CF: Nitagombea kipindi kimoja tu - Dr. Slaa

khee kumbe Zuma wa zamani hivi ..lakini ng'ombe hazeeeki maini..hivi huyu wa kwetu ana ngapi?khaa 60 kwa hiyo akikutana na obama ,obama anamuamkia shkamooo halafu anamuomba msaada

Sijasikia sehemu yoyote katika hotuba za Slaa akizungumzia suala la kuomba misaada.Amezungumzia kupunguza ukubwa wa serikali,kusimamia rasilimali,ukusanywaji mapato,uboreshaji wa mazingira kwa mtanzania wa kawaida aweze kujiajiri n.k. Hayo ndiyo mambo ya msingi ambayo yataifanya nchi iwe inajitegemea,kama wataleta msaada walete,uhusiano na usa au nchi nyingine yoyote utakuwa ni wakuzinufaisha nchi zote mbili,si danganya toto.Hiyo ndiyo misingi inayotakiwa kwa miaka mitano ijayo.hilo la misaada sijalisikia.
 
Nina mashaka na kijarida hiki kwanza kime skaniwa meaning huenda umeandika habari hizo mwenyewe kisha uka scan so cdhani kuwa dr. wa ukweli alishasema hivyo.
 
Hata JKN mlilia aendelee.

Kama kweli Slaa ana nia ya kufanya mabadiliko, miaka mitano inatosha na atakuwa na miaka 67 atakaa pembeni apumzike huku akipata HESHIMA kubwa sana kupita Marais wote waliopita ukiacha JKN.

Atakachotakiwa kufanya ni kuweka NJIA imara ambayo Tanzania itabidi ifuate.

Cha muhimu zaidi atakachoweza kukifanya chenye NGUVU kuliko VYOTE ni kuibadili katiba ya Tanzania. Hii ikibadilika na kuwa ya KISASA na kubadili mifumo yote ya kukipendelea chama kimoja, itatosha kabisa.

Ningelipenda zaidi aweke uhuru wa watu kugombea hata akiwa nje ya chama. Pia wabadili masharti ya chama kupata rusuku kuwa kwa mfano kama chama kina chini ya ASILIMIA 5 ya Wabunge basi KISIPATE ruzuku na wabunge wake wasiingie Bungeni. Hii itasaidia kuuwa VYAMA UCHWARA vinavyokuwepo kuleta usumbufu na kuwa Kitafunio cha chama tawala.

Kujenga Vyombo vya USALAMA wa TAIFA itakuwa nalo jambo jema. Kuwepo sehemu ambazo viongozi watachunguzwa na kupewa kibali cha kugombea kuwa MBUNGE, WAZIRI na hata RAIS. Hii itasaidia kuondoa uwezekano wa viongozi WABOVU ndani ya nchi. Kama kiongozi anadhaminiwa na Matajiri wasiojulikana basi asipewe hata uongozi wa chama. Mapema kabisaaa hawa watu wasiwe na nafasi ya kugombea. Hili lingelikuwepo Tanzania, leo hii watu kama akina Mziray, RA, Mramba, Chenge wasingeliweza hata kuthubutu kugombea.

La muhimu kuliko lote narudia tena KATIBA na kujenga vyombo vya Usalama imara, Mahakama na Bunge imara. Mengine yoote yataanza kujipeleka yenyewe kwani ukifanya Madudu, basi utajibu kwa madudu yako na si kufikiri utapeta tu kama ilivyo sasa.
 
Mtu kama Slaa twamuitaji kunyoosha baadhi ya mambo tuu then apumzike.
Kama suala la katiba mpya nina hamu nalo sana hatuwezi endelea katiba ya CCM
 
Nina imani kabisa umati wa watu unaokwenda kumsikiliza Dr. Slaa si kwamba unakwenda pale ''kumuangalia'' - la hasha, wanakwenda pale kumsikilIza na nina imani kuwa huwa wanarudi majumbani kwao tayari wamekata shauri kumpigia kura - hawa ni watu wambao huwa wanakwenda pale kwa mapenzi yao wenyewe tofauti na watu wanaopelekwa na malori kwenye kampeni za JK huku wameahidiwa ''per diem'', usafiri wa kurudi majumbani, tshirt, burudani kiingilio bure etc.

Kama uchaguzi utakuwa huru na haki, CHADEMA stand a good chance of nailing it!

Tukumbuke tu kura hata kura moja ina matter. Siku ya uchaguzi tuache uvivu au mizaha na kukwepa kupiga kura. Watu wengi (bahati mbaya sana walio na uelewa na wenye uwezo wa kuleta mabadiliko) huwa hawapigi kura ati kwa sababu tu vituoni huwa kuna foleni ndefu na wao ''wapo busy'' and have no time to waste. Nimewahi kushuhudia watu wanaamua kwenda kukaa bar badala ya kwenda kupiga kura kisa hawawezi kusimama vituoni.

Well, kama kweli unapenda mabadiliko na unataka kuiona Tanzania yenye neema, fanya hima ukapige kura siku hiyo. Tubadirike japo kwa masaa machache tu. I assure you - you will never regret dakika chache ''utakazopoteza'' kwenye kituo cha kupigia kura sababu ya foleni nk.

Sijui CHADEMA wameandaa utaratibu gani wa kuhakikisha kila kituo, nchi nzima kina wasimamizi wa uhakika na jinsi gani wanaweza kuyapata matokeo haraka iwezekanavyo kutoka vituoni kabla hayajachezewa. Nina imani chama kitateua wasimamizi makini na waadirifu na hawatatishwa na police, usalama wa viongozi wala kuvutiwa na rushwa.

Ingawa sintoweza kupiga kura kwa sababu sipo TZ, nina imani kubwa kwamba Dr. Slaa ataibuka kidedea.

Hata kama watu bado wana mashaka na uwezo wa Dr. Slaa katika kuleta yaliyo mema, surely he will do better than JK.
 
Jamani miye naamini hata miaka 5 ni mingi kama kweli watu wanafanya kazi, siyo per diem ya mikutano. Tukipata misingi mizuri kupitia Katiba mambo mengi yatakuwa fresh. Elimu ya Uraia imekuwa nayo tatizo tayari CHADEMA wanaifanyia kazi toka operesheni sangara.
 
Kwa kufahamu kuwa Madaraka si haki yake,bali ni Jukumu la kila Mmoja,Dr Slaa ametangaza hadharani kwamba atakuwa Rais kwa kipindi kimoja tu (miaka mitano).Dr Slaa ameuonyesha Umma wa Watanzania kwamba,kila mtu anawajibika kuongoza Nchi,ikiwa tu atatimiza masharti na akikubaliwa kwa njia ya Uchaguzi (Demokrasia).Katika kipindi chote cha kampeini zake ameonyesha Uvumilivu,Uuungwana na Ustaarabu wa kutodharau au Uchochezi wa namna yoyote.Leo Mimi binafsi nautumia uhuru wangu wa kikatiba kutamka hadharani kwamba kura yangu ya NDIO nitampigia Dr.Slaa.

Dr Slaa keshaweza kutushawishi kwa maelezo kwenye kampeini zake kwamba ni Kiongozi Mahiri...Tumpe nafasi ili tumuone kwa vitendo,Kipindi chake cha miaka 15 aliyokaa Bungeni kimethibitisha kwamba ni Kiongozi mzuri,ameweza kusimamia kwa dhati kile alichoamini.Chadema leo ina uhakika wa majimbo mapya mengi kutokana na Kampeni wanazofanya Nchi nzima.Mabadiliko hayaji usiku mmoja,Chama kimejengeka zaidi....Tumpe ushirikiano Dr ili ashinde Uchaguzi Oktoba/31.Mabadiliko ya kweli yanamuhitaji kila Mtanzania...Tukianzia na juhudi ya mtu mmoja mmoja na baadaye kundi kubwa la Watu.

Sisi katika umoja wetu hapa JF tumsaidie Dr. kwa kuwashauri wale undecided voters,ambao kwa mtazamo wangu bado wapo wengi.Mimi binafsi nimewashauri ndugu zangu 20 na nina uhakika kuwa watampigia kura Dr.Slaa.Katika ndugu hawa 12 ni new voters lakini 8 walimpigia kura Kikwete katika Uchaguzi wa 2005.Nimefarijika kwa sababu hata Mama Mzazi mwaka huu atampigia kura Dr.Slaa,Mama kama Wazee wengine alikuwa anasema Wapinzani wataleta machafuko.......najisikia raha zaidi na kujiona ni mmoja wa wapenda mageuzi baada ya mmoja wa Ndugu zangu na Mgombea Ubunge kwa CCM kunithibitishia kwamba atampigia kura ya Urais Dr.Slaa.Ndugu huyu ameniasa Mimi na wapenda mageuzi wengine tuwe macho katika usafirishaji na uhesabuji kura,Matokeo huchakachuliwa ktk uhesabuji wa kura.....Hivyo kila mmoja atakayepiga kura awe mlinzi wa kura yake,Tuwepo vituoni kwa amani mpaka matokeo yatangazwe...Tujihadhari kuvaa nguo zenye viashiria vya ushabiki wa Vyama,tuwe watulivu na kuhakiki kila nyendo ktk maeneo yetu ya upigaji kura.Siku ya tarehe 31 iwe maalumu kwa ajili ya zoezi la uchaguzi tu.

Ndugu zanguni naomba kila usiku kuanzia leo, kabla ya kulala uwapigie simu au kuwa-textia ndugu zako wa karibu,na kuwakumbusha ku-vote tarehe 31 na waambie wampigie kura ya NDIO Dr.Slaa...Lugha ya Kejeli,Uchochezi na Matusi isitumiwe katika Text hizo.Kipindi hichi cha wiki moja,ni lazima tufanye kampeini ya mtu kwa mtu.Kila mtu akumbuke kuwa matokeo ya siku moja yatakuwa na impact mwa miaka 5 na kuendelea na pengine kubadili kabisa Historia ya siasa za Tanzania.Tuepuke namna yoyote ya Uchochezi na Fujo...Kwa asili watanzania ni wastaarabu na wakarimu,tuuendeleze utamaduni huu katika kipindi hichi tete cha uchaguzi.Tukishindwa tukubali Matokeo,mwisho wa siku sisi sote ni wamoja,Umoja wetu hautenganishwi na Itikadi za vyama.

"Mwenyezi Mungu Ibariki Tanzania na Uwabariki watu wake"
 
Binafsi na narudia kusema binafsi sikupenda kabisa maneno haya ya Dr.Slaa hasa wakati huu wa Uchaguzi..Ni nzuri ktk sura mojawapo ambayo wengi mmeipokea nadhani sura ya pili inaonyesha wazi kwamba Dr.Slaa anachukulia IKULU kama sehemu ambayo hayupo tayari kuchukua majukumu ya muda mrefu na anapaogopa, isipokuwa amelazimika kugombea na kwa agenda za muda mfupi.

Mapokezi ya hotuba hii yatazidi kuwachanganya wananchi pale walipoweka matumaini yao na kuanza kuwaza kesho itakuwaje! Nadhani Dr.Slaa kafanya haraka sana kutangaza kitu hii kwa sababu hapakuwepo na Ulazima hata kidogo. Kila hoja ina sura mbili na hakika ukiwa na matumaini zaidi kutoka kwa Dr.Slaa maneno haya yanavunja nguvu..
- Nawakilisha mawazo yangu - nilikuwepo.
 
Watu wamempenda Dr Slaa na wangetaka awe kiongozi wa serikali yao kwa angalau miaka kumi. Ila Slaa angependa kufanya hiyo kazi kwa miaka mitano kisha aachie CHADEMA iendeleze. Miaka mitano inaweza isitoshe kutekeleza ahadi zote, lakini ni ahadi za Slaa kwa niaba ya CHADEMA. CHADEMA itaendelea kutawala kwa miaka hata zaidi ya kumi, kama Watanzania wataitaka ifanye hivyo.

Dr Slaa hakutaka kugombea Urais hata kwa kipindi kimoja. Ni msisitizo wetu umemlazimisha ajitolee. Mwaka 2015, msisitizo wetu utamlazimisha ajitolee kwa kipindi cha pili. Msisahau tuligombana sana hapa kumtaka ajitoe MHANGA. Tutafanya tena hivyo. Kwa sasa, tusisikitike bali tumchague aanze kazi tuliyotaka aifanye.
 
One term - GOOD

Two terms - GOOD

Chali - ???

Mwanakijiji ndugu yangu, hiyo Cheche ni ya kwetu peke yetu?.
 
Usiwe na wasiwasi.. kila kitu kina mikakati yake. Watanzania tumezoea viongozi wakiingia madarakani basi ni lazima wagombee kipindi cha pili hata kama hawana uwezo. Watu wanashindwa kuelewa kuwa kama serikali ya Dr. Slaa haitafanya vizuri tayari keshajifunga kuwa hatogombea tena! Lakini leo hii tumekubali utamaduni mbovu kuwa Rais anaingia halafu anatumia miaka miwili kujifunza. Na wapo watu ambao wameshaamini kuwa miaka mitano ya kwanza ya Rais ni kujifunza! Utamaduni huu mbaya, umewafanya baadhi ya viongozi kutokufanya vizuri kipindi cha kwanza wakitegemea kuwa kipindi cha pili ndio itakuwa hivyo.

Guess what? Mkapa wa 1995 na Mkapa wa 2000 ni tofauti sana. Mambo aliyoyafanya kipindi cha pili yote tunayajua.
 
Back
Top Bottom