Chadema, CCM yametimia

Wanabodi..
Mwenendo wa kisiasa, kati ya watani wa jadi CCM na Chedema sasa umeanza kuzua mijadala ndani ya jamii.

Wananchi wanahoji iko wapi kasi na upepo wa mabadiliko ilikuwa nao Chadema mwaka 2010 na mwaka jana ilikoyeyukia.

Huku CCM kilichokuwa kimeanza kudorora sasa kikionekana kupaa zaidi kuliko ilivyotarajiwa na wengi.

Mwamko wa Chadema ulianza kushika kasi mara baada ya Slaa, kuteuliwa kugombea Urais, mwamko huo uliendelea hata baada ya uchaguzi, na hasa baada ya chama hicho kuamua kufanya siasa zake kwa njia ya maandamo mikoa ya Kanda ya Ziwa hadi Nyanda za Juu Kusini.

Wadadisi wa mambo ya kisiasa wameanza kuhoji ni wapi kasi hiyo imeyeyeka ghafla na kukipa nafasi tena CCM kuanza kutamba katika maeneo mbali mbali nchini.

Hali hiyo ya kuanza kudorora kwa Chadema imelezwa pia kukikumba chama cha CUF kupoteza mvuto.

Chadema inatakiwa ibadili sera zake na falsafa mpya za kuendelea kuwashawishi Watanzania.

We naona umelishwa limbwata na ccm, hauhitaji akili nyiingi kuona mabo gani mengi CDM kama chma makini kimefanya. Kumbuka mwaka jana wabunge wa posho wa chama cha magamba walipitisha kwa ushabiki mswada wa kutafuta maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya ila CDM waligoma na kutoka nje.
Kwa busara zao ikabidi wamtafute rais na kumweka chini, nasema kumweka chini na kumpa darasa la ni nini katiba tunayotaka. Nafikiri utakuwa unajua ni siku ngapi CDM ilikutana na rais. Mswada uliokuwa tayari umesainiwa na kuwa sheria ilibidi urudishwe bungeni na kufanyiwa marekebisho makubwa kama Chadema walivyotaka - ukiondoa kile kipengele ambacho yule mama mnafiki alishupalia na kikapata support kama kaw ya wabunge wapenda posho wa CCM.
Sasa wewe king'asti wa FF unapayuka nini? Tumia akili kidogo au unataka kuwa kama mdogo wako yule aliyemliza form four pale Feza?
 
kwanza usiite chadema ni watani wa jadi.

ccm ni wezi chadema wanajaribu kulinda mali za uma.
huwezi kuita mtu anayefukuza mwizi kuwa ni mtani na yule mwizi,mmeiba mali za uma mnanunua kura kwa sababu ya umasikini wa watu,mnawapa sumu watetezi wao.

endeleeni na hizo njozi ila kuna siku mtakuja kujibu.
 
Katika kusoma kwangu huu uzi nimeshindwa kuona uhusiano uliopo kati ya kichwa cha habari na habari yenyewe. Labda ufikirie upya.
 
Sijui unataka data gani labda nikupe hii, matokeo ya uchaguzi mdogo wa majimbo mawili, Uzini, Igunga! au utasema Chadema waliibiwa kura?

Tafadhali usitoneshe watu vidonda kaa kimya.Mliweka pembeni utu wa kibinadamu mkasambaza vikaratasi kwenye nyumba za Ibada kuwachochea watu wapige kura kwa misingi ya udini.Udini utawatafuna na kuwarudia mpaka mtakapomalizika.Mmeona Arumeru kampeni ya udini haina nafasi mkamtuma kibaraka wenu Tendwa aanze kuchochea ukabila.Nakuhakikishia kwa hili hamtafanikiwa.
 
Nadhani kuna umuhimu kwa viongozi wa Chadema kubadili muelekeo na kufanya siasa za kistaarabu zaidi kuliko hata CCM yenyewe ili wananachi washawishike kuamini, pia amani na utulivu katika nchi hii inaweza kuendelea kudumishwa bila CCM.
 
Mwananchi wa kawaida wa huko vijijini, mfano wa Igunga, Uzini au hata Arumeru wanakojiandaa na uchaguzi mdogo, haoni madhara ya ufisadi, Ufisadi mnaujua nyie wa mjini yule wa mjini ana kero zake kutopata maji safi na salama, huduma ya afya, soko la uhakika la kuuzia mazao yake.

Hapo kwenye Red tutake radhi kwa kweli, hatuna nazi humu.
 
Tafadhali usitoneshe watu vidonda kaa kimya.Mliweka pembeni utu wa kibinadamu mkasambaza vikaratasi kwenye nyumba za Ibada kuwachochea watu wapige kura kwa misingi ya udini.Udini utawatafuna na kuwarudia mpaka mtakapomalizika.Mmeona Arumeru kampeni ya udini haina nafasi mkamtuma kibaraka wenu Tendwa aanze kuchochea ukabila.Nakuhakikishia kwa hili hamtafanikiwa.

Mkuu, JF sio kijiwe cha mbege usiwe unaokota maneno mtaani bila facts wala data za kutosha unaleta JF, weka ushahidi wa maneno yako!
 
Nadhani kuna umuhimu kwa viongozi wa Chadema kubadili muelekeo na kufanya siasa za kistaarabu zaidi kuliko hata CCM yenyewe ili wananachi washawishike kuamini, pia amani na utulivu katika nchi hii inaweza kuendelea kudumishwa bila CCM.

Mnavyochochea udini kwenye nyumba za Ibada ndio amani na utulivu? Sasa mmerukia kwenye ukabila huko Arumeru
 
Kibaraka mkubwa wewe wa chama cha majambazi CCM,unaandika vitu ambavyo havina kichwa wala miguu,Haya nenda sasa ukachukue posho kwenye ofisi za CCM.
 
Mkuu, JF sio kijiwe cha mbege usiwe unaokota maneno mtaani bila facts wa data za kutosha unaleta JF, weka ushahidi wa maneno yako!

Anayeokota maneno ya mtaani kati yangu mimi na wewe nani? Kamuulize Tendwa kilichomkurupua ofisini hadi Arumeru kwenda kutoa tamko huko Arumeru kwamba kabila la Washiri litamuua Lema akienda kwenye kampeni.Udini na Ukabila utawatafuna mpaka kaburini
 
Gud analysis mkuu ritz.
Tatizo la mashabiki na wanachama wa CDM hawayaoni haya. Kila siku chama kinazidi kudorora, wanashindwa kwenye chaguzi ndogo mbali mbali kwa tofauti kubwa, lakini halion hili!
Kazi kuimba tu Slaa, Slaa, Slaaa..

Mkuu Rejao,
Tatizo la Pro-Chadema JF ndio ilo, Inawezekana mkondo wa siasa za fujo na za kibabe wanazoziona ndio njia ndio umekipunguzia Chadema mvuto kwa wananchi watanzania hawana utamaduni wa kuendesha mambo yao kwa vurugu.
 
Ila kuchochea udini na ukabila kila wakati wa kampeni ndio utamaduni?
 
Wanabodi.. Mwenendo wa kisiasa, kati ya watani wa jadi CCM na Chedema sasa umeanza kuzua mijadala ndani ya jamii. Wananchi wanahoji iko wapi kasi na upepo wa mabadiliko ilikuwa nao Chadema mwaka 2010 na mwaka jana ilikoyeyukia. Huku CCM kilichokuwa kimeanza kudorora sasa kikionekana kupaa zaidi kuliko ilivyotarajiwa na wengi. Mwamko wa Chadema ulianza kushika kasi mara baada ya Slaa, kuteuliwa kugombea Urais, mwamko huo uliendelea hata baada ya uchaguzi, na hasa baada ya chama hicho kuamua kufanya siasa zake kwa njia ya maandamo mikoa ya Kanda ya Ziwa hadi Nyanda za Juu Kusini. Wadadisi wa mambo ya kisiasa wameanza kuhoji ni wapi kasi hiyo imeyeyeka ghafla na kukipa nafasi tena CCM kuanza kutamba katika maeneo mbali mbali nchini. Hali hiyo ya kuanza kudorora kwa Chadema imelezwa pia kukikumba chama cha CUF kupoteza mvuto. Chadema inatakiwa ibadili sera zake na falsafa mpya za kuendelea kuwashawishi Watanzania.
KAMA HUJAONA KUPANDA UMAARUFU KWA CHADEMA BASI WEWE INAWEZEKANA UMEFUFUKA LEO AU ULIKUWA UNAANDIKA THREAD HII UKIWAZA KWA KUTUMIA MASABURI? kifupi chadema ipo juu sana ila kama unafanya analysis kupitia ikulu au unaifanya kwa kushirikiana na Jusa huwezi ona kupaa kwa chadema na kuporomoka kwa CCM, mfano mtaani kwangu mm tulikuwepo wapenzi wa chadema wa 4 october 2010, Leo hii kuna wanachama zaidi ya 80 katika mtaa unaobeba kama watu 300 tofautisha wanachama na wapenzi ss 2015 najua tutachukua mtaa mzima CCM walikuwa na shina limekufa tukachukua mpaka na balozi toka nje uje kufanya analysis mkuu.KARIBU MWANZA UJIONEE!!!!! PEOPLESSSSSSSSSSSSS!
 
Kinachomtafuna mleta mada ni hila za Udini na Ukabila hasa nyakati za uchaguzi
 
Watanzania tuamke, tujifunze kwa Wamarekani kila mtu anapaswa kueleza ataifanyia nini nchi yake na sio nchi itakufanyia nini.
 
Back
Top Bottom