Chadema CUF TLP NCCR - LIVE from Urafiki Social Hall

Lunyungu
Pengine huhusiki sana, lakini kuna katatizo kadogo ka kiufundi sehemu fulani kwenye hiyo ripoti. Wanapohitimisha maelezo juu ya kampuni ya Deep Green...(sisiem colour), wanasema katika kipindi cha miezi 4 ziliingizwa shilingi....namba iliyowekwa ni milioni kumi na ushee. Nadhani walimaanisha us dola milioni kumi, au shing za kibongo...bilioni zaidi ya 10.
 
I think you are right!
 
Tukumbuke wakati huo Mkapa alikuwa bado ni incharge,tukumbuke kuwa kuna malalamiko ya rushwa wakati wa uteuzi,yaani mgombea mmoja aliitwa ATM sasa mjue kuwa mlikuwa mnakaangwa kwa mafuta yenu wenyewe.Kwa jinsi mambo haya yalivyo ni wazi kabisa JK anatajwa kama beneficiary atatumia kila linalowezekana kuzima hoja hizi hii pia inanikumbusha kauli yake kuwa mwacheni Mkapa apumzike kumbe sasa tumejua Mkapa ndo 'mentor' wake kwenye mambo ya ufisadi.Kuna mtu aliyeuliza nani ali-mastermind hizi dili,kwa ushahidi wa kimazingira inawezekana-IKULU na TISS ndo vinara wakiwa bega kwa bega na BoT,Wizara ya fedha,Mwanasheria Mkuu ,Wizara Nishati na Madini na Mambo ya nje zinaingia moja kwa moja.Ikumbukwe kwamba viongozi wengi kwenye taasisi na wizara hapo juu wametajwa pia kama viongozi/wanahisa TANGOLD.
 
mie nimeshawaambia hawana chao, na weshalijua hilo, hawa kazi yao kumwaga sumu tu, lkn wananchi wa tanzania wako macho sana hadi masaa ya usiku.

na safari hii watajua nani washenga wa mabibi zao

Excellent job,naona majemadari wanaoongoza vita dhidi ya ufisadi wameshika mahali penyewe,kazi wanayo mafisadi na washenga wao
 
Lunyungu,

Hata mimi ningetegemea kama uchaguzi wa nafasi za udiwani ni leo, basi viongozi karibu wote wa upinzani wangelikuwa huko mikoani kujaribu kunyakua hivyo viti.

Hii ni nafasi ya kwanza tokea suala la Zitto kufukuzwa bungeni, mungeitumia nafasi hii kutoa kipigo kwa CCM. Lakini kama viongozi wakuu karibu wote mmejazana Dar, naona inaweza kuwa ngumu sana kuishinda CCM huko vijijini.

Hii habari si mungeweza hata kutangaza mkiwa huko mikoani? Maana siku hizi hata huko sasa mnapata publicity ya kutosha.

Taarifa ya leo ni muhimu sana kwa taifa, lakini pia kuanza kushinda viti ni jambo muhimu. Mungeweza kuua ndege wawili kwa jiwe moja.

Tatizo akisema masatu, basi watu ni mawe tu bila hata kuangalia logic iliyoko kwenye hoja yake.
 
Ukiona watu wanaanza kupandisha munkari na jazba ujue wamekamatwa pabaya.Suala la ufisadi sasa limekuwa kawaida kwa baadhi ya wana-CCM kiasi kwamba wanaona ni jambo dogo kulinganisha na uchaguzi wa udiwani.Kwa sasa main topic ni hiyo post ya awali inayohusu yaliyojiri kwenye mkutano wa Viongozi wa upinzani na waandishi.Tunategemea kuona hapa taarifa na ushahidi wa kinyaraka zinazoonyesha uongo wa hawa viongozi wa upinzani kuhusiana na taarifa ya leo na si mambo ya uchaguzi wa madiwani,tathmini ya uchaguzi wa madiwani itajadiliwa kwa wakati wake
 
Kuhusu uchaguzi wa madiwani 16 nafikiri Wapinzani walipeleka swala hili mahakamani na sidhani kama tayari korti imesha pitisha maamuzi yake. Sasa imekuwaje kuwepo na uchaguzi huu ama ndio nimepitwa na taarifa zilizofuatia.

Ndugu Wapenzi wa CCM, hili swala ni zito kuliko chaguzi hizi kama mnavyoweza kumpeleka JK nchi za nje na El kuwa ofisini mwake akipata lunch na viongozi wengine wakiweka sahihi mikataba haraka haraka kabla ya zengwe halijapatiwa kikomo. Huyo diwani ataongoza kitu gani ikiwa nchi ni muflis... si ndio yale ya kusema Diwani fulani hafai hata kwa kulumangia!.. Huo udiwani chukueni lakini mchekecho utapokuja tokea pumba zote ikiwa ni pamoja na chaguzi kama hizi zitajitenga. Tunaanza na juu huko chini kutanyooka bila hata joto kali.
Vipi mnakuwa wepesi kutazama viongozi wa Upinzani ktk chaguzi za madiwani 16 lakini sio viongozi wa CCM ambao sii ajabu tayari fedha za benki zimeisha miminwa ktk wilaya zao kuhakikisha Ushindi pasipo kusimamisha Ufisadi.
 
kilitime,

sina uhakika kama upande wa pili utaweza kutoa majibu ya hizo tuhuma/shutuma, labda ambacho wanachoweza kufanya ni kutoa blanket statement itakayo-cover yote. jibu lililo rahisi kwao ni kusema kwamba walishatoa ufafanuzi bungeni au walijibu wakati ule wa list ya mafisadi na huo ndiyo utakuwa mwisho wa mchezo.

Ni kweli unaweza kuwa mchezo wa muda mrefu na inawezekana siri hizo zimevuja kutokana na mambo tunayoyaona sasa yakitokea na hivyo kuna watu wamevujisha siri za namna ambavyo mchezo mchafu huwa unafanyika.

Swali langu ni moja, hizo details za kibenki wapinzani wanawezaje kuzi-access wakati huwa ni siri kati ya benki na mteja wake? Nadhani mambo yamekuwa magumu na kwanini hizo account zote ziende kufunguliwa NBC? Kwanini wasifungue kwenye benki nyingine?

Kama wapinzani wanahisi kwamba fedha hizo zilitumika kwa ajili ya kampeni, je, JK na vyombo vyake vya dola vitakubali kufanyia kazi hizo tuhuma? Bado ninaona kuna utete wa aina fulani kwenye hili swala na liko complicated kwa kiasi fulani. Hao waliotoa tuhuma hizo bado wana kazi ya ziada nadhani wanahitaji kwenda mbali zaidi ili kuweza kupata majibu yanayoeleweka, vinginevyo tutasikia blanket statement na huo ndiyo utakuwa mwisho.

..maswali uliyojiuliza au kuuliza ni mazuri na yaliyojaa tafakari!

..ukweli ni kuwa,hizo tuhuma kama zilivyo ni tuhuma na zitabaki kuwa hivyo mpaka pale uchunguzi rasmi utakapofanyika na chombo rasmi na chenye kuaminika!

..sasa,hili kwa hali halisi halitotokea!na kama litatokea itakuwa ajabu ya mwaka! simply in our dreams!

..ila,hivi sasa nchi hii imefika sehemu viongozi inawabidi wawe waangalifu na waadilifu katika matumizi ya mali,watu na fedha za umma!

..hili pekee ndio litakaloondoa haya yote ya "nyie mafisadi wala rushwa wakuu" na "nyie wapinzani njaa na wababaishaji"

..siasa za nchi hii ndio zinabadilika hivyo! tupende tusipende!
 
mkandara, mahakama imeruhusu uchaguzi kufanyika, lakini kesi ya msingi bado ipo mahakamani. Kama kawaida badala ya kujibu hoja zilivyotolewa CCM na serikali yake watataka wananchi wapuuzie hoja hizo kwani "zimeshajibiwa huko nyuma" na "wapinzani hawana jipya".
 
Lunyungu,

Hata mimi ningetegemea kama uchaguzi wa nafasi za udiwani ni leo, basi viongozi karibu wote wa upinzani wangelikuwa huko mikoani kujaribu kunyakua hivyo viti.

Hii ni nafasi ya kwanza tokea suala la Zitto kufukuzwa bungeni, mungeitumia nafasi hii kutoa kipigo kwa CCM. Lakini kama viongozi wakuu karibu wote mmejazana Dar, naona inaweza kuwa ngumu sana kuishinda CCM huko vijijini.

Hii habari si mungeweza hata kutangaza mkiwa huko mikoani? Maana siku hizi hata huko sasa mnapata publicity ya kutosha.

Taarifa ya leo ni muhimu sana kwa taifa, lakini pia kuanza kushinda viti ni jambo muhimu. Mungeweza kuua ndege wawili kwa jiwe moja.

Tatizo akisema masatu, basi watu ni mawe tu bila hata kuangalia logic iliyoko kwenye hoja yake.

Anko Mtanzania
Kama wananchi wanataka kuchagua upinzani wanaweza kufanya bila kuwapo hao unaodai wana tunguri ya ushindi. CCM inashinda kwa sababu ya mtandao wa dola. Nilishaongea hayo kabla. Wananchi wakiacha woga kwa dola, haki itapatikana. Tutaelimishana pole pole.
 
Jamani huyu mtu wa pwana na majina yake mengi tumsamehe na kwenye mijadara ya msingi sana kama hii tuwe tunamacha bila kumjibu. Lengo lake kubwa yeye ni kututoa kwenye mada na sisi bila kutafakuri tumeingia kwenye mtego.

Tunajua kuna watu ambao wanamtizamo wa kuitetea chichiemu lakini wanajaribu kutetea kwa kujenga hoja kama wakina kilitime, lakini sio hawa wakina mtu wa pwani, masatu, kada, na Eng Mohamed. Tusiingie kwenye mtego wao hawa wakina tambwe. Hatuko level moja na hawa jamani ni mufirisi hawa tuwapishe kama ukoma ili ndugu zetu wapate kukombolewa. Nitafungua thread maalumu kwa ajiri ya kuwaomba wanachama wawapuuze hawa wapumbavu mpaka watakakapo jua kujenga hoja
 
lunyungu ukweli unaujua kama mnatwanga maji, lkn ndio uko kazini, tumika baba

Mtu yeyote anayetetea WIZI ni Mwizi namba moja, Mzee inaonekana wewe ni Kinara.

Mzee jitahidi make naona kazi inaelekea kukushinda.

Mzee Mwaka huu lazima MAFISADI warudishe pesa za watanzania.

wanatuibia matokeo yake wanapandisha kodi mbali mbali hili waendeshe nchi na kuomba misaada, tumechoka kutumiwa, Taratibu tutawakamata tu.
 
Sasa ni saa 10:20 toka katika Ukumbi wa Urafiki Social Hall . Viongozi wa Vyama vyote wapo nje ya Ukumbi wanafanya maongezi na wana Habari . Mrema yupo, Slaa yupo,Marando Mabere yupo na CUF sijamuona mwakilishi wao ila nangoja. Kwa upenda wa NCCR na CUF sijajjua nani mwakilishi wao ila niko hewani nitawapa yanayuo jiri .Wana habari wamejaa hapa sasa sijui kama watasema yatakayosemwa hapa kama yalivyo ama watakaa kama last time pia .

Hivi huyu Mabere Marando ni yule ambaye alitoka NCCR na kwenda sisi M baada ya kukorofishana na Mrema ama ni mwingine? Ina maana amerudi tena upinzani?
Naomba ufafanuzi.
 
Invincible,
Nilikuwa sijazipata habari hizo mpya ndio maana nilitanguliza kuuliza kama nimepitwa na taarifa hizo...
Shukran sana...
 
Jamani it is time tuache hoja za kipuuzi za mara oh Lunyungu chama chenu mara oh uko Chadema.Nasema sikatai kama nitakuwa siku moja CCM, CHdema, Chausta nk lakini kwa sasa naomba kusema nakata hoja wala si kama wengine ambao hapa Baba ,Mama nk wako CCM na wanashiriki uchafu wa kutuibia so wanakuja na hoja kila siku . Hivi ni vyama ambavyo viko kisheria na mujibu wa Katiba so I see no sin or fear to join them.

Mnataka kusema wale walio kuwepo wanawaletea kesho habari hizi katika magazeti ni wanachama wa vyama hivyo. Drop your narrow mind and shortage of thinking and view real issues at broad .Kila mara naleta habari hapa ina maana huwa niko kazini natumwa na hao wapinzani ? After all wapinzani ni watanzania ila sema tofauti ni kwamba wanawasema Baba zenu , Mama zenu nk kwamba wanatuibia mchana .

Unajenga hoja ya Mbowe kwenda kusimamia uchaguzi wa diwani mb ona hata CCM si Makamba wala Tambwe wako huko ? Mfumo mbovu wa uongozi na Tume kutumika kuiba kura na state security organs mnautimia kama kukubalika kwa CCM .Mnanidanganya ila kila chenye mwanzo kina mwisho .Siku naingia Chedama rasmi ama CUF nitatangaza so stya tuned .
 
Heshima mkuu,
Endelea kutupatia news na hizo check numbers zinazotolewa.
Kuna watu wamekasirika kuona kuwa hadi check numbers sasa hivi zinawekwa hapa kwa hiyo watafanya chochote kuleta vioja kama kawaida yao.
 
Back
Top Bottom