CHADEMA: Hatima ya Shibuda leo..

Hebu tuendeleze mjadala kama wachangiaji huru.ni kwa nini Shibuda afukuzwe? mtindo gani utumike kumfukuza? Je kuna madhara yoyote politically kwa wananchi na chama chake?Na je,asipofukuzwa kuna madhara yoyote kwa chama na wafuasi wake?Je,njia ya kumfukuza kupitia matamshi ya viongozi au kamati kuu tu inatosha kuonyesha dhamira ya dhati ya uwajibikaji kwa wapiga kura na matumizi mazima ya Demokrasia huru kupitia mfumo wa vyama vingi na mawazo huru?
Sababu ya kufukuzwa=Ameenda kinyume na ILANI, SERA pamoja na Maazimio ya CDM..kama mtu akienda kinyume na ilani ya chama chake mojakwamoja kwenye kampeni zilizopita ulikuwa unadanganya wapiga kura wako..mfano kipindi cha kampeni, Shibuda angesimama na KUSEMA "NATAKA POSHO ZIONGEZWE KWA WABUNGE" je wewe Ben Ungempa kura yako?
Asipofukuzwa kuna madhara mengi sana mfano mimi mpaka sasa sina imani na shibuda hata kidogo.
Mtindo wa kumfukuza=Apewe barua inayosema yeye sio mwaminifu kwa chama chake then barua imtake arudishe kadi ya chama halafu ndio mwisho wa mchezo huo.
 
Zitto amepotoka kidogo kwenye hili, hamuwezi mkajenga chama chenye watu wenye mawazo sawa, utakapokuwa na chama cha upinzani na viongozi wake wakawa wanakubaliana kila wakati, fahamu kuwa chama hicho bado hakina wigo mkubwa wa kiuongozi,na kadri kitakavyoendelea kuwa hivyo ndivyo kinavyozidi kufunga milango kwa watu wengine kujiunga na chama hicho na hivyo kujifungia milango ya kuuonyesha umma mtandao mkubwa wa kiuongozi uliotayari kuchukua nchi...Hii sio issue yenye hadhi ya kujadili kwenye kikao kikubwa kama cha kamati kuu, unless kama hawana vitu vya maana vya kuongelea so wameamua wauze chai tu...; ingetosha tu kupotezea kwa kusema msimamo wa chama ni kufutwa kwa posho zotejapo mbunge mmoja mmoja anaweza akawa na mawazo yake binafsi, unless kama kuna hoja nyingine kubwa kuliko hii na hili la posho linatumika tu kama kisingizio cha kumfukuza...
Hii point usingeitoa wewe ningeigongea ka-like. Hujawahi kuwa na mapenzi mema na chadema hata siku moja
 
Jana hapa jamvini alizushiwa karudi ccm, thread yake imechakachuliwa; leo akifukuzwa tutaambiwa alishaondoka mwenyewe.
 
Makao makuu CDM mnamiliki maamuzi ya kumfukuza au kutokumfukuza, ama Shibuda ana miliki wapiga kura ambao kwao yeye ndiye jembe lao la ukweli wako tayari kufa nae hata ahame chama chenu. Shibuda ataenda kwa Cheyo na bado atakuwa na vote kubwa sana.
Sio point ya kukubalika na wapiga kura wake, zitto amesema Chedema kinaendeshwa kwa taratibu, kanuni na katiba so kama hawezi aondoke CDM sasa ni chama kikubwa kisipo kisipotenda kulingana na standards na wanacho kiamini kitapoteza sifa na muelekeo wake sasa hivi.
 
Sababu ya kufukuzwa=Ameenda kinyume na ILANI, SERA pamoja na Maazimio ya CDM..kama mtu akienda kinyume na ilani ya chama chake mojakwamoja kwenye kampeni zilizopita ulikuwa unadanganya wapiga kura wako..mfano kipindi cha kampeni, Shibuda angesimama na KUSEMA "NATAKA POSHO ZIONGEZWE KWA WABUNGE" je wewe Ben Ungempa kura yako?
Asipofukuzwa kuna madhara mengi sana mfano mimi mpaka sasa sina imani na shibuda hata kidogo.
Mtindo wa kumfukuza=Apewe barua inayosema yeye sio mwaminifu kwa chama chake then barua imtake arudishe kadi ya chama halafu ndio mwisho wa mchezo huo.

Mkuu nakubaliana na yote uliyosema hapo juu.Tatizo tulilo nalo ni kwamba vyama vya siasa ni lazima tuangalie katiba zetu na kanuni ili kukidhi matakwa halali ya kidemokrasia kwa maana ya kuzingatia demokrasia na falsafa iliyosimama nyuma yake.Hapa chini ni baadhi ya conditions amabzao zinaweza kutoa mwanya na nguvu kwa chadema kumfukuza mbunge yeyote ingawa sitaenda deep kwa sasa kwa sababu maalumu

Kwanza kabisa kuna wajibu kama huu kwa mwanachama:
5.3.4 Kushirikiana na wanachama na viongozi wengine wote katika kutekeleza sera na mipango ya Chama."

.3 MAADILI

Maadili ya Chama ndiyo yatakayoainisha sifa, nidhamu, utii, uwajibikaji na dhamira yawanaChama, watendaji na viongozi wa Chama katika ngazi zote. Maadili haya yanajumuisha uongozi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee.

2.4 ITIFAKI

CHADEMA kama Chama kinachokua na kupanuka kwa kasi kitaifa na chenye nia yakuchukua dola wakati wowote hakina budi kujiwekea taratibu mbalimbali ambazo zitakisaidia Chama kuendesha shughuli zake za Chama katika mtiririko wa aina fulanibila kuonyesha utofauti kati ya viongozi na ngazi mbalimbali za Chama. Nia ya kuwekataratibu hizi ni kuleta umoja na mshikamano ndani ya Chama na kukitambulisha

CHADEMA kama Chama kimoja.
Kwa hiyo itifaki ya Chama inajumuisha pia uongozi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee ambayo ni sehemu tu ya muundo na uongozi wa chama.

Kufukuzwa Uanachama:

5.4.3 Kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake ama ngazi nyingine ya Chama, kwa mujibu wa katiba kwa kukosa sifa za kuendelea kuwa mwanachama ama kuwa na mwenendo usioendana na Itikadi, falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za Chama.

5.4.4 Bila kuathiri kifungu 5.4.3 cha katiba, Kamati Kuu inaweza kumwachisha amakumfukuza mwanachama yeyote kwa utaratibu utakaopangwa na kanuni za Chama.

Hizo ndiyo leaning walls/tables,

Sasa vipi kama tukitoa pendekezo la kutumia mbinu ya kisasa na ya kidemokrasia kwa mapana kwa kuitisha kura ya maoni jimboni ili kujua msimamo wa wanachama na wapiga kura wa jimbo la Maswa kuhuu tabia na mwenendo wa mbunge wao na pia kupata maoni yao juu ya adhabu itakayofaa/chukuliwa dhidi ya Mh.Shibuda

Sijui kama Collin Powel angekuwa mwanachama wa chama cha siasa Tanzania angekuwa nadni ya chama hicho baada ya kumpigia kampeni mgombea wa chama kingine.Je huu si usaliti kwa ideology na sera za chama husika?mwaka jana kwenye kampeni,tujiulize swali ambalo hatutaki au tumesahau kujiuliza,je kuna mgombea yoyote aliyempigia kampeni mgombea wa chama kingine?Tafsiri yake ni nini katika sera,philosophy and ideology of the party?

Julius Malema Mwenyekiti wa vijana wa ANC aliimba pamoja na wafuasi wake wimbo wa 'Kill the boers' ambao unaenda kinyume na falsafa ya sasa ya ANC na serikali yake ya kuponya majeraha ya kibaguzi,na hakufukuzwa lakini waliona fursa ya kum-shape psychologically ili awe fit na balozi mzuri wa kuponyesha majeraha na kujenga taifa moja kwa kutumia fursa komavu za kidemokrasia.

Tujiulize mbona ODM ya kenya hawakumfukuza Willium Ruto na akina Sally kosgei pamoja na sarakasi zote ndani ya chama chao,tuangalie faida waliyoipata as a serious political entity na hasara waliyoipata as a serious & weak political Entity.



 
By the way zitto is not trusted!!! anaonekana kuanzisha makundi ndani ya cdm just kwa kutumia ushawishi kidogo alio nao...Lakini sishangai just see the following analysis of kigoma politicians in cdm
Dr Aman Walid Kaburu------from kigoma....was in CDM kwa unafiki akarudi CCM
David Kafulila....From kigoma.....Was in CDM umbea na kutoa siri za chama caused him to go to NCCR MAGEUZI
Zitto Kabwe...From kigoma.....In CDM now but not Trusted.......to no one knows but i dought magamba part
from above analysis i don't tust zitto
Mkuu siku nyingine usitumie hiyo analysis
Kwamba watu kadhaa wa mkoa fulani wakiharibu basi unafikiri ni kwa sababu wanatoka mkoa huo, labda na wewe ungesema mkoa unaotoka ili kama kuna uwezekano tukupe mfano kama huo.
 
Nimesoma mwananchi uk wa 4 nashangaa zitto anasema shibuda afukuzwe kwa kutofautiana na chama. mimi naona tofauti za mawazo ni kawaida. kama basi ni kosa la kufukuzwa zitto awe wa kwanza maana alizungumza na waandishi kupinga msimamo wa chama wakati shibuda alizungumza bungeni anakolindwa na sheria. zitto anataka chadema ianguke nimwonavyo
zitto alitofautiana na watu sio chama
 
Kulikuwa hakuna haja ya kuzunguka sana kama pia,kwani tangu awali huyu mbunge alionekana ni msaliti, ni bora kuwa na wabunge wachache lakini makini kuliko kuwa na wabunge wengi wasio na maana,apigwe chini halaka iwezekanavyo
 
katika jamii ni lazima tukubali kwamba sio rahisi kwa watu wa itikadi moja kukubaliana kila wazo muda wote,ni lazima kuna wakati wa kutofautiana..jambo la muhimu ni kukaa chini na kutafakari kwa pamoja kupima uzito wa hoja toka pande mbili zilizotofautiana.
 
Mie namuona huyu jamaa ni pandikizi la Magamba ili kuivuruga CHADEMA ambayo magamba sasa hivi wanaiona CDM ni tishio kubwa kwao. Hivyo nitafurahi sana kama CHADEMA wataamua kumtema badala ya ya kuendelea kulea saratani inayokuwa taratibu ndani ya chama.
 
CDM wamuache huyo shibuda au mbunge yeyote ajifukuze mwenyewe.

kinachohitajika ni CDM wafanyae poilitical calcuation sahihi na sio tu waangalie vitabu vinasema nini. Siasa sio engineering

Unless conduct zake zinatishia kabisa uhai wa chama basi wamuache .

Baada ya bunge Cha kufanya CDM wanatakiwa kwenda maswa na majimbo mengine yenye wabunge wao wafanye mkutano kuelezea wamewasilishaje kilio cha wananchi. teh teh teh teh.
 
Lakini mbunge huyu anaonekana kama ni msaliti tangu awali,cdm hawana haja ya kuwa na mbunge kama huyu shibuda atawavuruga sana kwani kila wazo litokalo kwa chadema yeye hulipinga
 
Nadhani Colin Powel angekuwa mwanachama wa chama cha siasa Tanzania angekuwa ameshafukuzwa,pia Julius Malema mwenyekiti wa vijana wa chama cha ANC angekuwa mwanachama wa chama cha siasa Tanzania angekuwa ameshafukuzwa.
Ni kweli kabisa mtu kama julius malema (President - ANC Youth league) kwa siasa za Tanzania angekuwa ameshafukuzwa zamani, ni mtu ambae ana ushawishi mkubwa sana ndani na nje ya ANC, na mara nyingi amekua akitoa mawazo yake nje ya vikao vya ANC ambayo mara nyingi yanapishana na sera za ANC, mfano mzuri ni ile sera ya nationalisation of mines, hii sio sera ya ANC lkn Malema siku zote anaisimamia, na mara nyingi sana amekuwa mstari wa mbele kupinga na kukosoa sera za ANC hadharani ambazo hazileti haki na usawa kwa kwa weusi
 
Ninacho jua mgongano wa mawazo unonyesha watu wanafiri they are not static sasa kwa mchezo huu watafukuza wangapi ? mbona wengi wapo kinyume na mtazamo wa viongozi wakuu wa chama hadi hapo baadaye watakapo elekezwa vizuri kumbuka kuna " faster learners and slow learners " sasa kama kila slow learner atafukuzwa hali itakuwaje

siafiki kabisa kufukuzwa kwa SHIBUDA kwani hajatetea falsafa yake.
 
nawaambia viongozi wa chadema, character ya kiongozi mzuri pamoja na mambo mengine ni uwezo wa kuwa accomodate hata wale wanaotofautiana na msimamo wa chama. kwa kipindi hiki ambacho ccm wana matatizo ya ndani chadema wanapaswa ku take advantage na kuchukua jimbo kama la igunga na la chenge badala ya wao kujidhoofisha kwa migogoro. busara itumike kumaliza mgogoro wa shibuda na arusha bila mtu kutoka chadema
 
We ibange acha bange!
Huyo chupibuda katofautiana na chama, sera na sio mawazo ya watu!

Usiwe mrahisi kama nepi wewe!
 
Back
Top Bottom