Chadema bado hawajaonyesha msukumo wa kuleta mabadiliko

mpendadezo

Member
Jan 16, 2012
27
10
Nimekuwa nikifuatilia matamko mbalimbali ya cdm dhidi ya serikali lakini naona wamekuwa too soft kiasi kwamba hata serikali imeshawazoea.Sijui wameogopa baada kutishwa na kesi au ndio uwezo umefika mwisho. Kama chama kikuu CHA UPINZANI na serikali inayosubiri kuingia madarakani si lazima wasubiri 2015. mapambano yanatakiwa yaanze sasa.
Nimeona nitoe hoja hii kwani kuna mambo ambayo cdm waliyapigia kelele na hayajafanyiwa kazi lakini naona wamenyamaza.
Mfano ni SUALA POSHO MPYA ZA BUNGE, SAKATA LA JAIRO, MSWADA WA KATIBA MPYA.
Pia kuna masuala mengine kama BEI YA UMEME na masuala ya nyuma kama RICHMOND MEREMETA TANGOLD KIWIRA, SUALA LA RADA NA ZAIDI EPA. Haya yote yangetakiwa yafanyiwe kazi kwa MIGOMO NA MAANDAMANO HADI HATUA ZICHUKULIWE Lakini wapi nimeandaa mabango nasubiri watangaze wapi. Baadhi ya wananchi tumechoka hatuna ajira tupo tayari kulifia taifa letu kuliko kukaa tu vijiweni bora tupambane angalao hao mafisadi wakose usingizi ikiwezekana wahame nchi.
CHADEMA, TUNASUBIRI MUANDAE MAANDAMANO ANGALAO TUANZE NA HILI LA BEI YA UMEME NA EPA. HII ITASAIDIA KUNDAA WANACHI KUDAI HAKI ZAO NA SIO KUKAA VIJIWENI. MABADILIKO YANAWEZEKANA ILA YANAANZA NA MIMI NA WEWE. TUCHUKUE HATUA KUNUSURU TAIFA LETU.
 
Back
Top Bottom