Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Naomba kwa muda tuanze kumtambua mchawi wetu ccm kupitia Wassira. Uasi una vyanzo. Vyanzo vyaweza kuwa ni ushawishi, tamaa, utashi wa mtu, hata vitisho. Hili jambo twende nalo kwa akili. Bora imekuwa mapema haya yametokeza na mapema yapatiwe suluhu
Kwenye hil indugu yangu tuiweke CCM pembeni; hili ni la CDM tu. Kwani hawa watu wameshikiwa mapanga na bunduki na CCM kichwani? Au tunafikiri wamekaa kama maroboti ya kisiasa ambao wenye kuyaendesha wako Lumumba? Kuilalamikia CCM kwa yanayoendelea CDM ni sababu tosha ya kwanini CDM inahitaji kufanya kitu. Haiwezekani CCM wapike Lumumba chakula kiive Rufiji!