GeniusBrain
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 4,315
- 306
CHADEMA leo hii wanategemea kuzindua kampeni zao za uchaguzi wa Jimbo la Arumeru katika uwanja wa shule ya Msingi Liganga ambapo viongozi wakuu na wabunge wao wote wanategemea kuhudhuria. Wakati hayo yakitegemewa kutokea leo, hali bado ni tete ndani ya chama kuhusu mustakabali wa kampeni hizo. Kwani chama hakina rasilimali za fedha na vifaa kuendeshea kampeni hizo kwa sasa kwa ajili yakukidhi matumizi ya timu ya kampeni, Helikopta, magari nk,. Na mkakati pekee ambao wanaoutegemea ni kupitisha bakuli kwa wananchi. Kwa maana hii basi , ni wazi kabisa CDM kuendesha kampeni hizi kimkanda mkanda na wadadisi wa mambo wanaliona hili litakuwa ni tatizo kubwa tofauti na wenzao wa CCM ambao wanaonyesha wazi wako vizuri kifedha, watu na kimkakati.