CHADEMA imefanya nini kustahili dhamana ya Uongozi wa Taifa?

Je tunaweza kuamini kuwa Chadema ilivyo sasa inaweza kuongoza Taifa la watu karibu milioni 40, kuunda serikali na kuisimamia serikali hiyo kwa uaminifu kushinda CCM? Ni kitu gani kinawafanya watu waamini kuwa Chadema ikiingia madarakani basi matatizo kadhaa ya ufisadi yatakomeshwa na kutakuwa na nidhamu mpya ya matumizi ya fedha na raslimali za taifa letu?

NI jambo moja kuangalia suala kwa mwanga wa kisoma (intellectual perspective) na jambo jingine kabisa kulisimamia na kufuatilia jambo kiutawala. Mtu anayeweza kuona matatizo ya sekta ya madini kisomi ukimpa nafasi ya kutawala atalazimika kuangalia maslahi zaidi ya yale anayoyaona kisomi. Nyerere alitoa mfano mzuri sana kuhusu kutaifishwa kwa mashamba ya Mkonge. Alisema kuwa kiakili aliona umuhimu wake lakini ilipokuja utekelezaji kulikuwa na kuboronga kwa hali ya juu.

Sasa ni kitu gani kinawafanya watu waamini kuwa ati Chadema ikiingia madarakani sasa hivi basi matatizo kadha wa kadha ya kiutawala na utendaji yataondolewa na Tanzania itaanza safari ya kuelekea matumaini? Je tumejifunza lolote kutoka Kenya, Zambia, Malawi ambapo vyama vya upinzani viliingia na kushika madaraka.

Je ni kitu gani kitaizuia Chadema ikiwa madarakani kuanza kutengeneza mfumo wa kutumia serikali kunufaisha Chama kama CCM wanavyofanya? Tunategemea wema au ahadi za watu?
 
Kweli wadanganyika wepesi wa kusahau! Hii vita ya ufisi-adi ilianzia wapi kama sio kwa CHADEMA? Na "wapambanaji" toka CCM wanaotaka kuhamia CHADEMA unafikiri vyama vingine vyote hawavioni? Mlitaka chama cha upinzani kifanye nini zaidi ya hapo? CCM itakapokuwa chama cha Upinzania kama KANU ya Kenya nao watakosa nguvu waliyonayo sasa kwa kuwa uwezo wa kuchota manoti ya BOT na kuwahonga chumvi, khanga, kofia, vitenge, nk wadanganyika hawatakuwa nao! Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni jamani!
 
Wana JF wezangu salaam,

Ni ombwe la uongozi linalotuangazia,wanaoweza kuongoza hawapati nafasi wasioweza ndo hao, CHADEMA bado kuongoza nchi wakazane na serikali za mitaa na ubunge wapate nguvu kubwa pia watudhihirishie uongozi na utawala bora ndani ya chama na nje. CCM wanafiki wengi wanasema hili kumbe wanafanya lingine sio hivyo pamoja na wachumia tumbo wengi.

Na kama mwana JF mmoja alivyosema Heri zimwi likujualo kwa sasa..
 
Kweli wadanganyika wepesi wa kusahau! Hii vita ya ufisi-adi ilianzia wapi kama sio kwa CHADEMA?

Rudi nyuma kidogo uone ilianzia wapi. Waulize wenyewe watakuambia ilikoanzia. Haikuanzia Chadema.

Na "wapambanaji" toka CCM wanaotaka kuhamia CHADEMA unafikiri vyama vingine vyote hawavioni?

ndiyo sababu ya haya maswali. Kwa sababu kujiunga Chadema mtu akitoka CCM siyo jambo la kushangaza. Lakini wanataka kujiunga ili kiwe nini?

Mlitaka chama cha upinzani kifanye nini zaidi ya hapo? CCM itakapokuwa chama cha Upinzania kama KANU ya Kenya nao watakosa nguvu waliyonayo sasa kwa kuwa uwezo wa kuchota manoti ya BOT na kuwahonga chumvi, khanga, kofia, vitenge, nk wadanganyika hawatakuwa nao! Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni jamani!

Yaani unaamini kabisa kuwa Chadema kinaweza kuongoza taifa letu better kwa vile ni Chadema?
 
Mkuu Mwanakijiji asalaam aleikum

Kabla ya Kuuliza CHADEMA imefanya nini, nadhani tungeuliza kwanza CHADEMA kama chama cha Upinzani kilipaswa kufanya nini, namaanisha tujue kama CHADEMA kikiwa kama chama cha Upinzani kimetimiza majukumu yake!

Vinginevyo Swali lako litakuwa ni contradictory kidogo kwa maana halijatofautisha majukumu ya CHADEMA kama opposition party na majukumu ya CHADEMA kama kingekuwa ni ruling party.

CHADEMA kama opposition party nadhani kimejaribu sana kuisimamia Serikali na katika miaka mitano iliyopita tumeona namna wabunge wachache wa CHADEMA walivyoweza kuilzimisah Serikali kuamka kutoka katika usingzi mzito
 
Mkuu Mwanakijiji asalaam aleikum

Kabla ya Kuuliza CHADEMA imefanya nini, nadhani tungeuliza kwanza CHADEMA kama chama cha Upinzani kilipaswa kufanya nini, namaanisha tujue kama CHADEMA kikiwa kama chama cha Upinzani kimetimiza majukumu yake!

siangalii chadema kama chama cha "upinzani" tu. Naangalia chama hicho kama taasisi yenye uongozi, malengo na vile vile mipango mbalimbali. NI kwa kiasi gani imetekeleza mambo yaliyo ndani yake.

Vinginevyo Swali lako litakuwa ni contradictory kidogo kwa maana halijatofautisha majukumu ya CHADEMA kama opposition party na majukumu ya CHADEMA kama kingekuwa ni ruling party.

Chama cha siasa hakiachi kuwa chama kwa vile hakiko madarakani. Ili kiweze angalau kuwa madarakani kuna mambo ambayo kinaweza kufanya kuonesha kuwa kinaweza kuwa madarakani. Huu ndio msingi wa maswali yangu. Siulizi Chadema ifanye nini wakati najua haiko madarakani! Nauliza mambo yale ambayo kama chama kimeweza kufanya kwenye mahali na kitaifa na kuonesha kuwa kinastahili kudhaminiwa uongozi wa taifa.

NItakupa mfano, kimepush ajenda gani ya kisheria na kufanikiwa kupitisha ajenda hiyo? n.k

CHADEMA kama opposition party nadhani kimejaribu sana kuisimamia Serikali na katika miaka mitano iliyopita tumeona namna wabunge wachache wa CHADEMA walivyoweza kuilzimisah Serikali kuamka kutoka katika usingzi mzito

Wana CCM watadai ni wabunge wao wamefanya kazi kubwa zaidi kwani wabunge wa Chadema hata wakinuna Bungeni hawawezi kuathiri lolote zaidi ya kugusa wananchi kifikra. Wabunge wa CCM wakikataa ndio imekwisha.

Sibezi hata kidogo baadhi ya mambo ya kisiasa ya kuamsha ambayo yamefanywa na Chadema; sibezi mahubiri ya Mwembe Yanga; lakini is that all? Ndicho hicho kinachowafanya watu waamini kuwa wanaweza kupewa dhamana ya maisha ya watu milioni 40; yaani kuweza kutoa hotuba ya kuwaumbua mafisadi na ufisadi is the qualification for leadership of a nation?
 
Mwanakijiji, kwa hali ilivyo sasa, tunahitaji mabadiliko tena haraka sana. Kwa vyovyote vile Chadema haina resources ukilinganisha na CCM. Lakini Chadema is posed kuleta mabadiliko kwenye nchi kwa ujumla na kwa CCM pia (as a catalyst for change). CCM ime-maintain status quo kwa hiyo there is no way they can change. Let Chadema take the top leadership and the rest will fall in place.

CCM inashindwa hata ku-deal na vitu vidogo vidogo kama masuala ya madawati kwa wanafunzi (except for 800 shangingis ordered 2008/9 year alone) :)

Let CCM stay aside for a little while so that they can learn. At the same time, Chadema being the minority at the top leadership, they won't their way 100%, just the way CCM have.

Ni kweli Chadema ina matatizo, lakini je ni chama gani duniani kisicho na matatizo ?? At least ya Chadema yanaweza kutatuliwa kwa sababu yako based on few individuals. CCM yao yako kimfumo na kwenye ushirikiano (partnership) na kulindana kiasi kwamba si rahisi ku-engage in constructive feedback na kuleta maendeleo nchini. Lakini pia kwa hali ilivyo sasa, chama ambacho kinafaa kuongoza nchi ni chama chenye mwelekeo wa mabadiliko na chenye nia thabiti ya kuondoa kero za wananchi, na ambacho hakina migogoro hata chembe. Je chama hicho kipo ?? So...katika hivi tulivyonavyo (walau kwa sasa), hebu twende na kile kilichobora kuliko vingine.

My two cents.
 
Kwenye hivi vyama vidogo hii migogoro ndo inayotoa nafasi kwa wao kujikuza kama wataweza kumanage matatizo yao na kuendelea kukubalia kutokubaliana kwa manufaa ya chama.

Bado siamini kama CHADEMA wanao uwezo wa kukaa nafasi ya juu kabisa ya nchi mpaka waonyeshe kwamba wanao uwezo wa kuvuka salama kwenye bahari iliyochafuka bila kusambaratika kama ilivyokuwa NCCR. Hapo then ntaanza kuona kweli wako serious na wanajua wanachokifanya.

Vinginevyo naona kama ni hatari kuwapa watu dhamana kubwa bila kujua uwezo na fikra zao ziko upande gani wa maisha ya TZ. Inawezekana makucha halisi ya watu yakaonekana baada ya kupata madaraka.

Zambia, Malawi waliamua haraka na walikuja kujilaumu baadae maana opportunist wengi walitumia mwanya wa watu kutowajua vizuri.
 
Chama ambaco hakina dola hakiwezi kupimwa kwa yapi kimefanya isipokuwa kinapimwa kwa sera zake. Rais Obama wakakti wote wa kampeni zake alikuwa anawaeleza wamarekani atakavyo tekeleza mambo fulani ikiwemo mfumo wa afya, bima, elimu na kufunga Guantanmo bay prison.

Hakuna hata siku moja aliulizwa amefanya nini au chama chake kimefanya nini. Lakini kama atagombea tena 2012 basi wamarekani watamuuliza amefanya nini ktk miaka 4 ya utawala wake.
 
Tuwape nchi CHADEMA then tuone watafanya nini after 5 years, wakiboronga kama JK then tutawauliza wamefanya nini.
 
hapa sio kujaribu chama kuingia madarakani......kama ni sera basi ccm wanasera nzuri sana lakini zisizotekelezeka,,,tutajuaje kama sera za chadema zitatekelezeka? hapa mi bado naendelea kuota chama kipya kitakachomeguka kutoka ndani ya ccm hiki ndicho kina
Chama ambaco hakina dola hakiwezi kupimwa kwa yapi kimefanya isipokuwa kinapimwa kwa sera zake. Rais Obama wakakti wote wa kampeni zake alikuwa anawaeleza wamarekani atakavyo tekeleza mambo fulani ikiwemo mfumo wa afya, bima, elimu na kufunga Guantanmo bay prison.

Hakuna hata siku moja aliulizwa amefanya nini au chama chake kimefanya nini. Lakini kama atagombea tena 2012 basi wamarekani watamuuliza amefanya nini ktk miaka 4 ya utawala wake.
 
Nitakupa mfano, kimepush ajenda gani ya kisheria na kufanikiwa kupitisha ajenda hiyo? n.k

Wana CCM watadai ni wabunge wao wamefanya kazi kubwa zaidi kwani wabunge wa Chadema hata wakinuna Bungeni hawawezi kuathiri lolote zaidi ya kugusa wananchi kifikra. Wabunge wa CCM wakikataa ndio imekwisha.

Sibezi hata kidogo baadhi ya mambo ya kisiasa ya kuamsha ambayo yamefanywa na Chadema; sibezi mahubiri ya Mwembe Yanga; lakini is that all? Ndicho hicho kinachowafanya watu waamini kuwa wanaweza kupewa dhamana ya maisha ya watu milioni 40; yaani kuweza kutoa hotuba ya kuwaumbua mafisadi na ufisadi is the qualification for leadership of a nation?

Mwanakijiji naheshimu sana mawazo yako lakini naomba kutofautiana na wewe kwenye suala la kupush ajenda ya kisheria kwa CHADEMA!

Japokuwa CHADEMA ni wachache sana bungeni lakini sauti yao imekuwa kama wao ni nusu ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz. Linapokuja suala la kupush masuala ndio hapo uchache wao unapoanza kuwaathiri! Wabunge wa CCM wanatumia wingi wao kupitisha mambo!

All in all mchango wa CHADEMA wa kuiambia Serikali bila kuuma maneno (eg kutangaza orodha ya mafisadi) sio insignificant! Kuisubiri CCM isafishike ni kupoteza wakati! Wanaotakiwa kuisafisha ni wachafu wote kulingana na maelezo ya Waziri Sophia Simba!

CHADEMA uchafu wake bado sijauona na naamini wana uwezo wa kukalia usukani wa nchi! Kama hilo ni gumu wawe na wabunge wengi ili waweze kuishupalia Serikali vizuri kwenye masuala ya kitaifa!
 
Mwanakijiji,mbona huulizi kuhusiana na CUF?
Ama kwako CUF sio chama cha siasa?
Kwanini kila siku ni CHADEMA VS CCM?
Unaboa sana ,kila post CHADEMA na CCM tuu- vingine sio vyama ?badilikeni anzeni kuangalia na vyama serious kama CUF .
 
Mwanakijiji,mbona huulizi kuhusiana na CUF?
Ama kwako CUF sio chama cha siasa?
Kwanini kila siku ni CHADEMA VS CCM?
Unaboa sana ,kila post CHADEMA na CCM tuu- vingine sio vyama ?badilikeni anzeni kuangalia na vyama serious kama CUF .

Cuf for Zanzibar

umeshawahi kuhudhuria mikutano ya kisiasa ya Cuf??

ni aina gani ya watu huwa wanahudhuria?

Takbir zinapigwa kwenye mikutano ya kisiasa unataka tuwajadili humu? au hujui?
 
mawazo yote haya yameegemea kwenye mlengo fulani, kumbukeni kuwa kwa milengo mingine, hata ccm inaonekana haijafanya lolote la kustahili kupewa tena uongozi wa nchi, na huenda katika miaka hii mitano kimeharibu zaidi.

nashauri tuwe neutral and logical

tutende haki kwa wananchi zaidi ya hivi vyama
 
nadhani kupima uwezo wa CHADEMA wa kubeba dhamana ya uongozi kwa kilinganisha na CCM, unaweza usipate jawabu sahihi, kwa vyovyote CCM itaipita kwa mbali kwa sababu vyama hivi vinapishana karibu kwa kila kitu

Kwanza CCM imekuwepo kwa zaidi ya miaka 40 (ikijumihishwa na kipindi cha TANU) wakati Chadema hajamaliza hata miongo miwili tangu kuanzishwa kwakwe.

Pia CCM iko madarakani wengi waliomo, wanaoishabikia, kuisadia na kuipa nguvu si wana-CCM wa dhati ni kwa sababu wanajua ni chama ambacho kiko madarakani. kwa mfano wafanyabiashara wanaiunga mkono na kuichangia kukwepa rungu la dola na hii ni dhahiri kabisa

Vile vile viongozi wenye nafasi muhimu kama wakurugenzi wa wilaya na maafisa watendaji wa kata ambao ndo huwa wasimamizi wa uchaguzi unapofika wakati wa uchaguzi ni rahisi kupokea maelekezo ya kuipendelea CCM wakakti wa uchaguzi vinginevyo huofia kupoteza nafasi zao.

Nafasi hii iliyonayo CCM ndiyo inaipa kigezo cha kuendelea kutamba kwamba ni chama 'kinachoungwa mkono' kwa kiasi kikubwa na hata kuwatia upofu wale ambao hawawezi kupambanua, ni kwa vipi kinaonekana 'kuungwa mkono' kiasi hicho.

Hali kadharika kwa kuwa chama chenye dola, CCM inapata mwanya wa kuvinyanyasa na kuvikandamiza vyama vingine kwa namna mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuvisababishia migogoro katika vyama vya upinzani ikiwemo CHADEMA ili vionekane vichanga na visivyoweza kustahili kupewa dhamana ya uongozi wa nchi. na kwa hili walifanikiwa japo kwa kadiri siku zinavyoenda itabidi wabuni mkakati mpya.

Vyombo vya habari navyo kwa sababu zilizowazi, zikiwemo baadhi ya waadishi kununuliwa, kuhofia kukosa biashara ya matangazo, na kuhofia kufarakana na serikali, vimechangia kukuza migogoro katika vyama vichanga.

mfano mgogoro wa maafisa wa CHADEMA haukuwa na sababu ya kukuzwa na vyombo vya habari hata kama walioathilika hawakuridhika, na pengine 'kimgogoro' hicho kisingekuzwa kiasi hicho kama maafisa wa ngazi hiyo wangetimuliwa CCM.

Pamoja na hoja zote hivyo, bado Chadema ilivyo sasa imeweka msingi wa kuwa chama chenye uwezo wa kuongoza nchi ikiwa kitapewa dhamana hiyo. na hii haitakuwa mara ya kwanza hata PNU haikuwa imara kabla ya kupata uongozi

Cha msingi, ni dhamira ya walioshika usukani ndani ya chama kuweza kuvutia wanachama na wasiowanachama ili kukipa nguvu za kujenga vyombo vya ki-uongozi ndani ya chama na katika utawala wa nchi kwa ujumla.

Na hili linawezekana kwa kuanzia na viongozi waliopo, na wengine wengi ambao hawajihusishi na siasa kwa sasa, na wengine walioko CCM lakini hawakubaliani na yanayotendwa huko.

Ni imani yangu kwamba chama chochote chaweza kuongoza nchi, matatizo ya kiongozi au baadhi ya viongozi ni suala la mpito, chama kikiishajidhatiti wanachama wana nguvu ya kuwaengua wanaoonekana ni kikwazo na kuwapa nafasi wenye sifa zinazohitajika, na viongozi wakilijua hilo watatenda kulingana na matakwa ya chama, vinginevyo wanachama hawatachelewa kujua kuwa chama chao hakirekebishiki, watahama na hivyo kukiangusha na hiyo ndiyo demokrasia
 
Mkuu maoni yako ni mazuri sana lakini hoja yako tu General kiasi kwamba mimi binafsi naona kama inamiss vitu fulani.

Tukilinganisha uwezo wa watu, raslimali, historia na mwelekeo kati ya CCM na Chadema chama cha CCM kinaicha Chadema kwa mbali sana.

Tukilinganisha uwezo wa watu juu nini? Rasilimali ipi? Historia juu ya nini? na mwelekeo upi unaoiacha CHADEMA.
 
Mwanakijiji,
Ume-summarize vizuri sana. Kwa mawazo yangu;

  1. CHADEMA imefanya ya kutosha na mazuri sana kama chama cha upinzani kwa kufanikiwa kushawishi wananchi juu ya mapungufu ya CCM. Hili ndilo jukumu lao la kwanza na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
  2. Jukumu lao la pili na walilotakiwa kulikabili ni la kujipanga vema kiuongozi kuonyesha kuwa wanaweza kuaminiwa kuchukua uongozi wa nchi, sio na wanachama wa CHADEMA, bali kuaminiwa na watanzania wengine wasiofungamana na upande wowote? Jukumu hili inaelekea limewashinda.
Ukiacha kufikiria kishabiki sina shaka utakubaliana na mimi kuwa kwa utendaji tulioona hasa wa siku za hivi karibuni wa viongozi maarufu/wa juu wa CHADEMA, hakuna anayeonekana kujenga imani ya watu wasio mashabiki wao, kuwa watakuwa bora kuliko baadhi ya viongozi ndani ya CCM. Ndio maana wengi wanaanza kuangalia watu kama Salim A. Salim kuwa alternative ya Kikwete, na sio Mbowe, Slaa au hata Zitto.

Imani kwa viongozi kioo wa CHADEMA imeondoka kwa Watanzania walio wengi hasa wale wasio mashabiki wao wa dmu. Hivi ndio wanavyoonekana;

  1. MBOWE; Sio tu elimu yake ni ndogo kumfanya asiwe na uono wa mbali, bali pia ameonyesha kuwa na udikteta na pengine ukabila, vitu ambavyo watanzania wanavichukia sana.
  2. Dr. SLAA; Ameonekana kutokuwa na msimamo wa kishujaa baada ya kuonekana kama vile kibaraka wa Mbowe. Yeye kama msomi na mwenye umri zaidi ya Mbowe na Zitto na wengineo chamani, angetakiwa awe na uwezo wa kushawishi, kukemea na pia kufundisha hao makinda jinsi ya kuwa viongozi na wavumilivu wa watendaji wenzao.
  3. ZITTO; Ameonekana kuwa mpayukaji, mwenye maamuzi ya haraka bila kudadisi kiundani na kuangalia madhara ya hayo maamuzi na pia kutokujua ukomo wa ufahamu wake. Bahati yake mengi ya matatizo yake yanaweza yakatibika kwa kuwa bado ni kijana mdogo kwa kujipatia uzoefu zaidi wa uongozi na kutafiti zaidi kabla ya kutoa maamuzi au matamshi.
Kwa hiyo CHADEMA wako kwenye mwelekeo mzuri wa kupewa dhamana ya nchi kama matatizo yaliyopo yakipatiwa ufumbuzi. Tatizo ni kuwa 2010 iko jirani sana kupata ufumbuzi kwa kutumia waliopo madarakani hivi sasa. Ushauri wangu ni kuwa watafute Nyerere wao kama vile akina Mzee Sykes walivyomwingiza Nyerere kwenye uongozi wa TAA/TANU na wao kuachia ngazi.
 
Wakuu zangu,
Haya maswala ya kujiuliza kama Chadema inaweza kuongoza ni maswali yasiyokuwa na msingi kabisa.
Kina mama na wana JF wote mtanisamehe sana kwa mfano mdogo naotaka kuuweka hapa:-

Uongozi wa nchi ni sawa na uongozi wa nyumba (kwa udogo wake). Huwezi kumpima bwana mmoja na mwanamme mwingine kama anaweza wakati wote ni wanaume. Ati sababu unazotumia ni kwamba mume mmoja hajawahi kuoa..
Kama kuna sababu zinazowasukuma kuamini kwamba Chadema haiwezi kuongoza nchi bora mziorodheshe wazi na zenye maana lakini sii habari hii ya kupima uume wa Chadema wakati miguu yenu mmeifunga!
 
Wakuu zangu,
Haya maswala ya kujiuliza kama Chadema inaweza kuongoza ni maswali yasiyokuwa na msingi kabisa.
Kina mama na wana JF wote mtanisamehe sana kwa mfano mdogo naotaka kuuweka hapa:-

Uongozi wa nchi ni sawa na uongozi wa nyumba (kwa udogo wake). Huwezi kumpima bwana mmoja na mwanamme mwingine kama anaweza wakati wote ni wanaume. Ati sababu unazotumia ni kwamba mume mmoja hajawahi kuoa..
Kama kuna sababu zinazowasukuma kuamini kwamba Chadema haiwezi kuongoza nchi bora mziorodheshe wazi na zenye maana lakini sii habari hii ya kupima uume wa Chadema wakati miguu yenu mmeifunga!
Good point Mkandara,

Kama Chadema inaweza kujiendesha kama chama, na malengo ya chama cha siasa ni kushika nchi kwa mujibu wa katiba, Basi Chadema chaweza kuongoza nchi.
 
Back
Top Bottom