Elections 2010 CCM YATAMBUA NGUVU YA Dr. SLAA

mozze

Senior Member
Aug 27, 2010
185
28
....... Dk. Chegeni alisema, “Sisi tuna mtaji mkubwa, hao wasiolalamika hawana mtaji…hatuwezi kuacha ikawa taarifa ya (anataja gazeti) na Synovate. Hapa inagusa vyama na sisi tuna maslahi. Sisi hatumwogopi mtu. CCM inakubalika.”

Waandishi wa habari walipohoji ni jinsi gani chama hicho tawala kinajiridhisha kwamba Synovate haijawahi na wala haina takwimu hizo kama zilivyochapishwa, Dk. Chegeni alisema wao wanaamini kutokana na kukanusha hadharani

Alisema taarifa hizo zinataka kuwafanya wananchi waamini kwamba mgombea wa Chadema ni bora ili baada ya uchaguzi CCM ikishinda, wananchi walalamike kwamba hapakuwapo uchaguzi huru na wa haki.
source: HabariLeo | CCM yatishia kulishitaki gazeti

Sasa CCM kama ina Mtaji mkubwa nini kinawafanya waanze kuhaha! CCM wanatumia vyombo vyote vya Habari kupiga propaganda, kasoro magazeti Manne tu Mwananchi, Tanzania Daima, Raia Mwema na MsemaKweli! Je ni nani alitakiwa kulalamika?
KWELI CCM WAMEANZA KUNUSA DHAHAMA!
 
Ccm wanampango wakulazimisha ushindi nini? Mbona wanaogopa picha kamili ya tz ya leo?
 
Wandugu siku zote mfa maji haishi kutapatapa ili mladi aonekane alijaribu kujiokoa,Chadema Juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Msiwadharau CCM wanaonesha kana kwamba wanarudi nyuma mjue wanajipanga kwa one and last blast.
Cha msingi wanapoondoa hatua tunapaswa kuicover on the spot.
Kwa nini vyama vya upinzani havina mbinu za kiintelejensia?
Kwa nini wanangojea responce ya CCM all the way?

Tubadilike tuwe na ubunifu na sio kuakisi.
Wao (ccm) wanapowaza kuharibu wakute tumeimarisha kuta zetu.
mamluki woote wa ccm wafichuliwe na kurudishwa makwao salama.
Elimu izidi kutolewa kwa umma kuhusu demokrasia, uhuru, na wajibu
Tuwe mfano wa kwanza ktk kutenda yale tunayohubiri
Tuwe makini na kila hatua inayopigwa kwa kuweka maslahi ya Taifa (siyo ya Chama) mbele.
Nina mengi.......
 
msiwadharau ccm wanaonesha kana kwamba wanarudi nyuma mjue wanajipanga kwa one and last blast.
Cha msingi wanapoondoa hatua tunapaswa kuicover on the spot.
Kwa nini vyama vya upinzani havina mbinu za kiintelejensia?
Kwa nini wanangojea responce ya ccm all the way?

Tubadilike tuwe na ubunifu na sio kuakisi.
Wao (ccm) wanapowaza kuharibu wakute tumeimarisha kuta zetu.
Mamluki woote wa ccm wafichuliwe na kurudishwa makwao salama.
Elimu izidi kutolewa kwa umma kuhusu demokrasia, uhuru, na wajibu
tuwe mfano wa kwanza ktk kutenda yale tunayohubiri
tuwe makini na kila hatua inayopigwa kwa kuweka maslahi ya taifa (siyo ya chama) mbele.
Nina mengi.......

umesahau suala la kuichangia chadema kupitia namba za simu na akaunti za benki ili iweze kuendeleza kazi ya ukombozi wa tanzania kutka mikononi mwa mafisadi.
 
....... Dk. Chegeni alisema, “sisi tuna mtaji mkubwa, hao wasiolalamika hawana mtaji…hatuwezi kuacha ikawa taarifa ya (anataja gazeti) na synovate. Hapa inagusa vyama na sisi tuna maslahi. Sisi hatumwogopi mtu. Ccm inakubalika.”

waandishi wa habari walipohoji ni jinsi gani chama hicho tawala kinajiridhisha kwamba synovate haijawahi na wala haina takwimu hizo kama zilivyochapishwa, dk. Chegeni alisema wao wanaamini kutokana na kukanusha hadharani

alisema taarifa hizo zinataka kuwafanya wananchi waamini kwamba mgombea wa chadema ni bora ili baada ya uchaguzi ccm ikishinda, wananchi walalamike kwamba hapakuwapo uchaguzi huru na wa haki.
Source: habarileo | ccm yatishia kulishitaki gazeti

sasa ccm kama ina mtaji mkubwa nini kinawafanya waanze kuhaha! Ccm wanatumia vyombo vyote vya habari kupiga propaganda, kasoro magazeti manne tu mwananchi, tanzania daima, raia mwema na msemakweli! Je ni nani alitakiwa kulalamika?
Kweli ccm wameanza kunusa dhahama!

taarifa zilizopatikana hivi sasa zinazoonyesha kwamba dr chegeni kidogo kidogo anakabidhiwa majukumu ya ndg abrahaman kinana katika timu ya kampeni ya ccm kama matayarisho dhidi ya mabomu dr slaa anayotarajiwa kuyafyatua ukingoni mwa kampeni hizi.

hii inatokana na kuthibitika kwa taarifa kuwa kinana anahusika moja kwa moja na meno ya tembo yaliyokamatwa katika meli yake nje ya nchi; na mahusiano aliyonayao na wasomali wa kundi la al shabab, hususan baada ya mmoja wa magaidi waliohusika na milipuko ya kamapala kukamatwa mjini arusha ambako ndio makazi rasmi ya kinana.

hivyo ccm imeona kuwa ipo haja katika hatua hii, kuanza kumweka pembeni kidogo kidogo ili asizidi kuchafua kampeni za chama hicho kuelekea ukingoni.

god job wana jf, tuendele kuchapa kazi bila kuchoka!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Vyama vya upinzani na hasa Chadema tunao uwezo wa kuwaibia kura ccm ktk uchaguzi huu japo hatutafanya hivyo kwa sababu ya kufungwa na ustaarabu tuliojiwekea.
USHINDI WA KUUNDA SERIKALI IJAYO KWA CHADEMA HAUNA TASHWISHI KWANI NI DHAHIRI!!
 
Angalizo: Chadema waangalie wasilale watauwawa. Hii inaweza ikawa strategy ya CCM kubadilisha mwelekeo wa mambo baada ya wao kuridhika wameshashinda.
 
Hivi ukishindwa CCM hata kama hufai lazima upewe wadhifa? Naona kamati ya fanikisha JK ashinde kwa kishindo imejaa walioshindwa kwenye primaries. Mfano Chegeni, si alishindwa Busega huyu? Sasa ndo mjumbe wa kamati ya usemaji wa kampeni za Jk
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom