Chachu na tamu ya mapenzi

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,878
5,424
Mwanaume wa nchini ya Italia
ambaye alionja chachu ya mapenzi
baada ya kutorokwa na mpenzi
wake siku harusi ameenda
mahakamani kudai fidia ya dola za
Kimarekani 743,000 kwa kuvunjwa
moyo na kuchezewa hisia zake na
pia kupoteza kiasi kikubwa cha
pesa.

Mwanaume huyo mwenye umri
wa miaka 32 alitumia pesa nyingi
kwaajili ya maandalizi ya harusi na
mchumba wake huyo lakini siku ya
harusi mchumba wake aliroroka na
mwanaume mwingine.

Mwanaume aliyetajwa kwa jina
moja la Riccardo, alikodisha jumba
la kifahari kwaajili ya harusi yao
nje kidogo ya jiji la Rome,
alikodisha hoteli kwenye kisiwa
kimoja cha Pacific kwaajili ya
Honeymoon (fungate) na pia
aliifanyia marekebisho makubwa
nyumba yake ili kukidhi mahitaji
ya mke wake mtarajiwa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la
Italia, ANSA, siku ya harusi Riccardo
na familia yake na ndugu na jamaa
walikuwa tayari kanisani
wakimsubiri bi harusi awasili lakini
badala yake aliwasili kaka wa bi
harusi ambaye alimwambia
Riccardo kuwa dada yake hatakuja
kwenye harusi.

Mchungaji alilazimika kuvunja
shughuli zote za harusi baada ya
kuambiwa kuwa bi harusi
ameteroka na mwanaume
mwingine ambaye alikuwa na
uhusiano naye wa kimapenzi.

Taarifa zimesema kuwa Riccardo
amekodisha wanasheria kwaajili ya
kumfungulia kesi aliyekuwa bi
harusi wake akimtaka yeye na
familia yake walipe gharama zote
za harusi alizoingia.


:,;VIPI TANZANIA SHERIA KAMA HIZI ZINGETUNGWA INGEKUWAJE? KUSHTAKIANA NA PESA KURUDISHWA INAPOWEZEKANA.
 
Huu mchezo mbaya sana, its better angemwambia jamaa kabla hajafanya yote hayo. Ingawa hatuna story kamili upande wa the bride sidhani kama ilikua love at first sight na huyo jamaa alokimbia nae..
 
Mmmh matukio mengine hapa duniani, ni magumu kuelezeka na kuvumilika. Akishinda kesi na wamlipe kaka wa watu pesa zake.
 
Hiki ni kisasi kabisa, huwezi mfanyia mwenzako kitu kama hicho wakati ulikuwa na uwezo wa kukataa. ni kama huyu dada alikuwa analipiza kitu kwa huyo jamaa
 
Back
Top Bottom