CHADEMA bado mno Kupambana na CCM

Wachangiaji wengi wa JF ambao wanabeza CDM hua ni watu hoi sana ktk kujenga hoja na ufahamu wa mambo.... Hivi chama kilichopo madarakani Kenya kilikua na utayari lini? au vyama tofauti tofauti nchini Ghana vinawezaje kuongoza nchi yenye uchumi mkubwa km Ghana?

Au hata Mandela na ANC waliwezaje kuongoza nchi .... ? kabla ya kuchaguliwa Mandela ANC haikua hata na Mbunge mmoja....Au kwako wewe ukongwe wa chama ndio uongozi sahihi? TANU haikua kongwe ilipopokea madaraka Tanganyika au ASP ktk mapinduzi ya Zanzibar

Vizuri kwa kuchambua hoja Ya Kenya Na Ghana ni mabaya sana kupenda kupitia Ghana kunaviongozi waliuawa kikapitia kwenye kipindi kirefu cha gasia na wakabadili yama sana kwani ata vilivyochukua madaraka baada yakuvitoa vyama vikonge havikutimiza ndoto ilivyotazamiwa. Na Kenya ni kama vilevile na mwendo wa chadema nahisi ni huohuo ila ni muhimu kukipigania kiingie kwenye mamlaka ili tuingie kwenye mpito kuelekea democrasia ya kweli
 
Umejaribu kuandika ukweli mdogo sana lakini umeupamba na uongo mwingi sana na hivyo umeharibu kila kitu katika hoja yako.

Kwa mfano:
1/Ni kweli kuna haja ya CHADEMA kujieneza kwa njia mbali mbali lakini si kweli kuwa wanachokifanya CHADEMA kwa sasa hakina Faida. Why? Matunda yake yanaonekana wazi wazi tena sasa na wakati huo huo CCM wanahaha usiku na mchana tena bila mafanikio kutaka kuithibiti CHADEMA lakini wapi. Too late!!!

2/Mpaka sasa sijaona watu ndani ya CCM wenye uwezo wa kupambana na hoja za CHADEMA. Secretarieti mpya ya CCM ya sasa ambayo ndio timu ya CCM 2015 ina watu dhaifu sana kisiasa(Wachovu, wachafu, waoga, wapuuzi), kwa mfano watu kama Kinana, Mwigulu, Migiro, Nape, Khatibu, Meghji, Mangula, Kikwete nk. Ni nani katika hao ana ubavu na uhalali wa kwenda kuwaambia wananchi waendelee kuiamini CCM?

3/Si kweli hata kidogo kuwa wananchi hawatakuwa na Imani na CHADEMA 2015.
Ni juzi tu uchaguzi wa kata 22 za udiwani umefanyika, kampeni zake na matokeo yake yanaweza kutumika kama 'Pilot Study' ya 2015, swali kwanini CHADEMA wamekuwa na matokeo mazuri ya kiujumla kama hawaaminiwi na watanzania?

4/Japokuwa ni kweli kuna haja ya CHADEMA kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa wakina mama na wazee, Why? Ni wapiga kura wazuri sana kwenye uchaguzi.
Lakini bado ukweli unabaki pale pale kuwa uchaguzi mkuu 2015 utaamuliwa na vijana. Why? Ndio waliokuwa wengi katika jamii na hivyo ndio wenye uchawishi mkubwa. But good thing kwa CHADEMA ni kwamba vijana wengi ni wapenzi wakubwa sana wa CHADEMA.

kula za rika zote ni muhimu sana kwa CHADEMA. Ni makosa makubwa kujitathimini mafanikio kupitia uchaguzi wa madiwani ambao chadema walifika kila mtaa.
Je wataweza kufika kila mtaa uchaguzi mkuu 2015.

Nachosisitiza ni kati ya 25% ya watanzania wanaohudhuria mikutano ya hadhara vipi kuhusu wasiokuja kwenye mikutano hiyo. Ujumbe uwafikiaje au tuwabeze kuwa wajinga hao? Hawana akili maccm je itasaidia kuwabadili tafakari!!
 
Chadema inahusishwa ktk matukio mengi ya giza na ya kinyama. Hilo ndio linalowaogopesha watz wapenda amani
 
kaka unayoyasema ni sawa lakini,
kama ungekuwa kwenye game ungelijua mpambano ulivyo mkali,
hujui na hutaki kukiri mbinu za kimafia wanazofanyiwa na CCM vyombo vya dola??,

CDM kama mtoto yatima hapa TZ, anategemea nguvu ya umma tu,
anashindana na nguvu ya pesa za kifisadi nauharamia wa CCM,
si busara kuwalaumu ni vyema tuwatie moyo na tuwasapport katika mapambano

nitofautiane na tathimim yako, kwamba bado sana, CDM kwenda ikulu ni hivi, nikupe mfano katika uchaguzi wa juzi kulikuwa na kata 26, ccm kata 16 cdm kata 6,

kama uchaguzi ungelifanyika Arusha Cdm inachukua kata 4 ingelikuwa imepata kata 10, kwa 16 za ccm, kumbuka kuwa ccm ni chama dola, kinatumia mbinu nyingi za kiharamia kushinda

CCM KUIKABIZI NCHI CHADEMA mwaka 2015 ni sawa na Mzee mlevi kutaka kumkabidhi uongozi wa familia kijana anayeanza kubalehe.

Ni kweli Tanzania inahitaji mabidiliko makubwa ya kisiasa na uchumi ambayo yanaitaji mabadiliko makubwa yanayoitaji kung'olewa kwa mfumo wote yani chama tawala na vingozi wake wote hata kama wakiama chama. Lakini jinsi Chadema wanavyoreact dhidi ya Hujuma kutoka CCM Hakika wasitegemee kujijenga au kuongeza wafuasi ila ni kukosa kura za wanawake na wazee waoga.

Chadema pambaneni kwa upole toweni elimu ya uraia kwa njia mbalimbali watu wajue mnachopigania. Ongezeni mbinu za kujieneza. Tena ujumbe umfikie mtu alipo kwa upole. Wizi kwenye miradi, madeni ya taifa mfumo wa kodi na rushwa. Mikataba mibovu ndio turufu za chadema. Kwa kutoa Majarida na magazeti na ukurasa wa kati kuchapishwa kama vipeperushi vyenye maelezo mazuri machache na picha nzuri za rangi za mikutano ya Chadema. Kuonesha uongozi wa chadema Bara na Visiwani na kukomesha propaganda za udini Zinazokidumaza Chama chenu mikoa ya Pwani kuwa si za kweli.
Lazima muwe na vipindi kwenye TV NA redio vilivyosanifiwa vizuri vya kutoa elimu ya uraia na malengo yenu na kuacha kuwa watu wa kutupiana tuhuma kila siku na akina Mwigulu
mtikila na Mbatia na CUF NA KUONEKANA KAMA WATU WA KUGOMBANA NA KILA MTU.

MNAONEWA SANA RAKINI KUMBUKA HASIRA ZA MKIZI.

Kuna watu kama Jonas Savimbi na Akina Gadafi hawakuwa sawa lakini waliaminiwa sana na watu. Mfano mpaka leo Chama Cha UNITA. Kina wabunge wengi na Kinaaminiwa sana Angola ingawa kilitajwa kama kundi la kigaidi na Umoja wa mataifa. Kwahiyo si ajabu kwa CCM KUWA NA WAPENZI WENGI ZAIDI TANZANIA.
Na kubadili hili na busara ya hali ya juu inaitajika na kiburi, visasi na hasira haviitajiki kabisa.

Mfano Mandela, S. Biko na wanamziki wa S A kama Lucky Dube, Sarafina Ingawa wazungu waliwatesa na kuwabagua wao hawakuubiri visasi au chuki dhidi yao bali waliubiri kupinga ubaguzi Dhidi yao
na kusema watu watu wote ni sawa tupendane na kuheshimiana. Kwa siasa za Chuki na kutambiana kuujumiana kati ya Chadema na Vyama vya CUF NA CCM Ndipo napoiona chadema kama kijana anayebalehe.


"Wanaosema kuwa Chadema ni mpango wa Mungu hawajui Walisemalo wamepotoka labda kama ni mpango wa Mungu wao na si yule moja tunayemjua.

Safari bado ndefu kuelekea Democrasia ya kweli na Chadema kitusaidie kufikia huko
 
Chadema inajiharibia yenyewe. Tukio la kibanda imehusishwa, tukio la tindikali, tukio la kutishiwa bastola kwa mama zitto, nk hii sio picha nzuri kwa chama kinachokua
 
kwa taarifa chadema wanakura ya kina mama na wazee labda ya mke wako na babu yako tu

hajui kwamba wakina mama ni mamazetu na wake zetu? Siwezi kumwacha baba au mama wapotee kwenye uchaguzi,then wanipe shida
 
Pilipili usizozila zinaanzia wapi kukuwasha eti baba kunani, vipi umepita lumumba leo kupitia posho.
Ama kweli njaa ya mtu mojamoja haina adabu.
 
Si kweli hayo ni mawazo mgando!

Tunavyowatukana wanaotofautiana na sisi humu ndivyo tunavyowachukia wanaotukosoa mitaani huku kunatufanya tuonekana kama wakolofi.

Walioko sisiemu upeo wao umeishia hapo kuwabadili lazimaa uoneshe unawapenda wao unaheshimu mitazamo na akili zao na waelimishe kwa upole ata akibadilika awe ni msaada kwa chama nyie ishie kuwatukana humu eti waame vyama kwa kuogopa kutukanwa.

Watu wasioijua Chadema ni haki yao kuichukia.

Mwanafalsafa "Emmanuel Joseph" wa Israel mwaka 0031 alisema Mpende Adui yako. Kuönesha unamchukia uku anataka kuungana nawe ni kazi.

Tunaomba muandae CD , majarida magazeti.
Muwadokeze watu historia za tawala kandamizi na zilivyoondolewa.
MFano french Revolution, Chartizim uingereza na Marekan harakati za wakulima wakusini waliopuuzwa dhidi ya wenye viwanda wa kaskazini.
Naamini tayari kunamov
zinazoonesha harakati hizo hadi kukua kwa democrasia kwenye nchi hizo huku mkihusisha tawala hizo na utawala huu na kuonesha harakati za wanyonge zinavyofanana na hizi za chadema za sasaivi.
ANDAEN CD BAC muziuze bukubuku tu na muhakikishe kuwa harakati za sasa ni mabadiliko kwa njia ya Amani. Masikini tupendane na tushirikiane hata kama tunatofautiana itikadi na kutopambana
 
CHADEMA napenda kuifananisha kama kijana aliyefikia kwenye "balehe" basi anajiona yeye ndiyo yeye anaweza kufanya kila kitu anaweza kupigana na kila mtu na hata kufanya jambo lolote analotaka, nadhani wanaojua tabia za watoto walio kwenye balehe watakuwa wananielewa. CHADEMA kuchukua hii nchi 2015 bado sana ni ndoto za mchana kweupe....
Mimi nadhani hawa "mashabiki" wao wachache "wasiojielewa" waache upotoshaji kwa wananchi!! Wananchi wa kipato cha chini wasiokuwa na Elimu ya kutosha wanapelekeshwa sana na hasa hasa ukizingatia wale vijana wa umri wa kati ambao wako "ambitious" sasa hawa ndiyo haswa wanatumiwa na CHADEMA kama vile fimbo!!
 
Back
Top Bottom