Kizimkazimkuu
JF-Expert Member
- Nov 8, 2007
- 337
- 234
CCM yapata pigo jingine Mwananchi, Saturday, 11 September 2010 09:35
Waandishi Wetu
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimepata pigo lingine baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuyatupa mapingamizi yake dhidi ya wagombea ubunge wa upinzani katika majimbo ya Bahi mkoani Dodoma na Mbozi Mashariki mkoani Mbeya.
Hili ni pigo la pili katika kipindi cha juma moja lililopita baada ya Baraza la Ushauri wa Masuala ya Siasa kukitaka chama hicho kiondoe mabango ya mgombea wake wa urais Jakaya Kikwete yaliyopigwa Ikulu
Kutoka Bahi habari zimeeleza kuwa NEC, imetupa pingamizi lililowekwa na mgombea wa CCM katika Jimbo hilo, Omary Badueli dhidi ya mgombea ubunge wa Chama Cha Sauti ya Umma (SAU), Melkzedek Lesaka.
Awali Badueli aliwasilisha pingamizi hilo kwa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Bahi kwamba Lesaka hakutimiza idadi ya wadhamini waliotakiwa kwa mujibu wa sheria na alienguliwa.
Lakini mgombea huyo wa SAU hakuridhika badala yake aliamua kukata rufaa NEC kupinga kuondolewa kwake kwenye kinyang'anyiro hicho cha ubunge.
Hukumu hiyo ya NEC iliyotolewa kwa barua ya Septemba Mosi mwaka huu ambayo Mwananchi imefanikiwa kuiona, imeeleza kuwa kikao kilichofanyika Agosti 31, mwaka huu kupitia rufaa hiyo, imetengua pingamizi hilo la CCM.
"Tume imekubali rufaa yako (Lesaka). Imeona kuwa ulitimiza idadi ya wadhamini waliotakiwa kwa mujibu wa sheria. Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekurudisha katika orodha ya wagombea na hivyo wewe ni mgombea halali ilieleza sehemu ya barua hiyo.
Wakati hayo yakiendelea jimboni Bahi, Tume ya Uchaguzi Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, jana imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na mgombea ubunge wa CCM, Godrey Zambi dhidi ya Mgombea wa Chadema, Allan Mwampamba.
Zambi alimwekea pingamizi mgombea huyo wa Chadema kwa Msimamizi wa uchaguzi wa wilaya ya Mbozi akidai kuwa mgombea huyo wa Chadema hana sifa kwa kuwa amedanganya kwamba ni mwalimu, lakini pingamizi hilo lilitupwa.
Baadaye Zambi alikata rufaa NEC kupinga hukumu hiyo iliyotolewa na msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Mbozi Mashariki akitaka imwengue mpinzani wake huyo kwa kosa la kusema wongo.
Jana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi, Levison Chillewa alilieleza gazeti hili kuwa NEC imemrejesha mgombea wa Chadema kuendelea na kampeni baada ya kumwona hana tatizo la kisheria.
Kutokana na uamuzi wa NEC kutupilia mbali pingamizi la mgombea wa CCM limesababisha umati wa wanachama wa Chadema kusherekea rufaa hiyo ya ushindi kwa mgombea wake na kusababisha siasa kuwa ngumu katika jimbo hilo.
Akizungumza na gazeti hili jana mgombea huyo wa Chadema alisema kurudishwa kwake kwenye kinyang`anyiro hicho, ni dalili za ushindi kwenye uchaguzi huo.
Alisema kama Mtanzania, ameamua kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho kuwatumikia wananchi na dhamira yake kubwa ni kufikia malengo yake hayo.
Wakati huo huo, siku chache baada ya Baraza la Ushauri la Masuala ya Siasa kukitaka CCM kiondoe mabango ya picha za mgombea wake wa urais Jakaya Kikwete ambazo zimepigwa akiwa Ikulu, suala la mambango hayo linaonekana kuzidi kukikoroga chama hicho.
Wakati, NEC ikikutana siku mbili mfululizo sasa jijini Dar es Salaam kujadili suala hilo na kuwaita wawakilishi wa CCM na kuwahoji, ,mkoani Kagera moja ya bango kubwa lililokuwa limewekwa mjini Bukoba, limeondolewa.
Hata hivyo viongozi wa chama hicho wilayani hapa wameshindwa kutoa ufafanuzi kutolewa kwa bango hilo.
Bango lililoondolewa ni miongoni mwa mabango matatu yanayomwonyesha mgombea huyo akiwa katika matukio tofauti. Mabango hayo yaliwekwa eneo la Rwamishenye katika njia panda inayoelekea wilaya za Muleba na Missenyi.
Bango hilo, liliondolewa siku ya Jumatatu saa 4:30 asubuhi na vijana wawili ambao hawakufahamika kwa majina na badala yake kuwekwa bango la kampuni moja ya simu za mkononi.
Habari hii imeandaliwa na Fidelis Butahe, James Magai, Keneth Golima, Mbozi na Phinias Bashaya, Bukoba