Eric Ongara
Senior Member
- Sep 19, 2006
- 165
- 8
Leo ikiwa ni siku ya mwisho wa mwaka sambamba na kumskuru muumba kwa majaliwa yake kwa mwaka ulio ukingoni ni vyema pia tukafanya mapitio ya mwaka mzima ili tuchukue akiba na kubeba yalio mazuri na kufanya jitihada za kuepuka makosa tunavyoelekea mwaka mpya unao karibia. Kwa muktadha huo kwenye anga za siasa napendekeza kwenu liliodhahiri kwamba Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ndio Chama Bora kwa mwaka 2008.
Tutakubaliana kwamba CHADEMA ni Chama cha siasa kilichojadiliwa sana mwaka huu, kuna waliokikosoa, kitusi,wapo waliokisingizia na wapo walio kiunga Mkono. Waliioyafanya hayo wanatapakaa kwenye maeneo na kada mbalimbali iwe hapa JF, kwenye vyombo vya habari, kauli za wanachi wa kwaida, viongozi wa serekali, vyama vya upizani na hasa kile chama cha mafisadi. Watu wamefanya hivyo kwa miskumo mbalimbali inaweza kuwa kukipenda, kukikubali, kukichukia, kutokubaliana nacho, kukichukia au kukihofia lakini yote haya yanaweza kuwekwa kwenye kapu moja kwamba kazi yake INATAMBULIKA katika jamii ya watanzania.
Ili kujenga msingi mzuri katika kukitambua rasmi kama chama bora kwa mwaka 2008 ni vyema tukafanya mapitio ya jumla kwa muhtasiri mwenendo wa CHADEMA kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
1.Ndio chama pekee cha upinzani ambacho kimeweza kuwa na awamu tatu za uongozi: Mtei, Makani na Sasa Mbowe na hivyo kuonyesha ukuaji wa demokrasia ndani ya chama
2.Ukuaji wake ni wa kitaasisi zaidi badala ya ukuaji kutokana na umaarufu wa mtu binafsi au mazingira ya kihistoria ya eneo husika tofauti na vyama vingine vya upinzani na hivyo kujenga misingi imara na hivyo kutoyumbishwa pale viongozi wake wanapo hama chama, tumeshuhudia Kaboro(alie kuwa makamu mwenyekiti) na Shaibu Akwilombe(aliekuwa naibu katibu mkuu) wakihama chama pasipo kulete mtikisiko wowote.
3.Ni chama amacho hakikukurupuka kusimamisha mgombea wa uraisi mwaka 95 na 2000, mkazo wake ulikuwa kujenga miundo ya kitaasisi yenye uwezo wa kuhimili mikiki ya kisiasa.
4.Kimejitambulisha zaidi kwa sera kwa kutoa mapendekezo mbalimbali amabayo hata hivyo yamekutana na CCM amacho kinanongozwa na watu wenye uwezo duni na nia mbaya, matokeo yake kushindwa kutumia utajiri wa fikra wa CHADEMA kwa maslahi ya taifa.
5.Leo kinatambuliwa kama chama cha kizazi kipya kilichosheheni wanasiasa mabingwa wa kizazi kipa kama Freema Mbowe, Wilboard Slaa, Zito Zuberi Kabwe, Halima Mdee, Tundu Lissu, John Myika na wengi wanaoendelea kuibuka.
Tuangalie baada ya 2005.
Baada ya uchaguzi mkuu pamoja na Kasumba kuwa vyama vya upinzani ni vyama vya uchaguzi, CHADEMA waliweza kufutulia mbali Kasumba hii kwa kuendelea kufanya uwekezaji mkubwa sana wa kisiasa kwa hatua zifutazo:Uamuzi wa aliekuwa mgombea wake wa nafasi ya Uraisi kuamua kwenda kupokea matokeo pale Diamod ulikuwa uwekezaji mzuri sana wa kisiasa kwa kujitofautisha na wagombea wenzake, an kujenga taswira mpya ya mapambazuko ya kisiasa Tanzania.
Mwaka 2006 alifanya ziara nchi nzima kuwashukuru waliomuunga Mkono wakati wa uchaguzi pamoja na kueleza mikakati ya wanachama hapo badae na kuhakikishia umma kuwa yeye kwa pamoja na chama anachokiongoza watatimiza wajibu wao wa kisiasa katika kukiwajibisha Chama cha Mapinduzi kutekeleza ahadi zake na kuzingatia maslahi ya taifa katika uongozi wao kazi ambayo wameifanya na wanaendelea kuifanya vizuri sana.
Uzinduzi wa Tuamini jipya: CHADEMA imewezea kujikarabati na kuundwa upya ili kukomaza miundo yake ya kitaasi katika katika kukabilana na changamoto mbalimbali za kisiasa. Katika uzinduzi wa tumaini jipya walitoa Bendera mpya yenye mvuto zaidi ya ile ya awali na kufanya marekebisho ya katiba katika kukipeleka CHADEMA katika kitovu cha mapambano ya kisiasa. Uzinduzi huu uliandaliwa vipindi maalum na kurushwa katika luninga na hivyo kuweza mfiko wa moja kwa moja.
Ziara za utetezi wa rasilimali na kupinga ufisadi: Hapa walitumia vizuri sana mtaji wa kisisa baada ya Zito kusimamishwa bungeni kwa kuzunguka nchi zima na hata kuzaa azimio la songea lenye lengo la kutetea rasilimali na kuibukia msisimko wa aina yake katika jamii. Na huu ndio umakini wa chama cha siasa yaani uwezo wa kuona na kufanyia kazi vizuri fursa za kisiasa zinazojitokeza katika kujenga chama.
Tamo la orodha ya mafisadi 11: Dr. Slaa na Lissu walitumia umakini mkubwa sana katika kuaandaa taamko zito sana liliojitosheleza sana lenye vilelezo vya namna nchi inavyotafunwa. Tamko hili limewaamsha wananchi katika namna ambayo haiwezi kuelezewa na kuendelea kuwa mwiba mkali sana unatishia uhai wa CCM!
Walioyafanya mwaka 2008 na hivyo kustahili kiwa chama Bora.
Hapo juu tumeansiha maelezo hayo ili kujenga msingi kuwa huu ni muendelezo wa misngi imara mabayo CHADEMA imejiwekea. Sasa tuangalie maeneo yaliovutia zaidi kwa mwaka unaoisha: Matamko mazito juu ya kuonyesha hali na mwenendo wa nchi kisiasa, kijamii na kiuchumi matamko ambayo mara kwa mara yamefanikiwa kuitingisha serekali na kuwaamsha wananchi na hivyo CHADEMA kutimiza wajibu wake kikamilifu kama chama cha upinzani kinapaswa kusimamia serekali ipasavyo. Bila kusahau kuendelea kuwa maaskari wa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ufisadi
Kujibu mashumbulizi dhidi yake kwa umakini na ufasa mkubwa mathalani hoja ya uchaga na matumizi ya helkopta zilitolewa ufafanuzi wa kina na msingi mzito na hivyo kufifisha hoja laini za washindani wake
Umakini katika maswala nyeti. Tofauti na vyama vingine vya siasa CHADEMA haikikurupuka kurukia hoja za mahakama ya kadhi na sakata la OIC tofauti na wengine ambao taswira zao zimechuja kutokana na kutoa kauli ambazo zimesigana na maslahi ya makundi mbalimbali katika jamii.
Kufanikiwa kushinda umeya na hatiame kuwa chama tawala Tarime, hii ji baada ya wilaya ya Tarime kugawanyawa mara mbili, Tarime na Rorya, CHADEMA wamefanikiwa kuongoza halmashauri inazoongoza sambamba na Karatu na Kigoma mjini(katika ubia na CCM).
Kusimamisha kwa Chacha wangwe na Yaliojitokeza baada ya Kifo chake
Hapa CHADEMA wajipambanua kwa umahiri wake kwa mtazamo huu:
1.Walionyesha uwezo wa kufanya maamuzi magumu kwa kumsimamisha mmoja wa viongozi wake wakuu kutokana na kukiukaa taratibu na misingi ya chama. Kwa tafsiri pana huu ni ujasiri wa uongozi. Tumeona wapinzani wake CCM wakishindwa kufanya hivyo dhidi wa watuhumiwa wa ufisadi lakini CHADEMA walienda hatua moja mbele
2.Ukomavu wa kichama: wapo waliodhani kuwa sakata la wangwe kusimamiswa lingweza kusimbaratisha chama na hata kufikia hatua ya kufananisha na mgogoro wa NCCR mageuzi amabo ulikisambaratisha kabisa mnamo miaka ya tisini. Wanachosahau NCCR ilikuwa na ukuaji wa puto tafauti na CHADEMA iliyokuwa imekuwa kitaasisi. Ukuaji wa ghafla wa NCCR ulitokana watu maarufu kujiunga kwa wingi mda ule lakini hakukuwa na miundo thabiti ya kitaasisi kulelea na kukudumisha ukuaji ule, ndio maana ulipoibuka mgogoro ambao ni jambo la kawaida kwa taasisi yoyote ya kibinadamu hakukuwa na miundo au mfumo unaukubalika katika pande zote kutatua mgogoro ule iihali CHADEMA tayari imekuwa sana kitaasisi na hivyo kutoyumbishwa na migogoro. Kwa hulka za kibinadamu migogoro ipo, suala ni mifumo ya kuitatua na namna ya kuitatua. CCM wana migogoro mingi tu, ya NAPE, wabunge wa CCM na ngumi za UWT na wengine kufikia kutoa nguo za ndani lakini zipo jitihada mbaya za kuonyesha kuwa kuna migogoro upinzani pekee. Kwa namana walivyo kabili hili CHADEMA wanapaswa kupewa heko. Tunaweza kusema sasa zipo dalili njema kuwa kuna chama kingine imara kinachokuwa na kusukwa kila uchao pamoja na kukabiliana na mazingira magumu.
3.Hawakukurupuka kujibu kasfha zilizobuniwa na wapinzani wake hasa CCM, vyombo vya habari na badale viongozi wa CUF,NCCR na TLP, zilifanyika jitihada nyingi sana kupandikiza mbegu mbaya na chuki dhidi ya CHADEMA wakijenga hoja ya kukihusisha CHADEMA na viongozi wake wakuu kuwa wanahusika na kifo cha Wangwe!
Ilikuwa ni kama vile dunia nzima dhidi ya CHADEMA. Viongozi wa CHADEMA walikuwa watulivu na wakomavu sana, walitulia wakafanya maamuzi sahihi yakiwemo kuwasilisha malalamiko yao katika mamlaka sahihi na hatimae kuvuka katika kipindi kigumu.Kuweza kuvuka katika mtego uke mbaya, tuko tayari kumpenedekeza Freeman Mbowe kama kiongozi bora wa mwaka kwa namna alivyoongoza chama chake katika kipindi hiki kigumu.
Ushindi wa Tarime: CCM inafanya jitihadi kujaribu kujenga hoja kuwa ule ni ushindi wa kawaida kwa kuwa CHADEMA imeshinda na kutetea jimbo lake lakini ukweli ni kuwa ushindi ule ni mkubwa na una maana kubwa katika mapambano ya kidemokrasia nchini Tanzania.
Ieleweke kuwa huwa na vigumu kuishinda CCM katika uchaguzi mdogo na pia rekodi zinaonyesha kuwa ni mara ya pili kihistoria baada ya Mrema Temeke. Lakini uzito wa Tarime umekuja wakati ambapo kulikuwa na jitihada nzito zimefanyika kukichafua na kukiweka katika mazingira magumu sambamba na CCM kuungana na vyama vyingine vya upinzani kukishambulia lakini wapi nguvu ya umma ikajidhihirisha, wakachukua jimbo dhidi ya CCM na "muungano" wa vyama vingine vya upinzani hasa DP na NNCR mageuzi. Taathira ya Tarime imekuwa kubwa mno katika medani za sisa Tanzania.
Ubunifu: Operesheni sangara ni kielele cha ubunifu wa viongozi wa CHADEMA na ubingwa wao katika kutumia fursa za kisiasa zinazojitokeza. Kama ilivyokuwa kwenye ziara za utetezi wa rasilimali hapa waliamua kudumisha hamasa na kutumia fursa ya kufanya uwekezaji wa kisiasa kwa kubuni Operesheni sangara wakati ambapo vuguvugu la ushindi wa Tarime linatokota. Jina lenyewe lina mvuto wa aine yake. Wameweza kufanya ziara za unenezi zilizo amasha, sisimua na kulitikisa taifa kwa namna yake.
Mikutano wa vyuo: CHADEMA imeendelea kuwa makini kwa kufanya mikutano mingi na wanavyuo mbalimbali mathalani, Arusha, Iringa, Mwanza, Dar es salaam na Morogoro,hii inazidi kuijengea hadhina kubwa ya vijana wa kileo wenye uwezo mzuri wa kitaalamu na hivyo kuimarisha benki yake ya rasilimali watu.
Kwa ujumala wamechangamsha sana siasa za TZ mwaka 2008 na kudumu katika ramani ya siasa mwaka mzima.Tunawapongeza sana viongozi wa CHADEMA ni matumaini yetu mtaendelea kuimarisha chama chenu na kujenga demokarsia Tanzania mwaka 2009.Hasa tukikumbuka kutakuwa na uchaguzi wa serekali za mitaa. Hakika: Hakuna kulala mpala kieleweke.
Last edited by a moderator: