Kasheshe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 4,694
- 787
Ooo pu!, Nashukuru, nilisahau kaka yangu kwamba na wewe ulikuwa CCM, kwa ridhaa yako ukaondoka, alafu kwa ridhaa yako pia waweza urudi huko CCM... kweli bwana Katiba ina[wa|ku]lindai) Siasa ni mapenzi ya mtu ndugu yangu. Vyama vya upinzani sio walinzi wa kuhakikisha watu hawarudi CCM. Ni jukumu la mtu mwenyewe kuamua anataka chama gani na yupo huru kuhama na kuhamia chama kimoja kwenda kingine wakati wowote. Kwa hiyo Njelu Kasaka alikuwa na hiari ya kutoka CCM na kurudi huko kama alivyofanya kwa jinsi akili yake ilivyomtuma. Kwa vyovyote vile upinzani haukupaswa kuwajibika na wala sasa hauwajibiki kumlinda Kasaka asirudi CCM. Hiyo ni juu yake.
Kwa vyovyote vile mimi siye kabisaaa niondoe huko, angalia sijawahi thubutu hata kuwa mwanachama wa chama kimojawapo kama wewe ambaye tayari umeshakuwa mwanachama wa at-least vyama viwili..ii) In the second issue, you are really missing the point. Binafsi sipo hapa kutafuta kura. This is not a vote fetching forum. We are exchanging views about the fate of our beloved country. Kama wewe upo hapa kukitafutia chama fulani kura, endelea lakini usifikiri na wengine tunafanya kazi hiyo.
Lakini Nashukuru kwa kujua kwama kumbe hapa ni ThinkTank yenu,,,
iii) Niseme pia hili maana linajirudiarudia sana. Katika upinzani na hasa CHADEMA tunaamini katika tofauti ya mawazo, maadili na unyoofu. Hatuamini katika ghiliba. Kwa hiyo hatupo tayari kupata kura kwa ghiliba, na kama ghiliba ndio njia pekee ya kushinda uchaguzi Tanzania basi tupo tayari tubaki kuwa wapinzani milele! Tutauza mawazo yetu na wananchi watatupima kwa yale tunayoyafikiri, kusema na kuyatenda. Tunatekeleza wajibu wetu kama chama, uamuzi bado ni wananchi wenyewe.
Saafi sana, nimeipenda sana, umeiweka vizuri, kwa kweli umuandishi mzuri, na mpangiliaji point mzuri,,, naomba tu ili niipate kwa msisitizo unielekeze kwenye kifungu cha katiba yenu ili niweze kuhakiki kwamba hii ni kauli ya CHADEMA na wala sio kwamba ni imani yako,,, wakati wengine probably sio hivyo... Otherwise Nakuaminia ndugu yangu.
URL inatosha sana mkuu sipendi kukuchosha.