Elections 2010 CCM Z'bar Waitega NEC:Wasisitiza Bila ya Dr. Bilal Hawatachagua CCM

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
...Wapenzi kadhaa wa Dk Bilal.... walisema kwamba wanatarajia mara hii jina la Dk Bilal litarudishwa kwa sababu alikuwa muungwana mwaka 2000 Kamati Kuu ya CCM ilipompitisha Amani Karume kuwa mgombea wa urais CCM Zanzibar wakati kura za Kamati Maalum ya CCM Zanzibar ilimpa alama kubwa Dk Bilal. Kama vile haitoshi, mwaka 2005 Bila ilibidi alitoe jina lake na kukubali kumwachia Karume aendelee kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Yusuf Khamis mwanachama wa CCM, mshabiki wa tawi la Kisonge alisema ikiwa Bilal hatopitishwa, basi mara hii hawatakwenda kupiga kura Oktoba 31.

Mkereketwa mwengine Siasa Mwinyi Rehani alisema kwamba ahadi ni deni, Bilal kasubiri kwa miaka 10, sasa ni wakati wake kwa sababu aliambiwa asubiri naye alikubali kusubiri tena kwa utulivu kwa muda wote huo.

“Bilal ndiye anayeweza kukabiliana na Maalim Seif Sharif wa CUF, ikiwa Bilal hakupitishwa basi CCM itambue kuwa kundi kubwa la wanachama wa CCM litageuka,” alisema Rehani.

Rehani alisema iwapo maoni yao yatadharauliwa ya kutoteuliwa Dk Bilal wanakusudia kufanya mambo mawili kwa pamoja ikiwa ni kuharibu kura na kuwanyima CCM na jengine ni kuanzisha chama changine kimya.

Akizungumza na wanadishi wa habari kuhusiana na hisia za wanachama na wapambe wake Dk Bilal alisema pamoja na kuwepo hisia tofauti kuhusiana na suala hilo alisema yeye ameingia katika mchakato wa kuchukua fomu akiamini na kujua taratibu zote za chama chake ikiwa pamoja na kuchaguliwa na kutokuchaguliwa na kuahidi kuheshimu maamuzi ya vikao.

“Mimi nina haki ya kugombea na pamoja na haki lakini nina wajibu kwa hivyo tunafuata taratibu zilizopo aktika chama ambazo ni kwenda kwa wapiga kura wa halmashauri kuu ya CCM na lazima tukubali mchezo pale kwa hivyo nimefuata taratibu, mwananchi ana yake, mimi ni metetezi wa mawazo ya wengine kwa hivyo nimeingia katika mchakato na kuelewa taratibu” alisisitiza Dk Bilal.

Akijibu swali aliloulizwa iwapo NEC haitolirejesha jina lake mara hii atachukua hatua gani kwa kuwa alitakiwa aondoshe jina lake katika kipindi kile na kutakiwa asubiri Rais Karume amalize kipindi chake cha miaka mitano Dk Bilal alisema haikuwa dhambi kuchukua fomu wakati huo.

Alisema baadhi ya watu alimuona kama ametenda dhambi kwa kuchukua fomu lakini yeye mwenyewe anaamini hilo halikuwa tatizo kwa kuwa ni haki ya kila mmoja na ingelikuwa ni kosa lazima angeadhibiwa katika chama chake.

“Kila mmoja ana mawazo tafauti lakini kama ni dhambi ningeadhibiwa na ninachojua niliondosha jina langu kwa maadhishi na sijaahidiwa kitu kwa hivyo ….hiyo ya kuwa nimeahidiwa mara hii no no no hilo halikuwa hivyo chama chaetu kina taratibu” alisitiza hilo mbele ya waandishi wa habari.

Alisema iwapo akipata ridhaa ya wananchi ya kuingia madarakani katika uchaguzi wa mwaka huu wazanzibari wategemee mabadiliko makubwa ya kimaendeleo kuliko yalivyo hivi sasa.


source:zanzibar yetu web blog (msisitizo na editing ni wangu)


Baadhi ya wazee wa Zanzibar ambao wamepata kushika nyadhifa serikalini, Abdul Razak Mussa (Kwacha), Hamidi Amiri Ally na Ibrahim Aman Ibrahimu, walisema kwa nyakati tofauti kuwa ndiyo waliomtuma Dk. Bilal kuchukua fomu kwani safari hii, ndiyo chaguo lao.

Wazee hao walitaka viongozi wa juu wa CCM, kusikiliza matakwa na si kufanya maamuzi yao kama walivyozoea katika miaka mingine ya kipindi cha kumtafuta mgombea urais kwa tiketi hiyo.

“Vikao vya NEC vinatakiwa kujua kwamba mchujo wa kwanza tunao sisi wazee wa mkoa huu na si vinginevyo,” alisema Abdurazak Musa Simai maarufu kwa jina la Mzee Kwacha.

Mzee Kwacha ambaye aliwahi kushika nyadhifa tofauti za juu katika kipindi cha rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, alisema kwa kuwa walishawahi kumpigia kura mara mbili na kushinda katika nafasi hiyo, wanaviomba vikao vya juu vya CCM, safari hii vimpitishe kwani hawataki kuongozwa na mtu mwingine.

“Sijatumwa kuzungumza maneno haya na mtu yeyote…hii ni mara yangu ya kwanza kuzungumza maneno haya, hata nikiwa katika shughuli za chama na serikali…nasema Dk. Bilal sasa apewe nafasi ya kuongoza kwani wananchi ndiyo waliomchangia fedha za fomu,” alisema Mzee Kwacha.
source:Tanzania Daima (save editing)
 
Eee Mungu jaalia NEC ifanye mizengwe ile ile ya mwaka 2000 na 2005, natamani kuiona CCM baada ya kuzikwa Pemba, ikisomewa matanga Unguja, Amin
 
maneno haya wala hayana Ubishi... Bilal ndiye pekee chaguo la Wazanzibar na hakika akijiunga Upinzani CCM wamekwisha!
 
Mimi natamani wasimpitishe bila shaka yale yaliyotokea Bumbwini mwaka 1995(angry votes) yatatokea tena katika majimbo yote.
 
Sasa huyo Bilal kama anajiona ana uwezo na anakubalika kwanini aendelee kung'ang'ania kugombea kupitia kwene chama chenye mizengwe ambayo yeye mwenyewe anajua masaibu yake?

Akwende zake huko.
 
Zanzibar ya leo inahitaji kiongozi atakaye waunganisha wazanzibari wote; na si kiongozi wa mlengo wa kulipa visasi; na kiongozi kwa faida ya kina mzee Kwacha. Wazee acheni kuladhimisha mambo hapo kila mgombea katumwa na watu wake, hivyo tusubiri maamuzi ya wana ccm Zanzibar kumtoa kidedea.
 
"Bilal ndiye anayeweza kukabiliana na Maalim Seif Sharif wa CUF, ikiwa Bilal hakupitishwa basi CCM itambue kuwa kundi kubwa la wanachama wa CCM litageuka," alisema Rehani.

Nimesoma hii criteria ya kuchagua rais nikachoka. Hatuongelei nani anaweza kusukuma maendeleo ya wananchi mbele, hasha.Tunaongelea nani anaweza kukabiliana ma Maalim Seif.

Halafu unaweza kushangaa kwa nini hatuendelei kweli?
 
Kuna makala niliisoma katika gazeti litokalo kila wiki kati ya Mwanahalisi au Raia Mwema kuwa kuna mpango CCM kumpa Urais wa Zanzibar Dk. Shein, na kama hili ni kweli mi naomba litokee ili CCM ipotee kabisa Visiwani. Dk. Bilal ndo chaguo la wana CCM wengi ZNZ so huku bara wakimtosa kifuatacho ni....................................................
 
Dk Bilal sio chaguo la wazanzibari bali ni chaguo la wazanzibari wenye kupenda siasa za chuki zanzibar achaguliwe tu muone kama zanzibar CCM watashinda kwani watu wamechoka na ubaguzi unaoendelea zanzibar!!!!
 
shein atapitishwa na kupambana na maalim seif! hapo kama kweli bilal atamwaga mboga nitamwelewaaaaa...
 
Ngoja nikusaidie kuhariri kichwa cha habari:

Baadhi ya Wapambe wa Dr. Bilal wako tayari kupokea ushindi tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom