CHADEMA iko tayari kuongoza?

Saa nyingine ukiwa kijijini hata magazeti ya Dar Leo na Alasiri si rahisi kuyapata labda kwa Kibonde au RFA........ Wale walio Kigoma, Tarime na Karatu mtuambie mambo ya chadema huku......... ila la nchi na uwezo wa kuongoza tujadili. Hata sisi Chadema tunapenda kujadili......... Ila usituhukumu maana hatujapewa kukashindwa.......
 
Moja kati ya Majukumu ya Chama kinachopewa ridhaa na wananchi ya kutawala ni Kukusanya kodi na Kusimamia raslimali ( watu na vitu) na kuhakikisha kwamba kodi zinazokusanywa na raslimali hizo zinatumika katika kumletea maendeleo yule aliyetoa dhamana ya uongozi ( yaani mwananchi), kwamba kodi na raslimali hizo zitumike katika kuboresha huduma za Kijamiii ( Kama Afya, Elimu, Maji nk) kiuchumi na kisiasa vilevile. Sasa tangia Uhuru haya Majukumu watanzania wamekuwa wakiwakabidhi CCM

Sasa moja kati ya Majukumu ya vyama vilivyo nje ya Serikali ( CUF, TLP, CHADEMA) ni kuhakikisha kuhakikisha kwamba Serikali iliyo madarakani inatumia kodi na raslimali itakikanavyo ( Ingawa hii ni kazi ya Bunge lakini vyama vilivyo nje serikali vinawajibika kwalo). Vile vile ni wajibu kwa Vyama hivyo kuonyesha Uongozi Mbadala pale vinapopata Fursa sasa ni vyema tukaangalia katika yale maeneo ambapo vyama hivi vimepata fursa ya kuongoza vimefanya nini tofauti ya CCM ( in apositive way?

Tuipime CHADEMA kwa halmashauri ilizofanikiwa kuongoza na tuipime CUF kwa halmashauri ilizopata fursa kuziongoza, tufanye hivyo pasipo kuegemea misimamo yetu ya kivyama

Asante

Ndege ya uchumi umenena kabisa. Lakini sasa kwa hali inavyoelekea ni vigumu kwa CCJ kushiriki uchaguzi sasa nafikiri ni wakati muafaka kukawa na mazungumzo ya kuelewana kwani vinginevyo tutakuwa watu wakulalamika kila siku wakati CCM inazidi kuboronga na kufuja mali zetu. Ni wajibu wa viongozi wa vyama kama kweli wanayo nia ya dhati kuliokoa taifa letu wawe kitu kimoja na kuing'oa madarakani CCM katika makubaliano ambayo wataafikiana kwa faida ya nchi dhidi ya kugawa kura kila uchaguzi unapofanyika.
 
Kama nilivyouliza huko nyuma ni mambo gani Chadema wamefanya kustahili kuongoza leo naomba nidokeza swali hili ambalo ni muhimu.

this sounds fishy! Ivi argument hii haikutumika na republicans against Obama?...hahahaha! How was Obama ready then? kazi kweli kweli! ungeniambia kuna degree ya kuwa rais sawa...lakini kuweka requirements on what one has done...si ina maana CCM watabaki hapo forever. Lets cut the BS...Chadema can lead, and maybe CCJ also can...that is if they came out open and identified themselves!
 
Tunasukumiziwa katika makoo yetu chama kimoja tu kuwa ndicho pekee chafaa kuungwa mkono katika kuiangusha CCM. Tunaambiwa vyama vingine viungane nacho kwa sababu kimeonesha uongozi na kuwa ndiyo "upinzani" wa kweli. Wapo watu wanaoamini kabisa jambo hili. Wanaamini kuwa CHADEMA ndicho chama hasa mbadala kinachoweza kuchukua uongozi wa taifa letu toka mikononi mwa CCM.

Kama nilivyouliza huko nyuma ni mambo gani Chadema wamefanya kustahili kuongoza leo naomba nidokeza swali hili ambalo ni muhimu.

Je Chadema ilivyo sasa iko tayari kuongoza taifa la watu milioni 40 kwa ubora na kwa maono bora zaidi na mfano mzuri wa kiuongozi katika ngazi zote kuliko CCM? Ni nini msingi wa imani ya wale wanaoona kuwa iko tayari?

Mwenyewe ni na maoni yangu.. naomba nisikie ya kwenu.

Ukiwa makini utaona swali linahusu Chadema na utayari wao kuongoza.. nje ya hapo ni red herring.

Hii ni manefestation ya beast kwenye solomon temple "I hate Chadema"

Kwanza nakushukuru kwa kuwa umeamua kusema kilicho rohoni mwako. Wengi huwa hili litushinda na ni lazima nikupe hongera kwa ujasiri wako uliouonesha kwa miaka yote hii.

Wengi wa watu huwa wanadhani kuwa chama kingine kikichukua nchi basi kila uongozi wote unaondoka, jamani hili si kweli ccm hapendi watu wafahamu hili na mwanakijiji kwa sababu zake anazojua hataki watu wajue hili. Chadema inaweza kuchukua nchi hii na ikafanya mabadiriko ya watu wacchache sana na ambao ni wale wenye post za kisiasa ndiyo wanweza kubadirika. Tunajua kuwa kuwa lazima mawaziri na manaibu watabadirika na viongozi wa juu ni lazima wabadirike. waziri mkuu kama Chadema wakiwa hawana majority(2/3) itabidi wafanye compromise.

Makatibu wakuu, madirector na wafanyakazi wengine hao ni civil servant hawa hawaja ajiriwa na vyama hao wataendelea kubaki kwenye kazi zao. Chama kipya kinaweza kubadiri hata watu 30 tu na kutengeneza serikali mpya kama kikiona kuwa watu wanafaa ( wakuu wa mikoa na wilaya unaweza ukawaacha au ukawabadirisha taratibu sio lazima kubadiri kwa mpigo kama ccm wanavyofanya au mwanakijiji anavyotaka kuitumia ka tishio). Kikiona watu hawafai basi kinaweza kubadiri na hii inaweza kuwa by natural waste au wengine by voluntary redundacy. lakini pia kinaweza kuwashawishi watu wenye nia njema na nchi kuweza kujoin Gov na mifano iko mingi. Stop scare people jamani.

Haya ngoja turudi kwenye Uongozi, wewe si unajua kuwa karatu kama sio malecela sasa hivi kila nyumba ingekuwa na bomba la maji? Moshi kwa umakini tu wa chedaema huoni jinsi inavyosonga mbele?

Nasema kuwa chadema iko tayri kuongoza tanzania na watu wake million arobaini hata sasa hivi. Kuongoza siyo kubadiri kila kitu ila ni kutumia vit vilivyopo kwa manufaa ya wengi na chadema hilo wanalijua na wamesha onesha. Ungekuwa uko tanzania ungeweza kujionea mwenyewe njisi ambavyo wabunge wa Chadema wakisimama kuongea wabunge wa ccm wanavyotulia na kuwa makini bila kusahau kukunja uso. Wanawaheshimu kuliko hata viongozi wao. uko wapi wewe!
 
Jibu la swali hilo lipo kwenye matamshi ya Muasisi wa Chadema Mzee Edwin Mtei...

" amewataka viongozi wa Chama cha Jamii (CCJ), kuhamia Chadema, ili wawe katika nafasi mzuri ya kuendeleza upinzani wa kweli hasa kama chama hicho hakitapata usajili wa kudumu ndani ya mwaka huu.Mtei alitoa rai hiyo jana alipokuwa akizungumza na Gazeti la Mwananchi" kwa matamsha ya muasisi yanatupa picha ya kisakolojia ya Chadema na vyama vinginekwa kuelekea uchaguzi ujao 2010. Kwa sasa Mtei anaona role ya Chadema ni kutoa Upinzani wa kweli

Itakuwa ni maajabu kwa kipindi kifupi endapo CCJ ambayo matumaini yake makubwa ni CCM-B itaweza kuchukua serikali ktk uchaguzi huu 2010! Na kutoka CCM tusitarajie mabadiliko ya kweli hapa napingana matamshi ya Mwl J. Nyerere... nitumie mfano wake mwenyewe kwa CCM! Generation ya wanasiasa CCM na siasa za "clique" ni kama simba aliyeonja nyama ya mtu, wakihamia CCJ wataendeleza tabia zao... hayo tumeyaona kwa jirani zetu Kenya NARC na FORD O, FORD K...

Chadema ni mwanzo mzuri ni chama serious..., kinamapungufu, tujifunze kutokana na vyama vilivyopata mafanikio nchi nyingine kama vile ANC; kujisahihisha na kubadilika. Kama Chadema ni strong northern zone hiyo siyo ukabila au dhambi ila basi zifanyike juhudi kufanya popular south pia na penginepo, pengine hata kufanya mazumngumzo na CUF kuunganisha vyama kuunda chama kitakachukua tayari kuchukua serikali na kuondoa dhana potofu ya ukabila au udini. Hivyo ndivyo siasa zinavyofanywa pengine duniani...

Tahadhari kubwa kwa Chadema ni mapandikizi ya CCM kama walivyofanya kwa NCCR-Mageuzi. Mrema, Marando, Bagenda Mbatia na wenzake
 
Tunasukumiziwa katika makoo yetu chama kimoja tu kuwa ndicho pekee chafaa kuungwa mkono katika kuiangusha CCM. Tunaambiwa vyama vingine viungane nacho kwa sababu kimeonesha uongozi na kuwa ndiyo "upinzani" wa kweli. Wapo watu wanaoamini kabisa jambo hili. Wanaamini kuwa CHADEMA ndicho chama hasa mbadala kinachoweza kuchukua uongozi wa taifa letu toka mikononi mwa CCM.

Kama nilivyouliza huko nyuma ni mambo gani Chadema wamefanya kustahili kuongoza leo naomba nidokeza swali hili ambalo ni muhimu.

Je Chadema ilivyo sasa iko tayari kuongoza taifa la watu milioni 40 kwa ubora na kwa maono bora zaidi na mfano mzuri wa kiuongozi katika ngazi zote kuliko CCM? Ni nini msingi wa imani ya wale wanaoona kuwa iko tayari?

Mwenyewe ni na maoni yangu.. naomba nisikie ya kwenu.

Ukiwa makini utaona swali linahusu Chadema na utayari wao kuongoza.. nje ya hapo ni red herring.
CHADEMA wamefanya mengi kuliko CCM kwa nafasi yao..
(1) Mapamba dhidi ya UFISADI mzizi wake ni CHADEMA---reffer the list of shame by Dr. Slaa at Mwembe yanga...na hata hao wanaopelekwa mahakamani kwa kuzuga wapo kwenye ile list, thats is to say CHADEMAis against Corruption as compared to CCM.
(2)Reffer to Hoja za wabunge kama Dr. Slaa, Zitto (ingwa siku hizi simuelewi elewi) ambazo kimsingi ndo zimeibua mijadala mingi bungeni amabayo wabunge wa CCM hwana ujasiri hata wa kuizungumzia na familia yao.
(3) Chadema ni wavumilivu (political tolerant party)...reffer rafu walizochezewa Busanda na Kwa Marehemu Wangwe.
(4)CCM wamepoteza sifa za kuongoza nchi..so chama mbadala kwa Tanganyika ni CHADEMA

Mwisho kabisa wito wangu kwa brother MM
Kaka mi skuelewi kabisa..we una support CCJ,imefanya nini hadi kustahili sifa ya kuongoza nchi????si unaona madudu waliyofanya kwenye kuhakiki wanacha (labda ni fitna za CCM,me sijui,ila tutaona).
---->Sitaki kufikiria kuwa MM nawe unatumiwa kuua upinzani,.
 
Tunasukumiziwa katika makoo yetu chama kimoja tu kuwa ndicho pekee chafaa kuungwa mkono katika kuiangusha CCM. Tunaambiwa vyama vingine viungane nacho kwa sababu kimeonesha uongozi na kuwa ndiyo "upinzani" wa kweli. Wapo watu wanaoamini kabisa jambo hili. Wanaamini kuwa CHADEMA ndicho chama hasa mbadala kinachoweza kuchukua uongozi wa taifa letu toka mikononi mwa CCM.

Kama nilivyouliza huko nyuma ni mambo gani Chadema wamefanya kustahili kuongoza leo naomba nidokeza swali hili ambalo ni muhimu.

Je Chadema ilivyo sasa iko tayari kuongoza taifa la watu milioni 40 kwa ubora na kwa maono bora zaidi na mfano mzuri wa kiuongozi katika ngazi zote kuliko CCM? Ni nini msingi wa imani ya wale wanaoona kuwa iko tayari?

Mwenyewe ni na maoni yangu.. naomba nisikie ya kwenu.

Ukiwa makini utaona swali linahusu Chadema na utayari wao kuongoza.. nje ya hapo ni red herring.
Kuondoa aina ya utawala/uongozi uliopo si kuchomoa na kuchomeka just like that. Ni mchakato.
-unganeni au kuweni na nia moja ya kumuondoa huyo mnayetaka kumuondoa
-kisha muondoeni
-halafu tengenezeni kitu kipya (kizuri of course) kwenda mbele
-baada ya hapo miongoni mwenu mtaanza kutambuana yupi pumba, yupi mchele (kwenye hatua hii inazaliwa shida kidogo, lakini mwisho wake ni kupatikana kitu bora zaidi)

Mkianza kwa kusemana wenyewe kwa wenyewe (hata kabla ya hayo mabadiliko mnayoyalilia hamjayapata), hakuna yoyote atakayekuja kujulikana kuwa anaweza, achilia mbali kule kuweza kwenyewe. Tutaishia maneno, maneno maneno. Ndiyo criticism yangu kwenye forum hii - we talk, talk, talk and talk! Basi. Hebu tuuvue u-CUF, u-CCJ, u-CHADEMA, u-DP, nk. Tuuvae UZALENDO badala yake. Tufanye kazi. Kwa vitendo. Si maneno! Tutaweza kuleta madiliko kwa jinsi hii. Basi.
 
Moja kati ya Majukumu ya Chama kinachopewa ridhaa na wananchi ya kutawala ni Kukusanya kodi na Kusimamia raslimali ( watu na vitu) na kuhakikisha kwamba kodi zinazokusanywa na raslimali hizo zinatumika katika kumletea maendeleo yule aliyetoa dhamana ya uongozi ( yaani mwananchi), kwamba kodi na raslimali hizo zitumike katika kuboresha huduma za Kijamiii ( Kama Afya, Elimu, Maji nk) kiuchumi na kisiasa vilevile. Sasa tangia Uhuru haya Majukumu watanzania wamekuwa wakiwakabidhi CCM

Sasa moja kati ya Majukumu ya vyama vilivyo nje ya Serikali ( CUF, TLP, CHADEMA) ni kuhakikisha kuhakikisha kwamba Serikali iliyo madarakani inatumia kodi na raslimali itakikanavyo ( Ingawa hii ni kazi ya Bunge lakini vyama vilivyo nje serikali vinawajibika kwalo). Vile vile ni wajibu kwa Vyama hivyo kuonyesha Uongozi Mbadala pale vinapopata Fursa sasa ni vyema tukaangalia katika yale maeneo ambapo vyama hivi vimepata fursa ya kuongoza vimefanya nini tofauti ya CCM ( in apositive way?

Tuipime CHADEMA kwa halmashauri ilizofanikiwa kuongoza na tuipime CUF kwa halmashauri ilizopata fursa kuziongoza, tufanye hivyo pasipo kuegemea misimamo yetu ya kivyama

NDIYO!
CHADEMA-Ni chama mbadala na kinaweza kuongoza nchi kama ilivyoanza TAA,TANU NA HATIMAYE CCM.
Tuwaunge mkono si wa kelele tuu bali wa matukio ya kweli kama kupata kadi za uanachama na kuingia kwenye vikao halali vya chama.
Aksanteni sana kwa fikra za maendeleo ya nchi yetu.
 
Tunasukumiziwa katika makoo yetu chama kimoja tu kuwa ndicho pekee chafaa kuungwa mkono katika kuiangusha CCM. Tunaambiwa vyama vingine viungane nacho kwa sababu kimeonesha uongozi na kuwa ndiyo "upinzani" wa kweli. Wapo watu wanaoamini kabisa jambo hili. Wanaamini kuwa CHADEMA ndicho chama hasa mbadala kinachoweza kuchukua uongozi wa taifa letu toka mikononi mwa CCM.

Kama nilivyouliza huko nyuma ni mambo gani Chadema wamefanya kustahili kuongoza leo naomba nidokeza swali hili ambalo ni muhimu.

Je Chadema ilivyo sasa iko tayari kuongoza taifa la watu milioni 40 kwa ubora na kwa maono bora zaidi na mfano mzuri wa kiuongozi katika ngazi zote kuliko CCM? Ni nini msingi wa imani ya wale wanaoona kuwa iko tayari?

Mwenyewe ni na maoni yangu.. naomba nisikie ya kwenu.

Ukiwa makini utaona swali linahusu Chadema na utayari wao kuongoza.. nje ya hapo ni red herring.

Kwa hakika CHADEMA inaweza na ipo tayari kuongoza. Kwa vyovyote vile haitakuwa CHADEMA peke yake na wala hakuna chama cha upinzani peke yake kinaweza kuleta mabadiliko katika Taifa letu na kuongoza DOLA bila mashaka. CHADEMA lazima ishirikiane na vyama vingine vya siasa, vikundi vya kijamii vinavyodai mabadiliko katika Taifa letu na watu wengine mmoja mmoja ambao wana maono ya nini Taifa linataka.

Kwa vyovyote vile CHADEMA inaihitaji sana CUF katika kuhakikisha tunashika dola vizuri. najua kuna watu watasema mbona tuliweza wenyewe Biharamulo na Busanda au hata Tarime. Mazingira ya by election ni tofauti sana na mazingira ya Uchaguzi Mkuu na ndio maana CUF waliweza pia peke yao TUNDURU. Sote tukafanya kinyume na matarajio Kiteto na Mbeya Vijijini.

Ugonjwa uliowapata NCCR-M mwaka 1995 kuwa wanaweza peke yao ndio huo huo uliowapata CUF mwaka 2000 mpaka mwaka 2005 na CHADEMA is vulnerable to that mwaka 2010. Hata hivyo, coalition ya Watanzania kwenye CHADEMA, CUF, NCCR-M nk na sasa hawa waliopo CCJ na hata watu safi waliopo CCM tunaweza kuivusha nchi katika mpito.

Kwa vyovyote vile ushindi wowote ule tutakaoupata kama opposition lazima uwe ni wa kulipitisha Taifa katika mpito ili kufanya mabadiliko makubwa ya mfumo wetu wa utawala na uongozi wa nchi. Mabadiliko ambayo hayatateteresha dola letu na hata Muungano wetu.

Kama CCJ walikuwa wanadhani watafanya peke yao inawezekana ndio changamoto wapatazo sasa. Nimeshtuka kweli kusoma mwananchi kuhusu uhakiki wa CCJ ambapo hata 'viongozi wao' wanatishia mashaka umakini wao kwa kukosea vitu vya kawaida kabisa. Kama kawaida wanakimbilia kusema CCM imewahujumu. Tatizo lile la kila siku la vyama vyetu kutoangalia changamoto za ndani na kukimbilia kulaumu (actually ni tatizo la watanzania wengi sana kutafuta 'mbuzi wa kafara'.

Nina imani kubwa kabisa kuwa CHADEMA kwa kushirikiana na vyama vingine wanaweza kushika, kuongoza na kuendeleza Dola yetu.
 
Ugonjwa uliowapata NCCR-M mwaka 1995 kuwa wanaweza peke yao ndio huo huo uliowapata CUF mwaka 2000 mpaka mwaka 2005 na CHADEMA is vulnerable to that mwaka 2010. Hata hivyo, coalition ya Watanzania kwenye CHADEMA, CUF, NCCR-M nk na sasa hawa waliopo CCJ na hata watu safi waliopo CCM tunaweza kuivusha nchi katika mpito
.

Ndugu Zitto, kama umesoma maoni yangu hapo juu nadhani utakubaliana nami kuwa tumeafikiana kwa points nyingi, lakini tunapopishana kimawazo ni kuhusu kungojea watu safi kutoka CCM... kama mpaka sasa hawana ujasiri wakuchukua uamuzi kujiunga nasi, bas wao wapo wakingojea maslahi yao binafsi, siamini kama hao ni safi. Pili nikujipanga (rear future leaders)... ni jambo ambalo Chadema inapaswa kulifanya kwa makusudi na uangalifu tena bila upendeleo au kung'ngania madaraka
 
Wenye hofu ya mabadiliko siku zote huchelewesha maendeleo...chadema wapo zaidi ya tayari kuongoza.
 
Vipimo tunavyoweza kutumia kuwapima CHADEMA ni kupitia viongozi wao tuliowachagua kuwa Wabunge wetu au madiwani wetu, pamoja na utekelezaji wa sera zake. Kwenye ishu ya ukabila sipo kabisa.

Sina data sana ila nadhani Dr. Slaa amefanya vizuri sana kwenye jimbo lake na amekuwa kiongozi mzuri sana kwenye kamati ya Bunge aliyomo. Ukimwangalia Zitto Kabwe nae kuna mambo mengi sana mazuri amewafanyia wananchi wa jimboni kwake, na amesaidia sana kwenye kamati ya madini (though at some point nilitofautiana nae kimtazamo). Halima Mdee nae amehangaika sana na kuwasaidia kina mama, watoto na vijana.

Ila nadhani bado wahitaji watu zaidi kuweza kuiongoza serikali, maana ukiangalia watendaji wazuri tunaowajua toka CHADEMA sidhani kama wanazidi kumi. Na hapo ndio umuhimu wa kuungana na vyama vingine vya upinzani unapokuja. Ila suala la kuungana linahitaji kukaa chini na kuanza kuangalia mwisho utakuaje tukishaunga - kimadaraka, kimtazamo(ilani), uteuzi wa wagombea, jinsi ya kuiongoza serikali etc.

All in all nna imani kiutendaji CHADEMA wanaweza kufanya mambo mazuri, ila angalizo langu nikuwa, sio lazima mtendaji mzuri kuwa kiongozi mzuri.
Kabengwe nakubaliana nawe. Chadema kama chama chochote ni lazima kipimwe kwa uwezo wao wakipata nafasi ama bungeni au kwenye halmashauri zao hadi sasa. Sasa ni wazi kuwa kwenye siasa za kitaifa Slaa na Kabwe wamejitahidi kuelimisha umma na kulitumikia bunge kwa ujasiri.
Lakini vilevile ni wazi kwangu (neutral) kuwa wanaupungufu wa viongozi kitaifa, na hii ni kwa vyama vyote vya upinzani Tz. Inasikitisha sana kuon kuwa wapinzani wotw hawafiki hata robo ya wabunge wote sasa hili ni tatizo. Na kwenye serikali za mitaa ndio mbaya zaidi.
Hivo basi kwa jinsi ilivo sasa sidhani kama Chadema wana uwezo wa kuongoza dola.
Nami siku zote nasema hawa viongozi wa upinzani wakae chini waone jinsi gani wanaweza kushirikiana kwenye uchaguzi ili waweze kuingoa CCM ama majimboni au kwenye urais...Ukweli ni kuwa hapa kwetu Tz watu wengi bado ni CCM na bila kushirikiana Chadema, CUf, CCJ au yeyote zaidi ya CCM kuwa kwenye uongozi wa dola ni ndoto za mchana.
 
Kwa hakika CHADEMA inaweza na ipo tayari kuongoza.
Hilo halina ubishi,ni ukweli usiofichika,watu makini kama Dr. Slaa wanauwezo mkubwa kuongoza nchi.

na hata watu safi waliopo CCM tunaweza kuivusha nchi katika mpito.
Sikubaliani na wewe katika hilo,CCM ina watu safi,lakin je usafi wao unatusaidia nini hadi sasa,ni mambo mangapi mazuri kwa muhtasari wa taifa letu CHADEMA wameyaanzisha na CCM wameyapinga na kutaka kuyapeleka mahakamni...reffer Speaker Siita nd Documents za Dr. Slaa ambazo leo tunashuhudia kesi za kuzugia za kina Liyumba
Kama CCJ walikuwa wanadhani watafanya peke yao inawezekana ndio changamoto wapatazo sasa. Nimeshtuka kweli kusoma mwananchi kuhusu uhakiki wa CCJ ambapo hata 'viongozi wao' wanatishia mashaka umakini wao kwa kukosea vitu vya kawaida kabisa. Kama kawaida wanakimbilia kusema CCM imewahujumu. Tatizo lile la kila siku la vyama vyetu kutoangalia changamoto za ndani na kukimbilia kulaumu (actually ni tatizo la watanzania wengi sana kutafuta 'mbuzi wa kafara'.
Who knows that,inawezekana kweli wamehujumiwa..reffer to kauli za Tendwa na Viongozi wa CCM against CCJ,but time will tell.

Nina imani kubwa kabisa kuwa CHADEMA kwa kushirikiana na vyama vingine wanaweza kushika, kuongoza na kuendeleza Dola yetu.
Una maanisha CHADEMA kuungana na vyama vingine katika uchaguzi?
 
Tunasukumiziwa katika makoo yetu chama kimoja tu kuwa ndicho pekee chafaa kuungwa mkono katika kuiangusha CCM. Tunaambiwa vyama vingine viungane nacho kwa sababu kimeonesha uongozi na kuwa ndiyo "upinzani" wa kweli. Wapo watu wanaoamini kabisa jambo hili. Wanaamini kuwa CHADEMA ndicho chama hasa mbadala kinachoweza kuchukua uongozi wa taifa letu toka mikononi mwa CCM.

Kama nilivyouliza huko nyuma ni mambo gani Chadema wamefanya kustahili kuongoza leo naomba nidokeza swali hili ambalo ni muhimu.

Je Chadema ilivyo sasa iko tayari kuongoza taifa la watu milioni 40 kwa ubora na kwa maono bora zaidi na mfano mzuri wa kiuongozi katika ngazi zote kuliko CCM? Ni nini msingi wa imani ya wale wanaoona kuwa iko tayari?

Mwenyewe ni na maoni yangu.. naomba nisikie ya kwenu.

Ukiwa makini utaona swali linahusu Chadema na utayari wao kuongoza.. nje ya hapo ni red herring.

Mkuu swali lako ni kuona kama mnaweza kujiunga nao ama?Coz if thats the case swali hilo hilo hao wanachadema wakiligeuza kwenu ccj mtajibu nini?

Naelewa umesema tuzungumzie chadema tu na nje ya hapo ni red herring....Tukifanya hivyo ni swa na kuthink within or inside the box....Huo "Utayari" wa kuongoza unaouzungumzia umejikita kwenye misingi gani?Je unazungumzia kuhusu mafanikio waliyofikia ie idadi ya wabunge ama?

Maana kama ni matatizo kila chama kinayo,kumng'oa mkoloni mweusi kama ilivyokuwa kwa mweupe kunahitaji nia ya kweli na si kuremba temba,hata mwalimu na chama chake hawakuwa tayari kuongoza nchi,lakini nia ilikuwa ni kumwondoa mkoloni kwanza....Labda ungefafanua zaidi huo "Utayari wa kuongoza" unamaanisha nini haswa?
 
Una maanisha CHADEMA kuungana na vyama vingine katika uchaguzi?

Ninamaanisha vyama vya upinzani kushirikiana katika uchaguzi. Kuungana sio lazima maana kila chama kina malengo na msingi wa kuanzishwa kwake. Vyama vyaweza kubakia na misingi yao ya kuanzishwa na kushirikiana katika mambo ambayo vyama vinakubaliana, Vyama vinakuwa na election platform moja na kufanya kampeni pamoja kwamba vikishinda ndio mambo watakayofanya. Tanzania vyama vya upinzani vinapaswa kushirikiana kwa kuachiana majimbo na Kata ili kuunda Serikali (kwa kuwa Waziri Mkuu atatoka chenye wabunge wengi au Mbunge mwenye kuungwa mkono na wabunge wengi) na kuunda serikali za Halmashauri za Wilaya/Miji/ Manispaa. Mabadiliko yanawezekana kabisa in our life time. Strategy, message and keeping on message!!!!!! Pia knowing what we want and what we want to do with what we want........
 
Nimesema na narudia tena we as we need a strong parliament as a basic ground to overhaul the existing system, vyama vya Upinzani havina budi kushirikiana ili kuweza kupata Sauti ya kuweza kubadilisha mfumo wetu. Out of that tutaendelea kunyanyaswa na Mabalozi wa nyumba kumi kumi ( Of course mimi huwa nawafukuza) katika michango ambayo hata Taarifa zake hazijulikani.
 
Vyama vingi vya kisiasa hapa nchini vimeshindwa kujijenga kama taasisi kwa kuweka mfumo wa kiuongozi ambao unawapa nafasi kubwa na imani kwa wananchi kwamba wakipewa nchi wanaweza kuongoza. Badala ya kujenga taasisi za kichama, vyama vingi vya upinzani na CHADEMA ikiwemo vimejikita kwenye umaarufu wa mtu mmoja mmoja, mara Slaa, Ziito, Hamad Rashid n.k wakati vilitakiwa kujenga chama kuanzia kwenye mashina. Kwa sasa CHADEMA waweke nguvu kuchukua nafasi za uwakilishi na watumie muda huu kujenga chama kwa ajili ya kuongoza nchi hapo 2015.
 
Kwa hakika CHADEMA inaweza na ipo tayari kuongoza. Kwa vyovyote vile haitakuwa CHADEMA peke yake na wala hakuna chama cha upinzani peke yake kinaweza kuleta mabadiliko katika Taifa letu na kuongoza DOLA bila mashaka. CHADEMA lazima ishirikiane na vyama vingine vya siasa, vikundi vya kijamii vinavyodai mabadiliko katika Taifa letu na watu wengine mmoja mmoja ambao wana maono ya nini Taifa linataka.

Kwa vyovyote vile CHADEMA inaihitaji sana CUF katika kuhakikisha tunashika dola vizuri. najua kuna watu watasema mbona tuliweza wenyewe Biharamulo na Busanda au hata Tarime. Mazingira ya by election ni tofauti sana na mazingira ya Uchaguzi Mkuu na ndio maana CUF waliweza pia peke yao TUNDURU. Sote tukafanya kinyume na matarajio Kiteto na Mbeya Vijijini.

Ugonjwa uliowapata NCCR-M mwaka 1995 kuwa wanaweza peke yao ndio huo huo uliowapata CUF mwaka 2000 mpaka mwaka 2005 na CHADEMA is vulnerable to that mwaka 2010. Hata hivyo, coalition ya Watanzania kwenye CHADEMA, CUF, NCCR-M nk na sasa hawa waliopo CCJ na hata watu safi waliopo CCM tunaweza kuivusha nchi katika mpito.

Kwa vyovyote vile ushindi wowote ule tutakaoupata kama opposition lazima uwe ni wa kulipitisha Taifa katika mpito ili kufanya mabadiliko makubwa ya mfumo wetu wa utawala na uongozi wa nchi. Mabadiliko ambayo hayatateteresha dola letu na hata Muungano wetu.

Kama CCJ walikuwa wanadhani watafanya peke yao inawezekana ndio changamoto wapatazo sasa. Nimeshtuka kweli kusoma mwananchi kuhusu uhakiki wa CCJ ambapo hata 'viongozi wao' wanatishia mashaka umakini wao kwa kukosea vitu vya kawaida kabisa. Kama kawaida wanakimbilia kusema CCM imewahujumu. Tatizo lile la kila siku la vyama vyetu kutoangalia changamoto za ndani na kukimbilia kulaumu (actually ni tatizo la watanzania wengi sana kutafuta 'mbuzi wa kafara'.

Nina imani kubwa kabisa kuwa CHADEMA kwa kushirikiana na vyama vingine wanaweza kushika, kuongoza na kuendeleza Dola yetu.

Zitto nimefurahi uko hewani,twende kazi bro!
 
Back
Top Bottom