Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 3,832
- 2,790
Turudi kwenye hadithi ya nyoka kujichuma ngozi yake, hapa inafanana kwa ujumla chama kilikuwa kimechafuka sana kwa uchafu mbali mbali sasa ni wakati muafaka kimeamua kijichuma magamba yake kirudi kuwa kipya. Tuunge mkono, hotuba ya Mwalimu sikumbuki mwaka gani lakini aliitoa enzi za Mwinyi alisema tuhuma tu zinatosha kukufuzisha kazi maana kwanini utuhumiwe? Anasema "Huko Uingereza kuna waziri mmoja alituhumiwa kutembea na malaya wa barabarani, waziri yule akatakiwa ajieleze naye akaona bora aandike barua ya kujiuzulu waziri mkuu alisaini kuidhinisha kujiuzulu kwake" mwisho wa kunukuu. Kwa hiyo na sisi ukizingatia nchi yetu ni changa sana kidemokrasia inabidi tu-rely on this kwa sababu kama wewe ni kiongozi wa serikali na umeapa kuwa muadilifu kwanini utuhumiwe?