CHADEMA ilipotosha umma taarifa ya Membe?

Chadema wamezoea sana kuzidisha na kupotosha umma. hao hao walidanganya kuwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga amefariki, na hao hao tena jana tu wamezua kuwa magufuri kajiuzulu. Na kesho watasema mengine.

hakika Chama hiki kimejaa wanafiki na waongo wakubwa sana katika kutaka kuleta balaa nchini.

hapo kwenye red inaonyesha uwezo wako wa kuelewa ni mdogo na ni mpotoshaji,.dr slaa alisema kuwa na nanukuu"nimepata taarifa zisizothibitishwa kuwa mkuu wa mkoa wa shinyanga amefariki,kama ni kweli,kama ni kweli amefariki maana sijazithibitisha basi apumzike kwa amani maana jana nilimsema kwenye mkutano"..kifo walichokizusha CDM hapo ni kipi au uelewa wa ccm ni mdogo??
 
hapo kwenye red inaonyesha uwezo wako wa kuelewa ni mdogo na ni mpotoshaji,.dr slaa alisema kuwa na nanukuu"nimepata taarifa zisizothibitishwa kuwa mkuu wa mkoa wa shinyanga amefariki,kama ni kweli,kama ni kweli amefariki maana sijazithibitisha basi apumzike kwa amani maana jana nilimsema kwenye mkutano"..kifo walichokizusha CDM hapo ni kipi au uelewa wa ccm ni mdogo??

leta source acha unafiki hapa
 
Hawa jamaa kweli wamechanganyikiwa. Tulimshuhudia wenyewe kwenye Kioo Mheshimiwa Membe akisema kuwa wana taarifa kuwa kuna nchi moja ya magharaibi inafadhili chama kimoja cha siasa nchini ili kuleta machafuko.
CDM wametaka Membe ataje hizo Nchi zinazotuhumiwa kufadhili machafuko. Tatizo liko wapi?
Huwezi ukaamka tu na kudai kuwa kuna tuhuma ya baadhi ya nchi za magharibi kufadhili machafuko bila kutaja nchi zenyewe. Kama ulikuwa unataka kufanya uchunguzi kwanza UNGEKAA KIMYA na kufanya uchunguzi wako kimya kimya kabla hujazomoka hadharani.
Ilichotaka CDM ni Membe kutoa ufafanuzi wa hizo nchi zinazosemekana kufadhili machafuko. Upotoshaji uko wapi hapo??
Na mbona hawakuzungumzia kauli ya Mheshimiwa Sophia Simba ambaye aliitaja wazi CDM? Ama na yeye atamtuma Katibu Mkuu wa Wizara yake kuja kumfutia makosa?? Ama kweli Serikali hii kila sasa mtu na lwake!!!

Tatizo Runinga zetu tumezielekeza kwenye kucheza Bongo Fleva zaidi kuliko kuwaumbua watu ambao wamezoea kusema kwamba wamenukuliwa vibaya. Mimi nilitarajia Runinga zetu wakati zinarusha hatari ya huyu Katibu Mkuu aliyetumwa kukanusha zingekuwa zinaingiza video clips za Membe wakati akiongea na Waandishi wa habari. Tukifanya hivyo Watu wataona aibu ya kwenye kukanusha habari kwa kusema uongo tena.
 
acha kuzungusha visivyozungushika wewe.. kama kauambia uma kuna chama kinafadhiliwa manake anajua na ana vidhibitisho vyote

huwezi ukaongea hadharani wakati ni tetesi,, atuambie ni chama gani hicho

Huo sasa ni ujinga. kwani tetesi haziwezi kuzungumzwa kwamba ni tetesi. Yeye alijibu swali aliloulizwa kama ana taarifa na sms zinazozunguka mjini kuhusu chama fulani kufadhiliwa na balozi fulani na yeye moja kwa moja akasema anazo taarifa hizo na zimewasilishwa kwenye vyombo vya uchunguzi na taarifa zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika. Sasa mlitaka asema hana taarifa hata kama anazo? Mlitaka ataje chama wakati bado uchunguzi haujafanyika? Mtu makini hawezi kuwa muongo kwa kukanusha uvumi aliousikia eti kwa sababu tu ya kutaka asionekane ni mbaya. Hivi katika vyama vyote zaidi ya 18 kwa nini CDM wafikirie kwamba ni wao ndiyo wanalengwa.

Suala la kwamba Sophia Simba aliwataja haliwezi kuwa sababu ya CDM ku-react kwa jazba katika taarifa ya Membe maana hawa ni watu wawili tofauti na wala Membe hakuwa anamsemema Sophia na wala hakuwa anasahihisha au kufafanua statement ya Sophia. Ni umbumbumbu kuunganisha aliyoongea mtu mwingine na statement ya Membe kuhusu kama ana taarifa za uvumi au la. Hivi nyie mnaokosoa mtu kuuzungumzia uvumi mbona ndiyo mahodari wa uvumi. Jana mmezua la Magufuli na huko nyuma mkazua la Balele. Sababu za uvumi huo ni chuki zenu kwao na si vinginevyo. Halafu leo mnatoa wapi moral authority ya kuukemea uvumi? Tena bora Membe angekuwa ndiye aliyezua uvumi huo. Hapo tungemhukumu lakini kwa vile sasa inafahamika kwamba ujumbe huo wa kwenye simu ulikuwa umeenea hapa nchini kuan tatizo gani kama Membe naye ulimfikia kama ulivyowafikia wengine?

Kwa watu wanaotafakari na kuchambua sawasawa, wale wanaoshutumu walitakiwa kumpongeza Membe kwa kuamua kuwasilisha tetesi hizo kwa vyombo vyenye mamlaka na uwezo wa kuchunguza ili kujua ukweli au uongo wake. Kwa vyovyote vile, maamuzi yatayotegemea matokeo ya uchunguzi huo yatakuwa ni maamuzi ya haki na yaliyo na uhalali wa taratibu, badala ya kutolea maamuzi tuhuma zisizo na ushahidi. Halafu humu ndani sasa hivi kila mtu anayejaribu kufanya jambo anatafsiriwa tofauti. Likiwa baya basi huyo ni CCM na likiwa zuri basi hizo ni kampeni za 2015. Huu ni ufinyu ambao unatakiwa utazamwe upya!
 
Hivi cdm walipotosha kitu gani! TBC1 walimrekodi akisema juu ya chama kuadhiliwa na nchi za kigeni ikiwa i mwendelezo wa kile alichokisema waziri mwenzake SS ch10, ndugu usiongozwe na tumbo ukakiacha kichwa chako kimelala
 
sasa kama hakutaja chama nyie mlitakaje? membe kama mwanadiplomasia aliyebobea hawezi kumention jina la chama publically na cdm hawana audacity ya kumfanya ataje jina la chama! wanausalama wanalifanyia kazi hilo na hatua zitchukuliwa! cdm walipasawa wapambane na bi sophia simba aliyewataja hadharani

Ndugu yangu hawa ni kama mtu ambaye amejiandaa kupigana hata kama hajachokozwa. Walijiandaa tu kupambana pengine kwa kujua kwamba wao ndiyo wanufaika na kwamba labda wameshtukiwa kumbe Membe wala hajui hicho chama na wala hajui huo ubalozi, zaidi tu ya huo uvumi wa hao wanaosambaza. Wanachofanya CDM ni kama mtu ambaye amekaa baa na wenzie halafu mmoja wao nasema ghafla kwamba Polisi huyo anakuja! Halafu mtu huyo anatimua mbio. Conclusion hapo ni kwamba huyu bwana ni mhalifu na Polisi yulle anatakiwa kuchukua hatua za kumchunguza mtimua mbio huyo!
 
Chadema wamezoea sana kuzidisha na kupotosha umma. hao hao walidanganya kuwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga amefariki, na hao hao tena jana tu wamezua kuwa magufuri kajiuzulu. Na kesho watasema mengine.

hakika Chama hiki kimejaa wanafiki na waongo wakubwa sana katika kutaka kuleta balaa nchini.

Balaa iliyopo haitoshi kwa sababu imeletwa na CCM. Afadhali balaa nyingine ije isiyo ya CCM. Ya magufuli yanawahusu nini CDM mimi nadhani ni mgongano ndani ya uongozi wa utawala wa CCM. Na hizo siyo balaa.
 
umeona eeh? Sijui source yao ya habari huwa ni ipi? Slaa kipindi cha uchaguzi ashawahi kuzusha kuna contena lenye shahada za kupigia kura limekamatwa mahali,polisi kwenda wakakuta ni uzushi hakuna cha shahada wala nini! Hivi kwanini cdm wanamfeed kiongozi wao habari za uzushi? Hii inafanya watu kukosa imani nao

Hivi ni Chadema pia waliowazushia CUF kuwa ni chama cha kidini na kilihusika kuleta makonteina ya majambia huko visiwani? Ni Chadema waliomzushia Mrema kuwa amezaa na mwanamke nje ya ndoa wakati ule anagombea urais? Ni Chadema pia waliozusha kuwa ifikapo mwaka 2010 kila Mtanzania atakuwa na maisha bora? Kwamba mgao wa umeme utakuwa historia Tanzania? Ni Chadema waliozusha kuwa kuchagua upinzani ni kusababisha umwagaji damu? Kwamba kuandamana ni kuleta machafuko nchini na hayo machafuko yako wapi?
 
Japo kuna uhuru wa kila raia kutoa maoni yake,, napata tabu pale watu wanapokuwa biased. Mwanajamvi mmoja alipata kunena kwamba "ushabiki wa kufumba macho na kusema ndio kwa kila kitu kinacho husu chadema" wa baadhi ya wana JF hapa ni utumwa mkubwa sana ambao inabidi kuuepuka! Huu unaoitwa "uanachama damu,chadema damu,ccm damu" ni utumwa wa ajabu maana una kuzuia hata kuuliza kitu pale unapo ona hakiendi vyema! Kama CDM walipotosha,, ieleweke hivyo na wakiri makosa badala ya kuendelea kung'ang'ania ubishi. Wengi tulihoji kwamba ni wapi Mh. Membe alipotaja CDM? Kuna vyama vingapi vya upinzani nchini? Mbona wengine hawakukurupuka kama CDM? Nadhani Mh. Membe anastahili kuombwa radhi na CDM.

Nilichogundua ni kwamba humu jamvini ukionyesha kukosoa tu baadhi ya wale wanaojiona ni wanazi wa chadema basi wewe unakuwa very unpopular. Sasa kama tunawakemea akina Tambwe Hizza na wengine walio CCM kwa kutetea kila kitu cha CCM, hata ambacho hakifai, ni dhahiri kwamba hata hawa wa chadema wanaodhani na kuhisi kwamba chama chao hakistahili kukosolewa kwa lolote na sawa na Hizza Tambwe na wenzake. Sasa ni bayana kwamba Mh. Membe amesingiziwa na anatakiwa kuombwa radhi. Hata hivyo mkuu Salimia, hawa jamaa hawana ustaarabu huo na hilo tusilitarajie. Hiyo ndiyo fanatical support ambayo ina-impair reasoning. Mtu wa namna hiyo haamini katika mabaya ya kile anachokiamini na kukipenda, na huo ni umbumbumbu na ufinyu wa fikra.
 
Viongozi wa CCM akiwamo Sophia Simba na Lipumba ndio walioitaja Chadema moja kwa moja na maswali ya waandishi yalilenga kwa Waziri Mhusika na Mambo ya Nje kutaka kujua kama ni sahihi kwa viongozi wa serikali kama Sophia Simba kuzungumzia mataifa ya nje kufadhili machafuko kupitia chama cha siasa alichokitaja, sasa Membe kwa kuwa aliyesema ni Waziri asingeweza kusema Waziri mwenzangu ni mwongo, bali alijibu kidiplomasia kwamba tutachunguza na ikithibitika tutatumia mikataba ya kimataifa kulishughulikia. Kwa upande wa Chadema kama chama cha siasa ambacho ndicho kunahusishwa na vurugu (rejea hotuba ya Rais) ndio wanaoamini (ni kweli) kwamba walengwa ni wao na hivyo kumtaka Waziri MWenye dhamana na mambo ya nje, ambaye ni Membe kutaja chama na nchi maana wanamuona Sophia Simba, kama mropokaji ambaye maneno yake hayawezi kubeba uzito unaostahili. Kwa mantiki hiyo, Membe hajakosea (Kwa maoni yangu) kwa kuwa yuko serikalini (Ambayo JK ni bosi wake na Sophia ni mwenzake) na Chadema nao hawajakosea maana ni chama cha siasa ambacho kimeonyesha kupambana hadi kuonekana kama chama cha fujo (kama ilivyokuwa CUF enzi zake).

SIjaelewa hapo, Lipumba ni kiongozi wa CCM?
 
Kwani CHADEMA walichisema ni nini? Wao walisema akitaje hicho chama na awataje hao wafadhili, basi! Shida hofu imewashika hasa baada ya Mama Simba kukurupuka na sasa mnatoa kauli zisizo na kichwa wala mkia. Umeita waandishi wa habari ukasema kuna chama kinafadhiliwa na balozi, basi watu watataka ufafanuzi na balozi zitataka ufafanuzi. Balozi zimeinuka juu na vile kabajeti ketu ni tembeza bakuli basi serikali imehaha. Semeni sasa!

Nadhani Maishamapya alikuwa Loliondo ambako hata TV huwa ni shida. Yeye hakuita press conference kuzungumzia trivial issues kama hizo. This question came just by the way na akalijibu kwa usahihi kabisa na kama anavyofahamu yeye kwamba uvumi huo upo na anasubiri kuona kama utathibitishwa au la na vyombo husika. Kama umekasirishwa na unadhani chama chenu ndiyo kimelengwa so be it, lakini hilo halimo kwenye kauli ya Membe!
 
Wewe na Membe wote mna matatizo makubwa sana, Membe ni Decision Maker au hajui kazi yake? yaani CCM kila mtu hajui kazi aliyopewa sasa nchni mnaingoza vipi kwa nusu kibaba.

kitu chochote kinafika katika meza ya Decision Maker baada ya kufanyiwa uchambuzi na kuainisha chuya na Mchele ili Decision Maker afanye Decision sahihi, unataka kutwambia Membe ni mtoa Taarifa wa Vyombo vya Dola! unataka tuamini hivyo?! Kama unataka tuamini kuwa Membe siyo Decision Maker bali Mtoa taarifa kwa vyombo vya Dola je njia aliyotumia kuwapa taarifa vyombo vya Dola ndio njia sahihi kulingana na Upeo wako wewe na Membe?

Both are craps na nisingetegemea Kiongozi tena Waziri kutokujua majukumu yake kiasi hiki, angalia alafu twambie: -

  1. Kama Membe ni Waziri basi ni Decision Maker, maana yake jambo lolote linamfikia katika hatua ya mwisho kabisa ili kufanyike maamuzi kutoka na uchambuzi uliofanywa na wataalam wa Serikalini, kwa swala hili alipaswa kujitokeza kuongea baaada ya kupata taarifa sahihi kutoka katika vyombo vyote na hapo kama Decision Maker alikuwa anakuja kutoa maamuzi juu ya hili jambo na jinsi walivyolifanyia kazi na ushahidi uliopo na nini Serikali imeamu yaani Msimamo wa Serikali.


  1. [*]Hili la pili unalotaka tuamini "Ashakum si Matusi" ni Upuuzi zaidi na inamdhalilisha zaidi; kuwa aliitisha waandishi wahabari kuwapa taarifa vyombo vya dola juu ya kuwepo kwa Chama kinachofadhiriwa ili kuvuruga amani ya nchni yetu, sasa vyombo vya dola upewa taarifa kwa njia ya "Press Conference?" inakuwaje waziri hajui njia sahihi ya kuwapa taarifa vyombo vya dola! huoni hajui lolote!

A mega crap!
 
mijitu mingine (Kashaga et al) probably brains zao zipo mata..ni au nyayoni!! Hivi Waziri mzito kama Membe anapotoa statement yenye kutuhumu nzito kama hiyo ambayo ina-hang kwamba "kuna chama cha siasa nchini kinafadhiliwa na nchi fulani za magharibi ili kilete ghasia nchini", wewe Kashoga (ooohps sorry nilikusudia Kashaga kama mtanzania hupendi kujua inside out ya hizo tuhuma? Yaani huhitaji kujua ni chama gani na nchi gani zinazungumziwa na such senior government official? Nafikiri tuwaunge mkono CDM wanaotaka kujua nchi gani na chama gani wanaotaka kuleta ghasia nchini.
 
chadema wamezoea sana kuzidisha na kupotosha umma. Hao hao walidanganya kuwa mkuu wa mkoa shinyanga amefariki, na hao hao tena jana tu wamezua kuwa magufuri kajiuzulu. Na kesho watasema mengine.

Hakika chama hiki kimejaa wanafiki na waongo wakubwa sana katika kutaka kuleta balaa nchini.
mkweli wako wewe ni yupi? Ccm?
 
Atajitetea mahakamani na kama akionekana hana hatia ndio aje na huo utetezi. Jk anazunguka dunia kuomba misaada lakini hamseni nchi zinazosaidia zinataka kuvuruga amani, iweje leo chadema wasaidiwe mseme wanavuruga amani. Mbona CCM inasaidiwa na wahindi wanaoiba hela za serikali hiyohiyo lakini hawapelekwi kwenye vyombo vya sheria??
 
Chadema wamezoea sana kuzidisha na kupotosha umma. hao hao walidanganya kuwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga amefariki, na hao hao tena jana tu wamezua kuwa magufuri kajiuzulu. Na kesho watasema mengine.

hakika Chama hiki kimejaa wanafiki na waongo wakubwa sana katika kutaka kuleta balaa nchini.

shikamo mkubwa! Nakupa heshima yako ila wakati ukiandika kitu usidandie kwa mbele.
Hv a gud time
 
unajua mkuu kuna msemo unaosema'ukirusha jiwe gizani atakayesema yalaaah ujue limempata" Membe hakutaja chama sasa kwnini cdm wakurupuke?? kwanini TLP,DP ama SAU wasilalamike? au wanajihisi nini? mwaka huu wataglue kweli

Membe ni mnafiki kama anajiamaini kwanini hakukitaja Chama matokeo yake anaongea mafumbo kama wanawake wa Uswahilini napata wasiwasi na uelewa wa wana CCM mbona wanakua na mambo ya umbea umbea mbona CDM huwa wanasema kila kitu bila kumeza maneno kinachowashinda CCM ni nini? Wamepoteza thamani mbele za watanzania matokeo yake kila mtu anakurupuka na kua msemaji wa Chama na wendawazimu kama nyinyi mmekodiwa kuja hapa na kuleta upuuzi wenu, ushauri wangu: usifanye kitu hata ambacho moyo wako hautaki hapa unajilazimisha kuongea upupu na kupindisha ukweli wakati moyo wako unakusuta.
 
Back
Top Bottom