Celina Kombani akerwa na wanasiasa wanaomchafua

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
MBUNGE wa Ulanga Mashariki (CCM), Celina Kombani amewasihi viongozi wa vyama vya siasa nchini kutumia vizuri majukwaa ya siasa kwa kueleza sera zao, badala ya kutoa kashfa na maneno ya kejeli zinaweza kusababisha machafuko.

Kombani ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), alisema hayo wakati akizungumza na wazee wa Kata ya Vigoi Nawenge na Mahenge mjini wakati wa ziara yake ya kukagua na kuhimiza shughuli mbalimbali za maendeleo.

"Wapo baadhi ya wanasiasa waliwahi kuja hapa jimboni kwangu na wakakosa watu wa kuwasikiliza na kuanza kunitolea maneno ya kunikashifu bila ya kuangalia maendeleo niliyofanya, hiyo ni dalili kuwa wameshindwa siasa siwajibu ila najua walikuwa wapita njia tu," alisema Kombani.

Waziri kombani alisema wananchi wa jimbo hilo ni mashuhuda kuwa, yeye siyo mtu wa maneno mengi bali vitendo katika mipango yake mbalimbali ya kuwaletea maendeleo, kama alivyohaidi wakati wa kampeni za uchaguzi na kuwataka kutokukubali kudanganywa na viongozi wanaopita na kutumia maneno ya uongo.

CHANZO: GUMZO LA JIJI
 
Waziri kombani alisema wananchi wa jimbo hilo ni mashuhuda kuwa, yeye siyo mtu wa maneno mengi bali vitendo katika mipango yake mbalimbali ya kuwaletea maendeleo

Huyu mama ni kweli siyo Mtu wa maneno mengi sana, yeye anatoa statement fupi lakini nzito kwa mfano wa statement zake ni ile aliyoitoa kuhusiana na Katiba mpya yeye akiwa kama waziri wa sheria na katiba kipindi hicho alisema "Tanzania haihitaji katiba mpya iliyopo inajitoshereza sana"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom