Ch 10 muwe makini -- Kenneth Kaunda bado hajafa

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Wakati anatangaza habari za uboreshaji wa reli ya Tazara katika kutimiza miaka 35 tangu reli hiyo ianze kazi, mtangazaji wa Ch 10 Mcharo Mrutu alimtaja Rais wa zamani wa Zambia -- Kenneth Kaunda kama ni hayati yaani marehemu, sambamba na Mwalimu Julius Nyerere.

Navyofahamu mimi Kaunda bado hajafa. Watangazaji wa Ch 10 lazima wawe makini.

Chanzo: Taarifa ya habari Ch 10 saa moja usiku huu.

Nami nimemsikia hivyo nikashituka sana. Kweli vichwa vya watangazaji wa Ch 10 ni nazi kabisa.

Hawa ni dot com nini? Vijana wa kizazi hiki hawajui kabisa historia. Hebu fikiria huyo ndo mtagazaji ambaye tunaamini anaupate za kutosha katika taarifa kweli ameshindwa kujua kwamba Dr. Kenneth Kaunda yupo hai? Kwa taarifa yako, Dr Kenneth Kaunda yu hai na kwa sasa anaishi Johannesburg, Afrika ya kusini.

Wakati anatangaza habari za uboreshaji wa reli ya Tazara katika kutimiza miaka 35 tangu reli hiyo ianze kazi, mtangazaji wa Ch 10 Mcharo Mrutu alimtaja Rais wa zamani wa Zambia -- Kenneth Kaunda kama ni hayati yaani marehemu, sambamba na Mwalimu Julius Nyerere.

Navyofahamu mimi Kaunda bado hajafa. Watangazaji wa Ch 10 lazima wawe makini.

Chanzo: Taarifa ya habari Ch 10 saa moja usiku huu.

Nilipoona title tu, moja kwa moja akili yangu ikanipeleka kwa Mcharo Mrutu, huyu bwana huwa anaruka ruka sana, hayupo makini sometimes. Bora sana ya David Ramadhani!

Hawana budi kuomba radhi kwa tukio hili kwenye taarifa yao ya habari kesho saa 1 jioni ikiwa hab ari ya kwanza

kweli ni taaluma ya utangulizi wa habari na si utangazaji wa habari..................huh

Wakati anatangaza habari za uboreshaji wa reli ya Tazara katika kutimiza miaka 35 tangu reli hiyo ianze kazi, mtangazaji wa Ch 10 Mcharo Mrutu alimtaja Rais wa zamani wa Zambia -- Kenneth Kaunda kama ni hayati yaani marehemu, sambamba na Mwalimu Julius Nyerere.

Nafanya kazi hapo,
Kwa niaba ya Africa Media Group wamiliki wa channel ten,DTV,Magic FM,,bunco radhi kwa kosa hilo.
Asante.

Navyofahamu mimi Kaunda bado hajafa. Watangazaji wa Ch 10 lazima wawe makini.

Chanzo: Taarifa ya habari Ch 10 saa moja usiku huu.
Nafanya kazi hapo,
Kwa niaba ya Africa Media Group wamiliki wa channel ten,DTV,Magic FM,naomba radhi kwa niaba ya AMGL kwa kosa hilo.Ni tatizo la kibinadamu tu.

Mathias Byabato
Channel ten Reporter

Asante.

Tatizo kubwa la sisi vijana hasa, hao watangazaji na waandishi wa habari huwa hatuna utamaduni wa kutafuta na kufuatlia habari za kimataifa. kuna makosa mengi huwa yanafanyika na mengine ni madogo kiasi kwamba hadi mtazamaji au msomaji unakosa ladha ya habari. Na ndio maana zile Tv tunazo zitaja kama za maana zina idadi kubwa ya wazee ukilinganisha na vijana na wazee wengi wamekuwa makini katika kukusanya na kutangaza habari. Mfano mahojiano anayoyafanya Simonyo (dk.45) nimepesi mno ukilinganisha na mahojiano aliyokua akifanya General Ulimwengu kwenye General on Monday

tasnia ya habari tanzania imekumbwa na makanjanja wengi, vijana wengi wanaofeli kidato cha nne au sita wanakimbilia uandishi wa habari,kwa wenzetu ili uweze kuwa mwandishi wa habari lazima uwe na taaluma nyingine kama ya siasa,uchumi sheria uhasibu au uhandisi,mfano mzuri angalia BBC au CNN wale wanaoripoti habari za uchumi ni wachumi halikadhalika wale wanaoripoti haabri za siasa,( utasikia political corespondent au business corespondent nk) hapa bongo ukisoma magazeti habazri nyingi hazina mpangilio,ukisikiza habari wanatafuna tafuna hawatoi habari za kina,hawasomi vitabu na mitandao ili kunoa akili zao. inabidi vyuo uchwara hivi vilivoibuka viangaliwe upya na pia wamiliki wa vyombo vya habari nao wanataka watu wa kuwalipa mshahara kidogo ili mradi habari isomwe.
byabato kuomba msamaha hiyo haitoshi kutangaza rais wa nchi ni hayati wkt yuko hai ni kosa kubwa hata kama alishastaafu bado ana heshima ya rais,, huyo mwandishi inabidi afukuzwe kazi na chombo hicho kiombe msamaha ktk medias mbalimbali na fidia ilipwe kwa familia ya kaunda..hakuna mchezo kwenye habari.

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom