CCM yataka Uamsho Zanzibar ifutwe; Yataka Waziri wa Sheria ajiuzulu

Mi nina wasiwasi na serikali yetu..

Hata mimi naanza kuitilia mashaka. Hivi CCM walikubalije kuungana na CUF bila kujua "major differences" walizonazo? Je katika makubaliano yao waliweka wazi msimamo wa kila chama kwenye hili swala la Muungano, au kuna watu walifanya usanii wakadanganya wenzao? Nashangaa; mbona wanaonekana kutofautiana sana kwenye hii issue? Upande wa uongozi wa juu CCM/serikali ndio imepata kigugumizi kabisa ilihali wao ndio chama tawala. Naanza kupata wasiwasi labda CCM iliwaahidi Wazanzibari watauvunja muungano (ili makubaliano yao na CUF na uchaguzi upite salama) sasa wanaanza kuwaruka. Hivi CUF inamsimamo gani kwenye hizi lawama anazopewa waziri wa sheria?
 
Hilo la kufuta UAMSHO ni ndoto za CCM ambazo tafsiri yake ni kukaribisha mgogoro mwengine usioweza kusuluhishika.

Vuai kaona tonge hio inamtoka ndio maana anajikaza kisabuni.

Katiak Uislam huwezi kutenganisha Dini na Siasa kwa7bu siasa ni kajisehemu kadogo ktk Dini ya kiislam ambayo ni mfumo kamili wa maisha wa mwanadamu.

Sasa wewe unaposema nisichanganye Dini na Siasa naona unataka kuniambia nifuate uislam wangu nusu na robo na robo nyengine niiyachie ambayo ndio hiyo siasa, hilo alikubaliki hata kidogo, mwache huyo Vuai na ujinga wake maana hata huo Uislam wake haujui, ndio maana hajui maana ya Dini (Uislam) wala hiyo maana ya siasa yupo yupo tuu !!!!!
 
Kulazimisha waziri ajiuzuru inatokana na waziri huyo kushindwa kuifanya kazi alokabidhiwa kama alivyoeleza waziri, haina maana ndio suluhisho isipokuwa ndio mfumo wa utawala bora (Zero tolerance) ktk uwajibishaji wa viongozi wetu. Kama alivyotakiwa waziri mkuu Pinda kujiuzuru aliposhindwa kuwawajibisha mawaziri walioshindwa kazi zao ama kujiuzuru kwa mawaziri walishindwa kutekeleza wajibu na rais alifikia kubadilisha baraza la mawaziri ingawa yote haya hayakuwa suluhu ya matatizo yaliyopo.

Unaanza na Uwajibikaji ktk kurekebisha mamlaka kisha anatafutwa kiongozi anayeweza kusimamia kero na matatizo yaliyopo hasa kuhakikisha jumuiya na asasi za kidini haziwezi kutengeneza fitna ya kijamii kwa kutumia misikiti au makanisa wakati huo huo serikali nzima ikitafuta suluhisho. Kero hazitakwisha ndio mfumo wa maisha ya binadamu na hata hao Marekani wana kero ktk nyanja zote za maisha na ndio hapo umuhimu wa elimu inapochukua nafasi kubwa.

Lakini muhimu zaidi ni mtazamo wa kiongozi wetu Mzanzibar na Muislaam ktk swala zima la madsai ambayo binafsi yangu nina hakika majibu yapo palepale nyumbani haikuwa na haja wala sababu ya kumtafuta mchawi toka bara kufikia kuchoma moto makanisa kisha wakane hawakuhusika lakini wakati huo huo wanajisifu kwa msimamo wao na waliyoyafanya nyuma ya pazia la dini.

Hata huyo Allah hutazama na kuyawezesha yaliyo mema hata kama hufanywa na kafir na Sheitan humshawishi hata muumini kutenda yasiyo mema. Hakuna binadamu aliyehai alopigwa mhuri wa utakatifu kwetu sote tupo ktk mtihani mkubwa wa kiimani kwa yale tunayoyafanya kila siku ya uhai wetu. Hivyo kwanza ni makosa makubwa sana kwa kiongozi wa serikali au muumini kuweka dhana na watu waliofanya kitendo kibaya cha kuchoma moto kuwa sii Waislaam au wanazuo wa UAMSHO kwa visingizio vya Usalama wa Taifa wakati hakuna ushahidi lakini zipo sababu nyingi sana zinazopelekea makanisa kuchoimwa na waumini wenye chuki wakiitwa ati wenye siasa kali.

Tume ya katiba, Hakuna mtu anayechukua njia za mkato isipokuwa hawa walalahoi wanaoukataa Muungano ndio wenye kutafuta njia za mkato. hata Bara leo tukianzisha Kongamano utawaona watu wenye hasira na yaliyotokea Zanzibar, wana hasira na matusi mazito yanayoletwa na wahuni ambao hawakushiriki wala kuyaunga mkono Mapinduzi ya visiwa vya Zanzibar. Nimeziona video nyingi sana acha hii moja au mbili za majuzi, na watazame watu wenyewe wakijiita Ustadhi utajua kwamba ni NJAA tu ndio inawasumbua wala sii Muungano japokuwa wanapenda sana kutumia Uzanzibar kana kwamba sisi Bara hatuna Uraia.

Hawa watu hawawezi kukwambia hata jambo MOJA ambalo linawakandamiza Wazanzibar ktk UHURU, HAKI na USAWA dhidi ya WABARA isipokuwa umaskini ulokiuka kutokana na uongozi mbaya wa CCM na sasa hivi CUF. Wasomi wao wengi wamekwazwa tu na muundo wa Muungano kuwepo kwa serikali mbili chini ya kuunda Moja, jambo ambalo linatushinda hata sisi waislaam kuelewa Utatu mtakatifu, lakini bila kufahamu kwamba ya kwamba mfumo huo ndio ulolinda kuwepo kwa Zanzibar hadi leo. Tukiunda nchi mbili, serikali mbili chini ya moja ya Kitaifa amini maneno yangu Zanzibar kama nchi na jina lake ndio litakufa kweli na kabla ya kufa Wazanzibar watataka tena kujitenga kabisa ikiwa swala ni kuvunja muungano. Na ikumbukwe tu historia ya nchi hiyo kuuvunja muungano ni jambo ambalo HALIKUBALIKI. Mtoto hawezi vunja ndoa ya baba na mama kwa mapenzi yake hata siku moja na hata ikija vunjika basi ni maamuzi ya baraza la Mapinduzi.

Ila inawezekana kabisa ndani ya mgogoro huu tukalipata suluhisho na binafsi yangu ningewaomba viongozi wetu wa bara na Zanzibar kuja hapa Canada wajifunze kutokana na muungano wa nchi hii maana unafanana sana na Tanzania ambako sehemu kubwa ya nchi hii ni Waingereza na sehemu ndogo ya Quebec ni Wafaransa na wamekuwa na kero kwa muda mrefu lakini sasa wamefikia suluhisho japokuwa bado Waquebec wanataka kujitenga kutokana na kuwa chini ya Milki ya Malkia maana wao na Malkia wana na historia ndefu ya uadui. Sisi hatujawahi kuwa na uadui huo na ppengine ni mdugu zaidi ya muungano wenyewe kwa sababu historia ya nchi hii inajieleza wazi kwambza hata hiyo Zanzibar inayodaiwa sio Zanzibar nzima, kesho wanaweza dai mikoa yote ya pwani including Malindi, Lamu na Mombasa kuwa sehemu ya nchi hiyo. Hivyo kukubali kuvunja muungano ni mwanzo wa kujenga matatizo mengine ambayo yatatokana na historia ya dini na utawala wa Sultan.

Huwezi kufananisha muungano huo na huu feki hata kama unaona kwako wewe uko sawa lakini kwa wataalam kam J. Ulimwengu huu si muungano ila ni muumizano. Muungano ulikuwa mwisho ni 1974 lakini Nyerere (LTLLAH) alipoona Karume anataka nchi yake alimmaliza kwa kumuua kwa risasi na mwaka 1977 alinza kuhodhi kila kitu cha Z'bar. Napia Aboud Jumbe alipojaribu kujitutumua kutaka kujitoa ktk muungano alivuliwa uanachama na kumvua uraisi na kumfunga kifungo cha ndani mpaka amezeeka, alafu unasema muungano huu ni sawa na wa Canada hapo umepotea kaka tafuta ukweli usiropokwe tuu uliza kwanza kwa wataalamu.

Wazanziabri wanataka nchi yao msijitie visababu vya kipuuzi puuzi.

Kwakero zilomo haziwezi kusulihishwa kutokana na wingi wake ukaidi wa Watanganyika kujifanya mabwana wakubwa dhidi ya Wazanzibari, kwa hio kwa hapa tulipofika hakuna mjadala isipokuwa kura ya maoni iitishwe kwa Wazanzibari eidha kuukubali au kuukataa huu muungano, wacheni kunga'nga'nia Zanzibar kwa kisingizio cha cjui usalama, undugu, uasili na mambo mengine yasiyo na mantiki yyte.
Kama ni undugu nadhani pia tumo wengine asili yetu ni Mombasa Kenya, Somalia, Msumbiji Oman, Yemen, Iran, India< China, Comoro etc lakini hatujaungana nchi hizo, na hao wenye asili ya Tanganyika tunao hapa Zenji na waomba mungu uvunjike muungano wawe huru huku Zenji kwani huku ni kwao kama watu wengine.
 
CCM Wanafiki wakubwa, hakuna Waziri kujiuzulu maana hakuna utamaduni huo Zanzibar.
Mbona waziri wa uchukuzi hakujiuzulu wakati meli ya SPICE ISLANDER ilivyozama na kuua watu?
 
Haya ndio majibu yanayotakiwa kutoka kwa kiongozi Mzanzibar ambaye ni mjumbe wa baraza la Mapinduzi, na sii kuendelea kutukashifu kana kwamba sisi Wabara hatumtegemei Allah ktk matatizo yetu. Kusema kweli serikali lazima iwe makini sana na haya makundi ya hizi jumuiya za madhehebu ya dini yanayojitokeza kuchochea serikali za ubaguzi na hata kuzikosoa imani za dini kwa matakwa ya tafsiri zao wenyewe.

Hata mimi naamini tamko la CCM Zanzibar limeenda shule, ukweli kama huu huumzuii mwanaCCM kuitetea CCM. Lilo muhimu kwa kila mmoja wetu ni kona nchi inatawaliwa kwa amani. Sisi ni watanzania kwanza na uanchama wa vyama vyetu unafuata baadae. Hongera kwa tamko safi.
 
mie jamani naona kama hamuoni kwa njia moja Cuf wamo na aliyekuwa mfalme wa mwisho Jemshid anapiga chapuo kwani alikuwa anakuja kama mtali na alikuwa Hotel ya Cuf Mansons Hotel na mwenyewe ni Nassor Mazurui kwa sasa ni waziri ya Biashara zanzibar
Sasa hivi mjukuu wa Jemshid amejenga Hotel na kiwanja kapewa na Mansuri shemegi yake Rais mstafu Karume na mansuri yuko mbeli kukata mungano hata juzi Rais mstafu Fulani alikuwa anaongea na mtu anasema hebu wacheni wafanye mandamano si wanadai haki yao

Hivi karibuni Waziri wa katiba aliwaita watu wa Mchemsho ( Uwamsho ) akawambia msifanye hivo si vizu mungano ni mzuri Majibu ya watu wa Uwamsho akiwemo Faridi alimwambia leo Mhe Waziri unaturuka kwa kuwa upo mbele ya watui wengine si tunakutana kila siku na ukatwambia tupo pamoja nyie nendeni sasa leo unaturuka .

Hebu jamii leteni ushauri wenu lakini kwa vurugu hizi Malim Seif yumo, Abubakar Waziri wa katiba yumo, mansuri, Karume,Jemshidi
 
Hivi kila siku au bada ya siku moja Karume anaenda ikulu kuna nini ,Hivi Malim Seif hajasema kitu kuh vurugu za jama zake kuna nini
 
ccm kwa kulala hawajambo...hawa jamaa wakati wanafanya mikutano yao mbona walikua hawakamatwi?? wamesubiri mpaka kipele kimekua jipu ndio wameamka..ingekua ni cdm ndio wanafanya mikutano ya aina hiyo ungekuta viongozi washakamatwa siku nyingi lakini huko zenji wamekaa kimya...
 
1. Kwanza naona kauli ya Vuai ni kujikosha tuu. Serikali yake ilisajili kikundi hicho ikijua fika kina misimamo mikali, na kisichokuwa na dira ya kueleweka.

2. Serikali ya Zanzibar haijawahi kuwa na nia ya kupambana na wanaoanzishara vurugu na matusi kwa kigezo cha muungano. Tunafahamu wengi waliopita zanzibar na kuzua mengi kwa kigezo cha Muungano.

3. Kama kulalamika Muungano basi sisi Tanganyika tunayohaki zaidi. Hivi zanzibar wameonewa kipi? Ardhi yenu, bunge lenu, mahakama zenu, mna serikali yenu? Bado mapato ya muungano mnapata percentum! Kama haitoshi mmekuja bara, mmeingia bungeni, mahakamani, serikalini, shuleni na taasisi kibao!

4. Tatizo la zanzibar sio Muungano bali dini! Wajanja wachache wameenda kusoma uarabuni sasa wametengeneza network and they want zanzibar to an islamic country. They don see possibility if they remain part of the union! Because i ve never seen someone 'struggling for freedom while he is actually free'. Big figures are behind this scene, Islamisation of Tanzania, starting with zanzibar. Mark my words
 
Mnaacha kuangalia mzizi wa tatizo, mnatafuta simple and cheap solution.

Wakati wa rasimu ya katiba tuliona yaliyomtokea sitta, na wala haikuwa uamsho, vikundi vya jamii mbali mbali vilialikwa rasmi, lakini ukitazama zile video kila aliyesimama aliongea kwa jazba na mwisho ni kuukataa muungano tena kwa hasira, Kuna mwanajeshi mstaafu alilia.

Busara zinahitajika sana naamini, sio kufuta usajili.
No No No, uzoefu unaonyesha tunaelekea BOKO HARAM na Alshababu, busara ni kukifuta kwani kufutwa kwake hakuzui wao kuukataa Muungano, maana sio lazima uwe chini ya kivuli cha UAMSHO ndo uukate Muungano.
 
Kulazimisha waziri ajiuzuru inatokana na waziri huyo kushindwa kuifanya kazi alokabidhiwa kama alivyoeleza waziri, haina maana ndio suluhisho isipokuwa ndio mfumo wa utawala bora (Zero tolerance) ktk uwajibishaji wa viongozi wetu. Kama alivyotakiwa waziri mkuu Pinda kujiuzuru aliposhindwa kuwawajibisha mawaziri walioshindwa kazi zao ama kujiuzuru kwa mawaziri walishindwa kutekeleza wajibu na rais alifikia kubadilisha baraza la mawaziri ingawa yote haya hayakuwa suluhu ya matatizo yaliyopo.

Unaanza na Uwajibikaji ktk kurekebisha mamlaka kisha anatafutwa kiongozi anayeweza kusimamia kero na matatizo yaliyopo hasa kuhakikisha jumuiya na asasi za kidini haziwezi kutengeneza fitna ya kijamii kwa kutumia misikiti au makanisa wakati huo huo serikali nzima ikitafuta suluhisho. Kero hazitakwisha ndio mfumo wa maisha ya binadamu na hata hao Marekani wana kero ktk nyanja zote za maisha na ndio hapo umuhimu wa elimu inapochukua nafasi kubwa.

Lakini muhimu zaidi ni mtazamo wa kiongozi wetu Mzanzibar na Muislaam ktk swala zima la madsai ambayo binafsi yangu nina hakika majibu yapo palepale nyumbani haikuwa na haja wala sababu ya kumtafuta mchawi toka bara kufikia kuchoma moto makanisa kisha wakane hawakuhusika lakini wakati huo huo wanajisifu kwa msimamo wao na waliyoyafanya nyuma ya pazia la dini.

Hata huyo Allah hutazama na kuyawezesha yaliyo mema hata kama hufanywa na kafir na Sheitan humshawishi hata muumini kutenda yasiyo mema. Hakuna binadamu aliyehai alopigwa mhuri wa utakatifu kwetu sote tupo ktk mtihani mkubwa wa kiimani kwa yale tunayoyafanya kila siku ya uhai wetu. Hivyo kwanza ni makosa makubwa sana kwa kiongozi wa serikali au muumini kuweka dhana na watu waliofanya kitendo kibaya cha kuchoma moto kuwa sii Waislaam au wanazuo wa UAMSHO kwa visingizio vya Usalama wa Taifa wakati hakuna ushahidi lakini zipo sababu nyingi sana zinazopelekea makanisa kuchoimwa na waumini wenye chuki wakiitwa ati wenye siasa kali.

Tume ya katiba, Hakuna mtu anayechukua njia za mkato isipokuwa hawa walalahoi wanaoukataa Muungano ndio wenye kutafuta njia za mkato. hata Bara leo tukianzisha Kongamano utawaona watu wenye hasira na yaliyotokea Zanzibar, wana hasira na matusi mazito yanayoletwa na wahuni ambao hawakushiriki wala kuyaunga mkono Mapinduzi ya visiwa vya Zanzibar. Nimeziona video nyingi sana acha hii moja au mbili za majuzi, na watazame watu wenyewe wakijiita Ustadhi utajua kwamba ni NJAA tu ndio inawasumbua wala sii Muungano japokuwa wanapenda sana kutumia Uzanzibar kana kwamba sisi Bara hatuna Uraia.

Hawa watu hawawezi kukwambia hata jambo MOJA ambalo linawakandamiza Wazanzibar ktk UHURU, HAKI na USAWA dhidi ya WABARA isipokuwa umaskini ulokiuka kutokana na uongozi mbaya wa CCM na sasa hivi CUF. Wasomi wao wengi wamekwazwa tu na muundo wa Muungano kuwepo kwa serikali mbili chini ya kuunda Moja, jambo ambalo linatushinda hata sisi waislaam kuelewa Utatu mtakatifu, lakini bila kufahamu kwamba ya kwamba mfumo huo ndio ulolinda kuwepo kwa Zanzibar hadi leo. Tukiunda nchi mbili, serikali mbili chini ya moja ya Kitaifa amini maneno yangu Zanzibar kama nchi na jina lake ndio litakufa kweli na kabla ya kufa Wazanzibar watataka tena kujitenga kabisa ikiwa swala ni kuvunja muungano. Na ikumbukwe tu historia ya nchi hiyo kuuvunja muungano ni jambo ambalo HALIKUBALIKI. Mtoto hawezi vunja ndoa ya baba na mama kwa mapenzi yake hata siku moja na hata ikija vunjika basi ni maamuzi ya baraza la Mapinduzi.

Ila inawezekana kabisa ndani ya mgogoro huu tukalipata suluhisho na binafsi yangu ningewaomba viongozi wetu wa bara na Zanzibar kuja hapa Canada wajifunze kutokana na muungano wa nchi hii maana unafanana sana na Tanzania ambako sehemu kubwa ya nchi hii ni Waingereza na sehemu ndogo ya Quebec ni Wafaransa na wamekuwa na kero kwa muda mrefu lakini sasa wamefikia suluhisho japokuwa bado Waquebec wanataka kujitenga kutokana na kuwa chini ya Milki ya Malkia maana wao na Malkia wana na historia ndefu ya uadui. Sisi hatujawahi kuwa na uadui huo na ppengine ni mdugu zaidi ya muungano wenyewe kwa sababu historia ya nchi hii inajieleza wazi kwambza hata hiyo Zanzibar inayodaiwa sio Zanzibar nzima, kesho wanaweza dai mikoa yote ya pwani including Malindi, Lamu na Mombasa kuwa sehemu ya nchi hiyo. Hivyo kukubali kuvunja muungano ni mwanzo wa kujenga matatizo mengine ambayo yatatokana na historia ya dini na utawala wa Sultan.

1964 NYERERE ALIIVAMIA ZANZIBAR NA KUWAKAMATA VIONGOZI WAKE NA KUWATIA KATIKA JELA ZA TANGANYIKA HATA KABLA YA HUU UITWAO MUUNGANO YAANI APRIL 26 1964 , JEE KUNA MUUNGANO HAPA ???

Katika mwaka 1968 Hakimu Seaton, Hakimu wa Mahakama Kuu; alitembelea gereza la Mwanza. Nilimuuliza kama kuna uhalali wowote juu ya kuwekwa kwetu kizuizini. Mkuu wa gereza akamwambia Hakimu kuwa hakuna karatasi zozote zilizoletwa pamoja na mawaziri wa zamani wa Zanzibar. Hakimu akaahidi kulifuatilia suala hili. Baada ya miaka minne tangu wakati huo, nikiwa katika gereza la Bukoba, Katibu wa Mkuu wa Mkoa alitoa shauri kuwa nimuombe Raisi anitoe kizuizini. Nalimwambia kuwa kwa vile sijui nini kosa langu la kuwekewa kizuizini naona sina hoja za kimsingi juu ya ombi langu.

Alinijibu, "Hapana shaka ulipotiwa kizuizini ulisomewa amri ya kutiliwa kizuizini."

Nilimwambia kuwa, vile ninavyo kumbuka mimi hapakuwepo amri ya mimi kutiwa kizuizini. Suprintendent wa magereza akanambia kuwa ilikuwepo amri, hapo akanisomea hio amri ambayo ikionesha kuwa inatokana na Raisi na ambayo imeandikwa kwa lugha ya kisharia. Amri hio inasema kuwa Raisi baada ya kutoshelezeka kuwa, fulani na fulani; akiwataja mawaziri wote wa Serikali ya Muhammad Shamte, kuwa walikhusika na vitendo vya uchochezi wa kukhatarisha salama ya nchi, alitoa amri tutiwe kizuizini. Nalipomuuliza amri hio ilitiwa sahihi lini, ilidhihiri ilikuwa ni mwaka wa 1968, baada ya muda mchache tangu pale nionane na yule Jaji Mkuu, Seaton kwenye gereza la Mwanza!

Sisi tulivamiwa nchi yetu na kutiwa vizuizini katika mwaka wa 1964. Najuwa kulikuwa na mapinduzi (mavamizi) huko Zanzibar, na hicho kitendo cha kiharamia iwe kimetokea huko. Lakini tangu kati ya mwaka wa 1964 pale tulipotiwa vizuizini mpaka hii 1968 ambapo hii amri ya kutiwa kizuizini kutolewa na kutiwa sahihi; wakati huo wote - miaka minne - kuwekwa kwetu kizuizini na yeye Raisi Nyerere ambae ndie aliekuwa na hukumu yote huko Tanzania bara basi hakukuwa kisharia hata katika hio sharia ya kidhaalimu ya Tanzania. Kwa muda wa miaka minne kabla ya kutiwa sahihi hii amri ya kuwekwa vizuizini sisi tulikuwa basi ni wafungwa wake yeye Nyerere. Je, ndio inayumkinika katika muda huo iwe yeyote miongoni mwetu sisi tuweze kufanya vitendo vya uchochezi wa kukhatarisha salama ya taifa? Tujaalie kuwa inakusudiwa ule muda kabla ya kukamatwa na kutiwa kizuizini. Wakati huo sisi tulikuwa ni mawaziri wenye mas-ulia kwa vile tulichaguliwa kulingana na sharia ya kikatiba iliokuwepo nchini - Zanzibar - wakati huo. Je, sisi wakati huo tutaweza kuwa tutende kama vile ilivyoelezwa katika hio amri iliotiwa sahihi na Julius Nyerere? Kama itakavyokuwa, hilo taifa linalo elezwa kuwa ni Tanzania; halikuwepo kabla ya sisi kukamatwa na kutiwa vizuizini. Huyo ndio mkuu wa nchi, anaejigamba kuwa yeye ni mwenye kuweka haqi, anafika kuzuwa na kupanga uwongo kama huo; ni jambo la kushangaza sana; lakini kwa watu kama yeye sio ajabu kulitenda. Baada ya kupata hoja hizi ndipo nilipomwandikia Raisi, bila shaka maandishi yangu yalikuwa ni ya upole na kweli za hakika. Sikupata majibu. Kwa hakika sikupata hata mara moja jawabu au hata kuarifiwa kuwa zimefika, baruwa zangu kadhaa wa kadhaa nilizompelekea Nyerere, tangu niko kizuizini na hata baada ya kutoka. Utaritibu wa hishima kama hio Tanzania inaonekana ni mpango wa kikoloni uliokwisha pitwa na wakati.

Dr. Kleru alikuwa ni Mkuu wa Mkoa aliepigwa risasi na mkulima, Abdulla Saidi Mwamindi; siku ya krismasi mwaka 1971. Mkulima huyu, Abdulla Saidi, alikuwa ni miongoni mwa watu kadhaa wa kadhaa walionyang'anywa mashamba yao kwa kuwanzishia vile vijiji vya ujamaa. Jeuri ya Mkuu wa Mkoa huyu ilifurutu ada. Waliokuwa wakiteswa na kudhulumiwa na Mkuu wa Mkoa huyu walishitaki kwa wakuu wa chama. Kila wakishitaki huambiwa wakashitaki polisi; na wakifanya hivyo. Kamanda wa Polisi, Abubakar aliwaonya wakuu huko Dar es Salaam juu ya vitendo viovu na vya kuudhi vya Mkuu wa Mkoa huyu na juu ya ile tabia yake ya ulevi kufika kuanguka na kuingiliwa na wahuni. Baada ya kupigwa marisasi na kuuliwa, wale jamaa wote waliokuwa wakipeleka mashtaka yao Polisi walikamatwa na kuwekwa kizuizini mpaka Abdulla Saidi Mwamindi ahukumiwe na kunyongwa. Hata kabla ya kesi kumalizika, magazeti na vyombo vyote vya khabari vya Serikali na vya Chama, vyote vilianza shutuma zao, sio tu dhidi ya Mwamindi, bali dhidi ya wakulima wote, huku wakisemwa, "mabepari", "wanyonyaji", "wakoloni" na makhaini". Mudhahara uliopangwa na Sirikali ukaingia njiani kupita kuwashutumu na kuwalaani watu hawa. Kwa hali hii ikawa Mwamindi kesha hukumiwa na vibaraka vya Sirikali hata kabla ya kufikishwa mahakamani. Mashahidi wote wale ambao wangeliweza kutowa ushahidi japo kuthibitisha juu ya vitendo vya uchokozi vya yule Mkuu wa Mkoa walizuiliwa mpaka pale kesi kumalizika. Khatuwa hii ilikusudiwa kumtia khofu yeyote yule aliekuwa na fikra ya kutaka kutowa ushahidi upande wa mshitakiwa. Hivi ndivyo sharia inavyo firigiswa katika nchi kama hivi Tanzania wakati ambapo sharia ya kumtia mtu kizuizini bila ya kupelekwa mahakama inatumika. Watu kumi na mbili wa Iringa pamoja na yeye Mwamindi mwenyewe walikuwa pamoja na mimi gerezani Dodoma. Kamanda wa Polisi Abubakar, na yeye vilevile aliwekwa na sisi siku mbili gerezani akiwa yumo katika pirika za kuhamishwa kutoka gereza hii na kupelekwa gereza jengine.

Ilani nyingi zilitolewa na kutangazwa ulimwenguni juu ya maafa na mateso katika magereza ya Zanzibar na Pemba. Lakini hapana lililosemwa na kuelezwa walimwengu kukhusu mateso yanayowapata wazuiwa katika magereza ya Tanzania bara. Sio kuwa uwovu na mateso wanayotendewa wazuiwa magerezani huko Tanzania bara hayajuulikani; mengi yake hayafiki ulimwenguni basi kwa sababu ya kukosekana demokrasia na heshima ya haki za binadamu juu ya haki ya kueleza na kujieleza. Kutokana na hali hii, mateso na vitendo vya kikhabithi havielezwi nje kwa walimwengu kukhofia hao watakaoeleza kuadhibiwa na utawala wa kidikteta. Niliona kwa macho yangu nilipokuwa gereza la Mwanza, wakati ambapo Superintendent Odenyo ndie aliekuwa mkuu wa gereza wakati huo; niliona wafungwa walipozuiliwa chakula na maji kwa muda wa siku nne, kisha wakapelekwa hospitali (nusu maiti) na ripoti kuwa (ati) walikuwa wamegoma kula. Nilipokuwa Dodoma nilikuwa nikisikia kadhia kama hizo. Nikisikia, kwani baina yetu ilikuwa ni kuta, baina ya chumba niliokuwemo na vile vyumba vya mateso. Katika gereza la Dodoma aliekuwa katili hivyo ni Ofisa Mkuu, aliepangwa jina "Iron Face" (Uso wa Chuma), kwa vile akijuulika kuwa hajapata kuwa na huruma. Mkuu wa magereza hapa, alifika kuwa hajishughulishi tena na kazi yake; hivi ni kwa sababu kwa hichi cheo chake cha juu na daima kuwemo katika vikao na sherehe za kisiyasa, takribani alimuachilia uendeshaji wote wa gereza mikononi mwa msaidizi wake - huyu Ofisa Mkuu. Mabwana wawili hawa waliyafanya maisha ya gerezani hapa hayastahamiliki hata kidogo.

Ile mikutano ya kawaida ya kila Jumamosi ambapo ofisa mas-uli hutarajiwa asikilize malalamiko ya wafungwa ikawa haifanywi tena. Ziara za kila mwezi gerezani za Mahakimu mbalimbali nazo pia zikasita. Wafungwa hutiwa gerezani na kufika kutolewa bila ya kujuwa kuwa wanahaki ya kuwasiliana na watu wao. Inafaa ifahamike kuwa hivi kuharibika hali kiwango hichi, sio tu katika gereza la Dodoma. Niliiona hali kama hiyo katika gereza la Mwanza. Gereza la Bukoba ilikuwa haijambo pale nilipoondoka. Lakinibasi, wakuu wa kisiasa; kama vile Mkuu wa Mkoa na Mawaziri dhaahir shaahir walikuwa wakijiepusha kuyazuru magereza na kujuwa hali za wafungwa na wazuiwa waliomo humo magerezani. Ama Raisi na Makamu wa Raisi, si dhani kama iko siku wamewahi kuzuru gereza lolote lile katika Tanzania bara, licha kuzungumza na mabwana au mabibi waliowatia humo magerezani. Hali katika gereza la Dodoma ilizidi kufanywa kuwa mbaya kwa ukhabithi wa huyu "Uso wa Chuma" na kulemaa kwa ulevi wa marungi Msaidizi wa Superintendent.

Mpango ulifanywa kumuuwa "Uso wa Chuma". Mmoja wa wafungwa aliweza kupata kisu na akataka kumpiga nacho huyo "Uso wa Chuma", kwa bahati akaanguka kifudifudi, kichwa chake mbali na yule mfungwa ambae alikuwa na pingu za chuma miguuni mwake na yeye vilevile akaanguka upande wake. Wakati huo mfungwa aliweza basi kuipata miguu ya "Uso wa Chuma" na kuanza kumpiga visu vya miguuni mpaka pale ilipowezekana kuzidiwa nguvu akanyang'anywa hicho kisu. Hapo tena akaingiliwa mfungwa huyo kupigwa marungu mpaka akawahijiwezi ndipo alipotiwa pingu za mikono. Askari wa gereza akaamrishwa kumpiga marisasi ya miguu. Hivyo ikawa kafungwa kila upande na marisasi miguuni mwake, hapo tena akasukumizwa katika chumba cha adhabu. Baadae kidogo msaidizi wa superintendent akaja na yeye akaanza kumpiga vile alivyopenda. Vilio vyake tukivisikia kutokea katika hicho chumba cha adhabu alimokuwemo na tukamuona askari aliekuwa zamu kwenye kidungu akigeuza uso na kupiga ukelele: "Wanamuuwa huyu mtu!" Binadamu huyu akavurumishwa tena humo chumbani kisha bomu la kutowa machozi likatupwa katika hicho chumba ambacho sehemu yake ya kupitia upepo ni ndogo kabisa. Usiku uleule akajifia.

Asubuhi yake wafungwa wote wakasimamishwa kwenye uwanja na maiti ikaletwa mbele yao uchi kama alivyozaliwa. Hapo tena msaidizi wa superintendent akawa anamchocha maiti kwa gongo huku akimwambia yule maiti: "Inuka uwaambie wenzio vipi ulivyokuwa hodari, na nini mwisho wa uhodari wako?" Baada ya hivyo tena akawahutubia wafungwa kwa kuwaambia kuwa hivihivi ndivyo tutakavyomfanya yeyote yule miongoni mwenu asiposhika adabu yake. Hapo tena wafungwa wote wakafungiwa vyumbani mwao kisha mabomu ya kutowa machozi yakatupwa humo vyumbani mwao. Haya yalifanywa kwa makusudio ya kuwataka watajane wale waliokhusika na mpango huu. Haukupita muda isipokuwa wengi wakatajana na kukiri makosa yao. Lakini adhabu na mateso yaliendelea kwa wiki kadhaa wa kadhaa. Chakula kikapunguzwa, hata kwetu sisi wazuiwa. Kila mtu alitaraji mauwaji haya yatafanyiwa uchunguzi na hukumu ya haki kupitishwa. Askari wa gereza ikawa wanasema hadharani kuwa ukifanywa uchunguzi watawaambia askari Polisi hakika ya mambo ilivyo. Lakini hapana lilokuwa. Tulisikia katika redio, kama maneno ya kupita tu yaliosemwa Bungeni - kwa woga - na mmoja wa Wabunge kuwa kulikuwa na askari makhabithi walio waadhibisha wafungwa mpaka kufika kuwauwa. Kubwa lililotokea ni uhamisho wa kawaida wa maofisa wa magereza wa vyeo vya juu kutoka magereza mbali mbali nchini. Khabari ikamalizikia hapo.

Katika nchi yenye sheria ya kutiwa watu vizuizini bila ya kupelekwa mahakamani, kelele zozote zile ni sawa na mbwa mwenye kubweka hazina athari yoyote ile, na sharia basi ni kwa kumtumikia bwana mtawala aendelee katika utawala wake na atende vile anavyopenda.
 
Huwezi kufananisha muungano huo na huu feki hata kama unaona kwako wewe uko sawa lakini kwa wataalam kam J. Ulimwengu huu si muungano ila ni muumizano. Muungano ulikuwa mwisho ni 1974 lakini Nyerere (LTLLAH) alipoona Karume anataka nchi yake alimmaliza kwa kumuua kwa risasi na mwaka 1977 alinza kuhodhi kila kitu cha Z'bar. Napia Aboud Jumbe alipojaribu kujitutumua kutaka kujitoa ktk muungano alivuliwa uanachama na kumvua uraisi na kumfunga kifungo cha ndani mpaka amezeeka, alafu unasema muungano huu ni sawa na wa Canada hapo umepotea kaka tafuta ukweli usiropokwe tuu uliza kwanza kwa wataalamu.

Wazanziabri wanataka nchi yao msijitie visababu vya kipuuzi puuzi.

Acha uvivu wa kufikiri wewe.Wewe ni shaidi kuwa hakuna Mtanganyika wa kawaida anayefaidika na huu muungano so acha kutoa mapovu kushutumu upande wa bara kuwa tunang'ang'ania muungano.

Ungekuwa unamawazo yenye busara nyie upande wa Zenj mkesisitiza muungano.Mnaopinga muungano ni kikundi cha wachache wenye uchu wa madaraka.
 
Hilo la kufuta UAMSHO ni ndoto za CCM ambazo tafsiri yake ni kukaribisha mgogoro mwengine usioweza kusuluhishika.

Vuai kaona tonge hio inamtoka ndio maana anajikaza kisabuni.

Katiak Uislam huwezi kutenganisha Dini na Siasa kwa7bu siasa ni kajisehemu kadogo ktk Dini ya kiislam ambayo ni mfumo kamili wa maisha wa mwanadamu.

Sasa wewe unaposema nisichanganye Dini na Siasa naona unataka kuniambia nifuate uislam wangu nusu na robo na robo nyengine niiyachie ambayo ndio hiyo siasa, hilo alikubaliki hata kidogo, mwache huyo Vuai na ujinga wake maana hata huo Uislam wake haujui, ndio maana hajui maana ya Dini (Uislam) wala hiyo maana ya siasa yupo yupo tuu !!!!!

Siasa ni mfumo wa kuendesha serikali. Kama unavyosema hapo ni sahii basi ili lengo letu litimie, juhudi ni kuendesha nchi kwa sheria za kiislam jambo linalopigiwa kelele na Alshabab, Boko Haramu, n.k. ndo maana tumeona mambo ya kuchoma Makanisa kama huko Nigeria. This is practically impossible, we must go back in our teachings and see if we actually have the right direction or we are being swayed away by unknown wind.
 
waliochoma makanisa wote ni mawakala wa shetani wasitudanganye kwamba huo ndio uislam, wala makanisa hayamaanishi muungano kwa sababu hata wazanzibar wapo wakristo pia.
 
Huwezi kufananisha muungano huo na huu feki hata kama unaona kwako wewe uko sawa lakini kwa wataalam kam J. Ulimwengu huu si muungano ila ni muumizano. Muungano ulikuwa mwisho ni 1974 lakini Nyerere (LTLLAH) alipoona Karume anataka nchi yake alimmaliza kwa kumuua kwa risasi na mwaka 1977 alinza kuhodhi kila kitu cha Z'bar. Napia Aboud Jumbe alipojaribu kujitutumua kutaka kujitoa ktk muungano alivuliwa uanachama na kumvua uraisi na kumfunga kifungo cha ndani mpaka amezeeka, alafu unasema muungano huu ni sawa na wa Canada hapo umepotea kaka tafuta ukweli usiropokwe tuu uliza kwanza kwa wataalamu.

Wazanziabri wanataka nchi yao msijitie visababu vya kipuuzi puuzi.

Kwakero zilomo haziwezi kusulihishwa kutokana na wingi wake ukaidi wa Watanganyika kujifanya mabwana wakubwa dhidi ya Wazanzibari, kwa hio kwa hapa tulipofika hakuna mjadala isipokuwa kura ya maoni iitishwe kwa Wazanzibari eidha kuukubali au kuukataa huu muungano, wacheni kunga'nga'nia Zanzibar kwa kisingizio cha cjui usalama, undugu, uasili na mambo mengine yasiyo na mantiki yyte.
Kama ni undugu nadhani pia tumo wengine asili yetu ni Mombasa Kenya, Somalia, Msumbiji Oman, Yemen, Iran, India< China, Comoro etc lakini hatujaungana nchi hizo, na hao wenye asili ya Tanganyika tunao hapa Zenji na waomba mungu uvunjike muungano wawe huru huku Zenji kwani huku ni kwao kama watu wengine.
Nani alokwambia kwamba Muungano mwisho wake ulikuwa mwaka 1974 kama sii tungo za uongo na Unafiki wa hawa hawa watu wanaodai kuutumia Uislaam iiihali wapo radhi kuongopa kwa faida zao binafsi.

Nitakwambiua tu ya kwamba kati ya hawa wote wanaopiga kelele leo hii, hakuna hata mmoja wao alikuwa mujumbe ktk baraza la Mapinduzi, hawakuhudhuria hata kikao kimoja cha kuunda Muungano wala kuwa na ukaribu na sekretariet ya ASP wakati wa Mapinduzi. Hawa asili yao ni Hizbu woote wanaopiga kelele leo hii na hawajui mipango wala kilifanyika nini hadi Zanzibar kuyafikia Mapinduzi dhidi yao vibaraka wa Sultan kina Shamte waliojiunga na Hizbu makusudi ili kuchukua ushindi ili kumrudisha Sultan kwa mlango wa nyuma wakiahidiwa uongozi na vyeo ktk serikali, hawa hawana lolote ni tamaa tu ya madaraka na hawakuianza jana wala juzi. Ila nakuomba sana kazungumze na mtu kama Nassoro Moyo, huyu anaweza kwambieni yalojificha japokuwa naye bado hajui undani zaidi wa Muungano maana naye alikuwa Mjamaa au niseme Mkomunist..

Mpango wa Muungano baina ya Zanzibar na Bara ni mpango wa siri kubwa ilitokana na kupinga Ukomunist wa kina Abrahman Babu, Hanga, Moyo na wengineo. Ni mpango ulopangwa baina ya Tanzania bara, visiwani na CIA ktk kuhakikisha Zanzibar haiwezi kuwa nchi ya Kijamaa maana walijua mapema kuwepo kwa Mapinduzi yaloongozwa na Umma party. Hivyo, kilichotokea walisubiri tu Mapinduzi kisha wakawavuta kina Abrahman Babu kwa kutumia ushawishi wa wana ASP waliokuwa upande wa kushoto pia kina Hanga, Hassan Moyo na wengineo.

Umma party wakaingia mkenge wakavunja chama na kujiunga na ASP ili kuunda serikali ya Jamhuri ya muungano na kuwahakikishia usalama (peace) baina yao. Lakini kwa CIA hawa watu walikuwa bado hatari maana Ukomunist ni itikadi sii swala la kurubuniwa, walitakiwa kuuawa tu kuhakikisha Ukomunist haupati nafasi East Afrika ndipo njama za kuwaua na kuwasweka ndani zilipo pamba moto na kwa kumtumia Karume huyo huyo akiwasaka Wazanzibar ikiwa ni pamoja na wale walokuwa Hizbu (Waarabu). Hivi unafikiri kina Babu waliishi Bara kwa kupenda? kina Salim, Mwinyi na Waarabu wenye asili ya KiOman walohamia Bara mikoani wamejaa Singida na Usukumani wengine hadi wanaongea Kikerewe na kiisukuma unadhani walipenda kuhamia huko.

Lakini maajabu ya Mussa leo mmesahau kabisa fadhila za Bara ktk kuwalinda Wazanzibar japokuwa Hawa kina Babu ndio walombatiza Nyerere kuingia Ukomunist.. Aaaah Nasema sana miye weee ebu zungumza na wenyewe CIA kisha pembua pumba toka ktk mchele..BOFYA
 
Iwapo wazanzibari hawautaki muungano mbona dawa ni ndogo tu!!! Hivi ndio kusema Wanzanzibari hawana habari kwamba kati ya vyama vyote vya siasa ni Chadema tu ndio walio na sera za kutaka wazanzibari wenyewe wajadili aina ya muungano wanaoutaka?? Hivi hawa ndugu zetu waislamu wanaliona hilo? Mbona hata punguani anajua muungano ni wa ccm na cuf kwa maslahi ya wachache? Kazi ndogo sana hapo!! Vurugu za nini? Ipeni kura Chadema kupambazuke!!

Wao hawautaki muungano CDM wanashauri muundo wa Muungano ulekebishwe mkuu kuwe na serikali 3
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom