CHADEMA ilipotosha umma taarifa ya Membe?

Hivi cdm walipotosha kitu gani! TBC1 walimrekodi akisema juu ya chama kuadhiliwa na nchi za kigeni ikiwa i mwendelezo wa kile alichokisema waziri mwenzake SS ch10, ndugu {usiongozwe na tumbo ukakiacha kichwa chako kimelala}

Kwenye mabano hapo mzee... Kula tano
 
chama cha demokrasia na maendeleo pamoja na baadhi ya vyombo vya habari vinalaumiwa kupotosha taharifa ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mh Benard Membe

Taharifa kamili
WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imesema baadhi ya vyombo vya habari pamoja na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), vilipotosha taarifa ya Wizara hiyo kuhusiana na chama kinachofadhiliwa ili kuleta machafuko nchini.

Imesema Waziri Bernard Membe hakutaja jina la chama wala nchi kinachofadhiliwa na nchi za Jumuiya ya Ulaya ili kuleta machafuko nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Haule amesema, Serikali itachukua hatua za kidiplomasia chini ya Mkataba wa Kimataifa wa Vienna kuhusu Mahusiano ya Kidiplomasia wa mwaka 1961, ikiwa itathibitisha nchi na chama hicho.

Haule amesema , Wizara imepokea taarifa za ujumbe wa simu za mkononi unaosambazwa kuwa baadhi ya nchi za Jumuiya ya Ulaya zinatuhumiwa kukifadhili chama cha siasa nchini ili kuleta machafuko na kwamba, raia wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo wanakuwa na wasiwasi juu ya usalama wao.

“Tumepokea taarifa hizo na tumezipeleka kwenye vyombo vinavyohusika kwa uchunguzi na ikithibitika, Wizara itatoa taarifa,” amesema Haule leo.

Amesema, katika mkutano wa Waziri Membe alioufanya wiki iliyopita na waandishi wa habari, alijibu suala hilo bila kutaja jina la chama wala nchi inayofadhili, lakini Chadema kiliibuka na kumtaka Membe kuzitaja balozi hizo zinazofadhili chama hicho na kiasi cha fedha kinachotolewa

Kashaga,HM Hafif na Mbopo hivi Riz1 anawalipa nini?
 
Chadema wamezoea sana kuzidisha na kupotosha umma. hao hao walidanganya kuwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga amefariki, na hao hao tena jana tu wamezua kuwa magufuri kajiuzulu. Na kesho watasema mengine.

hakika Chama hiki kimejaa wanafiki na waongo wakubwa sana katika kutaka kuleta balaa nchini.


Ni lini na wapi CHADEMA wamotoa tuhuma kwa kwamba Membe amekituhumu CHADEMA kwamba kinafadhiliwa na balozi za nje?

Tamko la CHADEMA lilimtaka Membe ataje ni chama gani na ni nchi gani zinazofadhili hicho chama.


Hapa msemaji wa Membe kakurupuka
 
Ni lini na wapi CHADEMA wamotoa tuhuma kwa kwamba Membe amekituhumu CHADEMA kwamba kinafadhiliwa na balozi za nje?

Tamko la CHADEMA lilimtaka Membe ataje ni chama gani na ni nchi gani zinazofadhili hicho chama.


Hapa msemaji wa Membe kakurupuka
Mkuu uko sahihi kabisa, nyongeza: Mnyika alimtaka membe ataje kiasi cha pesa,
 
Jama huyu kashaga, hafifu na wengine wenye mlengo Kama huo watawasumbua vichwa vyenu bure maana wanafaam mpango mzima wa propaganda za chama nao pia ni watekelezaji! propagandaBadadaAdadadad
 
sasa kama hakutaja chama nyie mlitakaje? membe kama mwanadiplomasia aliyebobea hawezi kumention jina la chama publically na cdm hawana audacity ya kumfanya ataje jina la chama! wanausalama wanalifanyia kazi hilo na hatua zitchukuliwa! cdm walipasawa wapambane na bi sophia simba aliyewataja hadharani

mkuu sijui kama unafuatilia media. Mbona myika alisema vizuri,wanampelembesha dada sofi kwanza alafu wanamtaka membe atamke wazi ni chama gani ili tujue akina nani wanataka kuiujumu nchi. Na kama akitamka cdm bila ushaidi itakuwa kama ile ya kumtaka Lema athibitishe usanii wa Pm alafu wanamuita kimya kimya kuwa yaishe kishikaji. Membe muoga tu! Alaf unasema Membe hawezi daiwa kuthibitisha?yeye ni nani?above the law? Cdm go!
 
Chadema wamezoea sana kuzidisha na kupotosha umma. hao hao walidanganya kuwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga amefariki, na hao hao tena jana tu wamezua kuwa magufuri kajiuzulu. Na kesho watasema mengine.

hakika Chama hiki kimejaa wanafiki na waongo wakubwa sana katika kutaka kuleta balaa nchini.
hivi nikweli chadema kama chama ndio walio toa habali kwamba waziri amejiudhuru au unakulupuka tu?
 
Working on rumours is very dangerous muhimu sana watoaji hoja wafanyie uchunguzi tusiwe ma zezeta Wa habari na kuibebA jinsi ilivyo. nakumbuka kuna wakati Wa kampeni mwembe yanga tuliambiwa na dr slaa TBC wamekata matangazo wakati mimi nilikuwa namuangalia slaa kwa TBC, watu walimpelekea dr suala makontena ya kura feki akapanda nalo jukwaani, ikaja suala vigogo Wa CCM kukutana mwanza ambapo there was no proof. Kuna haja sana ya kuchunguza kabla habari hazier fika kwa waandamizi ANGalizo
 
Jamani masikini Membe, tetesi ni kwamba siyo Chadema inayomnyima usingizi kwa sasa bali kukurupuka kwake kwa kuyahusiha mataifa ya magharibi. Membe kama Waizri wa Mambo ya Nje kabanwa ndani na nje kwa kuropoka na sasa anatafuta pa kutokea, anatakiwa ayataje hayo mataifa na kutoa ushahidi. Membe ameyakoroga mwenyewe tena mchana kweupee mbele ya waandishi wa habari na sasa inabidi ayanywe hata kama yatakuwa machungu kiasi gani. Na hili linatakiwa liwe fundisho kwa viongozi wa serikali waropokaji na ambao wamezoea kuvikandia vyama vinavyowatetea wanyonge kama Chadema. Lakini safari hii watakoma kwani Waziri mzima hategemewi kumwaga upupu kama alivyofanya Membe, hayo angewaachia akina Makamba, Tambwe, Lipumba, Mrema, Cheyo, Kafulila, Yahya na wengineo.
 
Mimi sometimes nashindwa kuelewa uwezo wa kufikiri wa viongozi wetu. Yaani mtu kama Membe anaweza kupata ujumbe wa simu na kuita waandishi na kutangaza hiyo taarifa bila kufanya uchunguzi wala kuvitaharifu vyombo husika. Na kingine kwa nafasi kama ya Membe kama anafanya kazi kwa majungu anatangaza chama na balozi bila kutupa majina huo ni upuuzi ambao hauna mantiki yoyote
 
unajua mkuu kuna msemo unaosema'ukirusha jiwe gizani atakayesema yalaaah ujue limempata" Membe hakutaja chama sasa kwnini cdm wakurupuke?? kwanini TLP,DP ama SAU wasilalamike? au wanajihisi nini? mwaka huu wataglue kweli

CDM hawakakurupuka. Alianza Sofia Simba, akasema wazi CDM inafadhiliwa kuleta mauaji. JK mwenyewe akasema CDM wanafanya machafuko kuion'goa serkali madarakani, akaja Tyson akasema aliyosema, baadaye akaja Membe. Yote hiyo ni baada ya maandamano ya CDM. Mtu yeyote mwenye akili atajua Membe alikuwa anailenga CDM. But basis ya Mnyika wakati anaongea na waandishi wa habari ilikuwa kwamba two cabinet ministers wamezungumza jambo hilo, mmoja kaitaja CDM WAZI mwingine hakuitaja but akasema kweli hilo jambo huenda lipo. So what other clues you guys want kujua kuwa ni CDM?

Mnyika alisema, kwa kuwa Waziri mwenzake Membe keshaitaja bila woga CDM, it is obvious serekali inajua, na ndio maana wakamtaka Membe sasa ataje ni nchi gani na kiasi gani cha fedha, wala hwakumuomba akitaje chama kwa kuwa chama kilishatajwa na Sofia, na hizi habari zimekuja baada ya hotuba ya JK kuwalaumu CDM na hotuba hiyo ilikuja baada ya maandamano ya CDM. Kwani kuna chama gani tena nchini kinachoweza kuisumbua serekali ukiachia mbali CDM. Kwa akili ya kawaida Membe atahangaika kuongelea vyma wafu kama CUF, TLP, NCCR AU LND? HAAAAA

Sasa kuna watu wanapost vitu hapa kweli unasikitika kujua kuwa jinsi macho yamefunikwa na ujinga au ushabiki. Baregu hakukosea, nguvu ya ccm ni ujinga
 






membe_233.jpg





MIONGONI mwa watu wanaotajwa kuwa kwenye mzunguko wa mwisho kuelekea ikulu katika uchaguzi mkuu ujao ni Bernard Kamilius Membe.
Mbunge huyo wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa inadaiwa analalia mlango wazi bahati ya Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete waliowahi kuwa mawaziri wa wizara hiyo.
Wakati wote, Membe amekuwa makini katika kauli zake ili asichafue ‘CV’ yake.
Lakini wiki iliyopita, ‘rais huyo mtarajiwa’, alijibebesha furushi la uzushi akaenda kulifungua mbele ya wanahabari, “Ooh kuna chama cha siasa kinafadhiliwa na nchi za nje ili nchi isitawalike!”
Membe hakutaka kuwa muwazi lakini ukweli alikuwa anaungana na Waziri wa Jinsia, Watoto na Wanawake, Sofia Simba aliyekituhumu moja kwa moja Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa kinapokea fedha kutoka nje ili nchi isitawalike.
Kwa hiyo, Membe ameendeleza upotoshaji na kulialia kama katika hotuba ya Rais Kikwete, kauli za Waziri mkuu Mizengo Pinda katika ziara ya mkoani Kagera; Waziri Steven Wassira na katibu wa uenezi, John Chiligati.
Badala ya kujibu hoja, wameona njia inayofaa ni kujaza hofu watu, kutisha, kudanganya, kuzusha kuwa CHADEMA inataka nchi isitawalike.
Tujiulize, tangu lini kupokea fedha kutoka nje ni hatari kwa usalama wa nchi? Kama hivyo ndivyo, Membe aeleze hatari ya serikali ya Tanzania kupokea misaada kutoka kwa wahisani au wafadhili wa nje.
Mbona katika bajeti ya serikali kati ya asilimia 35-40 ya fedha zake zinatoka nje—Benki ya Dunia (WB), Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)? Nchi kama Uingereza, Uswisi, Ubelgiji, Uholanzi, Marekani ndizo hufadhili pia vyama vya siasa na asasi zisizo za kiserikali (NGO’s).
Je, si kweli kwamba CHADEMA inawaumbua viongozi wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ufujaji na wizi wa fedha za misaada? Rada na ndege ya rais vyote vimenunuliwa kwa bei ya ‘kuruka’, halafu wakabuni mikataba ya kifisadi kama ya Richmond/ Dowans.
Wakati serikali inaziita nchi wahisani kuwa ni marafiki wa maendeleo, vyama vya siasa vinaziita nchi hizo kuwa marafiki wa demokrasia. Mbona haikuwa nongwa CCM kupokea fedha kutoka chama cha kikomunisti cha China?
Inajulikana, marafiki wakubwa wa CHADEMA ni chama cha Conservative cha Uingereza. Hata wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana CCM walikuwa wanadai CHADEMA imetumia vibaya misaada ya marafiki zao hao.
Wamekuwa kama Muamar Gaddafi. Ulipoibuka uasi alidai ni Marekani lakini baadaye akasema ni al-Qaeda. Watu waamini vipi?
Upotoshaji huu unafanywa kwa makusudi na serikali ya CCM iliyochoka ambayo Membe anaungana kuficha ukweli kwamba serikali hiyo inatumikia mafisadi kwa sababu inapata fedha za kifisadi.
Serikali ya CCM ndiyo imetetea makada waliovimbiwa fedha za rushwa hadi wakaenda kuziweka kwenye mabenki ya nje.
Badala ya kujibu hoja, serikali ya CCM imejiingiza katika uzushi na vitisho vya kutumia dola kuzima elimu ya uraia inayotolewa na CHADEMA na sasa NCCR-Mageuzi kuhusu udhalimu wa serikali hii.
Tujiulize, nani alifukia watu wakiwa hai katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu mwaka 1996 ni CHADEMA au mwekezaji kwa msaada wa serikali? Nani amesababisha maelfu ya vijana kukosa ajira baada ya kuporwa maeneo ya kuchimba madini Nzega, North Mara na Bulyanhulu ni CHADEMA au serikali?
Vitabu vya Mungu vinasema alaaniwe mwenye kuabudi mafisadi, mwenye kuabudu fedha, mwenye kupunguza mipaka ya ardhi ya watu wengine. Yuda alimsaliti Yesu kwa sababu ya vipande vya fedha akalaaniwa akajiua, vipi serikali? Hata kama serikali itatumia dola kupiga watu, kuwatia ndani kwa madai ya uchochezi, kuwazushia uongo, ukweli utabaki serikali ya CCM wanayotumikia Sofia, Membe iko kwenye kwapa la mafisadi.
 
Hivi ikulu imebinafsishwa? mbona tetesi zinasema Membe ni mtoto wa nje wa Khalfani Mrisho? anyway hakuna tatizo upanga tunao watanzania, tuamua nani atakuwa nani 2015
 
"Rais mtarajiwa"
nani kasema membe ni rais mtarajiwa? mimi siku zote huwa nasema ccm hakuna m2 yeyote anayefa kuwa rais 2015 hata kama ni mwadilifu kwani ccm ni mfumo na co mtu. kwa ufupi ni kwamba ccm haifai kungoza nchi so hakuna haja ya kumwita yeyote kutoka ccm rais mtarajiwa
 
Hivi ikulu imebinafsishwa? mbona tetesi zinasema Membe ni mtoto wa nje wa Khalfani Mrisho? anyway hakuna tatizo upanga tunao watanzania, tuamua nani atakuwa nani 2015

Lakini kweli eh, Membe na Jakaya wamefanana sana.
 
Hivi hawa CCM wanasoma alama za nyakati kweli? Hivi kwa kupitia hizo pesa wanazodai zinatolewa na wafadhili kwa chadema kuvuruga amani ya nchi, kuna mwandamanaji yeyote aliyepewa hata nauli ya kushiriki maandamano?
Je, kuna mwandamanaji yeyote aliyepewa hata chakula au kinywaji na chadema?

CCM watambue kuwa watanzania wamechoka na utawala wa kidhalimu wa viongozi wake. Tunataka mabadiliko ya kweli, 2015 ni peopleeeeeeeeeeezzzzzzzzz!!!!!!!!.
 
Hivi ikulu imebinafsishwa? mbona tetesi zinasema Membe ni mtoto wa nje wa Khalfani Mrisho? anyway hakuna tatizo upanga tunao watanzania, tuamua nani atakuwa nani 2015

yaani alivyofanana na jk copyright, wapimwe DNA.
 
Ukiona watu wanamutaja Membe kuwa rais mtarajiwa ujue CCM imebaki kopo bovu tupu linalovuma. Yaani Membe? Kwa kitu gani special alichowahi kukifanya kwa nchi kuonyesha anastahili urais? Nusra tu nchi aigeuze kuwa ya kidini kama asingekomaliwa na watu watanzania wenye maono.
 
Back
Top Bottom