CHADEMA fuatilieni historia ya babu zenu walivyofanikiwa kukomboa nchi, laa sivyo mtapotea

Kakende

JF-Expert Member
Aug 18, 2012
2,741
1,231
Ndugu wanajamii Forum kutokana na Sakata la CHADEMA linaloendelea na mimi nimependa kuwaonya wana CHADEMA kama ifuatavyo—
Kama kuna makosa makubwa ambayo yanafanywa na viongozi wa CHADEMA hasa Zitto pamoja na viongozi wengine wasio na Subira ni kuanza ugomvi hata kabla ya AJENDA ya ukombozi haijafanikiwa. Ninaposema ukombozi ninamaanisha kuwa hakuna chama chochote ambacho kimewahi kuwa madarakani zaidi ya CCM. Tunafahamu kuwa hii ni nchi huru lakini tunahitaji chama mbadala ili kupata mbinu mbadala za kimaendeleo lakini pia ushindani.
Bara la Afrika hasa kizazi kipya tumekuwa na tatizo kubwa la tamaa za madaraka na kujilimbikizia mali, tofauti na wazee wetu waliokomboa nchi kutoka ukoloni, ninacho kiona CHADEMA ni tamaa ya madaraka wakati chama bado hakijafikia AJENDA ya kuchukua dola. Vijana na Watanzania wa aina mbalimbali taratibu walianza kuweka mioyo yao kwa CHADEMA lakini sasa baadhi tunaanza kuwa na wasiwasi juu ya mwenendo wa chama.
CHADEMA na Watanzania naomba mfuatilie historia ya vyama vya kiukombozi vilivyopigania haki na vita dhidi ya ukoloni. Vyama hivi vilihakikisha vinapambana hadi dakika ya mwisho bila kugawanyika. Mifano modogo ni Enzi za akina Karume na Nyerere, hawa wazee wetu walikuwa na subirá, wakati Nyerere anakuwa mwenyekiti wa Tanu si kwamba enzi zake hapakuwa na watu wenye uwezo wa kuwa wenyeviti. Wakati Nyerere anapendekezwa kuwa Rais kwa miaka 20 na kitu si kwamba katika Chama hapakuwa na watu wenye uwezo, lakini wazee wetu hawa walikuwa na subirá kwa maana walikuwa wanafahamu kuwa mapigano kati yao yangewatoa kwenye AJENDA. Wazee wetu walihamua hadi kuunganisha vyama vyao ili wawe na AJENDA moja

Mfano mwingine ni huu wa Akina Nelson Mandela, wakati Nelson Mandela anapigania uhuru si kwamba alikuwa peke yake, lakini wenzie walimuamini wakampa ngazi ya juu ANC. Wakati Nelson Mandela anatoka gerezani wanachama wote waliamini kuwa sasa wanakwenda kupewa nchi,lakini kwa miaka minne baada ya Mandela kuachiwa huru, ndani ya ANC kulikuwa na akina Jacob Zuma, Tabo Mbeki ambao pia wangeweza kugombea Urais, lakini walikuwa wavumilivu wakampa Mandela nafasi.

Hata wanyama wawindao wana akili. Mfano Simba, wakiwa wanawinda huwa wanashirikiana vizuri, kwenye kukimbiza mnyama huwa hawatofautiani, huwa inatokea kwa nadra sana wakagombania nyama baada ya kufanikiwa kumkamata mnyama waliekuwa wanawinda. Hivi kama wangeanza kupigana wakati wakiwa kwenye kukimbiza wangemkamata Swala?

Kuhusu Zitto.
Mimi nakubaliana na Demokrasia ndani ya chama. Sisi wanachama wa kawaida hatuoni kama kuna tatizo ndani ya chama kwa maana tunaona mambo yanakwenda sawa, tunaona umaarufu wa chama unaongezeka, operasheni mbalimbali nchi nzima zinaendelea vizuri. Hayo mnayogombania sisi tunayashangaa maana tunaona CHADEMA inafanya operasheni nyingi kuliko chama chochote Afrika. Sasa tatizo liko wapi?. Mheshimiwa Zitto na wenzako ambao mnadhani CHADEMA imekomaa sasa ni wakati wa kugombania madaraka mnajidanganya, CCM bado inawanachama wengi, kuna watu vijijini wana kura nyingi za CCM. Zito na wenzako, wewe kama kijana mdogo ambae umeanza siasa tukiwa tunakutazama, mimi naamini ungekuwa mvumilivu kwanza kwa kuwa umri wako kwanza ni mdogo, bado una chance. Kwa busara kabisa ungewaachia wakubwa zako kisiasa kwanza kama ilivyo vyama vyote vilivyokuwa na movement ya kukomboa nchi, mimi ninaamini kabisa kuwa bila hawa wakongwe kwenye chama CHADEMA itapoteza umaarufu mara moja. Namalizia kwa kusema kuwa, mkianza kufarakana wenyewe kwa wenyewe hamtafika kokote. Msizidiwe akili na wanyama wawindao.
 
Back
Top Bottom