eliesikia
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 787
- 755
Umeweka fikra nzito na umeona mbali! Kuishitaki NEC kwa kutofuata sheria, kwa kudharau maoni ya wapiga kura sio sawa na kukataa au kupinga kutwawazwa JK! Safi sana! Lakini usikate tamaa kiasi hicho. Najua wanasiasa wanapinda pinda njia hadi wafike wanakotaka! Vuta subira!
Mimi nasubiri kwa hamu kesi za kupinga matokeo ya ubunge kama kule Moshi Vijijini, Njombe Magharibi, Geita nk, lakini sioni kinachoendelea, CHADEMA angalieni msije mkatupelekesha kwingine!
Hakuna kitu yaelekea huyo Ruta sio mwanasheria... Kwenye mahakama sio urobot pale lazma utashindwa maana kila wakili anajua sheria sasa huko ni kupoteza kesi kirahisi.. Hata mimi ningepewa hiyo kesi siwezi maana hiyo sheria ya mwaka 1992 iliyoko ibara ya 41(7).. Huwezi kuifuta au kumzuia mwenzio kuitaja mahakamani.. Cha msingi mahakamani ni lazma uwe na kesi ya msingi lakini hiyo ibara inailinda hata NEC.. Na lazima mwenzio umweke kwenye mazingira ya kujibu kesi(shitaka) kama sivyo huwezi kufika mbali zaidi utaabika... Sisi wanasheria tunajua hilo... Waacheni CHADEMA waendelee na hilo ili CCM wakiloga wakaenda mahakamani kwa kesi ya kikatiba sasa hapo kazi itakuwa rahisi sana....