CHADEMA Arusha kwatifuka

@Nanyaro, unalofanya hapa Jamvini ni jambo la maana sana - kutoa taarifa kuhusu hali ya Arusha. Hii inauwa rumours na ningeshauri kwa kipindi hiki ambacho Arusha bado iko kwenye misukosuko basi uendelee kutoa taarifa (as events take place).

Ombi langu ni moja tu na naomba ufikishe juu - WATIMUENI MADIWANI WASALITI. Watanzania tunataka uhuru na haki.basi. Hawa madiwani wameshakuwa 'contaminated' hawafai hata kidogo, na wataleta shida huko mbeleni si tu kwa chama bali kwa Taifa zima. Tanzania tumefika hapa tulipo kwa sababu ya umamluki, hatusimamii yale tunayohubiri. Hawa madiwani waliandamana na wale marehemu 3 na wahanga wengine waliojeruhiwa. Leo inakuwaje wanasema yameisha huku yale yaliyowafanya wakakaa barabarani hayajatendeka?

kamanda naamini cc itatoa taarifa mara baada ya kikao kuisha,
Haya ya Arusha ni kikundi cha wahuni wenye lengo la kuvuruga chama ila pia hawatafanikiwa,ni moja ya majaribio dhalimu ambayo kamwe hayana nafasi,na hayakubaliki

• Thanks
Reactions: FJM
@Nanyaro madiwani hawa tayari wameshaharibikiwa,kabisa kama wameshindwa kuungwa mkono kwenye hii move basi lazima mulinde heshima ya chama na wananchi na musikae kimya lazima hatua kwa hatua toeni taarifa mukiweza kila kitu kiwe kinakuwa recorded si munajua akina Jambo leo,Uhuru,Habari leo,mzalendo Tazama wote hao watasema wanayoyajua mwenyekiti angeitisha mkutano kuelezea wananchi wa Arusha hilo sakata,Once again CCm lazima waaiishwe kwa sababu mchoro wote huo ni Mkuchika,wassira na Pinda

wanachama na wafuasi wa chadema waandamana na kufunga ofisi ya mkoa kwa nia ya kumpinga lema ambaye wanasema ndie chanzo cha mgogoro wa Arusha kwa kuwagawa madiwani, wale ambao wasio muunga mkono yeye huwaita wasaliti wa chama wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti yakimshutumu lema kukivuruga chama hicho, wameitaka kamati kuu kuketi mjini Arusha au aende Dr slaa akatatue mgogoro huo.

Hizi habari ni za uongo asilimia99% nimepita hapa chadema mkoa. Mbona hamna lolote "maandamano" ama ofic ya chadema kata ipi? Mod tukiendelea hivi bila source. Sijui kama tutafika. Mtu aliopo Arusha anipinge

@FaizaFoxy, soma mchango wa mdau No30 hapo juu. Hao vijana waandamaji (17!) wamekodoshwa, na sasa wanadai chao!
Na mchezo wa kukodisha umekuwa sugu sasa, Igunga waliaji, wazimiaji, na hata wabeba machela walikodishwa. Kwenye mikutano yenu mnabeba watu kwenye fusso! Sasa naona kwa Arusha mmemua kukodisha waandamanaji, lakini nakuhakikishia hapa mtaumbuka. Za mwizi 40.
Ushahidi wa picha huu hapa. ebu izoom FF aone vizuri maana anatumia miwani.
CCm2010.jpg

dah mkuu kweli nimekubali kwamba JF huwa hatuondoki bali tunajivua magamba tu

nimeona join date yako, na ulivyokumbuka GT ni Dr. WHO halafu nikajiangalia mwenyewe na kucheki slidingroof.... kumbe sote ni walewale tu

NIMEKUMBUKA KEKULE STRUCTURE... LOL

PROFESSOR.... HAYA MUZEYA KARIBU TENA

Arusha itajengwa na viongozi makini wenye kuelewa dhana ya maslahi ya taifa na cyo
viongozi wenye ubinafsi,kwa upande wangu binafsi napenda kuipongeza kamati kuu
kwa umakini wake wa kuelewa umakini wa jambo hili na maslahi kwa umma.keep it up

wanachama na wafuasi wa chadema waandamana na kufunga ofisi ya mkoa kwa nia ya kumpinga lema ambaye wanasema ndie chanzo cha mgogoro wa Arusha kwa kuwagawa madiwani, wale ambao wasio muunga mkono yeye huwaita wasaliti wa chama wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti yakimshutumu lema kukivuruga chama hicho, wameitaka kamati kuu kuketi mjini Arusha au aende Dr slaa akatatue mgogoro huo.

Arusha hakuna mgogoro na hayo unayoita maandamano yalikuwa ya watu 17,hawakuwa na hoja,pia ofisi haikufungwa,huu ndio ukweli,

Nawasilisha mawazo na mtizamo wangu kama ifuatavyo:

Arusha hoyee,Katika kutafuta haki uoga wa kuthubutu ni dhambi kubwa sana itakayo kwamisha maendeleo yenu, CDM inavunja taratibu na sheria kandamizi kwa wananchi na hata viongozi bila kujali kabila wala eneo analotoka mtu inaweka maslahi ya taifa lake mbele.

Makamanda, tulieni wakati tunaenda kushuhudia mabadiliko makubwa yenye kuleta maslahi ya kwenu ninyi na taifa kwa ujumla,ninaelewa umuhimu wa jambo hili hasa katika siasa za sasa,lakini hatuna budi kusimamia na kuishi katika yale tunayoyamini kuendelea kujenga umoja wetu tuliouonyesha tangu mwanzoni na mpaka sasa.

msigawanyishwe na viongozi wenye maslahi binafsi kwa wananchchi wao na hata kwa chama chao,Hawatufai na tutaendelea kuwapinga kabisa

Best regard
JOB SEEKER

• Thanks
Reactions: FJM
Msiongee sana hao madiwani si chadema tena maana wamenyang'anywa kadi.
pia si madiwani tena tusubiri uchaguzi mwingine.

Baada ya kupata taarifa ya madiwani kuvuliwa uanachama sasa tunataka kuona reaction ya akina Mboya na wahuni wenzake. Walidhani CDM ni kama nccr iliyosambaratishwa na maneno

Safi sana cc kuu ya CDM, bora tuzikose hizo kata kuliko kuwa na viongozi wasioheshimu katiba na sheria za chama. Hiilo ni funzo tosha kwa viongozi wengine. Ukitaka kujenga tahasisi imara uwe tayari kufanya maamuz magumu.

Nadhani c.c.m watajifunza kitu hapo!!! sio kila kukicha kelele tuuuu, kuvua gambaaa, mara siku 90, mara siku 120.

Huwa kila siku nasema,
Upinzani Tanzania badoo kabisa!
Tuendelee kujenga umoja wetu na CCM yetu! Hawa wanaoenda upinzani siyo kwamba wanapenda sana maslai ya TZ but ni kutokana na uchu wao wa madaraka hasa baada ya kuenguliwa CCM!

Kila mikwaruzano kidigo ndani ya CDM unarukia kusema upinzani bado na wapinzani wana uchu wa madaraka. Mbona husemi minyukano mikubwa mikubwa ndani ya chama chenu cha magamba, kutukanana wazi wazi kutokana na uchu wa kulimbikiza mali ya Watz (na wengine kujitoa kwa ajili ya "siasa uchwara" -- kwamba nayo ndiyo mwisho wa CCM?

Unakera kweli kweli kwa hoja zisizokuwa na mashiko. Yenu makubwa unaona sikitu, lakini ya CDM madogo unayafnya kuwa milima mikubwa!! Hata aibu hauna kabisa!

Kwani unalazimishwa kuchangia? Si ukae kimya tu kama wenzako wengi ambao hatuwaoni tena siku hizi humu ndani kwa kukosa hoja!

Back
Top Bottom