CHADEMA flip flopping at its best! Jisomee mwenyewe uone

next tym b sure of usemayo...una uhakika hiyo kamati iliyoundwa members wake hawana uhusiano na watuhumiwa???ndo yale yale kesi ya ngedere anapewa nyani

Mkuu kama maneno yako ni kweli basi wanakamati hiyo wanahitajika kutoka nchi nyingine, hivi ni nani Tanzania asiyemjua mwingine? Eti ni jaji wa mahakama gani bongo hamjui kiongozi yoyote wa CCM au upinzani? Sasa kesi zao tukazifanyie wapi?

Mkuu nadhani kumjua mtu siyo tatizo, tatizo linakuja pale ambapo wana uhusiano wa namna moja au nyingine kama vile biashara n.k. Labda huyo aliyesema kuwa kuna baadhi ya wanakamati wana uhusiano na mafisadi angetuwekea bayana huo uhusiano uliopo then tujadili.
 
ES hapo kweli umenena, pale ni nani asiyemjua mwingine ? maana sasa zitto kuwemo kwenye hiyo kamati kumekuwa tatizo, sasa wanaleta vioja vingine. and am sure tutasikia mengi tu soon !
 
Unafanya kazi nzuri ya mabwana(masters) wako eeeheh

Soma vizuri kauli ya Slaa "CHADEMA tunaona ni vyema Zitto akakubali kuwa mjumbe wa kamati hiyo, na pale tutakapoona vinginevyo, tutashauriana", unaelewa maana yake?

Soma katiba ya CHADEMA uone wasemaji wakuu wa chama ni wakina nani lakini utaona katika katiba hiyo pia wanachama wana haki ya kutoa maoni.

Mwanakijiji, mtafute Lissu ufanye naye mahojiano tujue ukweli na UNDANI wa alichokisema DDC Mlimani, mi siliamini kabisa MAJIRA!

CHADEMA mko wapi? Njooni mtoe ufafanuzi

Asha

lakini tanzania daima unaliamini, right ??
you need to DUMB IT DOWN BABY !!!!!!!!!!

tena nitafurahi sana huyo mwanakijiji akimtafuta huyo jamaa akamuintavyuu (asije tu akasema bandwith imekwisha, lol)!! hakuna misquotations made dada, au unataka na akina karamagi nao waseme walikuwa misquoted juu ya skendo zima lile ??
 
next tym b sure of usemayo...una uhakika hiyo kamati iliyoundwa members wake hawana uhusiano na watuhumiwa???ndo yale yale kesi ya ngedere anapewa nyani

Mkuu kama maneno yako ni kweli basi wanakamati hiyo wanahitajika kutoka nchi nyingine, hivi ni nani Tanzania asiyemjua mwingine? Eti ni jaji wa mahakama gani bongo hamjui kiongozi yoyote wa CCM au upinzani? Sasa kesi zao tukazifanyie wapi?

Mkuu heshima mbele. Tatizo lililopo siyo la nani kumjua na nani bali baadhi ya wanakamati ndio waliohusika na madudu yaliyofanywa kuhusiana na mikataba ya madini. Pia miaka ya nyuma wameshawahi kuwemo kwenye kamati za madini ambazo ripoti zake hazijatangazwa kwa Watanzania. Hivi kweli hakuna Watanzania wengine wenye sifa za kuwemo katika kamati hiyo!? Hao waliohusika na kuandika mikataba feki kwa nini tena wawemo kwenye kamati hiyo!? Sidhani kama Lissu anaweza kutoa data kama hizi bila kuwa na ushahidi wa uhakika wa kile anachozungumza. soma hapa chini.

Mwanasheria Tundu Lissu, ambaye aliposimama kuzungumza alishangiliwa na mamia ya washiriki wa kongamano hilo, alisema haungi mkono kuwepo kwa kamati hiyo na haikupaswa kuwepo, huku akiwachambua wajumbe wake, mmoja baada ya mwingine.

"Tuna historia ya ‘ku-miss use' hizi kamati, inapaswa tujiulize hii kamati ya Zitto ni ya nini wakati kuna kamati nyingine tano zinazohusu masuala ya madini zilishaundwa na zimewasilisha ripoti zao, lakini hazijawekwa wazi mpaka leo na hatujui nini ripoti hizo zimependekeza?" alisema.

Lissu aliitaja kamati ya kwanza kuwa iliundwa mwaka 2001 chini ya uenyekiti wa Jenerali Mboma, ambayo ilikamilisha kazi yake, lakini mpaka leo ripoti yake haijawekwa hadharani.

Alisema mwaka 2002 kamati nyingine iliundwa na mwenyekiti wake alikuwa Brigedia Mang'enya, ambayo ilitoa ripoti yake kimya kimya mwaka 2003 na haijulikani nayo ilipendekeza kitu gani.

"Kamati ya tatu iliyoundwa ni ile iliyoongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1994-1995, Dk. Jonas Kipokola. Mmoja wa wajumbe wake kwa sasa anaonekana tena kwenye Kamati ya Zitto… Maria Kejo alikuwepo kwenye kamati hii… ripoti haijatolewa," alisema Lisu huku akionekana kusikitika.

Lissu, katika madai yake alimuelezea Kejo kuwa ndiye aliyehusika kusaini mkataba mbovu wa IPTL, hivyo kuteuliwa kwake katika kamati hiyo, kunaonyesha jinsi Rais Kikwete alivyofanya uteuzi wenye shaka.

"Maria Kejo, miaka ya 1994/95 alijibadilisha jina akijiita Maria Ndosi, miaka ya hivi karibuni ameanza tena kujiita Maria Kejo, huyu ndiye aliyehusika kusaini mkataba wa IPTL, hii ipo kwenye ripoti ya Transparence International ya IPTL, na kwamba zipo kumbukumbu zinazoonyesha kuwa alihusika kuwashawishi baadhi ya viongozi kuchukua rushwa ili mkataba huo usainiwe.

Mjumbe mwingine aliyetajwa na Lissu kuwa hafai kuwa kamati hiyo, ni Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic (UDP), John Momose Cheyo, kwa vile alikuwa mpiga debe mkubwa wa kusainiwa kwa IPTL.

Akizungumza kuhusu ushiriki wa Zitto katika kamati hiyo, alisema bila kuingia kiundani kuwa, uteuzi wake hauna maana kwa sababu hana cha kufanya katika kamati hiyo iliyojaa tuhuma nzito za rushwa.

Lissu pia alimgusa Machunde akidai kuwa ni hatari kuwa katika kamati hiyo kwa vile kuna ushahidi wa kualikwa kwake bungeni na Karamagi kwa ajili ya kushawishi baadhi wa wabunge wasilivalie njuga suala la Richmond.

Mwingine aliyetajwa katika orodha hiyo ya kutofaa kuwa katika kamati hiyo ni Salome Makange, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini anayedaiwa na Lissu kuwa si muadilifu na kwamba ni mmoja wa watu waliohusika kusaini mkataba wa Buzwagi.

"Mkataba wa Buzwagi au wowote ule ni lazima usainiwe na mwanasheria wa wizara, leo wapo kwenye kamati… Mark Bomani (Jaji) ambaye ni Mweyekiti wa Kamati hiyo, historia inaonyesha kuwa ni mwana CCM na Harrison Mwakyembe hajawahi kusema chochote kuhusu madini. Tume inakwenda kufanya nini, haina ‘term of reference?" alihoji Lissu.

Alisema mbali na wajumbe wa kamati hiyo kutokuwa na sifa, hata muundo wa kamati yenyewe hauna nguvu za kutosha za kufanya kazi kwa uhuru na uwazi.

Alisema kama Rais Kikwete ana nia ya dhati ya kuunda kamati ya kupitia mikataba ya madini, anapaswa kuunda kamati teule ya Bunge ambayo ina mamlaka na nguvu kisheria za kumuita mtu yeyote na kumhoji.

"Kamati ya Bunge ina nguvu, kwenye kamati hii unaweza kumuita Karamagi na ukamwambia lete mikataba, akikataa unamfunga, Kamati ya Rais haina ‘judicial power', mimi naona rais anajitakasa tu kwa wananchi," alisema Lissu.
 
Hata mimi nilikuwa najiuliza hivi ni kwa nini kila skendo inaundiwa kamati...yaani kamati kibao zishaundwa bongo lakini hatima zake hazijulikani. Eti hata rushwa iliundiwa kamati..ipo siku itaundwa kamati kuchunguza picha za Kikwete alizonazo Mwanakijiji kama ni za kweli....tehehetehe
 
Hiyo ni danganya toto kuwanyamazisha wananchi.Kwamba hapo kuna miezi kama mitatu ya kupumua na mingine kama mitatu ya kusoma na kuitafakari ripoti,na mingine tena.....na mingine ya kuiweka ripoti kabatini, mpaka unashtukia 2010 hii hapa, uchaguzi tena na mbinu chafu za kutwaa dola zinaanza tena.
 
Acheni kupayuka, Chadema mnajua wazi hamna chochote sasa mmeanza.

Zitto kama anafikiria mbele ajiuzulu kutoka ktk kamati hiyo (akae uteuzi)

Anajikaanga na mafuta yake mwenyewe!
 
na kilichobaki hapa ni kwamba aidha zitto hajui awe pande gani lakini watu wanajifanya kama kutoa maoni then baadae zitto ajifanye kumake choice kuonekana kwamba watu walimtaka afanye hiyo decision !
sasa wanatapatapa !
 
Dawa ya kuondoa aibu na uzushi aliouzua bungeni ni kujitoa tu..

Ni afadhali nini kuliko fedhea vile? aibu kuliko fedhea au fedhea kuliko aibu? kiswahili kigumu! kwi kwi kwii
 
Ama kweli MJENGA NCHI ni MWANANCHI na MVUNJA NCHI NI MWANANCHI PIA.La msingi hapa sio the so-called flip-flopping ya CHADEMA bali whether hao wajumbe watakaokabidhiwa mamilioni ya taxpayers' money watatekeleza kile kinachokusudiwa.Let's be honest,kama mtu alishiriki kuandaa mkataba mchafu like ule wa Buzwagi,then ukimchagua kwenye tume ya kupitia mikataba,hapo tutarajie nini?

Siku zote nimekuwa nakerwa sana na watu wanaoweka mahaba ya kisiasa mbele ya maslahi ya nchi.Suppose tume hiyo isingekuwa na mjumbe kutoka chama cha upinzani,je kwa wenye mapenzi na nchi na wanaowajua wajumbe wa tume hiyo wanaweza kuturidhisha kuwa malengo yatafanikiwa?Lissu amezungumzia pia powerlessness ya tume hiyo,lakini hilo sijaliona hapa pengine kwa vile aliyelizungumzia hachukuliwi kama mwanasheria bali kiongozi wa CHADEMA.

CHADEMA may die,and so is CCM,but TANZANIA should there to stay by hooks and crooks.Let's act like grown-up patriots who think beyond party lines.

As to CHADEMA's internal affairs,mie naiona kama hatua kubwa ya demokrasia ndani ya chama cha siasa kwani tumezowea kuona unafiki uliotawala ndani ya CCM ambapo disgruntled leaders tend to keep quiet kuhofia "adhabu hewa" according to MSEKWA.Na pengine mfano mzuri ni Kamati ya Shelukindo ambayo japo almost a year ago ilisha-smell something fishy about mkataba wa Richmond bado ilikaa kimya na kukurupuka muda huu.Whta if wangeibua hoja zao kipindi kile tunazugwa kuwa Richmond wataanza kuzalisha umeme next week,mara next month,etc?Nadhani mchango wa yule mbunge Shelukindo "wa kike" sums it all.

When it comes to ubabaishaji katika maamuzi ya viongozi wetu,tunaoumia ni sote kama watanzania na wala sio wana-CHADEMA,CCM au CUF pekee.
 
next tym b sure of usemayo...una uhakika hiyo kamati iliyoundwa members wake hawana uhusiano na watuhumiwa???ndo yale yale kesi ya ngedere anapewa nyani

Mkuu kama maneno yako ni kweli basi wanakamati hiyo wanahitajika kutoka nchi nyingine, hivi ni nani Tanzania asiyemjua mwingine? Eti ni jaji wa mahakama gani bongo hamjui kiongozi yoyote wa CCM au upinzani? Sasa kesi zao tukazifanyie wapi?

waonaje tukazileta Kwako????!!!
 
Mkuu nadhani kumjua mtu siyo tatizo, tatizo linakuja pale ambapo wana uhusiano wa namna moja au nyingine kama vile biashara n.k. Labda huyo aliyesema kuwa kuna baadhi ya wanakamati wana uhusiano na mafisadi angetuwekea bayana huo uhusiano uliopo then tujadili.

point!!!!lets wait n see as lisemwalo lipo its just a matter of time
 
Mkuu heshima mbele. Tatizo lililopo siyo la nani kumjua na nani bali baadhi ya wanakamati ndio waliohusika na madudu yaliyofanywa kuhusiana na mikataba ya madini. Pia miaka ya nyuma wameshawahi kuwemo kwenye kamati za madini ambazo ripoti zake hazijatangazwa kwa Watanzania. Hivi kweli hakuna Watanzania wengine wenye sifa za kuwemo katika kamati hiyo!? Hao waliohusika na kuandika mikataba feki kwa nini tena wawemo kwenye kamati hiyo!? Sidhani kama Lissu anaweza kutoa data kama hizi bila kuwa na ushahidi wa uhakika wa kile anachozungumza. soma hapa chini.

Mwanasheria Tundu Lissu, ambaye aliposimama kuzungumza alishangiliwa na mamia ya washiriki wa kongamano hilo, alisema haungi mkono kuwepo kwa kamati hiyo na haikupaswa kuwepo, huku akiwachambua wajumbe wake, mmoja baada ya mwingine.

“Tuna historia ya ‘ku-miss use’ hizi kamati, inapaswa tujiulize hii kamati ya Zitto ni ya nini wakati kuna kamati nyingine tano zinazohusu masuala ya madini zilishaundwa na zimewasilisha ripoti zao, lakini hazijawekwa wazi mpaka leo na hatujui nini ripoti hizo zimependekeza?” alisema.

Lissu aliitaja kamati ya kwanza kuwa iliundwa mwaka 2001 chini ya uenyekiti wa Jenerali Mboma, ambayo ilikamilisha kazi yake, lakini mpaka leo ripoti yake haijawekwa hadharani.

Alisema mwaka 2002 kamati nyingine iliundwa na mwenyekiti wake alikuwa Brigedia Mang’enya, ambayo ilitoa ripoti yake kimya kimya mwaka 2003 na haijulikani nayo ilipendekeza kitu gani.

“Kamati ya tatu iliyoundwa ni ile iliyoongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1994-1995, Dk. Jonas Kipokola. Mmoja wa wajumbe wake kwa sasa anaonekana tena kwenye Kamati ya Zitto… Maria Kejo alikuwepo kwenye kamati hii… ripoti haijatolewa,” alisema Lisu huku akionekana kusikitika.

Lissu, katika madai yake alimuelezea Kejo kuwa ndiye aliyehusika kusaini mkataba mbovu wa IPTL, hivyo kuteuliwa kwake katika kamati hiyo, kunaonyesha jinsi Rais Kikwete alivyofanya uteuzi wenye shaka.

“Maria Kejo, miaka ya 1994/95 alijibadilisha jina akijiita Maria Ndosi, miaka ya hivi karibuni ameanza tena kujiita Maria Kejo, huyu ndiye aliyehusika kusaini mkataba wa IPTL, hii ipo kwenye ripoti ya Transparence International ya IPTL, na kwamba zipo kumbukumbu zinazoonyesha kuwa alihusika kuwashawishi baadhi ya viongozi kuchukua rushwa ili mkataba huo usainiwe.

Mjumbe mwingine aliyetajwa na Lissu kuwa hafai kuwa kamati hiyo, ni Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic (UDP), John Momose Cheyo, kwa vile alikuwa mpiga debe mkubwa wa kusainiwa kwa IPTL.

Akizungumza kuhusu ushiriki wa Zitto katika kamati hiyo, alisema bila kuingia kiundani kuwa, uteuzi wake hauna maana kwa sababu hana cha kufanya katika kamati hiyo iliyojaa tuhuma nzito za rushwa.

Lissu pia alimgusa Machunde akidai kuwa ni hatari kuwa katika kamati hiyo kwa vile kuna ushahidi wa kualikwa kwake bungeni na Karamagi kwa ajili ya kushawishi baadhi wa wabunge wasilivalie njuga suala la Richmond.

Mwingine aliyetajwa katika orodha hiyo ya kutofaa kuwa katika kamati hiyo ni Salome Makange, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini anayedaiwa na Lissu kuwa si muadilifu na kwamba ni mmoja wa watu waliohusika kusaini mkataba wa Buzwagi.

“Mkataba wa Buzwagi au wowote ule ni lazima usainiwe na mwanasheria wa wizara, leo wapo kwenye kamati… Mark Bomani (Jaji) ambaye ni Mweyekiti wa Kamati hiyo, historia inaonyesha kuwa ni mwana CCM na Harrison Mwakyembe hajawahi kusema chochote kuhusu madini. Tume inakwenda kufanya nini, haina ‘term of reference?” alihoji Lissu.

Alisema mbali na wajumbe wa kamati hiyo kutokuwa na sifa, hata muundo wa kamati yenyewe hauna nguvu za kutosha za kufanya kazi kwa uhuru na uwazi.

Alisema kama Rais Kikwete ana nia ya dhati ya kuunda kamati ya kupitia mikataba ya madini, anapaswa kuunda kamati teule ya Bunge ambayo ina mamlaka na nguvu kisheria za kumuita mtu yeyote na kumhoji.

“Kamati ya Bunge ina nguvu, kwenye kamati hii unaweza kumuita Karamagi na ukamwambia lete mikataba, akikataa unamfunga, Kamati ya Rais haina ‘judicial power’, mimi naona rais anajitakasa tu kwa wananchi,” alisema Lissu.

i support you ni just kuwafanyia mazingaombwe watz kwa kuunda kamatiz kede kede zikispend fweza nyiiiingi for nothing...
 
Acheni kupayuka, Chadema mnajua wazi hamna chochote sasa mmeanza.

Mkuu hapa sasa unaleta unazi,hivi kweli wewemkuu unasurpport udiktete uliopo ndani ya CCM huku unasema unataka kuweka mbele maslahi ya taifa?Unajua mkuu watu kama ninyi ndio mlioifikisha ccm ilipo? Na ndio maana leo hii hali ya kimaisha na umaskini uliokithiri kwa wananchi nasema sehemu kubwa ya lawama CCM itabeba.Kama CCM wanaweza kuzuia wabunge wao kusema,je kwA mwananchi wa kawaida asiyejua ni nini maana ya Demokrasia itakuaje? Ndio maana Elimu ya urai kw wananchi inakua ni mwiba kwa CCM.

Zitto kama anafikiria mbele ajiuzulu kutoka ktk kamati hiyo (akae uteuzi)

Mkuu acha kutia aibu,hapa umetia aibu.Ajiuzulu ili iweje?Wewe mkuu kweli ndio una dhamira ya kuleta fikra za kulikomboa taifa letu lililodumazwa kwa miaka 46? Hoja ya maana ni kwamba Zitto aingie humo humo awe na msimamo wake afanye mambo yanayofaa kufanywa na mzalendo wa kweli ingawa ameteuliwa kimtego lakini anaweza kufanya mabo ambayo hawakutarajia.Aliibua hoja bungeni na kama ni kujitoa atajitoa pale atakapoona kuna kiini macho kutoka kwa wale waliomzunguka.Pale akapoona kuna mwenendo usio wa kizalendo unaofanywa na wale wajumbbe wengine kama walivyozoea according to their backgrounds

Anajikaanga na mafuta yake mwenyewe!

Mkuu,mbona unaleta vitisho! Kwani ina maana huyo aliyemteua alikua na matarajio gani?Mbona watu mnataka kuandika kana kwamba mnaweza hata kupiga parapanda ya mwisho?

Kwani lengo la kumteua zitto kwenye hiyo kamati lilikua ni nini?
 
sidhani kama kuna vitisho vyovyote vile vilivyotolewa humu !

tuendeleeni salama kujadili ishuz !
 
CCM wajanja sana, wameamua kutumia media kupunguza umaarufu wa kijana zito na kutaka kukitia porojo za migogoro chama cha demokrasia na maendeleo. Hakika wanapoteza muda tu, zitto na chadema vitaendelea kuwa imara zaidi pamoja na kuwepo propaganda hizi za kizushi. Naamini baada ya miezi hiyo mitatu, zitto kama si kamati nzima lazima itaibuzwagi mikataba mibovu.

Hivi wewe kada unayedisplay passport huna kazi nyingine za kufanya nini, 24hrs unarespond kwenye JF, kila thread upo, du!! Ina maada umeajiliwa na mafisadi, hadi breakfast, lunch na dinner wanakuletea ukiwa unacheza na kiboard ya pc amd laptop ulogawiwa na mafisadi.
 
Mkuu heshima mbele. Tatizo lililopo siyo la nani kumjua na nani bali baadhi ya wanakamati ndio waliohusika na madudu yaliyofanywa kuhusiana na mikataba ya madini. . Hivi kweli hakuna Watanzania wengine wenye sifa za kuwemo katika kamati hiyo!? Hao waliohusika na kuandika mikataba feki kwa nini tena wawemo kwenye kamati hiyo!? Sidhani kama Lissu anaweza kutoa data kama hizi bila kuwa na ushahidi wa uhakika wa kile anachozungumza. soma hapa chini.

Wakuu hebu muende mukaziweke priroties zenu sawa, maana kila mnalopewa hamtaki, mmelilia kamati imetolewa, sasa kwa nini hamkusema then ni nani wawemo kwenye kamati maana inaonekana kuwa ni nyinyi tu wenye ukweli, uchungu na nchi, yaani kila kitu kizuri kwa taifa mnakijua nyinyi tu, wengine wote hapana,

yaaani sasa mpaka mwenyekiti wenu wenyewe wa vyama vya upinzani Cheyo, hafai sasa kweli mnategemea wananchi tuwachukulie serious? Lisu ni nani? Wakuu sasa tukae kusubiri mkao wa kusikiliza results za kamati, halafu tutaangalia from there.
 
Hivi wewe kada unayedisplay passport huna kazi nyingine za kufanya nini, 24hrs unarespond kwenye JF, kila thread upo, du!! Ina maada umeajiliwa na mafisadi, hadi breakfast, lunch na dinner wanakuletea ukiwa unacheza na kiboard ya pc amd laptop ulogawiwa na mafisadi.

Yupo kwenye payroll ya chama dume cha mafisadi....teh teh teh
 
chama dume

Better kuliko majina mengine yote ambayo yanatushusha hadhi wananchi tulioichagua CCM kututawala, kwa kuzikubali sera zake na kuzikataa sera za vyama vingine, Chadema included.
 
Back
Top Bottom