CHADEMA chama Mbadala kwa CCM

Nina imani kubwa kuwa pole pole mambo yanabadilika - miaka 40 na ushee ina madhara yake na inachukua muda kudadilisha mtazamo katika jamii. Ni kweli muumgano wa vyama vya upinzani hauwezi kuwa rahisi kwani viongozi wake wengi ni uzao wa ukiritimba wa chama kimoja. Hata hivyo naanza kuona dalili za kizazi kipya kinaanza kupenya kwenye hizi anga na wazee pole pole wanawekwa kando. Muda si mrefu kuna vyama itabidi vife "natural death".

Chadema imeweza kufanikiwa kwa kiasi fulani katika hili wimbi hili la mabadiliko ya fikra. Tunaanza kuona viongozi wa vyama wakitofautiana wazi wazi na wanachama wao kwenye uchaguzi kama wa Tarime. Tulishuhudia kwa mfano wanachama wa NCCR wakitofautiana na viongozi wao na kushirikiana na Chadema licha ya maelekezo kutoka makao makuu kuwa wasitoe ushirikiano. Pia katika uchaguzi wa Busanda nina hakika wanachama wa CUF waliipigia kura Chadema.

Kuhusu Biharamulo pamoja na CUF kupoteza kada wake maarufu kwa Chadema, ni wazi waliokuwa wanachama wa CUF watakuwa nyuma ya mgombea wa Chadema na hivyo hivyo NCCR. Ni ukweli ulio wazi kuwa Chadema hivi sasa inaanza kuwa tishio kwa vyama kamaa NCCR, CUF, UDP, na vyama vingine vya upinzani na viongozi wake wanaanza kuinyooshea vidole Chadema badala ya CCM. Hili ni thibisho kuwa Chadema ina kila sababu ya kujiita chama mbadala.

Wazo la kutaka vyama viungane hivi sasa vina lengo la kuidhoofisha Chadema na mimi ningewashauri wawe waangalifu sana kwenye hili. Kuna kila dalili kuwa hivi vyama tayari vinachungulia kaburi na vina hatari ya kutumiwa - ushauri wangu ni kuwa kama chombo kinazama, wakati wa kutoka ni sasa kama alivyofanya Lwakatare. Wale wasioipenda Chadema wanaweza kurejea CCM lakini wale walio na nia ya kweli ya kulikomboa taifa mikononi mwa mafisadi, wajiunge na Chadema.
Kama kawaida woga unawaingia CCM
Homa ya Chadema umelitikisa Bunge
Mwaka 2010 wengi wataachwa kwenye mataa.
Labda Tume ya Uchaguzi na Jeshi la Polisi
ziipakate CCM - kama kawaida yao.
Napenda sana kwa vyama hivi vife kipo cha natural death ili tupate watu makini na walio na uchungu wa Kweli na Taifa letu Tanzania. Na pia kuna kila Dalili kwa CHADEMA kupewa au kusurvival katika mabadiliko haya, na pia hata haya ya CUF ni mtikisiko ambao utavikumba vyama karibu vyote, Kizazi cha Dot.com kinakuja na wala hawawezi kuzugwa na mambo ya CCM. Sisi tunasema kuwa mwanga wa Kweli upo mlangoni ni vyama husika kuona vinajitayarisha kukubali matokea haya. Chadema Kina Kizazi ambacho wao wanaweza kujua na kutambua na pengine hata CCM watashindwa kujua alama hizi na kutojua miiko yao ya uongozi na ndio maana unaona more contradicts za ajabu kati yao kuhusu ufisadi.
 
Migogoro ndio inafanya vyama viwe Imara na pia kuna watu watakufa natural death kama vile mende. Kuna faidi ya kuwa na vyama makini
 
Chadema kinaweza kuwa mbadala sahihi kama watajijenga kuanzia shinani, matawini kisha udiwani na ubunge uprezidaa wawaachie hao ccm kuanzia hapo tutapata kipimo sahihi
 
CHADEMA ingeongeza nguvu mikoani wilayani na vijijini, ikakamata majimbo mengi ili idadi ya wabunge waongezeke na wanachama waongezeke....wananchi wengi hawapati hizi habari kama tunavyozipata wa mijini.

Halafu hizo sera za CHADEMA kuzimwaga hadharani si ni kuwapa mwanya CCM kuiga na kuwamaliza?
 
CHADEMA ingeongeza nguvu mikoani wilayani na vijijini, ikakamata majimbo mengi ili idadi ya wabunge waongezeke na wanachama waongezeke....wananchi wengi hawapati hizi habari kama tunavyozipata wa mijini.

Halafu hizo sera za CHADEMA kuzimwaga hadharani si ni kuwapa mwanya CCM kuiga na kuwamaliza?
CHADEMA WANaweza kufanikiwa kama wakijipanga vizuri. hivyo kama upinzania wa kweli upo mijini kwanini wabunge wengi wanatoka Mikoani na sio Mijini?? Watu wanasubiri CHama Mbadala na wana Hamu ya kuona haya. Tazama na sikia watu kwenye Vituo vya Mabasi, Kwenye Daladala watu wamechoka kabisa ,na hata maisha pia wamechoka, Serikali imechoka, vyama Vimechoka na watu wamechoka. Nani Mkombozi wa Kweli Tanzania
 
Kuna wakati unakuja ambazo watu watasema na Vyombo vya Dola havitaweza, Yale ambao vyama wameshindwa kusimamia na badala yake NGO's na activators wanafanya badala ya vyama vya Siasa
 

Sera ya Miundombinu​
Nchi yetu ina maeneo mbalimbali yenye bidhaa, neema na utajiri wa rasilimali tele zinazohitajika sana maeneo mengine. Karibu kila kitu kinapatikana hapa hapa nchini kwa ajili ya maisha yetu na ya wengine.

Lakini kutokana na kukosekana kwa miundombinu, maeneo mengi nchini yanakosa bidhaa kutoka maeneo mengine, na kisha kuathiri ukuaji wa soko la ndani na kuwafanya wananchi wakose mahitaji muhimu. Tunashuhudia watu wakiwa na njaa maeneo fulani ya nchi huku wengine wakiharibikiwa na mazao. Katika hali hii, uchumi wa nchi umekuwa ukidorora kwasababu ya kukosa miundombinu ya uhakika na kusababisha watu wengi kushindwa kuendelea.
  1. Miundombinu inayotakiwa kujengwa, kuimarishwa na kupanuliwa katika nchi kavu ni barabara, reli na mabomba. Hivyo basi, wahandisi na makandarasi wa barabara na reli, watapewa zabuni za ujenzi kwa usimamizi wa vyombo vya kuchaguliwa na wananchi, yaani Bunge na halmashauri. Pia washindi wa zabuni watapitishwa na Bunge na Halmashauri kwa uwazi.
  2. Hivi sasa upo mpango wa kujenga barabara kuu muhimu katika kiwango cha lami ambao utagharimiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAM). CHADEMA haitasubiri mpaka nchi tatu ziafikiane, ila itahakikisha kwamba barabara zote kuu zinaounganisha mikoa na kanda zinajengwa katika kiwango cha lami.
  3. Sheria ya Usalama barabarani (Road Traffic Act 1973) itakuwa chini ya Wizara mpya ya Miundombinu badala ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Usalama wa barabara na magari utatofautishwa na usalama wa raia. Wahandisi wa magari na barabara ndiyo watahusika na ukaguzi wa magari na barabara badala ya askari polisi.
  4. Kwenye miji mikubwa, na hususan Dar es Salaam, ujenzi wa barabara zinazopita juu (flying roads) utaanzishwa maramoja ili kupunguza msongamano wa magari na uchelewaji kazini.
  5. Matumizi na ujengaji wa reli utaendelezwa pamoja na kurudishia reli iliyong’olewa ya Mtwara hadi Nachingwea. Njia nyingine mpya za reli zitatafitiwa, kupimwa na kujengwa. Maeneo ambayo yanafaa kujengwa reli haraka ni Mtwara hadi Songea kupitia Nachingwea na Tunduru; Makambako hadi Mbambabay kupitia Mbinga; Arusha hadi Musoma kupitia Serengeti; na Tunduma hadi Mpanda kupitia Sumbawanga.

    Pia CHADEMA itaweka utaratibu wa kupanua reli ya kati kutoka Shinyanga hadi Bukoba kupitia Nyakanazi na Biharamulo; na Dodoma hadi Tanga kupitia Kondoa, Kiteto na Handeni. Maeneo mengine yanayohitaji reli ni Singida hadi Arusha kupitia Katesh; Tabora hadi Mbeya kupitia Chunya; Iringa hadi Singida kupitia Manyoni; Ifakara hadi Tunduru kupitia Mahenge na Liwale; na Dar es Salaam hadi Mtwara kupitia Lindi.
  6. CHADEMA itaanzisha utaratibu wa kusafirisha mafuta kutokea Dar es Salaam au sehemu zenye mafuta kwenda mikoa iliyo mbali kama Kagera, Mwanza, Arusha, Musoma, Ruvuma, Tabora, Manyara, Rukwa, Singida na Kigoma kwa kutumia mabomba ya mafuta ili kuondoa gharama za kutumia usafiri aghali wa barabara au reli na hivyo kupunguza bei ya mafuta mikoani.
  7. Serikali ya CHADEMA itaweka jitihada za makusudi kwa wafanyabiashara wazawa zitakazowawezesha au kuwapa nguvu za kuimudu biashara ya uchukuzi na usafirishaji majini.

    Uwezo wa wazawa kuendesha bandari umejionyesha katika kitengo cha upakiaji na upakuaji katika bandari ya Dar es Salaam ambacho kilikuwa kinaleta faida ya shilingi bilioni 10 kwa mwaka tofauti na sasa ambapo kimeshuka hadi kufikia bilioni 0.4 baada ya kubinafsishwa na wageni.
  8. Sera ya CHADEMA itakazania katika ujenzi wa viwanja vya ndege utakaoendana na kutangaza utalii na vivutio vya kitaifa. Serikali ya CHADEMA pia itanunua ndege kwa ajili ya kuwakodishia au kuwakopesha wafanyabiashara wazalendo ili kuwapa uwezo wa uendeshaji na ushindani katika usafiri wa uchukuzi wa anga.

Mifugo yetu imesahaulika?
  1. Tanzania ni nchi ya tatu kwa wingi wa mifugo barani Afrika.
  2. Makabila ya wafugaji hayasaidiwi kuwa wafugaji wa kisasa.
  3. Mchango wa ufugaji katika pato la Taifa bado ni mdogo mno.
  4. Watalaam wa mifugo wanaozalishwa na vyuo vyetu hawakidhi haja na waliopo hawatumiki ipasavyo.
  5. Maeneo ya wafugaji yametelekezwa – hakuna huduma za kijamii kama maji, shule.
  6. Sekta ya usindikaji ya mazao ya mifugo imeuwawa.
  7. Uuzaji wa mazao ya mifugo nje ya nchi umedorora.


Serikali ya CHADEMA itafanya nini kuboresha maisha ya wafugaji?
  1. Tutarejesha viwanda vyote vya usindikaji wa mazao ya mifugo – mfano Tangayika Packers.
  2. Tutafufua soko la nje la mazao yatokanayo na mifugo.
  3. Tutatoa motisha kwa watalaamu wa mifugo.
  4. Tutaboresha huduma za jamii katika maeneo ya mifugo.
  5. Tutaelekeza halmashauri za wilaya kujenga majosho.
  6. Tutatoa chanjo za mifugo bure.
  7. Tutaimarishaji uzalishaji wa kuku wa kienyeji katika mikoa ya kanda ya kati kukidhi hususan haja ya soko la utalii.

Sera ya Rasilimali​
Tanzania ni moja kati ya nchi zilizojaliwa utajiri wa maliasili. Ni nchi yenye mito, mabonde, maziwa, vito vya thamani, wanyamapori, milima, misitu na vingine vingi ambavyo kama vitatumika vizuri vinaweza kuliletea taifa letu maendeleo ya haraka katika sekta karibu zote.

Lengo kuu la sera hii ni kurudisha rasilimali za nchi mikononi mwa wananchi wenyewe ili wawe na wajibu na haki katika matumizi, ugawaji na utunzaji wa rasilimali zilizopo kwa manufaa ya Taifa letu.

Kimsingi sera hii ya maliasili inalenga sekta kuu sita:
1. Sekta ya Wanyapori
  1. Kuhimizwa kwa wananchi wenye nia na uwezo wa kuwekeza katika maeneo yafuatayo: Ufugaji wanyamapori; Kuendesha shughuli za safari za uwindaji; Kuendesha shughuli za upigaji wa picha za wanyamapori kitalii; and Kujihusisha na biashara ya bidhaa zitokanazo na wanyamapori.
  2. Kuwapa kipaumbele wazalendo katika kujifunza na kufanya utafiti wa wanyamapori.
  3. Itakuwa ni marufuku kwa wageni kusafirisha au kuhamisha wanyama walio hai, badala yake kazi hiyo itafanywa na wananchi wenyewe.
2. Sekta ya Uvuvi
  1. Kuwawezesha wawekezaji wazalendo kupata teknolojia ya kisasa ili kuongeza pato la Taifa kwa kuongeza kiasi cha mazao ya uvuvi.
  2. Kuweka mkakati utakaowawezesha wavuvi wadogowadogo kuwa na uhakika wa soko la mazao yao. Aidha Kuweka sheria itakayowalazimu wavuvi wakubwa hasa wenye viwanda vya usindikaji kununua toka kwa wavuvi wadogo wadogo.
3. Sekta ya Ufugaji wa Nyuki
  1. Lengo la sera hii ni kufanya ufugaji wa nyuki kuendeshwa kibiashara zaidi, na hii inatokana na kwamba mazao yatokanayo na nyuki bado hayajapatiwa soko la uhakika ukizingatia kwamba aina ya nyuki wanaopatikana katika nchi yetu ndiyo wanaoongoza kwa utoaji wa asali nzuri katika soko la dunia.
  2. Kutolewa kwa elimu muafaka juu ya ufugaji mzuri wa nyuki kibiashara.
  3. Kuongeza juhudi za kutafuta soko la nje na kuchukua jitihada za makusudi katika kuitangaza asali yetu.
4. Sekta ya Misitu
  1. Kufuta utaratibu holela wa uvunaji wa misitu iliyopo hivi sasa.
  2. Kuweka upendeleo kwa wananchi kuvuna na kuuza mazao ya misitu.
  3. Kuhimiza uwepo wa misitu ya kupandwa.
5. Sekta ya Nishati
  1. Kufanywa kwa utafiti wa kina zaidi juu ya matumizi ya kuni vijijini ili kupata nishati mbadala na isiyo aghali, ili kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na kukatwa kwa miti.
  2. Kuwekeza katika utafutaji wa mafuta katika mwambao wa nchi yetu na kuendesha uchimbaji wake iwapo itathibitika kwamba uchimbaji wake unaweza kufanyika kwa manufaa ya Taifa na wananchi wake.
  3. Kuchukuliwa kwa hatua za makusudi ili kupunguza bei ya umeme. Na hili litawezekana iwapo tutakuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika.
  4. Sehemu za vijijini ambako umeme haujafika, CHADEMA kitaweka utaratibu maalum wa kusambaza vifaa vya kutumia nishati ya jua kwa gharama nafuu ili wananchi waweze kulitumia kama nishati mbadala.
6. Sekta ya Utalii
  1. Kuchukua hatua za makusudi ili kuimarisha miundombinu yote inayoelekea sehemu za kitalii.
  2. Kuhakikisha kwamba moja kati ya kazi za balozi zetu ni kutangaza vivutio vyetu vya utalii.
  3. Kuboresha na kuimarisha vituo vya utalii wa mambo ya kale, ili kuinua mapato yanayotokana na eneo hilo.
  4. Wananchi waishio katika maeneo yazungukayo sehemu za kitalii washirikishwe katika mipango yote ihusuyo maeneo hayo. Aidha mipaka ya sehemu zilizotengwa kwa ajili ya utalii ni lazima ikubalike na wananchi hao.

Sera ya Maji​
Hali ikoje?
  1. Tanzania ni nchi ya maji – imezungukwa na maziwa makuu, bahari, mito, chemchem na maji ya mvua.
  2. Asilimia 95% ya wananchi hawapati maji safi, salama na kwa uhakika.
  3. Wananchi hawa, hususan wanawake, hutumia nguvu na muda wao mwingi kuyatafuta maji
  4. Kumekuwa na ahadi hewa za upatikanaji wa maji – Kwa miaka zaidi ya 30 wananchi wote wameahidiwa maji bila mafanikio!


Serikali ya CHADEMA itafanya nini?
  1. Itawekeza katika uvunaji wa maji ya mito, maziwa, chemchem na mvua.
  2. Mamlaka ya Usambazaji ya maji itakuwa chini ya halmashauri za manispaa, miji na wilaya
  3. Itawezesha vijiji kutunza vyanzo vya maji ili visiharibiwe.
  4. Upatikanaji wa Maji kwa Wananchi itakuwa ni kipaumbele muhimu cha serikali ya CHADEMA.
  5. Itaingiza kwenye mitaala kuanzia shule ya msingi hadi sekondari dhana ya utumiaji na utunzaji wa maji.
  6. Tutaboresha na kukarabati miundombinu ya maji iliyopo ili kuzuia upoteaji wa maji.
  7. Tutahakikisha kila Mtanzania anapata maji safi na salama katika kipindi kifupi iwezekanavyo.
  8. Hatutabinafsisha sekta ya Maji na makampuni yote yaliyobinafsishwa yatarejeshwa chini ya mamlaka za Maji katika Halmashauri za Wilaya. CHADEMA haitaweka MAJI chini ya mikono ya Makampuni ya kigeni, ni hatari kwa usalama wa Nchi.
 
Ila ni muda upinzani nao ukawaelimisha vizuri juu ya sera zao. Vyama vingi vya upinzani havisemi wao vitafanya nini bali wana kazania tu na CCM wameshindwa kufanya nini. Sasa kwa mwananchi wa kawaida atajuaje kuwa na wewe unaweza fanya kazi bora kuliko ya CCM? Je CCM isipo kosea na upinzani watakosa cha kusema? It is time upinzani ukakazania kujiimarisha badala ya kujaribu tu kuiua nguvu CCM. Ikija kwenye maneno ya jukwaani na kutumia pesa upinzani hawawezi kuishinda CCM. Ni muda muafaka sasa upinzani kujiwekea mikakati ya muda mfupi na mrefu. Ni muda sasa wa upinzani kusema sisi tutafanya hivi. Ni muda sasa upinzani ukatambua kuwa kila uchaguzi ukiisha basi kampeni zingine zimeanza na siyo kusinzia kwa miaka mitano uchaguzi mwingine ukifika wana lalamika hawana uwezo wa kutembelea majimbo yote. It is time they set realistic goals na kuacha ndoto za alinacha. Inabidi waone sasa kuwa mikakati yao mpaka muda huu imeshindwa na wanabidi wajipange upya.
 
Ila ni muda upinzani nao ukawaelimisha vizuri juu ya sera zao. Vyama vingi vya upinzani havisemi wao vitafanya nini bali wana kazania tu na CCM wameshindwa kufanya nini. Sasa kwa mwananchi wa kawaida atajuaje kuwa na wewe unaweza fanya kazi bora kuliko ya CCM? Je CCM isipo kosea na upinzani watakosa cha kusema? It is time upinzani ukakazania kujiimarisha badala ya kujaribu tu kuiua nguvu CCM. Ikija kwenye maneno ya jukwaani na kutumia pesa upinzani hawawezi kuishinda CCM. Ni muda muafaka sasa upinzani kujiwekea mikakati ya muda mfupi na mrefu. Ni muda sasa wa upinzani kusema sisi tutafanya hivi. Ni muda sasa upinzani ukatambua kuwa kila uchaguzi ukiisha basi kampeni zingine zimeanza na siyo kusinzia kwa miaka mitano uchaguzi mwingine ukifika wana lalamika hawana uwezo wa kutembelea majimbo yote. It is time they set realistic goals na kuacha ndoto za alinacha. Inabidi waone sasa kuwa mikakati yao mpaka muda huu imeshindwa na wanabidi wajipange upya.
Sasa wewe unataka waseme nini kama hawpo kwenye serikali. Hivyo tu kusema tutfanya hivi ama vile ni tosha kabisa kuongoza Serikali. Vyama vya Upinzani ni mbdala ya serikali navyo vinaongoza Serikali tarajiwa
 
Sasa wewe unataka waseme nini kama hawpo kwenye serikali. Hivyo tu kusema tutfanya hivi ama vile ni tosha kabisa kuongoza Serikali. Vyama vya Upinzani ni mbdala ya serikali navyo vinaongoza Serikali tarajiwa

Hata kama hawapo serikalini wanaweza kusema nini watafanya tofauti iwapo wakipewa madaraka. My point is watu wengi hawajui sera za upinzani na CCM inashinda kutokana na name recognition. Mkuu unataka kusema wewe utachagua chama bila kujua itafanya nini tofauti ukiwapa kura zao? The fact remains as long as wananchi hawajui nini haswa sera za upinzani na zina unafuu gani ukilinganisha na za chama tawala wataendelea kuchagua zimwi walijualo which is CCM.
 
Nafikiri waheshimiwa tunasahau kitu kimoja.Si jukumu la chadema pekeyake kuiondoa CCM ni jikumu la kila mtanzania ambaye amechoka na hasa vijana
kushiriki kikamilifu kwenye gurudumu la siasa

Mfano wakati wa mbio za kugombania uhuru vijana wakina mchonga walivyopambana
 
Nafikiri waheshimiwa tunasahau kitu kimoja.Si jukumu la chadema pekeyake kuiondoa CCM ni jikumu la kila mtanzania ambaye amechoka na hasa vijana
kushiriki kikamilifu kwenye gurudumu la siasa

Mfano wakati wa mbio za kugombania uhuru vijana wakina mchonga walivyopambana

Ni jukumu la Chadema na upinzani mkuu that is a fact. Kwani aking'olewa CCM nani atatawala? Si moja ya vyama vya upinzani? Lazima waonyeshe kuwa wao ndiyo the better alternative to CCM. Ukweli ni kwamba tunaongelea sana kuiondoa CCM bila kujiuliza kama kuna chama cha upinzani kipo tayari kuongoza serikali. Sijaona bado chama cha upinzani ambacho kimeelezea na kuelimisha vizuri umma kuhusu sera zake. Sana sana we have fanatics of the opposition and those who hate CCM with a passion. Inabidi tuviangalie vyama hivi sera kwa sera, hoja kwa hoja siyo kung'ang'ania tu CCM aondoke au fulani aingie. Tunaweza tukajikuta tukisema heri CCM baadae kama tusipo angalia. Ukweli una baki pale pale kuwa ni jukumu la vyama vyenyewe kuonyesha wananchi kwa nini wao wanafaa and so far they have failed miserably to convince wananchi.
 
Watu wanajua nini vyama hivi vitafanya na pia kujua kama watafanya nini, labda kwa sababu wewe umemezwa na ukada na kuwapo muda mrefu katika chaka chako
 
Watu wanajua nini vyama hivi vitafanya na pia kujua kama watafanya nini, labda kwa sababu wewe umemezwa na ukada na kuwapo muda mrefu katika chaka chako

Si hilo tu mkuu, hili pia ni swala ambalo tumekuwa tukilipinga hapa, la serikali kuundwa na wabunge! Tunacho tegemea ni chama mbadala kama kitashinda uchaguzi, kinachukua vichwa safi kama Magufuri bila kujali itikadi ya mtu, na kuvipa post bila kuendekeza uswahiba na umwenzetu, vichwa vina badilisha utendaji kazi maramoja. Na kwa resources tulizo nazo ni myaka mitano tu, mambo yatakuwa yamebadilika sana!

Mfano ni kuchukua pesa ambazo serikali ina zitumia vibaya kama vile za chai, safari za wakubwa zisizo na tija, mashangingi, na kuzielekeza maramoja katika kitu kimoja, mfano kilimo, yaani within 2 yrs mabadiliko yataonekana. Na hiki ndicho tuna kikosa CCM ambao wamesahu jukumu lao badala yake wamebaki kutetea uozo wao kwa garama yoyote zile!
 
Si hilo tu mkuu, hili pia ni swala ambalo tumekuwa tukilipinga hapa, la serikali kuundwa na wabunge! Tunacho tegemea ni chama mbadala kama kitashinda uchaguzi, kinachukua vichwa safi kama Magufuri bila kujali itikadi ya mtu, na kuvipa post bila kuendekeza uswahiba na umwenzetu, vichwa vina badilisha utendaji kazi maramoja. Na kwa resources tulizo nazo ni myaka mitano tu, mambo yatakuwa yamebadilika sana!

Mfano ni kuchukua pesa ambazo serikali ina zitumia vibaya kama vile za chai, safari za wakubwa zisizo na tija, mashangingi, na kuzielekeza maramoja katika kitu kimoja, mfano kilimo, yaani within 2 yrs mabadiliko yataonekana. Na hiki ndicho tuna kikosa CCM ambao wamesahu jukumu lao badala yake wamebaki kutetea uozo wao kwa garama yoyote zile!
Hapana Shaka kuwa lazima tufanye hivyo lakini inabidi tupate wapapandaji hodari sana na mahiri sana huku wakisaidiana na watu wengine makini sana katika kufanikisha haya malengo
 
Tunaweza kuifanya serikali ya pamoja na watu kuwa na wajibu wa kuwajibika na kuleta maendeleo ya watu wote
 
Chadema kuwa mbadala wa CCM inakuwaje kuhusu "zanzibar" maana hawana hata mbunge moja wala sioni juhudi zozote za kufanya haya kutoka kwa chadema, ina maana CHADEMA ni chama cha mainland tuu au ndio mwisho wa muungano.
Ndio maana nafikiri CUF has more represantive (national wide-unity) than Chadema
 
Watu wanajua nini vyama hivi vitafanya na pia kujua kama watafanya nini, labda kwa sababu wewe umemezwa na ukada na kuwapo muda mrefu katika chaka chako

Ukisema watu wanajua ni watu gani hao unaoongelea? Isije ikawa hiyo idadi unayo ongelea ni watu wachache tu unaowafahamu wasio represent majority ya Watanzania. The proof kuwa upinzani umeshindwa kuwaeleza vizuri nini upinzani utafanya ni boksi la kupigia kura. Kama watu wameeleweshwa vya kutosha basi ungeona idadi kubwa zaidi ya wabunge wa upinzani na pia CCM isingepata 80% ya kura kwenye uchaguzi wa raisi. Mimi in fact sishabiki chama chochote ila natoa maoni unbiased. Kada ni yule ambaye anapigia debe chama fulani.
 
Back
Top Bottom