Chadema hizi pesa mtalizipaje?

images
kooooo.jpg

Vigumu kumwuliza swali yule asiyeshika dola kwamba atarudishaje pesa, ni sawa na mtoto anavyolelewa na wazazi halafu uulize wazazi mtoto atarusishaje gharama za malezi kwa wazazi wake.

Ungeuliza Rais Kikwete atarudishaje mikopo anayoendelea kukopa kwa vile anachukua mikopo hiyo kwa kutegemea kodi za wananchi anazokusanya.
 
wananchi wanachanga mil 300, chadema wanatumia billion 3. We hujiulizi hizo zingine zinatoka wapi? Au wanamajini yanayo leta hela?

Mkurugenzi wa fedha na utawala wa CHADEMA Anthony Komu alikuwa Channel Ten akimchanachana NAPE juu ya tuhuma zake juu ya CHADEMA kupokea fedha kutoka nje na kwamba inafanya usanii katika harambee zake.

Komu anasema ni kweli CHADEMA inashirikiana na KAS shirika la Kijerumani kama wao CCM wanavyoshirikiana na FES shirika la Kijerumani.

Komu anasema CCM wanapokea fedha kutoka NDI kama wao CHADEMA kupitia TCD lakini mpaka leo hii CCM hawajawahi kutoa mrejesho wa fedha hizo kama wao CHADEMA wanavyofanya.

Komu ameweka wazi kuwa CHADEMA inapokea ruzuku ya shilingi milioni 230 kwa mwezi. Ameweka wazi pia mapato ya harambee zote za Arusha, Dar es salaam na michango ya Jangwani.
quote_icon.png
By Mdutch
Nape kakurupuka kapiga simu anaambiwa ataje majina ya hao wanaotoa fedha chafu CHADEMA akabwabwaja maneno kama kawaida kwa kushindwa kuwataja.

Mwandishi kamwambia ataje kiasi cha fedha kilichoingia CHADEMA kutoka nje akabwabwaja tena maneno kwa kushindwa kukitaja kiasi chochote.

NAPE kaulizwa aseme vyanzo vya fedha vya CCM kabwabwaja maneno kwa kushindwa kuvisema vyanzo hivyo. Kashindwa kuwataja hata washirika wao wa CHINA na aliposhindiliwa kuwa na ushirikianao na FES ndio akakubali kishingo upande.

quote_icon.png
By Mdutch
KOMU kamlima kishoka NAPE kamwambia kama yeye anadhani CHADEMA inapokea fedha chafu kutoka nje basi ni uzembe wa serikali yao dhaifu inayounda serikali yenye mamlaka na BOT inayosimamia benki zote za Tanzania ambamo CHADEMA ina akaunti zake kwa kuitaka itoe hizo taarifa.

Pia Komu kasema TRA ni chombo cha serikali chenye mamlaka ya kufuatilia vyanzo vya mapato vya CHADEMA na kuvikagua. Kama CCM wanaona kweli kuna fedha chafu zinaingizwa CHADEMA basi Tanzania haina serikali

quote_icon.png
By Mdutch
Wachangiaji wamemjia juu bwana mdogo NAPE kwa kumtaka kama moto wa CHADEMA umekuwa mkali kiasi hicho basi na wao wajaribu kuchangisha fedha kutoka kwa wananchi kama wanauwezo huo ili wakijenge chama chao kinachokufa.

Kijembe kimerushwa kwa NAPE kutoka kwa mchangiaji kuwa ni kwanini CCM waliopokea fedha chafu za EPA, KAGODA na Deep Green mpaka leo wameshindwa kuwachukulia hatua. Fedha hizi zilitumika kuiingiza CCM madarakani mwaka 2005 na 2010.

Komu kaja juu tena kwa kusema kuwa CCM wana vyanzo vingine vya mapato kwa mfano umiliki wa majengo na viwanja vya michezo ambavyo wamevipora kwa kuwa vilijengwa na umma enzi za chama kimoja lakini mpaka leo hiii hawawezi kuweka wazi mapato yao ukiacha yale ya ruzuku.

quote_icon.png
By Mdutch
Eti NAPE amedai kuwa hajaona maswali ya wachangiaji kwa kuwa ameshatoka nyumbani kwenda ofisini.

NAPE anarudi tena hewani na kudai kuwa CHADEMA ni dhaifu na haina social base kwa hiyo haihofii CHADEMA. Anajitetea kuwa yeye ni mkweli na ndio maana yuko tayari kukisema hata chama chake.

Analalamika kuwa wanaosema anaiua CCM wanamuonea kwa kuwa anajitahidi kukijenga chama chake. Anaambiwa ataje majina ya watu wanaotoa fedha chafu anacheka cheka anapata kigugumizi.

Anasema kuwa kama CHADEMA wasipochukua hatua za kuweka wazi vyanzo vya fedha zao watachukua hatua anaulizwa ni hatua gani watachukua anashindwa kusema.

Kauli yake hii ya kuonyesha kuihofia CHADEMA ni kwamba eti yeye NAPE anafanya hivi kuikosoa CHADEMA kwa kuwa ni chama kinachotaka kuiongoza nchi na CHADEMA wajisafishe ili nchi yetu isije ikatawaliwa na watu dhaifu.

quote_icon.png
By Mdutch
"CCM ni kama panya. Mtu ukiwa hupo nyumbani panya huingia mpaka sebuleni. Ila mwenye nyumba anapokuja panya hukimbia sebuleni na kuingia uvunguni na maeneo mengine ya nyumba. CHADEMA ndio mwenye nyumba na yuko nyumbani kwa hiyo panya wamekimbia sebuleni kuelekea uvunguni.

Kwamba sebule ni majimbo yote ya mjini kama Mwanza, Arusha, Mbeya , Ubungo, Kawe, Moshi, Iringa na sasa CHADEMA inaingia mpaka uvunguni yaani majimbo ya vijijini kumsakanya panya. Operesheni sangara inayoendelea Morogoro na mikoa ya Iringa, Dodoma, na Manyanya kukijenga chama ni sawa na kumtimua panya uvunguni."

Kauli ya kumalizia ya Anthony Komu.
 
Nchi itawekwaje rehani na watu wasioiongoza?kama ni rehani kweli labda ingekuwa silaha,kwasababu nani atatoa pesa kama vile tayari chadema wana madaraka?Gazeti la kijinga ndo maana wamemweka cameroon hapo ili kuwaaminisha wananchi kitu gani?Kwamba chadema imeingia mkataba na Uingereza?Huyo cameroon anayedili naye si JK?
 
Pesa kama inaingia kinyume na sheria nani alaumiwe kikwete, waziri wa fedha au nje au niudhaifu nape anathibitisha kuwa ssm cheo kikubwa wanachokimudu ni ujumbe wa nyumba kumikumi
 
Mtaa wa UFIPA leo wamekulipa sh ngapi?

Kwa nini tuamini kauli ya Nape Nnauye na Fisi Wenu?

MAMBO mengine kwenye hii kaya yetu unabaki ukishangaa tu. Ni jambo lililoko bayana kabisa kwamba mimi siwezi kupata afya njema kwa kuomba mtu mwingine augue. Kama ninataka mimi kupata afya bora, kazi yangu na juhudi zangu zinapaswa kujitunza na kufuata mashauri ya wataalam.
Katika hali ya kushangaza, unapomsikia kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi, akisema kwamba CHADEMA wanapokea fedha kutoka nje kwa siri kutoka kwa wafadhili ili hao "wafadhili" waje kuifaidi Tanzania ni kiwango cha juu kabisa cha kushindwa kujua tatizo lililopo. Kabla ya kujadili hiyo kauli na kuangalia matege yake, kwanza tujiulize kama bado kuna sababu yoyote ya kuamini kauli inayotoka Chama Cha Mapinduzi, hasa kwa wakati huu. Nitakumbusha kauli chache tu halafu tuone kama kwa kauli hizo, hii kauli dhidi ya CHADEMA inafaa kuaminika japo kidogo.
Wakati Chama Cha Wananchi (CUF) kilipokuwa na upinzani uliokuwa unafanya CCM watoke macho mithili ya mjusi aliyebanwa na mlango, walizushiwa kila aina ya uchafu ikiwemo udini na hali ilipokuwa tete kabisa, propaganda kali zikapigwa kwamba kuna kontena la visu vyenye nembo ya chama hicho limeingizwa nchini. Bila shaka, habari hii ililenga kuwaambia watanzania kwamba CUF sio chama makini wala watu wasijaribu hata kidogo kukiingiza madarakani.
Hadi leo, sijawahi kusikia huyo mwana-CUF aliyeingiza visu hivyo kwa nia ovu akikamatwa, akishtakiwa na kuhukumiwa. Yawezekana porojo zile ziliyumbisha mwelekeo wa CUF, lakini ukweli ambao hauna mjadala ni kwamba, kuyumba kwa CUF hakukuifanya CCM iwe imara. Badala ya kutumia muda mwingi kushambulia wapinzani wao, wangetumia muda kujijenga na kukijenga chama chao labda mambo yangekuwa afadhali. Kama hadi leo hatujaoneshwa ushahidi wa hawa CUF na visu vyao, kwa nini tuamini haya yanayosemwa dhidi ya CHADEMA? Kalaghabao!
Ni Chama hiki cha Mapinduzi (CCM) kilichojiapiza kwamba kinawapa mafisadi miezi inayohesabika kwenye vidole vya kiganja cha mkono ili wajiondoe wenyewe, vinginevyo wangetimuliwa. Tukaanza kusikia hadithi ya tunawapa mwezi mmoja, miezi miwili mara tunarudisha hili kwa wanachama. Kauli yao wenyewe ya kuwaondoa mafisadi ndani ya chama, imedhihirika kwamba haitekelezeki na walichokisema kwamba wana nia ya kusafisha chama, kumbe ilikuwa porojo. Kwa nini tuwaamini sasa kwamba wanayosema dhidi ya CHADEMA yana ukweli?
Ni CCM hii hii ndiyo iliyokula yamini ya kutuletea maisha bora kwa kila mtanzania. Hivi hadi sasa tukichukulia katika wingi wetu, ni nani ameyaona hayo maisha bora? Labda tuwaulize walimu na madaktari. Hivi hawa watanzania wanaokufa kwa ajali zinazoepukika, ndio wanaoishi maisha bora kwa kila mtanzania? Hivi ni hawa watanzania wanaofanya kazi kwa amri za mahakama ndio wanaotekeleza sera za ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi (ANGUKA)? Kama utekelezaji wa ahadi za chama umekuwa na kigugumizi hivi, kwa nini tuamini haya mengine wanayoyasema? Mwenye macho haambiwi tazama.
Ni CCM hii hii katika kujaribu kughilibu umma, wakati wa mazishi ya mwasisi wa CHADEMA Bob Makani ilijaribu kuleta mzaha ndani ya kilio kwa kutaka kuwalisha watu uongo mchana wa jua la utosi eti Bob Makani ndiye alikuwa muasisi pekee wa CHADEMA asiyetoka Kaskazini. Mola mkubwa, waliokuwa wakifahamu historia wakatoa majibu pale pale, yakawashuka waliotaka kuleta siasa ndani ya kilio! Kama waliweza kujaribu kupotosha umma kwa kiwango hicho cha kutisha, kwa nini leo hii tuwaamini wakizungumza mambo hasi dhidi ya CHADEMA?
Ni kada wa CCM aliyejaribu kusimama na kutaka kuwalaghai watanzania kwamba eti Dk. Wilbroad Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA, aliiba kanisani. Mungu wakati mwingine hujibu hapa hapa duniani. Maaskofu wakafungua mdomo na kusema huo wizi unaosemwa na kada wa CCM, haupo. Uongo mwingine wa wazi wazi kabisa. Kimya kilichofuata hapo ni zaidi ya kile cha makaburini usiku wa manane.
Na mara nyingi tunashuhudia CCM wanavyodanda na kujidanganya wenyewe kuhusu kupendwa kwake. Wanapoitisha mkutano wa hadhara, hawana uthubutu wa kuwataka wanachama waende wenyewe kwa usafiri wao wenyewe. Sikiliza, ukisikia kuna mkutano wa hadhara, tafuta wafanyabiashara wenye daladala wakueleze namna wanavyopata tenda ya kusomba watu na kuwapeleka mkutanoni. Mitaani pia tunasikia tetesi kwamba kuna kuwepo pia posho za alfu moja moja kwa wahudhuriaji. Ndipo walipofika, na bado mnataka tuwaamini wakituambia wanayosema leo?
Tangu tusikie kwamba eti wanaachana na mpango wa kununua magari ya kifahari maarufu kama mashangingi, huu ni mwaka wa ngapi? Tunapishana nayo huku na kule utadhani kauli ile ya kutotumia magari hayo au ilitolewa nchi jirani, au wewe ndiye uko nchi jirani. Kimojawapo kati ya hivyo, maana kauli haziendani na macho yanayoshudia. Hayo ni machache sana kati ya mengi ambayo yamesemwa, lakini hayakutekelezwa. Kwa maana nyingine, ni kwamba CCM haina kauli thabiti na kwa mtazamo huo na historia yao, inakuwa mashaka sasa kuyaamini wayasemayo hasa dhidi ya wapinzania wao wakubwa.
Tukirudi kwenye hoja ya Nape Nnauye kwamba hawa CHADEMA wanapata ufadhili ili hao wakubwa kutoka nje, waje wafaidi rasilimali zetu, tuna maswali zaidi ya elfu moja na moja ya kuuliza. Hivi hadi sasa watu wa nje hawafaidi rasilimali za Tanzania? Wale twiga waliosafirishwa kwenda nje walikuwa wanasafirishwa wakati wa utawala wa chama kipi? Ile ripoti ya wataalam kuhusu kodi tunayopoteza kwenye madini imesomwa na ndugu yetu Nape? Wanaofaidi unono wa misamaha na vivutio vya uwekezaji ni watu gani? Katika utwawala wa chama gani?
Walioleta wageni kuja kukusanya Ankara za umeme ni serikali ya wakina nani? Nadhani dada yangu Stella Manyanya atakuwa anakumbuka sana hilo sakata wakati ilibidi nguvu itumike kuruhusu wageni wachukue menejimenti ya shirika la umeme. Ajabu ya Tanzania ni kwamba, mambo yanaenda kinyume nyume. Yaani wakati ule tuliona hatuwezi kuwa na wataalamu wa kuendesha shirika, lakini tuna wataalamu wa kuendesha wizara! Sijui kipi ni kigumu kuliko kingine. Tuna haja ya kuzungumza kwamba Tanzania sio muuzaji anayeongoza kwa kuuza tanzanite duniani? Tunahitaji kuzungumzia chochote kuhusu dhahabu? Tuna haja ya kuuliza mikataba tata ya kuzalisha na kuuzia TANESCO umeme?
Labda Nape aanze kutuambia CCM ililipwa kiasi gani hadi ikaua na kuzika Azimio la Arusha na kuumba Azimio lisilo rasmi la Zanzibar.
Tumalizie kwa kuhoji kidogo. Hivi inawezekana vipi, CCM kama chama kikafahamu mipango thabiti ya CHADEMA kupatiwa fedha kutoka nje kwa makusudi ya kuja kuwafaidisha wageni rasilimali zetu (utadhani sasa hivi hawazifaidi) halafu serikali ya chama hicho hicho ikashindwa kujua mipango hiyo na kuizuia? Hakuna sheria inayoelezea uchangiaji wa fedha kwa vyama vya siasa? Nani anapaswa kuisimamia? Lakini, hawa mahasimu wetu wanaotaka kuja kufaidi maliasili zetu ni akina nani?
Bila majibu ya maswali haya, ni ngumu kuupokea ujumbe wa CCM kwamba CHADEMA wanapewa hela kwa hila ili maliasili zetu zije kufaidiwa na wageni. Badala ya kusambaza propaganda ingekuwa vyema kujenga chama maana hata kama CHADEMA watachafuka na kuanguka, wananchi wamechoka, watatafuta mbadala mwingine.
 
Kwa nini tuamini kauli ya Nape Nnauye na Fisi Wenu?

MAMBO mengine kwenye hii kaya yetu unabaki ukishangaa tu. Ni jambo lililoko bayana kabisa kwamba mimi siwezi kupata afya njema kwa kuomba mtu mwingine augue. Kama ninataka mimi kupata afya bora, kazi yangu na juhudi zangu zinapaswa kujitunza na kufuata mashauri ya wataalam.
Katika hali ya kushangaza, unapomsikia kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi, akisema kwamba CHADEMA wanapokea fedha kutoka nje kwa siri kutoka kwa wafadhili ili hao “wafadhili” waje kuifaidi Tanzania ni kiwango cha juu kabisa cha kushindwa kujua tatizo lililopo. Kabla ya kujadili hiyo kauli na kuangalia matege yake, kwanza tujiulize kama bado kuna sababu yoyote ya kuamini kauli inayotoka Chama Cha Mapinduzi, hasa kwa wakati huu. Nitakumbusha kauli chache tu halafu tuone kama kwa kauli hizo, hii kauli dhidi ya CHADEMA inafaa kuaminika japo kidogo.
Wakati Chama Cha Wananchi (CUF) kilipokuwa na upinzani uliokuwa unafanya CCM watoke macho mithili ya mjusi aliyebanwa na mlango, walizushiwa kila aina ya uchafu ikiwemo udini na hali ilipokuwa tete kabisa, propaganda kali zikapigwa kwamba kuna kontena la visu vyenye nembo ya chama hicho limeingizwa nchini. Bila shaka, habari hii ililenga kuwaambia watanzania kwamba CUF sio chama makini wala watu wasijaribu hata kidogo kukiingiza madarakani.
Hadi leo, sijawahi kusikia huyo mwana-CUF aliyeingiza visu hivyo kwa nia ovu akikamatwa, akishtakiwa na kuhukumiwa. Yawezekana porojo zile ziliyumbisha mwelekeo wa CUF, lakini ukweli ambao hauna mjadala ni kwamba, kuyumba kwa CUF hakukuifanya CCM iwe imara. Badala ya kutumia muda mwingi kushambulia wapinzani wao, wangetumia muda kujijenga na kukijenga chama chao labda mambo yangekuwa afadhali. Kama hadi leo hatujaoneshwa ushahidi wa hawa CUF na visu vyao, kwa nini tuamini haya yanayosemwa dhidi ya CHADEMA? Kalaghabao!
Ni Chama hiki cha Mapinduzi (CCM) kilichojiapiza kwamba kinawapa mafisadi miezi inayohesabika kwenye vidole vya kiganja cha mkono ili wajiondoe wenyewe, vinginevyo wangetimuliwa. Tukaanza kusikia hadithi ya tunawapa mwezi mmoja, miezi miwili mara tunarudisha hili kwa wanachama. Kauli yao wenyewe ya kuwaondoa mafisadi ndani ya chama, imedhihirika kwamba haitekelezeki na walichokisema kwamba wana nia ya kusafisha chama, kumbe ilikuwa porojo. Kwa nini tuwaamini sasa kwamba wanayosema dhidi ya CHADEMA yana ukweli?
Ni CCM hii hii ndiyo iliyokula yamini ya kutuletea maisha bora kwa kila mtanzania. Hivi hadi sasa tukichukulia katika wingi wetu, ni nani ameyaona hayo maisha bora? Labda tuwaulize walimu na madaktari. Hivi hawa watanzania wanaokufa kwa ajali zinazoepukika, ndio wanaoishi maisha bora kwa kila mtanzania? Hivi ni hawa watanzania wanaofanya kazi kwa amri za mahakama ndio wanaotekeleza sera za ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi (ANGUKA)? Kama utekelezaji wa ahadi za chama umekuwa na kigugumizi hivi, kwa nini tuamini haya mengine wanayoyasema? Mwenye macho haambiwi tazama.
Ni CCM hii hii katika kujaribu kughilibu umma, wakati wa mazishi ya mwasisi wa CHADEMA Bob Makani ilijaribu kuleta mzaha ndani ya kilio kwa kutaka kuwalisha watu uongo mchana wa jua la utosi eti Bob Makani ndiye alikuwa muasisi pekee wa CHADEMA asiyetoka Kaskazini. Mola mkubwa, waliokuwa wakifahamu historia wakatoa majibu pale pale, yakawashuka waliotaka kuleta siasa ndani ya kilio! Kama waliweza kujaribu kupotosha umma kwa kiwango hicho cha kutisha, kwa nini leo hii tuwaamini wakizungumza mambo hasi dhidi ya CHADEMA?
Ni kada wa CCM aliyejaribu kusimama na kutaka kuwalaghai watanzania kwamba eti Dk. Wilbroad Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA, aliiba kanisani. Mungu wakati mwingine hujibu hapa hapa duniani. Maaskofu wakafungua mdomo na kusema huo wizi unaosemwa na kada wa CCM, haupo. Uongo mwingine wa wazi wazi kabisa. Kimya kilichofuata hapo ni zaidi ya kile cha makaburini usiku wa manane.
Na mara nyingi tunashuhudia CCM wanavyodanda na kujidanganya wenyewe kuhusu kupendwa kwake. Wanapoitisha mkutano wa hadhara, hawana uthubutu wa kuwataka wanachama waende wenyewe kwa usafiri wao wenyewe. Sikiliza, ukisikia kuna mkutano wa hadhara, tafuta wafanyabiashara wenye daladala wakueleze namna wanavyopata tenda ya kusomba watu na kuwapeleka mkutanoni. Mitaani pia tunasikia tetesi kwamba kuna kuwepo pia posho za alfu moja moja kwa wahudhuriaji. Ndipo walipofika, na bado mnataka tuwaamini wakituambia wanayosema leo?
Tangu tusikie kwamba eti wanaachana na mpango wa kununua magari ya kifahari maarufu kama mashangingi, huu ni mwaka wa ngapi? Tunapishana nayo huku na kule utadhani kauli ile ya kutotumia magari hayo au ilitolewa nchi jirani, au wewe ndiye uko nchi jirani. Kimojawapo kati ya hivyo, maana kauli haziendani na macho yanayoshudia. Hayo ni machache sana kati ya mengi ambayo yamesemwa, lakini hayakutekelezwa. Kwa maana nyingine, ni kwamba CCM haina kauli thabiti na kwa mtazamo huo na historia yao, inakuwa mashaka sasa kuyaamini wayasemayo hasa dhidi ya wapinzania wao wakubwa.
Tukirudi kwenye hoja ya Nape Nnauye kwamba hawa CHADEMA wanapata ufadhili ili hao wakubwa kutoka nje, waje wafaidi rasilimali zetu, tuna maswali zaidi ya elfu moja na moja ya kuuliza. Hivi hadi sasa watu wa nje hawafaidi rasilimali za Tanzania? Wale twiga waliosafirishwa kwenda nje walikuwa wanasafirishwa wakati wa utawala wa chama kipi? Ile ripoti ya wataalam kuhusu kodi tunayopoteza kwenye madini imesomwa na ndugu yetu Nape? Wanaofaidi unono wa misamaha na vivutio vya uwekezaji ni watu gani? Katika utwawala wa chama gani?
Walioleta wageni kuja kukusanya Ankara za umeme ni serikali ya wakina nani? Nadhani dada yangu Stella Manyanya atakuwa anakumbuka sana hilo sakata wakati ilibidi nguvu itumike kuruhusu wageni wachukue menejimenti ya shirika la umeme. Ajabu ya Tanzania ni kwamba, mambo yanaenda kinyume nyume. Yaani wakati ule tuliona hatuwezi kuwa na wataalamu wa kuendesha shirika, lakini tuna wataalamu wa kuendesha wizara! Sijui kipi ni kigumu kuliko kingine. Tuna haja ya kuzungumza kwamba Tanzania sio muuzaji anayeongoza kwa kuuza tanzanite duniani? Tunahitaji kuzungumzia chochote kuhusu dhahabu? Tuna haja ya kuuliza mikataba tata ya kuzalisha na kuuzia TANESCO umeme?
Labda Nape aanze kutuambia CCM ililipwa kiasi gani hadi ikaua na kuzika Azimio la Arusha na kuumba Azimio lisilo rasmi la Zanzibar.
Tumalizie kwa kuhoji kidogo. Hivi inawezekana vipi, CCM kama chama kikafahamu mipango thabiti ya CHADEMA kupatiwa fedha kutoka nje kwa makusudi ya kuja kuwafaidisha wageni rasilimali zetu (utadhani sasa hivi hawazifaidi) halafu serikali ya chama hicho hicho ikashindwa kujua mipango hiyo na kuizuia? Hakuna sheria inayoelezea uchangiaji wa fedha kwa vyama vya siasa? Nani anapaswa kuisimamia? Lakini, hawa mahasimu wetu wanaotaka kuja kufaidi maliasili zetu ni akina nani?
Bila majibu ya maswali haya, ni ngumu kuupokea ujumbe wa CCM kwamba CHADEMA wanapewa hela kwa hila ili maliasili zetu zije kufaidiwa na wageni. Badala ya kusambaza propaganda ingekuwa vyema kujenga chama maana hata kama CHADEMA watachafuka na kuanguka, wananchi wamechoka, watatafuta mbadala mwingine.

View attachment 61985. Hili nalo?
 
Unauliza kulipa CDM haijakopa fedha kutoka sehemu yeyote na hilo NEPI ameonyesha kushindwa kutoa ushahidi. Kwa nini usiulize kwa hili la kupewa vyandarua tunalipa Dhahabu, Tanzanite na Almasi?
 
magazeti ya mafisadi Jitu Patel ,wameunguna na ccm kuishambulia cdm wanajua siku si nyingi wahindi hao mafisadi watakimbia nchi maana ni wanufaika wa EPA,KILIMO KWANZA
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom