Chadema:"Heri kufa nimesimama" kuliko "kuishi nimepiga magoti"

Haka ka msemo nimekapenda japo utekelezaji wake umekuwa mgumu kupindukia.

"Heri kufa nimesimama" kuliko "kuishi nimepiga magoti". Huu ni moja kati ya semi za makamanda wa jeshi lililo hai la CHADEMA wanapokuwa vitani. Nimekwazwa sana na utekelezaji wa usemi huu ambapo wasiousema ndio wanautimiza kama jamaa zetu watatu pale Arusha.

Juzi mkuu wa usemi dakika chache tu baada ya kunena alitenda tofauti na kujikabidhisha polisi (kwa maana ya kuishi akiwa amepiga magoti). Kale kadada kangu na maandamano kaliukana tena usemi na kuchagua kupiga mbio baada ya wapiganaji wa kweli kuibuka na vya moto vinavyotoa uhai.
Bahati mbaya mbio hazikutosha leo nasikia kanaungurumia kisutu (kupiga magoti).

Jamani misemo hii tuwaachie akina Mkwawa, Mirambo, Isike n.k sio sisi akina Kinjekitile Ngware. Iwapo hatuna uwezo wa kutimiza basi tusiwaumize vijana wetu na misemo mfu kama ilivyokuwa "vita ya majimaji".

Wengi wetu ni waoga na mara kwa mara tumekuwa tukikimbia hasa viongozi kipindi wapiganaji wa kweli wanapozifyatua, hii hali hatukuizoe sasa mbona tunailazimisha wakati hatuimudu?

Viongozi wa CHADEMA sijaona yeyote kati yenu aliyekufa amesimama wote mnaishi mmepiga magoti, chondechonde msitumalize sisi.
Next time kama mtaendelea na msemo huu basi mtuonyeshe mfano wa "kufa mmesimama".

Hicho ndio chama cha siasa? sijapata kusikia.
 
Unajua kama una cha kusema hapa JF ni bora uende ukafanye umbea wako huko vijiweni.....unaongea upumbavu sana na inaelekea una uwezo mdogo wa kufikiri na kuamua mambo,kama akili yako imekutuma uandike haya basi wewe ni "bogus"....

umempatia huyu kilaza,mercenary wa magamba.
 
Back
Top Bottom