Kwa kawaida uongo huwa hauna uwezo wa kuhimili test of time. Leo asubuhi nilikuwa naangalia taarifa ya habari nikakutana na habari ambayo imenishtua ya kwamba CHADEMA wamekana muafaka wa Umeya wa Arusha. Alipoulizwa Mbowe akajibu kuwa wanafanya uchunguzi juu ya suala hilo huku Lema akisema kuwa hatambui muafaka huo. Kitendo cha kutokuwepo kwa kauli thabiti inayoonekana kuwa imetokana na azimio la kikao rasmi, ni kielelezo cha kutoaminika kwa CHADEMA. Nasema hivi kwa sababu zifuatazo: Kwanza, taarifa za kuwepo kwa muafaka tumezipata siku nyingi zilizopita. Kama muafaka huo ungekuwa ni batili, CHADEMA wangeukana immediately au hata kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Naibu Meya. Pili, kuna tofauti kubwa sana katika kauli kati ya Mbowe na Lema kitendo kinachoashiria kuwa kuna misimamo tofauti kati ya Mbowe na Lema. Tatu, inaonekana kuwa CHADEMA hawana shida na maendeleo bali wanataka mapinduzi bila ya kujali gharama zake. CDM wanatuhadaa! Hawaaminiki!!