CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

[h=2]
icon1.png
ccm kuanzisha al shabab mikoa ya pwani[/h]
KATIKA HALI YA KUWAGAWA WATANZANIA CCM IMEANZA KUWATUMIA BAKWATA KUWAGAWA WANANCHI.WAZIRI WA ELIMU NI MUISLAM MAKAMU WA RAIS MISLAM KATIBU ITIKADI CCM NI MUISLAM,RAIS WA NCHI MUISLAM MKUU USALAMA WA TAIFA NI MISLAM SASA VP LEOBAKWATA WASEME WANA FELISHWA HIZI NI MBINU CHAFU ZA CCM KUWATOA WANANCHI KWENYE WIMBI LA MAGEUZI YA KISIASA NA KUIINGIZA UDINI KWENYE JAMII NI HATARI NA NI LAANA KWA HAWA WANAMTANDAO HUU TUNASEMA ILI TANZANIA IWE NA AMANI 2015 CCM LAZIMA IONDOKE ISITULETEE MAAFA.WAMEANZA UAMSHO NA HAKUNA KARIPIO KALI LILILOTOLEWA KUONESHA CCM INAVYOHUSIKA VILIVYO KABLA YA UCHAGUZI 2015 WASHINDWE WALEGEE NA WASAMBARATIKE.MUNGU IBARIKI TANZANIA:confused2:​
 
Chadema leo wameanza kutapatapa tangu asubuhi, mtatunga kila aina ya uongo, CCM inazidi kusonga mbele
 
kumbe inawezekana hata zile kadi zinazokusanywa na cdm kwenye mikutano nazo huwa ni feki,na wanachama mamluki
 
chama cha mapinduzi (ccm), kimedaiwa kutumia mamilioni ya fedha kugharimia mkutano wake wa hadhara unaotarajiwa kufanyika leo katika viwanja vya jangwani jijini dar es salaam, katika kile kinachoonekana kujibu mapigo ya mahasimu wao, chama cha demokrasia na maendeleo (chadema).

Kinyume na madai ya ccm kwamba lengo la mkutano huo ni kuhamasisha uhai wa chama na kutolea ufafanuzi mambo kadhaa yanayojitokeza ndani ya chama hicho, lakini duru za siasa zimedai kuwa, lengo kuu ni kujipima nguvu na chadema ambacho wiki mbili zilizopita kilifanya mkutano wa hadhara katika viwanja hivyo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Katika mkutano huo wa chadema ambao ulirushwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha itv, maelfu ya wanachama waliofurika, walifika katika viwanja hivyo kwa njia zao bila kusombwa na magari, wala kupokea posho.

Ili kuhakikisha mkutano wa leo unafunika ule wa chadema kwa kupata watu wengi, ccm imeamua kuwasafirisha wajumbe wake kwa magari makubwa ya kukodi kama vile malori na mabasi kutoka kila tawi na kuwafikisha katika viwanja hivyo.

Mbali ya kusombwa kwa magari, ccm pia imeamua kugawa bure fulana na kofia, na kuna madai kuwa chama hicho kitatoa posho kwa wanachama wake watakaohudhuria mkutano huo.

Mkakati wa kuhakikisha mkutano huo unapata watu wengi, umesukwa kuanzia ngazi ya matawi, wilaya hadi mkoa kwa zaidi ya wiki moja sasa.

Kana kwamba hiyo, haitoshi, ccm imeandaa baadhi ya wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya (bongo flava) watakaotumbuiza mapema kabla ya kuanza mkutano kwa nia ya kuwavuta wanachama.

Baadhi ya wasanii hao ni diamond, marlaw, frola mbasha na wengine wengi ambao walipata kutumika wakati wa mikutano ya kampeni ya rais jakaya kikwete.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, katibu wa uenezi na itikadi ccm, nape nnauye alisema baadhi ya mawaziri na makada maarufu ndani ya chama hicho tawala, watahutubia katika mkutano huo.

Alisema mkutano huo unaotarajiwa kuwa wa aina yake, ulipangwa siku nyingi kwa lengo la kuwakutanisha pamoja viongozi wa chama wa mashina na matawi waliochaguliwa hivi karibuni katika uchaguzi wa ccm unaoendelea katika ngazi mbalimbali.

"kuna vyombo vimesema mkutano huo utahutubiwa na mzee mkapa, mwinyi. Hiyo sio kweli maana hata mwenyekiti wa chama taifa, rais jakaya kikwete hatakuwepo jukwaani," alisema nape.

Aliwataja mawaziri watakaohutubia mkutano huo kuwa ni pamoja na waziri wa uchukuzi, dk. Harrison mwakyembe, naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, januari makamba, waziri wa nchi ofisi ya rais (mahusiano), steven wassira, waziri wa ushirikiano wa afrika mashariki (eac), samuel sitta, waziri wa ujenzi, john magufuli, mjumbe wa halmashauri kuu (nec) na kamati kuu (cc), abdulrahman kinana na nape mwenyewe.

"mzee kinana atazungumzia masuala ya katiba na sheria na atatoa kauli kuhusiana na vurugu zilizotokea visiwani zanzibar na kueleza msimamo wa chama kuhusu kikundi cha uamsho cha visiwani humo kinachodaiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo.

"wasira atajikita kwenye uchumi, dk. Mwakyembe atazungumzia jinsi serikali inavyoshughulikia masuala ya uchukuzi, magufuli atazungumzia utekelezaji wa ilani katika eneo la ujenzi na mkakati wa kuondoa foleni jijini dar es salaam," alisema nape.

Kama ilivyokuwa kwa chadema, ccm nao wameamua kurusha mkutano huo moja kwa moja kupitia kituo cha televisheni ya taifa (tbc) na televisheni ya itv na baadhi ya vituo vya redio.

Aliwataka wananchi, wanachama wa ccm na wakereketwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo ili kuwasikiliza viongozi wa chama na serikali watakaozungumzia kuhusu utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya ccm ya mwaka 2010/2015.

chadema yaipa masharti magumu
akizungumzia mkutano huo wa ccm, katibu mkuu wa chadema, dk. Wilbroad slaa, aliponda juhudi za kukusanya watu ili kuonesha kuwa chama hicho tawala bado kinapendwa.

Akizungumza kutoka jimbo la mtama, mkoani lindi kwa njia ya simu, dk. Slaa alisema ccm inatakiwa kuwaambia watanzania na wananchi namna gani imetimiza ahadi zake ilizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, zikiwemo za kuwaletea wananchi maisha bora badala ya kusomba watu kwa magari.

Dk. Slaa aliongeza kuwa, hali za watanzania kwa sasa ni mbaya mara mbili hata kabla ya uchaguzi mkuu na kila mtu amepigika vibaya, kinyume kabisa na namna alivyoahidiwa na watawala.

Chadema pia kimewataka viongozi watakaohutubia wananchi, waseme waziwazi idadi ya viongozi wa ccm waliokwisha vuliwa magamba hadi sasa, tangu wawatangazie watanzania kuwa wanapambana na watu hao miaka miwili sasa.

"ccm isijisumbue wala kujidanganya kusomba watu na kuaminisha umma kuwa bado inapendwa. Watu wameichoka kwa sababu imewadanganya.

"tunataka waseme, wamewaleteaje watu maisha bora kama walivyowaambia wakati wa kampeni, na pili waseme ni magamba mangapi yamevuliwa tangu wajitape kufanya hivyo," alisema dk. Slaa.



kwani nani aliikataza chadema kumwaga ile pesa ya kanisa wanayopewa ???au hutafunwa na mbowe na slaa
 
Ninacho ona ccm wanafanya taarabu na maigizo hapa jangwani hawaelezi wamefanya nn ila wanaeleza kuwanajua kuwa watanzania wanashida. Na wanachama wa ccm wakiambiwa mchele bei juu wana shangilia sasa haya sio maigizo
 
Ninacho ona ccm wanafanya taarabu na maigizo hapa jangwani hawaelezi wamefanya nn ila wanaeleza kuwanajua kuwa watanzania wanashida. Na wanachama wa ccm wakiambiwa mchele bei juu wana shangilia sasa haya sio maigizo

Ndio maana wapo hapo. wapo hapo kwaajili ya kushangilia kila kitu kisemwacho. Kwani hukumbuki mitusi ya LUSINDE? nawalishangilia vile vile
 
Ni dhahiri kuwa mkutano wa ccm, ni faida kwa wafanyabiasha wadogo wadogo/wamachinga. Kwa kweli biashara ya maji, bagia, barafu, pipi, pamoja na juice. Mbali na hapo nape kaporosha matusi kikundi cha uamsho kwa kuwaita majambazi. Tusubiri majibu ya uamsho.
 
Nimeamini kwamba chama cha mapinduzi kimeishiwa, na inaonekana hakuna wa kukirudisha kwenye mstari. Nilifikiri kuiga kwao kufanya mkutano jangwani walitaka kujibu hoja zile zilizotolewa na wenzao wa CDM. Cha kushangaza wanapiga mipasho tu. Tukumbuke wenyewe ndo chama tawala. Eti wanajua maisha magumu ya wananchi. Eti UAMSHO ni mashetani. Malalamiko yote hayo ya nini. Wachukue hatua. Mafisadi wako chamani kwao huko huko. Wachukue hatua! CCM MMEKOSA MSHAURI KABISA KABISA NA SIJUI NANI ATAWAPONYA! CCM KWA HERI. Mtabaki kwenye historia. Hivi na hao mnaowapanga kuongea hamwoni wanawadondosha tu!!
 
Mkutano huu sioni kama una mantiki kubwa kama nilivyotarajia, zaidi ya kile nilichosema awali, show-off dhidi ya CHADEMA, na kukurupuka pale unaposikia hoja za upinzani kiasi cha kujicontradict wenyewe. Sasa hapa sijajua kampeni za uchaguzi ndio zimeanza au?

Uwiano wa mafanikio una kasoro kubwa sana utaeleweka kwa mtu ambaye hajaenda shule ila ukintajia idadi ya infrustructures, au idadi ya wanafunzi au vyuo ni lazima ueleze kulingana na idadi ya watu an ukubwa wa nchi, zaidi ya hapo ni kuwa wewe kama kiongozi unaamini unaowahutubia ni mambumbu so nani yuko hapo uwanjani ukiahca viongozi? Je ndio maana hamtaki kuwekeza kwenye elimu na vyuo na utafiti badala yake mnawekeza kwenye yale yatakayowaweka madarakani milele ikiwemo vyombo vya dola na siasa zenu? Huku mkihakikisha no critical mind emerge or prosper, ikiwemo kupuuzia kudumisha ubora wa elimu badala yake mnatudanganya na quantity!!!

Ninachokiona ni kueleza serikali imefanya nini.... simply a typicle order from JK, sababu ndio stile yake ya hotuba habadiliki... angalau Mwakyembe ingawa nae sehemu kubwa pia alinasa kwenye mtego maana lazima atekeleze maamuzi ya mkutano wa maandalizi.

Nataka kusikia miaka 50 ijayo Tanzania itafananaje, ili tuwabakize mtekeleze... hizi siku mbili zijazo mnatufanya tuendelee kuganga njaa kisa mnagombania kura wala hamjali nchi hii itafananaje huko mbeleni

Dah ma-engeneers wa Siasa wako wapi? Vipi sikuizi hampeleki watu kusomea political engeneering Bulgaria na Cuba? Maana wale waliofuzu najua wengi ni wale waliosoma wakati wa vita baridi.
 
KINYESI ...... aCHA KUFANYA WATU HAYAWANI


icon1.png
ccm kuanzisha al shabab mikoa ya pwani


KATIKA HALI YA KUWAGAWA WATANZANIA CCM IMEANZA KUWATUMIA BAKWATA KUWAGAWA WANANCHI.WAZIRI WA ELIMU NI MUISLAM MAKAMU WA RAIS MISLAM KATIBU ITIKADI CCM NI MUISLAM,RAIS WA NCHI MUISLAM MKUU USALAMA WA TAIFA NI MISLAM SASA VP LEOBAKWATA WASEME WANA FELISHWA HIZI NI MBINU CHAFU ZA CCM KUWATOA WANANCHI KWENYE WIMBI LA MAGEUZI YA KISIASA NA KUIINGIZA UDINI KWENYE JAMII NI HATARI NA NI LAANA KWA HAWA WANAMTANDAO HUU TUNASEMA ILI TANZANIA IWE NA AMANI 2015 CCM LAZIMA IONDOKE ISITULETEE MAAFA.WAMEANZA UAMSHO NA HAKUNA KARIPIO KALI LILILOTOLEWA KUONESHA CCM INAVYOHUSIKA VILIVYO KABLA YA UCHAGUZI 2015 WASHINDWE WALEGEE NA WASAMBARATIKE.MUNGU IBARIKI TANZANIA:confused2:​
 
Hiki ni kitendo kinachoruhusiwa kwenye siasa?

Naomba msaada

Ndugu wanajamvi,

Katika siasa mbaya watawala wetu wanazoleta zitatupeleka pabaya. Ktk mkutano wa ccm leo jangwani mh magufuli kaomba wanaorudi ccm walete kadi,ghafla wakatokea wawili, babu na mtoto mmoja na apo apo kundi la watu kama 30 wakaja mbele na kadi ambazo kwa mbali zote ni mpya pamoja na bendera mbili.

Ni kinyume na sheria zetu za nchi. Mh Magufuli kasimamia kuchana bendera na kadi zimechanwa vipande vipande mpaka Nape aliposema kadi ziachwe kuchanwa ila zikusanywe, vijana walikuwa wanaendelea na kuchana bendera ya CHDEMA, kwa maelekezo haya ya Nape na Magufuli kuchana bendera ya chama pinzani ni kuwaruhusu waovu wawe wanachana na hata kuchoma moto nembo za mahasimu wao na mwishowe ni kuandaa mapigano ya kichama na kuleta machafuko.

NIMECHUKIZWA SANA NA MAAMUZI AYA YA NAPE NA MH MAGUFULI... MNAZIPELEKA SIASA SAFI KABURINI, MNAANDAA HATARI.
 
Ni kweli kaka, ni vizuri wangetumia hii nafasi kujibu tuhuma za kutoka chadema na kuelezea wananchi mambo ya maana kama;Kuvua gamba, Katiba mpya, ugumu wa maisha & Muungano. Kwa staili hii wanachokifanya jangwani ni kuendelea kukibomoa chama chao.
 
Binafsi hata siku ile VIONGOZI wa juu wa chadema walivyokanyaga kanyaga kadi za CCM huku wakichekelea sikufurahia hata kidogo. Hao waliochana kadi hapo ni wanachama walioondoka chadema na wamefanya hivyo kwa hasira za yaliyowafika huko.

Si umemsikia Nape akiwakataza kabisa kuchanachana?
 
JF!Namuona Magufuli anaorodhesha barabara zilizojengwa na ccm kwa "misaada".Kwa nini asiseme "kwa hela zetu?"Mnaonaje JF
 
Ndugu wanajamvi,

Katika siasa mbaya watawala wetu wanazoleta zitatupeleka pabaya. Ktk mkutano wa ccm leo jangwani mh magufuli kaomba wanaorudi ccm walete kadi,ghafla wakatokea wawili, babu na mtoto mmoja na apo apo kundi la watu kama 30 wakaja mbele na kadi ambazo kwa mbali zote ni mpya pamoja na bendera mbili.

Ni kinyume na sheria zetu za nchi. Mh Magufuli kasimamia kuchana bendera na kadi zimechanwa vipande vipande mpaka Nape aliposema kadi ziachwe kuchanwa ila zikusanywe, vijana walikuwa wanaendelea na kuchana bendera ya CHDEMA, kwa maelekezo haya ya Nape na Magufuli kuchana bendera ya chama pinzani ni kuwaruhusu waovu wawe wanachana na hata kuchoma moto nembo za mahasimu wao na mwishowe ni kuandaa mapigano ya kichama na kuleta machafuko.

NIMECHUKIZWA SANA NA MAAMUZI AYA YA NAPE NA MH MAGUFULI... MNAZIPELEKA SIASA SAFI KABURINI, MNAANDAA HATARI.
 
Vyama Vingi Vya Upinzani Nchi za Magharibi Havina Bendera wala Kadi za Wanachama; Unajiandikisha kwenye Computer System basi wanajua wewe ni Chama Gani.

Kubebe kadi na Bendera Hakuna... Kwahiyo hivyo ni vitu vya kuondolewa kwenye Vyama Vya Kisiasa

Kinachobani ni Bendera ya Taifa Lenu tu na Bendera ya Rais Wa Nchi
 
Back
Top Bottom