CCM yatoa tamko juu ya mauaji ya Daudi Mwangosi

Iringa
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Itakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu Ndg. Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa *askari watatu wa kuzuia fujo.

Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao. CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine.*

Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi.*

Pamoja na wito wetu wa kuchunguzwa suala hili kwa umakini na weledi mkubwa, pia tunatoa rai kwamba uchunguzi huu ufanyike kwa kutumia muda mfupi ili ukweli uweze kubainika mapema na hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Vilevile CCM inasikitishwa sana na mfululizo wa matukio ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mikutano na operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na CHADEMA nchini hasa zile zilizofanyika kwa kukaidi amri halali za vyombo vya ulinzi na usalama. *

Kutaja matukio baadhi tu ni pamoja na lile la kuuwawa kwa kada wa CCM Mkoani Singida, kuuawa kwa Ndg. Ally Hassan mjini Morogoro, kuuawa kwa Ndg. Daudi Mwangosi Mjini Iringa hivi majuzi,kujeruhiwa kwa askari polisi Iringa na matukio mengine mengi ambayo yametokea wakati wenzetu wa CHADEMA wakiendesha operesheni zao mbalimbali nchini.

Matukio haya si mazuri kutokea kwenye shughuli za Chama cha siasa. Kwakweli ni aibu, inayohitaji uwajibikaji,hata kama ni wa kisiasa. Inapotokea shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri wa aina yake.

Inakuwa mbaya zaidi pale vifo hivi vinaposababishwa na Chama hicho kutotii amri halali zilizotolewa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi inayovipa pia uhalali *vyama vya siasa kuwepo na kuendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria.*

Laiti Chama hicho kingesubiri siku chache zilizobakia kabla ya Sensa kuisha kabla ya kuendelea na mikutano yake ni dhahiri mauaji haya yasingetokea. Lakini kauli za kukebehi na uamuzi wa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi na kusema "tupo tayari kwa lolote" ni ishara kwamba Chama hiki kiliandaa na kujiandaa na fujo zilizotokea.

Tunatoa wito kwa vyama vya siasa na wanasiasa kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria. Amani na utulivu vulivyopo nchini ni kazi nzuri iliyojengwa kwa muda mrefu na waasisi wetu kwa kujenga utamaduni wa kuzingatia utawala wa sheria.

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.

Napitia sehemu chache ya Hii taarifa na kutoa maoni yangu (kwa baadhi ya Mistari niliyoinenepesha na kuipaka rangi nyekundu)

1. Inaskitisha kama mwangosi alikuwa ni ndugu yenu na mkaruhusu mazingira yanayoashiria kuuwawa na vyombo vya usalama

2. nchimbi alishasema siku 30 wewe mda mfupi unaousema ni upi? wewe na kaka yako nchimbi nanai zaidi?

3. Hatua zinazostahili zichukuliwe kwa haraka... hapa sijakuelewa.. Nape unatoa hilo tamko ukiwa unamuagiza nani? na Unaongea kama nani?

4. Inapotokea shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri wa aina yake.

Waliosababisha vifo ni chama au Polisi? Hivi huu uwajibikaji unautaka ufanywe na vyama vya siasa ILA SIO VIONGOZI WA SERIKALI YA CHAMA CHAKO? Yalipolipuka mabomu Mbagala Husein Mwinyi alijiuzulu? meli Mbili zimezama nanai alijiuzulu? Sasa hapa nani anaroho ngumu? Ni vyama vya siasa au Viongozi wa Serikali?

Kama Nape Haufanyi makusudi Utakuwa ni Mgonjwa wa akili.
 
hakuna propaganda yeyote itakayowasaidia ccm katika hili la mwangosi...maji yameshamwagika...
 
Kinyaa gani hiki? Hivi CCM ni viumbe gani, hawa si wanadamu.

Haiwezekani hawa ni binadamu kama sisi. Hapa JF itatubidi tuweke jukwaa la viumbe fulani.......Ila hawa kina jamaa sio wanadamu 100%, so waundieni jukwaa lao mle na wajimwage kwa mambo yao ya kishetani....huku wanatuchefua kweli!
 
Nape Nnauye,
Huhitaji kuwa japo na certificate ya Nursery School kujua kuwa mauaji yanafanywa na polisi kwa vile ni wababe, Wana silaha, wana itikadi ya chama cha mapinduzi, wana chama kinachowatuma ili kufifisha kampeni za kumkomboa Mtanzania nk.

Lakini ndugu yangu mpendwa, usidhani kumwagia maji tofali la saruji ni kulidhoofisha. Mambo mnayoyafanya CCM yanatupeleka kubaya. Hebu acheni utawala wa kiimla.
 
Maelezo ya Naue yanatia hasira kwa vile yanajaribu kuficha ukweli. Polisi wanafanya kazi chini ya maelekezo ya serikali ya CCM. Kazi waliyoifanya huko Morogoro na Iringa ni mbaya sana hata kwa mtoto mdogo ni dhahiri. Mbona hakuna tamko la serikali kukemea haya matukio? Nape ni nani kwenye serikali au hao polisi ni wana mgambo CCM?

Kama ni wa CCM, jeshi la polisi la serikali ya Tanzania liko wapi? Halafu anazuga tu hajakemea hao polisi. Picha zote zianaonyesha polisi wakiwa na silaha wakati wananchi hawahashika silaha yoyote hata jiwe au fimbo ndogo!!!!!! Sasa wanaambiwaje kuwa ndio wahusika wa hivyo vifo?
 
Nape alini block facebook baada ya kumuuliza swali gumu, mweupe kabisa kichwani.
 
Kwanza Nape ndio mtabiri wa hizi vurugu, lazima ana husika!
 
Iringa
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Itakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu Ndg. Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa *askari watatu wa kuzuia fujo.

Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao. CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine.*

Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi.*

Pamoja na wito wetu wa kuchunguzwa suala hili kwa umakini na weledi mkubwa, pia tunatoa rai kwamba uchunguzi huu ufanyike kwa kutumia muda mfupi ili ukweli uweze kubainika mapema na hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Vilevile CCM inasikitishwa sana na mfululizo wa matukio ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mikutano na operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na CHADEMA nchini hasa zile zilizofanyika kwa kukaidi amri halali za vyombo vya ulinzi na usalama. *

Kutaja matukio baadhi tu ni pamoja na lile la kuuwawa kwa kada wa CCM Mkoani Singida, kuuawa kwa Ndg. Ally Hassan mjini Morogoro, kuuawa kwa Ndg. Daudi Mwangosi Mjini Iringa hivi majuzi,kujeruhiwa kwa askari polisi Iringa na matukio mengine mengi ambayo yametokea wakati wenzetu wa CHADEMA wakiendesha operesheni zao mbalimbali nchini.

Matukio haya si mazuri kutokea kwenye shughuli za Chama cha siasa. *********Kwakweli ni aibu, inayohitaji uwajibikaji,hata kama ni wa kisiasa. Inapotokea shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri wa aina yake.***************

Inakuwa mbaya zaidi pale vifo hivi vinaposababishwa na Chama hicho kutotii amri halali zilizotolewa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi inayovipa pia uhalali *vyama vya siasa kuwepo na kuendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria.*

Laiti Chama hicho kingesubiri siku chache zilizobakia kabla ya Sensa kuisha kabla ya kuendelea na mikutano yake ni dhahiri mauaji haya yasingetokea. Lakini kauli za kukebehi na uamuzi wa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi na kusema "tupo tayari kwa lolote" ni ishara kwamba Chama hiki kiliandaa na kujiandaa na fujo zilizotokea.

Tunatoa wito kwa vyama vya siasa na wanasiasa kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria. Amani na utulivu vulivyopo nchini ni kazi nzuri iliyojengwa kwa muda mrefu na waasisi wetu kwa kujenga utamaduni wa kuzingatia utawala wa sheria.

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.

## ANGALIA *********
 
NAPE NNAUYE alikuwa wapi wakati wajumbe wake walipokuwa Wanatoleana PISTOL ? Mbona hatukusikia kauli zake? Na pia

hakukuwa na POLISI Sasa Mbona yeye NAPE hakuwajibika ? ILA Hao WOTE NI MARAFIKI ZAKE WAPENZI aliwatembelea kimya

kimya na kuwaambia MAGAZETI Wasiseme CHOCHOTE; na WAANDISHI WOTE WAKANYAMAZA... SASA Kwanini Anataka Dr.

SLAA sasa AJIUZULU SUALA la WATU KUFARIKI KWENYE MELI HAKUSEMA CHOCHOTE; WAZIRI WA ZANZIBAR

ALIJIUZULU wa BARA HATA KIDOGO? HUU SI UNAFIKI?
 
Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao. CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine.*

Hili zuzu ndiyo linaibuka leo (baada ya siku 3 nzima) na masikitiko/pole feki!?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nape wakati mwingine sio lazima kila kitu utoe kauli, jaribu kujifunza kuwa kimya baadhi ya vipindi. Hukuwa na sababu kusema chochote kwenye hili suala la Daudi, nadhani ingesaidia zaidi.
 
Hii statement ya Nape Nnauye inatia hasira sana. Inaonesha ni jinsi gani CCM anavyodharau watanzania. Na mbaya zaidi ni pale madharau haya yanatolewa na mwanasiasa kijana!

Nape Nnauye na wenzake waliokaa chini kuandaa hii statement pengine sasa wako majumbani mwao, jioni walikaa mezani na watoto wao wakala chakula cha jioni na sasa wamelala usingizi mnono. Kesho wataamka na kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

Lakini kwa watoto wa Daudi Mwangosi, life will never be the same, kiti cha baba yao kitabaki wazi forever. Na wanajua baba yao alikufa kifo cha kinyama mikononi mwa polisi! Polisi ambao wanajukumu la kulinda usalama wa raia including baba yao.

Nape ametoa hii statement akijua fika hakuna hata polisi mmoja aliyekuwepo kwenye tukio lililochukua uhai wa Daudi Mwangosi amehojiwa! Hata kama ni kutafuta mtaji wa kisiasa, kuna limit. Nguvu kubwa sana imetumiwa na CCM kugeuza haya mauaji ya Daudi Mwangosi kuwa mtaji wa kisiasa!

CCM ndiyo yenye dola, ina intelleginsia ya kubaini fujo days kama ya tukio, sasa ilikuwaje Iringa? Hivi ni kweli Nape na CCM wanathamini uhai wa watanzania? Morogoro, Songea, Arusha, Nyamongo (tena maiti zilitupwa barabarani) Nape alikuwa wapi?

Jambo moja li wazi, huu msiba umeonesha jinsi CCM ilivyo nyuma. Watanzania wamepiga hatua lakini bado CCM wanafikiri as if ni mwaka 47. Wakubwa hawa wanaweza kulaumu 'vyama vya siasa' lakini CCM imeuliwa na CCM yenyewe.
 
Nape juu ya hili hamuepuki lawama.
Ccm mmeshindwa siasa za jukwaani mmeamua kutumia mtutu wa bunduki.
Watanzania wamegundua kuwa ccm ni wauaji na wabakaji wa demokrasia.
Kila jambo linalofanywa na ccm linazidi kuimaliza ccm.
Nafurahi sana kina baba, mama, bibi,babu, vijana mpaka watoto wamegundua ccm ndiyo wauaji.
Kuitetea ccm inahitaji uwe na akili ya maiti.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Nape-Nnauye.jpg

CCM imevitaka vyombo na tume zilizoundwa kuhusiana na kifo cha mwandishi wa habari Daudi Mwangosi, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini kila kitu ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira yaliyosabaisha kipigo

hadi kufa mwandishi huyo.
Aidha imetaka uchunguzi usichukue muda mrefu ili ukwelikuhusiana na kadhia hiyo ujulikane mapema na hatua zichukuliwe kwa kila atakayebainika kuwa sababu au chanzo cha vurugu na kifo cha mwandishi huyo.

Aidha imesema imepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari watatu wa Polisi wakati wa vurugu hizo na kimetoa pole kwa wafiwa, wanahabari wote nchini na wote walioguswa na msiba huo kwa namna moja au nyingine.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye katika taarifa ya CCM kwa vyombo vya habari, leo jijini hapa, kuhusiana na sakata la vurugu hadi kifo cha mwandishi huyo, juzi mkoani Iringa.
 
Back
Top Bottom