATASHINDWA! NA KUONEWA HURUMA KWENYE VITI VYA UBUNGE! YES kwani tume yao? kwani watafanya nini, kuna wa kuingia msituni nchi hii? Tarime JK ndiyo alisema wapeni ubunge hao!!!

KWA NINI NISIAMINI KUWA VYAMA VYA UPINZANI VIKO KWA AJILI YA MALENGO YAO BINAFSI NA SI KWA TAIFA HILI?
Imani ni kitu kingine na suala la binafsi kama uanaamini hivyo hiyo ni juu yako

Mkandara hupo?
 
You have missed the point!

Author amesema CCM hamna kitu ''zimwi likujualo' ila tunawajua kuwa hamna kitu, tumewaprove na kuhakikisha kuwa hawana kitu.

ana compare kati ya hawa wasio na kitu tunaowajua na hawa tusiowajua, haja confirm ameuliza, mpe majibu!
.

Then you must be nuts. Kama mna akili timamu mnafahamu kuwa hawana kitu ni ujhu uliopindukia kuanza kuhoji watu ambao hamjawapa nafasi . Neno moja tu linawafaa; "******"
 
Unajua tatizo ni katiba halafu ung'ang'ana kuwalaumu upinzani amakweli wewe mtu wa ajabu kwelikweli. Kwani hawajwahi kuilalamikia hiyo katiba? acha uzandiki wako

wamefikia wapi katika kudai mabadiliko ya katiba?

.

Then you must be nuts. Kama mna akili timamu mnafahamu kuwa hawana kitu ni ujhu uliopindukia kuanza kuhoji watu ambao hamjawapa nafasi . Neno moja tu linawafaa; "******"

Nuts-You meant nuts as eulogy? because language is changing, or you meant as kooky? If that nuts meant to praise me, I will not take it , but if you meant as 'mental irregular' that suits me best. I need your help to answer my questions in sensible way! genius!

I thought you will take this as challenge! watu wameshaamua kwa kupiga kura na mwakani wataamua tena.

Ndugu yangu I personally love Chadema, na hii ni mijadala ya ukweli uliopo na nini tufanye, ndiyo maana ya forums, ukifikiri kuna mtu ana hujuma na Chadema humu unakosea sana.

I believe what was proposed before by MKJJ is just a challenge na ni njia nzuri ya Chadema kuwa karibu na watu, .Ishu za kutoka povu la hasira hapa, wakati kila siku Chadema inashindwa chaguzi nadhani haujitendei haki mwenyewe!

This a forums lets discuss issue , jamani matusi haya hayajengi, wala hayatibu tatizo.

Tatizo ni CCM waondoke madarakani, we are discussing how to remove them, IS THIS WRONG?

Kaka kwa hiyo upo tayari yeyote yule aingie madarakani? nilifikiri utatoa sababu ya kwa nini tuipe Chadema nchi! na mpaka INAJADILIWA CHADEMA BADO HAUJASHTUKA KUWA NI CHAMA KIKUBWA NA KINAWEZA KUSHIKA NCHI, KUULIZWA KWA NINI TUIPE NCHI , MAJIBU YAKE MATUSI! LOL! HIVI KINA MBOWE WANAVYOENDA KUOMBA KURA KWA WANANCHI WANATUKANA?

Napata issue nyingine hapa

Chadema bado hakijawa chama cha wananchi, maana wanachama wake hawaenezi habari njema na sera za Chadema, makazini, kwenye daladala hata makanisani na kwenye forums, wanachama wa chadema hawa , hawajajifunza kuwa wapole na wenye kuvutia watu kuingia Chadema, hawa inawezekana kuna walioingia Chadema pasi kujua ni nini, sera zao n,k.Wameingia kwa mkumbo, maana ukiamini Chadema, sera zake, basi mwanachama yuko tayari kukitetea hata kubidi kufa!

Kutowatumia wanachama mmoja mmoja kuitangaza na kueneza sera za chadema is another indicator kuwa itawachukua miaka mingi kushika nchi.
 
Hata CCM wana mivutano ya kipuuzi kaka. Chama kingine hakijaonekana kinafanyaje mambo yake kwa sababu hakijapewa nafasi kufanya ili kuonyesha kina uwezo kiasi gani. Ni sawa na wale wanaotaka mfanyakazi lakini wanataka awe na uzoefu wa kazi hiyo. Kila mtu anataka apewe nafasi ndio uone anafanyaje. Kama kila mwenye uzoefu ndio anafaa kwa kupewa dhamana, unafundishwa wapi uzoefu kama sio kazini?

Wapeni chadema tu, si umeona walikochukuwa halmashauri za vijiji na mitaa na wilaya? Kama sio kuingiliwa na CCM wangefanya vizuri zaidi.

Leka
 
Mzee mwanakijiji,
Mkuu wangu kama ungekuwa mwanamke basi hadi leo usingekuwa na Mume na kama ungekuwa naye bila shaka angekuwa abusive kwako..

mifano yako kama siyo ya mambo ya chumbani basi inakuwa ile mingine..

Nasema hivi kwa sababu, ni Wadanganyika wengi wenye mawazo kama yako na ndio maana tunaburuzwa na CCM kwa sababu hatuoni mwanaume zaidi ya CCM. Maisha yetu yanaishia na CCM..Cases za namna hiyo tunaziona kila siku na hujiuliza hivi kuna watu wengine wanapenda kiasi hicho jamani.. unakubali hakufai lakini hutaki kumwacha!

no comment
 
CHADEMA wajipange upya hasa uongozi wa juu. Pia wapunguze "umiliki" wa chama unaoonekana wazi ni wa watu fulani. CHADEMA imilikiwe au ionekane inamilikiwa na WANACHAMA wote.
 
Cha ajabu mkandara swala la katiba ni history, vyama vya siasa vinaenda kwenye uchaguzi wakijua fika kuna tatizo la katiba na tume ya uchaguzi, wakishindwa utasikia kelele nyingi.

Kwa nini sasa wasipiganie hayo
.....

Kwanini na wewe usipiganie hayo? Unakwenda kuchagua viongozi wako wakati unajua fika kuna tatizo la katiba na tume ya uchaguzi. Utapataje viongozi waliyo bora? Hata kama wewe huna mpango wa kuchagua kiongozi kutoka kambi ya upinzani bado viongozi waliopo kwenye ballot box wa CCM wamefika hapo kwa njia ambayo sio ya haki. Kuwa na katiba na tume ya uchaguzi ambayo haiwezeshi chaguzi kuwa huru na haki sio tatizo la wapinzani pekee, ni tatizo kwa mwanaCCM pia, actually ni tatizo kwa Watanzania wote. Kama unamapenzi na nchi yako unatakiwa udai katiba iliyo huru na tume ya uchaguzi itakayotoa haki na kutupatia chaguzi zilizo huru. Wapinzani hawadai katiba na tume huru kwa faida yao. Wadai hayo mambo kwa faida ya Watanzania wote. Lazima ifike mahali tulielewe hili amasivyo wote, mimi na wewe, tutakuwa tunaburuzwa na wajanja wachache kwenye kila chaguzi.

napigania kupitia chama, na chadema ndio nataka wafanye hivyo, by the way wamefikia wapi kuhus mabadiliko ya katiba? mkuu tuko pamoja n mijadala hii tu
 
Duh! Mkjj, hapa umeua, umemaliza kabisa

1. Haya yote uliyoonyesha hapo juu si tu yataipa chadema indicator ya viongozi wazuri, bali watakuwa karibu na wananchi na hivyo kupelekea kupata kura

Hivi sasa chadema; Haina viongozi 'critical thinkers ambao wako tayari kucheza na kununua every opportunity ya makosa ya CCM' mfano juzi Sofia simba ametokota, nilitegemea angalau chadema watoe mabango na picha kubwa ya SS akisema hakuna msafi CCM! lakini wapi!

Tumeshawahi kuchangia hapa kuwa Cahdema kikwe chama cha wananchi, kwa mfano ishu ya ruzuku inawalevya sana , lakini katika ruzuku hiyo mkatoa laki 5 na kununua madaftari ya sh. 50 na kugawa kwa wanafunzi kwenye baaadhi ya shule, hilo goal tosha sana kisiasa

Hayo yote aliyosema MKJJ hapo juu ni moja ya nji rahisi ya kuwafikia wananchi kuliko helkopta! wakifanya hivyo miaka kama 3-5, baadae utashangaa root ya chadema iko imara sana. Hii ndiyo Obama anasema tulipita kwenye nyumba tukaomba dola 5, 10 kupata fedha ya kampeni! Angalieni na igeni Vodacom foundations-hawachezi wale! Tigo na zain wanakuja na kila style, lakini wapi Voda wako juu, ona Tigo nao wanavyotoa misaada. Hii ishu MKJJ awafundishe??

Kutofanya hayo kunaleta impression ya kuwa hivi vyama vimekaa ki-NGO zaidi, hata kama hamko ki-NGO. Chama ambacho viongozi wana hakika ya kula kwa mwezi na wala hawafanyi jambo lolote kwa jamii, ni ishara tosha kuwa hawana lengo la kuiondoa CCM. Au wanataka waiondoe CCM kwa huruma ya wananchi kitu ambacho si kizuri

Kenya mfano mazuri wapinzani wameingia serikalini , hwataki kutoka! LOL!

Issue za uchaguzi ndani ya chadema hivi karibuni,maneno yasiyoeleweka ya akina Mtei, udikteta wa Mbowe na kuburuzwa kwa slaa , vinatupa wasiwasi hata kama tunaipenda chadema.

MKJJ nimefurahi umeongelea swala la 'KUPITISHWA KWENYE TANURU' kila mwenye mawazo ya kuwapitisha wapinzani kwenye tanuru ana lengo zuri na nchi yetu. CCM wameshajifia, wameishathibitika wameshindwa, ila anayekuja lazima tuamini ataweza! kuna watu humu wanakipenda Chadema hata maswali ya msingi kama haya hawajiulizi mpaka unafikia point na kusema, hivi hawa jamaa ni mbumbumbu, wajinga, wapumbavu, wana lao jambo? hizi challenge watu wanazo-zipose ndiyo njia nzuri ya Chadema kubadilika.

Hayo aliyoshauri MKJJ yatakifanya chadema kupendwa, just imagine mtoto wa mkulima anaandikia kwenye daftari alilopewa na chadema! just imagine mama mjamzito kwenye zahanati fulani alilalia kitanda cha chadema, akamweleza mtoto wake jinsi alivyozaliwa.Jamani chadema ingekuwa midomoni na mioyoni mwa watu.

Chama hiki kikiwa cha wananchi wote, kiasi ambacho kila mtu anakuwa na matumaini ya kuwa na kupata uongozi kwa demokrasia kwa namna anavyotaka alitumikie taifa, basi mmewapata watu. Hii ishu ya juzi ya kuibaka demokrasia waziwazi nachelea kusema imewarudisha wengi nyuma

Ubishi andikeni humu, teteni, semeni vibaya, ila ukweli ndiyo huu, lazima mmpite kwenye tanuru, na tanuru hili si JF ninyi ni mashahidi wa jinsi mnavyopigiwa kura. kuwabadili watu ni kazi , Chadema haiitajiki kuwa na doa

Kulaumu CCM wanawaua wapinzani ni utoto, hata nyie mngefanya hivyo hivyo, you need extra brain to overcome those issues.

Zitto ukipitia hapa hizi ni challenge, mkianza sasa 2015 nchi yenu hii, mwakani hadithi ni ile ile , I am pretty sure about that

Asante MKJJ

Kwa taarifa yako Vodacom wanatengeneza Bilioni Moja kwa siku. Narudia bilioni moja kwa siku. CHADEMA wanapata ruzuku ya milioni 60 kwa mwezi. Na hao wakurugenzi wa CHADEMA mnawawaona wanananeemeka na hiyo ruzuku wanapata laki mbili kwa mwezi. Kulinganisha Vodacom na CHADEMA is not fair.

Hili la helikopta naona mmelikamia sana. Helikopta ni njia rahisi, cheaper na quicker KUFIKIA wapiga kura kuliko gari au pikipiki au kwa miguu au kwa ndege.

.
 
napigania kupitia chama, na chadema ndio nataka wafanye hivyo, by the way wamefikia wapi kuhus mabadiliko ya katiba? mkuu tuko pamoja n mijadala hii tu

Katiba mpya itapatikana bungeni najua unalifahamu hilo. Wabunge wa CCM ni wachache sana, kama wapo, ambao wanaunga mkono katiba mpya. Hivyo lazima zifanyike juhudi nje ya bunge kwa kipindi hichi kuelekea uchaguzi mkuu. Juhudi za Hakielimu, TAMWA, vyama vya wafanyakazi na hata miongozo ya kuchagua viongozi bora inayotolewa na madhehebu ya dini zinatakiwa ziungwe mkono. Tukiwa na institution kama ishirini zenye ujasiri kama Hakielimu na TAMWA, wakiunganisha nguvu na vyama vya upinzani vyenye nia dhabiti ya kumkomboa Mtanzania tunaweza kuwalazimisha CCM kuchukua action.

.
 
Mwanakijiji kweli!! Maana maswali ni muhimu na yanahitaji majibu. Lakini mwanakijiji umejiuliza kweli kama chadema imeshakabidhiwa hazina ya kodi za wananchi kuzisimamia? Ndio busi tujiulize wamefanya nazo nini. Angalia halimashauri inayoshikiliwa na chadema (karatu) hukumu mwenyewe kwa jinsi mapato ya hii halmashauri inavyofanya yaliyokusudiwa. Ccm ndio tulipaswa kuwauliza kodi amvazo wanakusanya zaidi ya bil 360 kwa mwezi zinafanya nini wakati panado hospitalini zinauzwa, maji hakuna, umeme ndio hivyo tena shule mwanafunzi anatakiwa aende na dawati lake bila kujali kuwa ashalipa ada, achilia mbali maswala ya miundo mbinu inayohusu idara zote. Ona wabunge wachache tu wa chadema bungeni wamebadili atmosphere ya bunge letu na kuwezesha kuondoa ile hali ya ndio mzee kwa kila jambo. Sasa wakiongwzeka itakuwa je? Sembuse kuchukua dola. Watu wenye akili wapo tatizo ni system(chama) ukiondoa greeds za ccm kungaliko tumaini kwa watz
 
CHADEMA WAMEFANYA NINI, Jibu: Wameleta challenge bungeni, wameibua ufisadi (remember list of shame), wamewaamsha CCM kutokubweteka na kufanya mambo kama they own the country etc Kama opposition party changa wamefanya vya kutosha.
 
Zitto angekuwa mbinafsi asingemwachia dikteta wenu Mbowe nafasi ya uenyekiti.

Hakumwachia, alishinikizwa afanye hivyo kwa manufaa ya umoja ndani ya Chama. Zitto ana tamaa zisizo na msingi! Kumbe kazaliwa mwaka 1977 haraka ya nini?
 
Kwenye hivi vyama vidogo hii migogoro ndo inayotoa nafasi kwa wao kujikuza kama wataweza kumanage matatizo yao na kuendelea kukubalia kutokubaliana kwa manufaa ya chama. Bado si amini kama Chadema wanao uwezo wa kukaa nafasi ya juu kabisa ya nchi mpaka waonyeshe kwamba wanao uwezo wa kuvuka salama kwenye bahari iliyochafuka bila kusambaratika kama ilivyokuwa NCCR. Hapo then ntaanza kuona kweli wako serious na wanajua wanachokifanya.
KUna ukweli mkubwa hapo. Kumpa mtu zawadi ya kwanza ati kwa vile umemkuta anahema baada ya kukimbia ni kutokuwa makini; mtu huyo ni lazima ashindanishwe na aweze kustahili zawadi hizo. Hatupaswi kutoa zawadi kwa vile mtu anatoka jasho!

Nimeangalia kwa kina sana suala hili; tutakuwa tusiowajibika endapo tutaamua kuweka dhamana ya watu milioni 40 mikononi mwa Chadema ilivyo sasa!

Wanayo miaka mingine sita ijayo kusahihisha pale walipokosea, kujiimarisha, kujenga zaidi chama chao na imani ya wananchi kwa chama hicho. CHADEMA kilishajidhihirisha kwamba ni Chama 'KINACHOWEZA' ni kiasi tu cha tafuta mbinu za kuzidi kuwa karibu na wananchi na kupata wafuasi wa kutosha. Hilo linawezekana sana katika mazingira ya sasa hadi mwaka 2015 wakati viongozi wa CCM bado wanaumana wao kwa wao na hakuna anayetaka kukubali kwamba kwa 'mchezo' wao wanaipeleka nchi kubaya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom