CHAD 1 - 2 Taifa Stars: Tanzania Kidedea!

Hongera zetu, kama Chad wangetuchapa ingekuwa mbaya sana maana sitarajii ushindi mwingine wowote kwenye kundi letu.
 
Hongera vijana kwa kazi nzuri ugenini nadhani huo ndo ushindi wa kwanza kwa babu poulsen akiwa nje ya tanzania
 
Chadi nayo ni ya kufungwa na Tanzania tena 2-1 tukashangilia!!!!! ni vibonde hao ilitakiwa Tanzania ishinde gori zaidi ya 5.
 
Kipofu kaona mwezi hapo wabongo mtabonga kweli na mechi zilizobaki mnaeza chapwa zote kwakulewa sifa
 
Katika watu ambao sijafurahi katika hili ni mimi!
Niulize kwa nini?
>>Kwanza Chad iko chini kiwango ukilinganisha na sisi kwa zaidi ya nafasi kumi!! SHANGWE YA NINI?
Pili tukumbuke kwamba tukivuka hapa tunakutana na nani? ( MOROCCO,IVORY COST) Ni kwa mantiki hiyo basi nasmea kuwa tulipaswa tushinde zaidi ya bao tatu bila! ANYWAYS hongera Stars si Mwanzo Mbaya maadamu ni Ugenini!
Tusibweteke ila tujipange sisi tumeweza wao washindwe wa nini? Tuzingatie kauli hii
 
Sasa watapelekwa bungeni kupongezwa. Tanzania bwana?

Pia wataitumia kisiasa, tumejaribu tumeweza na ujinga ujinga mwengine


tuache ujinga tuungane kama taifa ili tuweze kusonga mbele
 
Nchi kama Chad si ya kudharau hata kidogo, kumbuka Niger walisababisha Bafana Bafana washindwe kukwalifai kwenda Gabon...
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom