Chadema, CCM yametimia

Watanzania tuamke, tujifunze kwa Wamarekani kila mtu anapaswa kueleza ataifanyia nini nchi yake na sio nchi itakufanyia nini.

Hapo umenena mkuu.Ila hila zote za udini na ukabila tuzilaani.
 
Huna kingine cha kuandika zaidi ya hayo maneno mawili..UDINI na UKABILA?

Mimi nimekunywa maji ya bendera ya mwl Nyerere,uchochezi wa udini na ukabila kwangu ni laana kubwa.Nimejitolea kuwa kamanda wa kupambana na laana hii
 
Watanzania tuamke, tujifunze kwa Wamarekani kila mtu anapaswa kueleza ataifanyia nini nchi yake na sio nchi itakufanyia nini.

Viongozi wetu wa CCM wataendelea na vitendo vyao vya ufisadi na sisi wananchama wa CCM tukiwaunga mkono hadi tufie kwenye ufisadi kama inzi anavyofia kidondanI. Ndiyo tutakavyoifanyia nchi na Mungu atusaidie.

Adui yetu mkubwa CDM tutamdhibiti kwa kila njia hata kuua kwa sababu dola ni yetu. Wananchi wanalia maisha magumu ni wavivu lakini tutagawa ngawira ya ufisadi hasa wakati wa uchaguzi kuwasahaulisha. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Chadema inaendeshwa kisomi.Hatuokoti watu kwny vijiwe kama ccm na kuwapa kazi ya kuendesha CHAMA.Tuna mikakati kwa kila kipindi,usiwe unakariri kijana.Sasa tuko kwenye kujenga CHAMA ngazi za chini kabisa na ngazi ya kati.Tunabadilika sisi!
 
Huna kingine cha kuandika zaidi ya hayo maneno mawili..UDINI na UKABILA?

Huyu jamaa kwa kweli uwa namshangaa halafu ukimuliza tafsiri ya udini ni ni asemi.
 
Huyu jamaa kwa kweli uwa namshangaa halafu ukimuliza tafsiri ya udini ni ni asemi.

Mkuu kama hujui uchochezi wa kidini ni nini nenda Igunga na Uzini kawaulize wananchi watakufafanulia kila kitu mkuu wangu
 
Mwamko wa Chadema uliokuwa umesukumwa kwa kiasi fulani na falsafa ya nguvu umma na Ufisadi.

Lakini falsafa ya Ufisadi inaonekana kuchuja na kuchosha masikioni mwa wananchi.
 
Sijui unataka data gani labda nikupe hii, matokeo ya uchaguzi mdogo wa majimbo mawili, Uzini, Igunga! au utasema Chadema waliibiwa kura?
Hata kama waliibiwa au hawakuibiwa kura! Huoni matokeo ya Igunga na Uzini yanaonyesha improvement kwa CHADEMA?
Ukichukulia kwamba ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa CHADEMA kusimamisha mgombea maeneo hayo? Au analysis zako unazifanyaje?
 
Wanabodi..
Mwenendo wa kisiasa, kati ya watani wa jadi CCM na Chedema sasa umeanza kuzua mijadala ndani ya jamii.

Wananchi wanahoji iko wapi kasi na upepo wa mabadiliko ilikuwa nao Chadema mwaka 2010 na mwaka jana ilikoyeyukia.

Huku CCM kilichokuwa kimeanza kudorora sasa kikionekana kupaa zaidi kuliko ilivyotarajiwa na wengi.

Mwamko wa Chadema ulianza kushika kasi mara baada ya Slaa, kuteuliwa kugombea Urais, mwamko huo uliendelea hata baada ya uchaguzi, na hasa baada ya chama hicho kuamua kufanya siasa zake kwa njia ya maandamo mikoa ya Kanda ya Ziwa hadi Nyanda za Juu Kusini.

Wadadisi wa mambo ya kisiasa wameanza kuhoji ni wapi kasi hiyo imeyeyeka ghafla na kukipa nafasi tena CCM kuanza kutamba katika maeneo mbali mbali nchini.

Hali hiyo ya kuanza kudorora kwa Chadema imelezwa pia kukikumba chama cha CUF kupoteza mvuto.

Chadema inatakiwa ibadili sera zake na falsafa mpya za kuendelea kuwashawishi Watanzania.


Sijakuelewa kabisa, hivi umefanya uchunguzi gani unaojastify madai yako? CDM kiko makini kuliko unavyofikiria. Sera za CDM baadhi yake zimeshaaza kutekelezwa na ccm.eg katiba mpya.
 
Sababu za CCM kuwa ni chama cha kushinda uchaguzi.
1. Umasikini. Huu ni mtaji namba moja wa uhai wa CCM. Watie njaa ili uwanunue siku ya kupiga kura, maana mwenye njaa hafikirii kesho yake. Hivyo wataiba kwa mabilioni kushibisha matumbo yao, watachota sehemu kidogo ya walichoiba kununulia kura kwa pilau, kofia na vitu visivyo na thamani yoyote kwa utu wa mtu.
2. Ujinga. Huu ni mtaji namba mbili kwa uhai wa CCM. Watie ujinga kwa kuwanyima elimu, maana ukiwaelimisha watajitambua na kuujua ubaya na udhaifu wetu, na wakijitambua hakika watatutoa madarakani.
3. Rushwa. Huu ni mtaji namba tatu kwa uhai wa CCM. Tutaunda vyombo bandia vya kupambana na rushwa ili kuhakikisha wapinzani hawapati nafasi ya kutumia rushwa kama sisi ili kushinda uchaguzi. Kisha tutatoa rushwa bila kificho, kwani makada wetu ndio watakuwa watendaji wakuu wa vyombo hivi vya kudhibiti rushwa. Kelele zikizidi tutafungua mashtaka bandia kwenye mahakama zetu bandia.
4. Vyombo vya ulinzi na usalama vyilivyokosa tumaini. Huu ni mtaji muhimu sana kwa uhai wa sasa wa CCM. Unawapa hali ngumu ya maisha polisi, usalama wa taifa, TAKUKURU n.k. Tumaini lao linakuwa ni mfumo wa rushwa na posho za operesheni mbalimbali. Kwakuwa wana njaa, watatamani operesheni zitokee kila siku ili wapate posho zao. Hivyo makundi ya kijamii yakiibuka tu kudai haki, wapate kichapo cha kufa mtu. Mifano mnayo juzi tu imetokea Songea. Polisi na usalama wa magamba wako tayari kuua kaka na dada zao ili wapate posho na vyeo. Njaa mbaya jamani.
Kwa mitaji hiyo CCM itadumu mpaka pale wananchi watakapotoka tongotongo machoni. Lakini kisiasa CCM ni marehemu wa siku nyingi. CCM ya sasa ni dikteta kama Nduli Iddi Amini Dada!!!!
 
Hata kama waliibiwa au hawakuibiwa kura! Huoni matokeo ya Igunga na Uzini yanaonyesha improvement kwa CHADEMA?
Ukichukulia kwamba ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa CHADEMA kusimamisha mgombea maeneo hayo? Au analysis zako unazifanyaje?

Hivi kupata kura 281 kwenye kura 5.903 na kupata Asilimia 4.8 ndio improvement? wakati mshindi kapata kura 5,377 sawa asilimia 91.1
 
Mimi nimekunywa maji ya bendera ya mwl Nyerere,uchochezi wa udini na ukabila kwangu ni laana kubwa.Nimejitolea kuwa kamanda wa kupambana na laana hii

Si vizuri vilaza wanaoigiza uzalendo wakajilinganisha na Mwl Nyerere.
Nyerere ndiye mwasisi wa CCM.... Sera za majimbo za CDM zilipigwa vita na Nyerere tangu uhuru.
 
Hivi kupata kura 281 kwenye kura 5.903 na kupata Asilimia 4.8 ndio improvement? wakati mshindi kapata kura 5,377 sawa asilimia 91.1
Ni
Ni ushindi mkubwa! ukichukulia CHADEMA haikuwa ikitambulika vizuri maeneo hayo kabla! Mbona hujaweka matokea ya Igunga!
 
Mkuu Mkeshaji,
Huu ndio ukweli unajua kila siku unapiga kelele za ufisadi ufisadi, zimewachosha watanzania lazima Chadema kama chama ibuni falsafa mpya kutegemea kuhubiri ufisadi kama kete yake haitakisaidia Chadema huko tuendako.

Si lazima uanzishe thread bandugu ili nawe uonekane humo,huu ni utumbo wa kupindukia,nani kakuambia cdm sera yao ni ufisadi ufisadi tu?unajua maana ya sera kweli wewe?unashangaza unaposema cdm inadorora,wakati kasi ndio inazidi,me niko sehemu moja mkoani morogoro inaitwa bigwa ilikua ni moja wapo ya ngome ya c.c.m lakini baada ya mwaka kupita nimekuja huku tena,hali niliyo iona upepo ni mbaya kwa cdm,uwe una tembea na kufanya tafiti kabla ya kupost kitu,sio umekaa kwenye computer tu una andika unalojisikia kichwani mwako!
 
Back
Top Bottom