CHADEMA imefanya nini kustahili dhamana ya Uongozi wa Taifa?

Wakuu zangu,
Haya maswala ya kujiuliza kama Chadema inaweza kuongoza ni maswali yasiyokuwa na msingi kabisa.
Kina mama na wana JF wote mtanisamehe sana kwa mfano mdogo naotaka kuuweka hapa:-

Uongozi wa nchi ni sawa na uongozi wa nyumba (kwa udogo wake). Huwezi kumpima bwana mmoja na mwanamme mwingine kama anaweza wakati wote ni wanaume. Ati sababu unazotumia ni kwamba mume mmoja hajawahi kuoa..
Kama kuna sababu zinazowasukuma kuamini kwamba Chadema haiwezi kuongoza nchi bora mziorodheshe wazi na zenye maana lakini sii habari hii ya kupima uume wa Chadema wakati miguu yenu mmeifunga!

Mkuu Mkandara,
Sidhani kama kuna anayesema kuwa hawawezi kuongoza, bali swali ni kuwa je Watanzania wakipewa sasa hivi kuchagua kuongozwa na mmojawapo wa viongozi wa CHADEMA wanaofahamika, say Mbowe, Zitto au Slaa ili wawaondoe CCM ambao ndani yake wana watu kama Salim A. Salim, Dr. Mwakyembe, Prof. Mwandosya, S. Sitta n.k. watawakubali? Jibu hatulijui lakini tunapoongea na waliokaribu yetu, majibu yao ni overwhelmingly NO.

Viongozi wa CHADEMA lazima waonyeshe kuwa ni tofauti na bora kuliko wa CCM bila ya hivyo haitakuwa rahisi kubadilisha CCM na CCM-b.
 
Mkuu Mkandara,
Sidhani kama kuna anayesema kuwa hawawezi kuongoza, bali swali ni kuwa je Watanzania wakipewa sasa hivi kuchagua kuongozwa na mmojawapo wa viongozi wa CHADEMA wanaofahamika, say Mbowe, Zitto au Slaa ili wawaondoe CCM ambao ndani yake wana watu kama Salim A. Salim, Dr. Mwakyembe, Prof. Mwandosya, S. Sitta n.k. watawakubali? Jibu hatulijui lakini tunapoongea na waliokaribu yetu, majibu yao ni overwhelmingly NO.

Viongozi wa CHADEMA lazima waonyeshe kuwa ni tofauti na bora kuliko wa CCM bila ya hivyo haitakuwa rahisi kubadilisha CCM na CCM-b.


Mkuu Siasa si Dini kwamba useme kuna Kuokoka au Kuongoka, Hao uliowataja wengi wao wamekuwa madarakani tangu baba yangu hajazaliwa, na ndio hao wanaokumbatia mfumo unaozidi kuwanyonya na Kuwadumaza watanzania, wangi wameanzia enzi za Tanganyika mpaka sasa Tanzania
 
Simple...CHADEMA kwangu wanafaa kwa sababu waliunyima msafara wa makamu wa Rais mamilioni ya ruzuku ulipoenda Karatu wakati waliishapewa pesa Ikulu. Inaonyesha wanajali pesa za wananchi.
 
Mkuu Siasa si Dini kwamba useme kuna Kuokoka au Kuongoka, Hao uliowataja wengi wao wamekuwa madarakani tangu baba yangu hajazaliwa, na ndio hao wanaokumbatia mfumo unaozidi kuwanyonya na Kuwadumaza watanzania, wangi wameanzia enzi za Tanganyika mpaka sasa Tanzania

Ndege,
Mapenzi yako kwa CHADEMA ni makubwa sana kiasi kuwa hakuna anayeweza kukuambia kitu kisichoisifia CHADEMA ukasoma na kukidadisi. Kwa hiyo maoni yangu ambayo mara nyingi ni critical kwa CHADEMA sidhani kama yanaweza yakakusaidia. Just ignore them.
 
Kuna mapungufu mengi katika CCM lakini bado hatujapata chama cha upinzani chenye nguvu na ambacho watanzania wanaweza kukipa dhamana ya kuongoza nchi.

Chadema wameanza kugombana mapema sana na watu wenye uwezo wa kuongoza ndani ya chadema ni wachache sana. Kwa sana nguvu yao ipo kwa wabunge wao Dr.Slaa, zito, Halima Mdee na said Arfi. Kwa bahati mbaya kuna dalili zote kuwa bwana Zitto yupo njia moja kuondoka Chadema na tusishangae kama atakwenda CCM hapo mwakani.
 
Ndege,
Mapenzi yako kwa CHADEMA ni makubwa sana kiasi kuwa hakuna anayeweza kukuambia kitu kisichoisifia CHADEMA ukasoma na kukidadisi. Kwa hiyo maoni yangu ambayo mara nyingi ni critical kwa CHADEMA sidhani kama yanaweza yakakusaidia. Just ignore them.

Mkuu hata wewe Chuki yako kwa CHADEMA ni kubwa sana kiasi kwamba unatoa Tuhuma ambazo hazina Ushahidi
 
A wrong question will certainly give you a wrong answer. A political party in opposition cannot be judged on the basis of what it has done to deserve people's support during election. A political party in opposition is judged on the basis of the vision and policies it has displayed that address short and long-term problems of a country, as well as the preparedness of the leadership in articulating those problems and proposing sound solutions, both practically and philosophically.
 
Mwanakijiji, kwa hali ilivyo sasa, tunahitaji mabadiliko tena haraka sana. Kwa vyovyote vile Chadema haina resources ukilinganisha na CCM. Lakini Chadema is posed kuleta mabadiliko kwenye nchi kwa ujumla na kwa CCM pia (as a catalyst for change). CCM ime-maintain status quo kwa hiyo there is no way they can change. Let Chadema take the top leadership and the rest will fall in place.

Uongozi wa juu kabisa chama hakiwezi kupewa kama zawadi ndugu yangu; ni lazima kistahili. Msingi wa swali langu hapa ni mastahili ya Chadema. Tusije tukaamua kuing'oa CCM kwa sababu tunaichukua CCM na kuiweka Chadema ilivyo sasa na kujikuta katika kile cha methali "kuruka mkojo..."..

CCM inashindwa hata ku-deal na vitu vidogo vidogo kama masuala ya madawati kwa wanafunzi (except for 800 shangingis ordered 2008/9 year alone) :)

That is my point; kama CCM chama chenye wasomi, mtandao mkubwa, historia ndefu na mipango na sera nyingi madhubuti imeshindwa hata hayo ya madawati ni kitu gani kinawafanya watu waamini Chadema katika uchanga wake kitaweza kuleta mabaliko makubwa? this is the crux of the matter kwangu.


Let CCM stay aside for a little while so that they can learn. At the same time, Chadema being the minority at the top leadership, they won't their way 100%, just the way CCM have.

Hofu yangu kubwa siyo kuingia madarakani bali waingie madarakani ili kiwe nini?
Ni kweli Chadema ina matatizo, lakini je ni chama gani duniani kisicho na matatizo ?? At least ya Chadema yanaweza kutatuliwa kwa sababu yako based on few individuals. CCM yao yako kimfumo na kwenye ushirikiano (partnership) na kulindana kiasi kwamba si rahisi ku-engage in constructive feedback na kuleta maendeleo nchini.

Hivi unafikiri once they taste power Chadema hawataingia kwenye mtego huo huo? Angalia muundo wao wa chama ulivyo unatofauti gani na ule wa CCM? Unafikiri na wenyewe wakianza kuingia kwenye matatizo hawatajaribu kukiokoa na kukikinga chama chao ili kiendelee kuwa madarakani? Si ndiyo tuliyoana kwenye ngwe ya kwanza ya Kibaki na hata ya pili huko?

Lakini pia kwa hali ilivyo sasa, chama ambacho kinafaa kuongoza nchi ni chama chenye mwelekeo wa mabadiliko na chenye nia thabiti ya kuondoa kero za wananchi, na ambacho hakina migogoro hata chembe. Je chama hicho kipo ?? So...katika hivi tulivyonavyo (walau kwa sasa), hebu twende na kile kilichobora kuliko vingine.

HIli nalo ndilo swali kubwa; Je Chadema ndiyo chama hicho? Ni kero gani au matatizo gani kwa wananchi kimeweza kuyaondoa? Ni kwa kiasi gani kimeweza kuleta ushawishi na hata kuleta mabadiliko ya kisheria kwa kuwavuta wanaCCM wakubaliane nao kupitisha sheria yenye maslahi ya nchi (bipartisan)?


My two cents.

taken!
 
A wrong question will certainly give you a wrong answer. A political party in opposition cannot be judged on the basis of what it has done to deserve people's support during election. A political party in opposition is judged on the basis of the vision and policies it has displayed that address short and long-term problems of a country, as well as the preparedness of the leadership in articulating those problems and proposing sound solutions, both practically and philosophically.

A misunderstanding of the question might lead one to a wrong analysis of the same. What I queried in the original post is fundamentally this question:
tunalazimika kujiuliza kama Chadema kimefanya mambo yoyote, kuonesha uongozi katika jambo lolote au kwa namna yoyote ile kuamsha Watanzania katika kujiletea mabadiliko kiasi cha kuweza kustahili mapenzi, imani, na ufuasi wa watu wengi sasa hivi.

You will see the question has nothing to do with the party being in power or not!
 
Chama ambaco hakina dola hakiwezi kupimwa kwa yapi kimefanya isipokuwa kinapimwa kwa sera zake. Rais Obama wakakti wote wa kampeni zake alikuwa anawaeleza wamarekani atakavyo tekeleza mambo fulani ikiwemo mfumo wa afya, bima, elimu na kufunga Guantanmo bay prison.

Huhitaji kuwa na dola ili upimwe. Kwa mfano, tunaweza kupima katika chaguzi ndogondogo kimeshinda vipi, kama chama kimeweza kujijenga vipi matawi mangapi, makada wangapi, kimeweza kupenya vipi vijijini n.k Hivi unajua zimefanyika chaguzi ndogo ngapi hadi hivi sasa na Chadema imeshinda ngapi kati ya hizo katikati ya "mwamko" wa mapenzi ya Chadema? Jibu la kuwa CCM inaiba kura limepitwa na wakati!


Hakuna hata siku moja aliulizwa amefanya nini au chama chake kimefanya nini. Lakini kama atagombea tena 2012 basi wamarekani watamuuliza amefanya nini ktk miaka 4 ya utawala wake.


Ndiyo lakini democrats wakiwa nje ya madaraka waliongoza upinzani wa wazi na dhahiri wa vita ya Iraq, waliandamana kumpinga Bush, walifanya warsha za wazi za kubeza utawala wa Bush; waliandamana kuwaunga mkono immigrants n.k haya hawakuhitaji kuyafanya wakiwa madarakani. Obama alijenga pale ambapo democrats walikuwa wanakipanda kwa miaka nane ya Bush!
 
Kwenye hivi vyama vidogo hii migogoro ndo inayotoa nafasi kwa wao kujikuza kama wataweza kumanage matatizo yao na kuendelea kukubalia kutokubaliana kwa manufaa ya chama. Bado si amini kama Chadema wanao uwezo wa kukaa nafasi ya juu kabisa ya nchi mpaka waonyeshe kwamba wanao uwezo wa kuvuka salama kwenye bahari iliyochafuka bila kusambaratika kama ilivyokuwa NCCR. Hapo then ntaanza kuona kweli wako serious na wanajua wanachokifanya.

KUna ukweli mkubwa hapo. Kumpa mtu zawadi ya kwanza ati kwa vile umemkuta anahema baada ya kukimbia ni kutokuwa makini; mtu huyo ni lazima ashindanishwe na aweze kustahili zawadi hizo. Hatupaswi kutoa zawadi kwa vile mtu anatoka jasho!

Vinginevyo naona kama ni hatari kuwapa watu dhamana kubwa bila kujua uwezo na fikra zao ziko upande gani wa maisha ya TZ. Inawezekana makucha halisi ya watu yakaonekana baada ya kupata madaraka. Zambia, Malawi waliamua haraka na walikuja kujilaumu baadae maana opportunist wengi walitumia mwanya wa watu kutowajua vizuri.
Nimeangalia kwa kina sana suala hili; tutakuwa tusiowajibika endapo tutaamua kuweka dhamana ya watu milioni 40 mikononi mwa Chadema ilivyo sasa!
 
Nikiangalia paji la uso la siasa zetu Tanzania kichwa kinaniuma sana, hasa viongozi wa vyama vyetu vya siasa.
Ukianza na viongozi wa serikali waliopo madarakani ni dhahir nawaona hawajitumi na hawana moyo wa dhati kwa taifa.Nikija kwa vyama vya upinzani naona wazi kabisa kuwa kuna maslahi binafsi kuliko ya taifa.
 
Mwanakijiji, toka umetoa hii mada, nimekaa nikijiuliza swali moja la muhimu, katika taifa kama hili letu, chama kisicho madarakani kinatakiwa kifanye nini ili kistahili kupewa dhamana ya Uongozi wa Taifa. Tukumbuke kuwa Chadema waliwaomba Watanzania wawape ridhaa ya kukamata madaraka, wananchi wakawanyima na hivi sasa tunashuhudia vidudu vya hao waliopewa. Wenye madaraka wanasema wataendesha nchi kulingana na sera zao na kutimiza ahadi kama walivyozitoa kwenye ilani ya Uchaguzi, sasa Chadema kwa mfano ina nafasi gani hapa kutekeleza sera zake kwa sasa ?

Ninavyofahamu jukumu la chama cha Upinzani popote pale duniani ni kuwaelimisha wananchi juu ya mapungufu ya utawala uliopo, je Chadema wameweza kufanya hivyo. Pili kwa nchi kama Tanzania ambapo ni vigumu kutenganisha nafasi za mihimili hii mitatu (serikali, bunge na mahakama) kwa kuwa inahodhiwa na Chama Tawala, Wapinzani watakiwa wafanye nini zaidi ya wanachofanya Chadema. Wamedai mabadiliko ya katiba wakapuuzwa, wamedai tume huru ya uchaguzi wakakataliwa na wamedai haki na usawa mbele ya sheria wakadhihakiwa.

Mwanakijiji, labda ungeanza kwa kututajia machache ambayo yako ndani ya uwezo wao na wangeweza kuyafanya lakini wakashindwa. Hapa naomba tujiepushe na mawazo ya kijuha ya kudai wameleta maendeleo gani kwa wananchi ama wabunge wake wamewafanyia nini wapiga kura wao. Serikali ikishaingia madarakani inatakiwa iwahudumie wananchi wote bila ubaguzi na hakuna tena swali la eneo kuwa na mbunge au diwani kutoka upinzani. Mbunge atawakilisha kilio cha wananchi wake bungeni/serikalini na hapo ametimiza wajibu maadamu wananchi wanalipa kodi.

Mwaka 2005 wananchi walipewa fursa ya kuchagua chama walichoridhika nacho kuwa kinafaa kuongoza nchi na kama kawaida yao kwa miaka hamsini, wakachagua CCM. Miaka hamsini chama kile kile na watu wale wale lakini bado wananchi wakategemea mambo tofauti na sasa twavuna tulichopanda. Ukipanda mahindi utavuna mahindi na ukipanda mihogo utavuna mihogo, tatizo la Watanzania ni kuwa kila msimu wanapanda mihogo wakiwa na imani kuwa watavuna mahindi ! Sasa kivumbi ni pale wanapoanza kuvuna mihogo, watakwaruzana na kulaumiana, CCM hiyoo !

Chadema kama Chama mbadala wamejitahidi kadri ya uwezo wao kwani wameendelea kuwakumbusha wananchi kuwa miaka yote watavuna kile walichopanda na si vinginevyo. Zaidi ya hapo wamebakiza tu kuingia mitaani na kutembeza bakora, bahati mbaya walafi na mafisadi ndani ya CCM hawakawii kujihami kwa kutumia vyombo vya dola na kujibu mashambulizi kwa vifaa vya moto!
 
Hapo mtoa mada unalinganisha tembo na sisimizi....ccm imekaa madarakani miaka chungu mzima, inatumia rasilimali za "watanzania", inapata misaada lukuki kutoka kwa wafanya biashara na vyama na tassisi 'rafiki' nje ya nchi, pia inamiliki vyombo vya dola, ina mtandao iliorithi kutoka tanu na afro shirazi.....na mambo kadha wa kadha.

....tuje kwa chadema ....inategemea kwa kiasi kikubwa rasilimali za vingozi wake na misaada kutoka vyama "rafiki" nje ya nchi na kwa kiasi kidogo wanachama.

Kuna ulinganishi hapo?
 
Mwanakijiji, labda ungeanza kwa kututajia machache ambayo yako ndani ya uwezo wao na wangeweza kuyafanya lakini wakashindwa. !

Mag3..

- Kuanzisha shule ya sekondari ya kuchukua wanafunzi na yenye kutoa elimu bora. Wazazi bila kujali itikadi zao wangepeleka watoto wao kwenye shule hiyo kama ingeonekana kufanya vizuri zaidi kuliko zile za "wazazi" za CCM!

- Kuanzisha Kliniki au Hospitali kwenye maeneo kadhaa ya nchi aidha kwa mchango wao wenyewe au kwa kuandika project ya mradi na kuhakikisha kuwa taasisi hiyo inatoa huduma inayoshinda na kliniki au hospitali za serikali au binafsi. Watu wangeona Chadema in action. Hilo halihitaji kuwa madarakani.

- Kuanzisha mipango ya usafishaji mji, mitaro n.k JIjini Dar au programu ambayo itatofautisha CCM na CHadema kwenye suala la usafi wa mji. Sidhani kama hili linahitaji kuwa madarakani kuweza kulifanya.

- Kutoa elimu ya uraia au kuanzisha programu ya elimu ya demokrasia kwenye matawi yao na kuwaalika wananchi kuja kusikiliza au kujifunza bure. Hata kutoa Warsha au Semina kwa wananchi au wanaotaka juu ya Uongozi, Demokrasia n.k na watu wakajiandikisha kuja kushiriki kwa ada kiasi na hilo likawa chanzo cha mapato. Hapa wangeweza kuwa na Idara ya Elimu ya Demokrasia ambao wangekuwa wanapita kutoa semina kikanda, kimkoa au kiwilaya! - halihitaji kuwa madarakani..

Ninayo mengi kweli.. ambayo naamini mahali penye uongozi mzuri wangeweza kabisa kuyafanya. So far, wanasubiri kuingia madarakani ili waweze kufanya! I don't think so, ndugu yangu.
 
....tuje kwa chadema ....inategemea kwa kiasi kikubwa rasilimali za vingozi wake na misaada kutoka vyama "rafiki" nje ya nchi na kwa kiasi kidogo wanachama.

Kuna ulinganishi hapo?

katika hali hii kweli tunataka kuwapa dhamana ya maisha ya watu takribani milioni 40? Not in my watch.
 
katika hali hii kweli tunataka kuwapa dhamana ya maisha ya watu takribani milioni 40? Not in my watch.

Mwanakijiji, get straight to the point, unataka hasa kusema nini - kuwa CCM iendelee kubaki madarakani kwa sababu ya iliyoyafanya kwa miaka yote hiyo kwa kutumia kodi zetu ? Je, CCM kama ilivyo sasa kuzidi kupewa dhamana ya hao watu milioni 40 ni sawa under your watch ? Je, ni wakati gani inakuwa ni heri kuanza upya kuliko kuendeleza yale yale yasiyokufikisha popote ? Mwanakijiji, we have hit rock bottom and CCM is making sure we stay DOWN, so whatever change we undertake - the only way out of the quagmire is UP.
 
Mwanakijiji, get straight to the point, unataka hasa kusema nini - kuwa CCM iendelee kubaki madarakani kwa sababu ya iliyoyafanya kwa miaka yote hiyo kwa kutumia kodi zetu ? Je, CCM kama ilivyo sasa kuzidi kupewa dhamana ya hao watu milioni 40 ni sawa under your watch ? Je, ni wakati gani inakuwa ni heri kuanza upya kuliko kuendeleza yale yale yasiyokufikisha popote ? Mwanakijiji, we have hit rock bottom and CCM is making sure we stay DOWN, so whatever change we undertake - the only way out of the quagmire is UP.

hapana.. CCM isibaki madarakani kwa sababu inastahili! Lakini tusiwapandishe watu wengine madarakani pasipokustahili.. maanake ni kuwa kwa yeyote anayetaka kuja juu yetu we have to set the bar very high not very low.. Hivyo, siyo kuiondoa CCM for the sake of kuindoa CCM.. we have learned in Kenya.. we have to remove the ruling party kwa sababu we got something better!.. Na njia pekee ya kupata "better" ni kuhakikisha tunawapitisha kwenye tanuru ya moto kwanza...
 
Mzee mwanakijiji,
Mkuu wangu kama ungekuwa mwanamke basi hadi leo usingekuwa na Mume na kama ungekuwa naye bila shaka angekuwa abusive kwako..
Nasema hivi kwa sababu, ni Wadanganyika wengi wenye mawazo kama yako na ndio maana tunaburuzwa na CCM kwa sababu hatuoni mwanaume zaidi ya CCM. Maisha yetu yanaishia na CCM..Cases za namna hiyo tunaziona kila siku na hujiuliza hivi kuna watu wengine wanapenda kiasi hicho jamani.. unakubali hakufai lakini hutaki kumwacha!
 
Back
Top Bottom