Chadema chamburuza kortini Mkurugenzi wa Wilaya

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani chato mkoani kagera kimemburuza kortini mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya chato Hamida Kwikwega kwa madai ya kubatilisha ushindi wa mwenyekiti wa kijiji cha Nyakakarango Zamda Kusoya (Chadema) aliyekuwa amechaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 15 mwaka huu.

Zamda S. Kusoya alishinda kwa kura 178 dhidi ya mpinzani wake John Athanas (CCM) aliyepata kura 155 na ushindi huo kutangazwa na kaimu mtendaji wa kijiji Peter George.
Baada ya kutangazwa ushindi huo inadaiwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo alitumia nafasi yake vibaya kupinga na kutotambua

matokeo ya mwenyekiti huyo kwa madai uchaguzi haukuzingatia taratibu na kanuni ikiwemo kutoapishwa kwa msimamizi Peter George wa uchaguzi huo.

Kutokana na hali hiyo Chama Cha Demokrasia na maendeleo kilimtaka Mkurugenzi huyo kuyatambua matokeo hayo na kwamba iwapo kuna kanuni ambazo hazikuzingatiwa hana budi kuweka pingamizi mahakamani na si yeye kubatilisha matokeo hayo.

Katibu wa Chadema wilayani Chato Mange Sayi amesema Chama chake kimelazimika kumburuza mahakamani mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa kuwa ameshindwa kuzingatia kanuni za uchaguzi kama zinavyomuelekeza.

“Sisi kama Chadema tumelazimika kumfikisha mahakamani Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato kwa kuwa amekuwa akishindwa kusimamia taratibu na kanuni za chaguzi kutokana na maslahi ya chama tawala”.alisema Sayi

Aidha katibu huyo amesema kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusomwa machi 14 mwaka huu katika mahakama ya wilaya hiyo.
Mbali na Mkurugenzi huyo kaimu mtendaji wa kijiji cha Nyakakarango Peter George ataunganishwa kwenye mashitaka hayo kutokana na kusimamia uchaguzi kisha kutangaza matokeo hayo na baadaye kushinikizwa na Mkurugenzi wa halmashauri kutomtambua mshindi halali.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

 
Back
Top Bottom