CCM yanaanza kuchanganyikiwa na kasi ya CDM, yajipanga kuihujumu.

Bado Kidogo 2015

JF-Expert Member
May 24, 2012
207
78
Kutoka jikoni, kuna tetesi Chama cha Mapinduzi kimeanza kuweweseka na kasi ya CDM kila kukicha hasa operation zake ambazo zimeonekana kuwa na uamusho mkubwa sana wa wananchi na kukiweka chama hicho msambweni!!!!

Maafisa usalama wanahaha kutafuta njia mujalabi itayoiyumbisha CDM lakini taasisi hiyo imegundua wananchi ni wepesi sana wa kusameheme makosa yanayofanywa na wapinzani hasa CDM na wepesi wa kulaumu na kuilaani serikali kama haijafanya kitu toka uhuru vile!!!!

Jambo hilo linamuumiza mkuu wa kaya asijue nini kifanyike ili kukinusuru chama chake ambacho kimegubikwa na migogoro mikubwa ambayo suluhu inaonekana ipo mbali kupatikana!!!

Mshambenga wangu akazidi kunyetisha, endapo mkutano wa kesho utafanikiwa angalau kwa 75% basi siku za usoni vibali vya vyama hasa CDM vitakuwa vigumu sana kutoka kwa kisingizio cha sababu za kiintelejensia!!

Wakuu nimeamua niwapakulie udaku huo ambao ni wa moto kabisa ni kwa kadri ya urefu wa kamba yangu.
 
Hawawezi tena kuokoa chochote kile hata mswaki utaungulia ndani kadri moto wa CDM unavyozidi kuwaka
 
Kazi wanayo! Mimi tayari nilishapiga kura ya mwaka 2015!

Nadhani hutaharibu kura yako kabisa, la mwisho tuombe Mungu panapo majaliwa historia mpya iandikwe Tanzania kwa kuiondoa serikali inayoshindwa kusimamia rasilimali za taifa kikamilifu.
 
Hawawezi tena kuokoa chochote kile hata mswaki utaungulia ndani kadri moto wa CDM unavyozidi kuwaka

Kamanda Rweye kama ningeitwa angalau nitoe suluhu ya kuchukiwa CCM ningesema maneno machache sana " Iache kukumbatia watu wachache ambao hawakisaidii chama" Hao ndiyo wanaotoboa jahazi ili lizame. Mfano wa wazi ni watu kama akina Kova wanachokiunda kwa wananchi ni chuki dhidi ya Polisi na CCM kwa ujumla.

Mwisho wa siku hata kama CDM hakitakuwa chama kitakachowasaidia wananchi lakini kitapigiwa kura ili kuikomoa CCM.
 
Hakika kazi wanayo! kamwe huwezi kuzuia mafuriko kwa kuchimba tuta!
 
niko nyuma kidogo kesho mkutano saangapi jamani tipitie kombati mapema kwa fundi maana kanikela leo hajanipa
 
Mimi siaangaliii tena wala kuchunguza wala kutafakari. ni kama mke kwa WAKRISTO ukioa ni milele tu, HIVYO MIMI NI GWANDA TU
 
Kwa hatua tuliyo fikia hujuma sasa haiwezekani tena.

Hujuma zipo na zinawezekana lakini kama angalau CCM ingeonekana kujikaza kuelekea kujirekebisha.

Lakini ukweli ni kuwa CCM inaipigia CDM kampeni indirect sana kwa kutowajibika kwa serikali.

Wasomi kushindwa kupata mikopo intime, madawa kutopatikana hata ya malaria, kupanda juu kwa gharama za maisha, serikali kukosa fedha na kujiendesha kisanii sanii, ufisadi na kuleana kuliko kubuhu!!!

Hayo yote yanawshitua wananchi kuliko mikutano yote wanayoweza kuifanya CDM.

Nachukia sana ubabaishaji.
 
niko nyuma kidogo kesho mkutano saangapi jamani tipitie kombati mapema kwa fundi maana kanikela leo hajanipa

Mkutano ni kuanzia saa kumi za jioni lakini unatakiwa uwahi mapema maana kutokana na hali inavyoonyesha kesho watu watajaa sana.
 
Hujuma zipo na zinawezekana lakini kama angalau CCM ingeonekana kujikaza kuelekea kujirekebisha.

Lakini ukweli ni kuwa CCM inaipigia CDM kampeni indirect sana kwa kutowajibika kwa serikali.

Wasomi kushindwa kupata mikopo intime, madawa kutopatikana hata ya malaria, kupanda juu kwa gharama za maisha, serikali kukosa fedha na kujiendesha kisanii sanii, ufisadi na kuleana kuliko kubuhu!!!

Hayo yote yanawshitua wananchi kuliko mikutano yote wanayoweza kuifanya CDM.

Nachukia sana ubabaishaji.

CCM haina uwezo tena wakujirekebisha, bado wanadhani ulimwengu wa propaganda, vitisho na intelijensia unaweza kuzuia mabadiliko!!!. Kwa hali ilivyo sasa CCM basi tena!
 
CCM haina uwezo tena wakujirekebisha, bado wanadhani ulimwengu wa propaganda, vitisho na intelijensia unaweza kuzuia mabadiliko!!!. Kwa hali ilivyo sasa CCM basi tena!

Wamezoea kuchezesha wanaita gemu tume ya uchaguzi lakini safari hii tutatoana macho kabisa.

Dhulma ni mbaya sana.
 
Naapa nitapigia kura mgombea wa chadema kuanzia rais,wabunge na madiwani! No comment
 
mi sisemi ila natunza kweli kile kikadi changu cha kupigia kura.....sitadanganyika na kutetereka 2015..yaani nimeshakata shauri
 
Back
Top Bottom