CCM Zanzibar, Lao nini Khasa?

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Walipokuwa Butiama walishikana mashati na kutoleana kauli chafuchafu. Kwenye kikao cha Bunge cha Juni 2009, mashati yakaendelea kushikana na mikakati ya usuluhishi ikafanywa. Kwenye baraza la Wawakilishi usisikie, ni vurugu bin balaa, kilio kuhusu Mafuta, Muungano na mengine yasiyoeleweka.

Walipokuwa wakigombea 2000, nusura wachaniane mashati, ikabidi wakalishwe kitako ati Chimwaga au sijui ni Kizota.

Je CCM Zanzibar lao ni nini? Wanalilia nini huku wako madarakani? ni nani hao wasiofungamana na kuelewana ndani ya CCM Zanzibar?
 
Wataka kupanga mikakati ya ajabu hata kuona kuwa Zanzibar inatakuwa na uchaguzi usio wa huru na haki, ni ajabu sana kuona wanapanga mbinu za kishetani za ajabu na kutisha watu kama hivi..!!
 
Wataka kupanga mikakati ya ajabu hata kuona kuwa Zanzibar inatakuwa na uchaguzi usio wa huru na haki, ni ajabu sana kuona wanapanga mbinu za kishetani za ajabu na kutisha watu kama hivi..!!

Josh Michael,

CCM Zanzibar kutaka kuchukua ushindi wa jumla hilo si ninalotafuta, bali ni mgonganoo ndani ya CCM Zanzibar na mgongano kati yao na wenzao wa Bara (CCM Muungano).
 
Hamna kitu ,hawa wajamaa wanaelewana vizuri sana tu,ila mikakati yao ya kuelewana ni kuonyesha picha kama hawaelewani machoni mwa Watanzania waliolala.
Hali hiyo inasababisha kujenga tamaa miongoni mwa watu na kuonekana hiki kitavunjika na kile kitapatikana.

Kwa zaidi ninavyowaelewa wanapanga mipango ya kuwababaisha wananchi na pia kupanga mipango ya kuihadaa dunia ,ila wanasahau kuwa dunia ya leo kuna wanaowaelewa na mbinu wanazotumia za kutoleana mijicho ni za kinafiki.

Unaweza kuwa ndani ya majambazi na kushirikiana nao kila kitu wakati wewe si jambazi na ikitokea kukamatwa wewe unaachiliwa kivyakovyako ,jamaa wa usalama wananielewa nazungumza kitu gani.

Kuliona wanalocheza nalo CCM ,angalia ushirikiano wao katika ufisadi na kauli zao, utawasikia wanalishughulikia na wengine watafikishwa mahakamani ,wakati siku zinaongezeka na hakuna la maana linaloonekana.

Mikwaruzano unayoiona iweke katika kundi la propaganda ,hapo utaielewa vizuri sana ni usanii ambao inabidi tushikane mashati na kutoana nishai ,lakini letu moja tunaelewa tunachokifanya ,ila wale wasiotuelewa wanaona kuna tatizo kubwa sana.
 
Back
Top Bottom