CHADEMA iko tayari kuongoza?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Tunasukumiziwa katika makoo yetu chama kimoja tu kuwa ndicho pekee chafaa kuungwa mkono katika kuiangusha CCM. Tunaambiwa vyama vingine viungane nacho kwa sababu kimeonesha uongozi na kuwa ndiyo "upinzani" wa kweli. Wapo watu wanaoamini kabisa jambo hili. Wanaamini kuwa CHADEMA ndicho chama hasa mbadala kinachoweza kuchukua uongozi wa taifa letu toka mikononi mwa CCM.

Kama nilivyouliza huko nyuma ni mambo gani Chadema wamefanya kustahili kuongoza leo naomba nidokeza swali hili ambalo ni muhimu.

Je Chadema ilivyo sasa iko tayari kuongoza taifa la watu milioni 40 kwa ubora na kwa maono bora zaidi na mfano mzuri wa kiuongozi katika ngazi zote kuliko CCM? Ni nini msingi wa imani ya wale wanaoona kuwa iko tayari?

Mwenyewe ni na maoni yangu.. naomba nisikie ya kwenu.

Ukiwa makini utaona swali linahusu Chadema na utayari wao kuongoza.. nje ya hapo ni red herring.
 
Mie nashindwa kusema wanaweza au hawawezi..swala ni kuingia ulingoni ..
5 years ndio itaamua kama wanaweza au hawawezi
 
Mkuu kwa hali ilivyo sasa ndani ya CCM naona CHADEMA iko tayari kama chama mbadala. Tuipe miaka 5 tutajua mbele ya safari tumeshachoka na ufujaji wa rasilimali zetu. Mtoto akizaliwa anakua kulingana na mazingira yanayomzunguka. Tayari wameonyesha mwanzo mzuri ktk kupambana na ufisadi japokuwa 'finishing' yake imekuwa mbovu upande wa serikali.
 
Ni chama chenye individuals wazalendo! Wame risk sana kufichua maovu yanayofanywa na serikali ya CCM. Vyama vingine vya upinzani viko wapi? CHADEMA wanamchango mkubwa sana katika kubadili mwelekeo wa siasa ya Tanzania wamekuwa waaanzilishi wa hoja muhimu sana, wafichuzi wa mafisadi na wanaangazia watanzania kuhusu mbwa mwitu ccm aliyejivika ngozi ya kondoo!
 
Mimi siamini kama Chadema ndio chama mbadala kuongoza tz kwa sasa. mfumo wa Chadema wa kulalalia mikoa ya kaskazini na mikoa michache mengine tangu ipate usajili wa kudumu ni dalili tosha kwamba bado kuongoza.

Propaganda zile zile.kweli uko nyuma kisiasa..Huelewi unachokisema..By the way napoteza muda wangu bure kujibishana na wewe sin sababu ya kukuleza.Lol
 
Mkuu kwa hali ilivyo sasa ndani ya CCM naona CHADEMA iko tayari kama chama mbadala. Tuipe miaka 5 tutajua mbele ya safari tumeshachoka na ufujaji wa rasilimali zetu. Mtoto akizaliwa anakua kulingana na mazingira yanayomzunguka. Tayari wameonyesha mwanzo mzuri ktk kupambana na ufisadi japokuwa 'finishing' yake imekuwa mbovu upande wa serikali.
Tunaweza tukasema wanaweza kwa hizo sababu zinazotolewa kama vile kupambana na mafisadi na kufichua maovu ya serikali. Lakini bado hatuna uhakika kwa kweli kama wanaweza kwa sababu bado wana mapungufu mengi kama vile ukabila n.k licha ya hayo mazuri yake!
 
GS............Where art thou?

Balantada mimi nikijibu humu itaonekana navutia kwangu nitakuwa bias kama Mwanakijiji anavyokuwa bias,yeye tayari ni mCCJ kwahivyo hoja zake zitakuwa ni kuiponda CHADEMA tu ili kuipa nguvu na uhalali CCJ ionekane ndio chama mbadala.Hajui kuwa mpaka chama kionekane kinaweza kuongoza nchi sio kazi rahisi kama anavyodhani.Anafikiri kuwepo kwa CCJ leo ndio kukubalika kwake,haya yanawezekana nchi nyingine lakini sio kwetu Tz kwa wapiga kura wasiojua wajibu wala maana ya kura yake.Mwanakijiji nadhani CCJ watachukua nchi kirahisi wakati hata kupata hao wabunge kwao kwa mwaka huu ni kizungumkuti.Anafikiri ni sawa na mijadala ya humu JF rahisi rahisi. Field ni kugumu kuliko anavyodhani. Mie ni bora niwe msomaji tu nisije kujipendela ila ikibidi sana kuchangia itabidi nifanye hivyo..naangalia maoni ya watu wenye dhamira ya dhati(wanaosema ukweli na sio ushabiki wa kivyama)
 
Moja kati ya Majukumu ya Chama kinachopewa ridhaa na wananchi ya kutawala ni Kukusanya kodi na Kusimamia raslimali ( watu na vitu) na kuhakikisha kwamba kodi zinazokusanywa na raslimali hizo zinatumika katika kumletea maendeleo yule aliyetoa dhamana ya uongozi ( yaani mwananchi), kwamba kodi na raslimali hizo zitumike katika kuboresha huduma za Kijamiii ( Kama Afya, Elimu, Maji nk) kiuchumi na kisiasa vilevile. Sasa tangia Uhuru haya Majukumu watanzania wamekuwa wakiwakabidhi CCM

Sasa moja kati ya Majukumu ya vyama vilivyo nje ya Serikali ( CUF, TLP, CHADEMA) ni kuhakikisha kuhakikisha kwamba Serikali iliyo madarakani inatumia kodi na raslimali itakikanavyo ( Ingawa hii ni kazi ya Bunge lakini vyama vilivyo nje serikali vinawajibika kwalo). Vile vile ni wajibu kwa Vyama hivyo kuonyesha Uongozi Mbadala pale vinapopata Fursa sasa ni vyema tukaangalia katika yale maeneo ambapo vyama hivi vimepata fursa ya kuongoza vimefanya nini tofauti ya CCM ( in apositive way?

Tuipime CHADEMA kwa halmashauri ilizofanikiwa kuongoza na tuipime CUF kwa halmashauri ilizopata fursa kuziongoza, tufanye hivyo pasipo kuegemea misimamo yetu ya kivyama

Asante
 
Kumbe kazi uliyokuwa unaifanya kwa miaka minne sasa ndiyo inaanza kuonekana at least now unaanza kuonyesha a true colour of you, kuzunguka kote huko kumbe mwisho wako ndio huu, Nina sababu 51 kwanini nisimchague Kikwete LOL! lakini umewahi sana kujionesha ungevuta muda kidogo uwakamate wengi, tchao.
 
Mimi sina imani na CHADEMA katika kuiongoiza hii nchi.
Ni afadhali kipindi kile cha 1995 NCCR kuliko kipindi hiki CHADEMA.
Warekebishe kwanza mfumo wa chama chao, waondoe ukabila ndani ya chama chao.
 
Kumbe kazi uliyokuwa unaifanya kwa miaka minne sasa ndiyo inaanza kuonekana at least now unaanza kuonyesha a true colour of you, kuzunguka kote huko kumbe mwisho wako ndio huu, Nina sababu 51 kwanini nisimchague Kikwete LOL! lakini umewahi sana kujionesha ungevuta muda kidogo uwakamate wengi, tchao.

Ha ha ha,Luteni umenichekesha sana,wewe ndio unagundua leo.Lol.
 
Hivi, hizi kelele za 'ukabili' ni halisi au basi tu ni ile tabia ya waTanzania kulalamika?

Kuna watu mnaomba mambo msiyoyajua bila kujua. Eti ukabila!!
 
Hili ndilo lengo la kuanzisha chama cha siasa kokote duniani. Tatizo ni namna ya kuupata huo UONGOZI wa NCHI. Ni lazima CHADEMA iishinde CCM iliyoko madarakani tena kwa kujikita hasa. Wananchi hawajawa tayari kuongozwa na chama kingine chochote. Vyombo vya DOLA havijawa tayari kukubali Commander-in-Chief kutoka chama kingine zaidi ya CCM. Huu ndio ukweli unaoumiza sana. Naamini CHADEMA wako tayari hata leo.
 
Vipimo tunavyoweza kutumia kuwapima CHADEMA ni kupitia viongozi wao tuliowachagua kuwa Wabunge wetu au madiwani wetu, pamoja na utekelezaji wa sera zake. Kwenye ishu ya ukabila sipo kabisa.

Sina data sana ila nadhani Dr. Slaa amefanya vizuri sana kwenye jimbo lake na amekuwa kiongozi mzuri sana kwenye kamati ya Bunge aliyomo. Ukimwangalia Zitto Kabwe nae kuna mambo mengi sana mazuri amewafanyia wananchi wa jimboni kwake, na amesaidia sana kwenye kamati ya madini (though at some point nilitofautiana nae kimtazamo). Halima Mdee nae amehangaika sana na kuwasaidia kina mama, watoto na vijana.

Ila nadhani bado wahitaji watu zaidi kuweza kuiongoza serikali, maana ukiangalia watendaji wazuri tunaowajua toka CHADEMA sidhani kama wanazidi kumi. Na hapo ndio umuhimu wa kuungana na vyama vingine vya upinzani unapokuja. Ila suala la kuungana linahitaji kukaa chini na kuanza kuangalia mwisho utakuaje tukishaunga - kimadaraka, kimtazamo(ilani), uteuzi wa wagombea, jinsi ya kuiongoza serikali etc.

All in all nna imani kiutendaji CHADEMA wanaweza kufanya mambo mazuri, ila angalizo langu nikuwa, sio lazima mtendaji mzuri kuwa kiongozi mzuri.
 
kua Tayari kuongoza kunapimwa na vigezo vipi ?
kulipua mabomu ya kisiasa pale Mwembe Yanga ni seheMU tu ya harakati, na halikua kosa kisiasa, walitimiza wajibu wao kama raia wema wa nchi hii, walisaidia kuokoa baadhi ya pesa za Umma, binafsi nawashukuru sana, kazi nzuri.
CHADEMA, Linganisha na vyama vingine hapa Tanzania bara, hakika kiko nyuma ya CCM kwa mtandao toka ngazi ya shina hadi Taifa.
CHADEMA inaongoza halimashauri chache sana huku bara, lakini je wamefanya vizuri / wamefanikiwa hata baadhi ya sera zao ?
Je kuna chama Kingine cha Upinzani mfano TLP, UDP, CUF wenye mtandao mkubwa huku bara kuifikia CHADEMA ?
Kama Watanzania wako tayari kwa mabadiliko ni lazima wakipe CHADEMA ama chama kingine cha upinzani halmashauri za kutosha hii itaongeza uzoefu kwa vyama hivi kabla ya kutwaa madaraka makubwa ya nnchi.
CHADEMA tayari inajiimarisha huku chini , ndio maana viongozi woote maarufu wa chama wameamua kwenda majimboni ili kuongeza nguvu na kupata uzoefu.
kwa maoni yangu CHADEMA ni bora kuliko vyama vingine vyoote, hata hiko CCJ ambacho bado kinahangaika kuhakiki wanachama huko mitaani , sijui mwembe Yanga wanachama wangapi walijitokeza kuhakikiwa.
 
Back
Top Bottom