CDM yaanza kukokomboa wakazi wa Bagamoyo huku uwepo wa CCM ukitatanisha.

Mlalila

Member
Nov 19, 2011
35
17
CDM wameanza kuangamiza ngome ya CCM Bagamoyo. Leo wamefanya mkutano ktk viwanja vya Majengo S/M. Mkutano umefanyika wakati mvua kubwa ikinyesha na watu wakinyeshewa na mvua ya kufa mtu huku wengine wakishindwa kufika uwanjani hapo kutokana na mvua hiyo kubwa.

Hali ya hewa iliendelea kuwa mbaya watu wakitepeta na wengine simu zikiingiwa maji wakiwa bado wamekomaa kusikiliza makamanda wakitoa hoja za ukweli!, nguvu!, na kumharibia siku kila kada wa ccm.

Wwananchi wengi wameonekana kufunguka na kutamani kupata kadi za uanachama (CDM) ambazo kulingana na hali ya hewa kuwa mbaya wengi wamerudi nyumbani wakidai kuwa mvua haijawatendea haki huku wengine wakitamani kujua lini tena makamanda watakuja kuongea nao.

Ktk hali isiyotarajiwa, Nimeshuhudia Kimbunga cha mabadiliko wilayani hapa kikiendelea kuvuta kasi
kila kukicha na baadhi ya vijiwe vya CCM vikikosa washabiki na wafuasi. Leo nikipita mtaani na bendela ya CDM kuelekea mkutanoni, vijana wa bodaboda na wachoma Chipsi waliniomba bendela ya CDM kisha wakaitundika ktk moja ya kijiwe ambacho Shukuru Kawambwa alikizinduwa kama shina la tawi takribani mita 100 toka ofisi ya rais wa wilaya.


CCM inakufa jamani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!, Hamia CHADEMA!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ccm ilishajifia muda mrefu sana, wananchi walishaichoka, ila tatizo lilikuwa ni chama gani IMARA cha kuwakombo. Sasa wamepata chama icho ambacho walikuwa wanakitafuta au kukingojea, sasa wamekipata. Ukombozi umefika... M4C.
 
mbona bagamoyo palaini sana tu kesho akienda Nape atazawazisha mambo
 
Mkuu radi ilipiga? Sisi wa enzi zile za Joseon tunaamini kama radi zilipiga basi Miungu ilikuwa inakabidhi wilaya kwa CDM na CCM hawana chao.
 
mbona bagamoyo palaini sana tu kesho akienda Nape atazawazisha mambo

Ukweli ni kwamba CCM imekosa mvuto mpaka basi. Nape akija lazima alambe vidole viwili kuanzia jimbo la Mdee mpaka kwa Kawambwa. Akichelewa kuja kubadilisha hii dhoruba ya CDM anaweza kuvulia gamba lake Bagamoyo badala ya DSM.
 
Wacheza bao wanahitaji tu fweza kidogo ya kunywa kahawa na dafu baaaaasi umemaliza. Hawa siyo watu wa kuaminika ni mamwinyi vigeugeu
 
Back
Top Bottom