CDM kususa kwenu bado hakujaisha?

GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,315
306
Kinachowashangaza watanzania na wenye kuitakia mema nchi hii ( sio CDM ) ni pale ambapo CDM kususia sherehe zote za kitaifa japokuwa hupewa mualiko rasmi. Hivi hizi sherehe zote za kitaifa hazina maana kwenu ? je mngechukua nchi hii na kushika dola mngezifuta ? . Hili kwa CDM halionyeshi picha nzuri kabisa mbele ya watanzania, na wengi wameisha anza kuwadharau na kuwaona kuwa hamkuwa na nia njema na hamna nia njema na nchi zaidi ya maslahi yenu binafsi. Na nukuu maneno ya Mh. Shibuda , mbunge wa CDM Maswa wakati wa kikao cha wabunge wa CDM kilichofanyika Bagamoyo kuwa ‘…………hiki si chama cha kisiasa bali ni kundi la wahuni wachache wenye uroho wa madaraka’ mwisho wa kunukuu. Tafakari zingatia
 
Wale wanaoonyesha picha nzuri ni wepi? Ni wale wanaomwaga mamilioni ya pesa kujinafasi kwenye kila sherehe kila kukicha wakati hatuna madawa hospitalini? Ni unafiki na uvivu unaoifanya nchi maskini kama yetu kuwa na public holiday kibao. CHADEMA wanamsiba, viongozi wakuu wako huko sio muda muafaka wao kusheherekea.
 
Karibu viongozi wote wa vyama vya siasa walikuwepo na wengine walituma wawakilishi wao, kasoro CDM tu. Sherehe za kitaifa lazima zienziwe, huko ndiko kulitambulisha taifa na watu wake, na anae dharau sherehe za taifa lake basi huyo ana fikra za kitumwa. Msisingizie msiba hata mlipokuwa hamna msiba huwa mnasusa tu
 
attachment.php
 
Ni design zetnu ninyi mnaofuata ubwabwa kuziona zina maana. Kuna haja gani ya kusherekea wakati maisha ya wakati wa mkoloni wakati wa Tanganyika yanasemakana yalikuwa mazuri kuliko maisha ya Mtanzania baada ya miaka 50 ya uhuru??

Binafsi nilishaacha kusherekea sikukuu za kitaifa mpaka siku CCM itakapondoka madarakani.
 
Karibu viongozi wote wa vyama vya siasa walikuwepo na wengine walituma wawakilishi wao, kasoro CDM tu. Sherehe za kitaifa lazima zienziwe, huko ndiko kulitambulisha taifa na watu wake, na anae dharau sherehe za taifa lake basi huyo ana fikra za kitumwa. Msisingizie msiba hata mlipokuwa hamna msiba huwa mnasusa tu
Ukitoa za jana zipi zingine sherehe za kitaifa....
 
Hivi hizi sherehe unaweza kuziita kweli za kitaifa?wewe umesherhekea kivipi?umeguswa kwa namna gani kama si kufurahia kutofanya kazi?mfikirie mtanzania wa kawaida kule kijijini kama anajua hizi sikukuu zipo?hizi ni ulaji wa viongozi na kupata posho za safari na kuliingizia taifa hasara pasipo na sababu fikiria mamilioni yaliyoteketezwa kwa sherehe ya masaa isiyo na tija kwa taifa letu na raia wake ni sherehe za kukamilisha ratiba tu kwa viongozi
 
Hivi sherehe za muungano,kuwasha na kuzima mwenge zinaboresha maisha ya mtanzania kwenye sherehe hizo utasikia ahadi zilezile miaka nenda rudi hakuna kinachofanyika shame on u kwa kutumia kodi za Watanzania ovyo.
 
Asiye heshimu cha kwake ni mwenye fikraza utumwa, nisije kuku conclude kwenye group hilo !
 
CDM wamezoea kususa, hata madiwani wa Kinondoni wamesema watasusia vikao vya kupitisha bajeti ya halmashauri yao. Itabidi wapatiwe ushauri chanya, kususia kila jambo hakutasaidia kumwinua mtanzania!
 
Hivi hizi sherehe unaweza kuziita kweli za kitaifa?wewe umesherhekea kivipi?umeguswa kwa namna gani kama si kufurahia kutofanya kazi?mfikirie mtanzania wa kawaida kule kijijini kama anajua hizi sikukuu zipo?hizi ni ulaji wa viongozi na kupata posho za safari na kuliingizia taifa hasara pasipo na sababu fikiria mamilioni yaliyoteketezwa kwa sherehe ya masaa isiyo na tija kwa taifa letu na raia wake ni sherehe za kukamilisha ratiba tu kwa viongozi

Hizi sherehe zipo tangia mwasisi wa Taifa hili , ww umezaliwa juzi tu hujui lolote !
 
CDM wamezoea kususa, hata madiwani wa Kinondoni wamesema watasusia vikao vya kupitisha bajeti ya halmashauri yao. Itabidi wapatiwe ushauri chanya, kususia kila jambo hakutasaidia kumwinua mtanzania!

Madiwani wao wa kinondoni hata wakisusa hawawezi haribu kitu, kwani ile quorum ya two third CCM wanayo, watajiabisha wenyewe. Ila kwenye posho hawa jamaa wako makini hawasusi aisee, utawaona wa kwanza kwanza kwenye kupokea bahasha.
 
Haina maana hata kidogo kubeba dhambi ya kujishibisha na kujistarehesha kwa sherehe zilizogharimu mamilioni ya shilingi ilihali masikini wakikosa mlo mmoja kwa siku! Huo mwaliko ungeenda tu mwenyewe bwana Genious! Nadhani we ni masalia ya huu utawala mufilisi ambao mwisho wake hauko mbali! Yes! Km ilivyo binadamu,CCM ilizaliwa,ikakua,ikazeeka,ni juzi tu wamejivua gamba(km nyoka mzee) na soon watapotea kabisa ibaki tu historia!
 
Kinachowashangaza watanzania na wenye kuitakia mema nchi hii ( sio CDM ) ni pale ambapo CDM kususia sherehe zote za kitaifa japokuwa hupewa mualiko rasmi. Hivi hizi sherehe zote za kitaifa hazina maana kwenu ? je mngechukua nchi hii na kushika dola mngezifuta ? . Hili kwa CDM halionyeshi picha nzuri kabisa mbele ya watanzania, na wengi wameisha anza kuwadharau na kuwaona kuwa hamkuwa na nia njema na hamna nia njema na nchi zaidi ya maslahi yenu binafsi. Na nukuu maneno ya Mh. Shibuda , mbunge wa CDM Maswa wakati wa kikao cha wabunge wa CDM kilichofanyika Bagamoyo kuwa '…………hiki si chama cha kisiasa bali ni kundi la wahuni wachache wenye uroho wa madaraka' mwisho wa kunukuu. Tafakari zingatia

sema ni wewe usisemee watu au tupe minitues za kikao
 
Hawa ni viongozi wa mialiko na sherehe kuzitafuna kodi zetu.
CDM ni viongozi wa kutetea na kuzilinda rasilimali za nchi na kodi zetu kwa ajili ya maendeleo yetu sote.
.
 
Back
Top Bottom