Zimmermann
JF-Expert Member
- Sep 28, 2010
- 2,790
- 1,232
Duh..yaani mtu unabebwa kwenye fuso kama gunia la viazi!?
Duh..yaani mtu unabebwa kwenye fuso kama gunia la viazi!?
maskini baba/mama/kaka/dada zangu hawa..!
natamani wangeijua kweli ili kweli iwaweke huru.
RC apiga marufuku malori kubeba abiria | Send to a friend |
Saturday, 09 June 2012 08:15 |
0digg Salim Mohammed, Tanga MKUU wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, amepiga marufuku magari ya mizigo kubeba watu kwenda kwenye mikusanyiko ya watu wengi, ikiwamo misibani na harusini lengo likiwa ni kuepusha maafa yanayotokana na ajali. Agizo hilo limekuja baada ya kukithiri kwa vifo vitokanavyo na ajali za barabarani, ambazo husababishwa na magari ya mizigo kubeba watu kwenda misibani, maharusini na minadani. Mwaka jana watu 24 walipoteza maisha na wengine 39 kujeruhuiwa na kupata ulemavu wa maisha. Akizungumza kwenye kikao cha wadau wa usafirishaji na wamiliki wa magari ya mizigo juzi, Gallawa alisema kuanzia sasa ni marufuku magari ya mizigo kubeba watu na kuwapeleka katika mikusanyiko. Gallawa alisema imekuwa kawaida kwa watu wa Tanga kutumia magari ya mizigo kwenda katika shughuli za jamii na kusahau maafa ambayo yanaweza kutokea, huku wakiacha usafiri wa mabasi. Kuanzia sasa ni marufuku kwa magari ya mizigo kubeba watu na kuwapeleka katika sherehe au misibani, tunashuhudia maafa ya mara kwa mara yanayotokana na ubebaji watu kwenye malori, sasa basi! alisisitiza Gallawa. Aliwata wakazi wa mijini na vijijini kuacha kutumia usafiri huo, kwani umekuwa ukipoteza roho za watu wengi na watumie mabasi ambayo ndiyo wenye haki za kisheria kubeba abiria. Kuhusu tabia ya baadhi ya madereva kuweka miti na majani barabarani gari linapoharibika, Gallawa alisema watu hao wamekuwa wakichafua mazingira kwani gari hilo likitengenezwa hawaondoshi uchafu huo. Alisema tabia hiyo imekuwa kero na wakati mwingine husababisha ajali bila sababu za msingi, hivyo kila kijiji kinatakiwa kuwa na walinzi ambao watanakili namba za magari yanayofanya hivyo. |
Duh..yaani mtu unabebwa kwenye fuso kama gunia la viazi!?
Jamaa yangu mbona unaharaka, ebu fafanua huo usemi wako!Waliwezaje kukodi madaladala kwa macho yako?Kwani hawabebani mi kwamacho yangu siku ya mkutano wa chadema jangwani wanakodi madaladala.sasa kunatofauti gani na CCM wakiamua kuwakodia magari wanachm wao tatizo ni nini kwani na kwani watt wanalazimishwa kupnda kwenye hayo magari si hiyari Yao wenyewe magwanda kinawauma nini watt wakienda jangwani si muwaache Kila Mtu na maamuzi yake
Chadema wana beep sisi tunapiga.
wenye akili wanafahamu ccm ni chama kikubwa huwezi linganisha na chadema.
Zomba....i like your name kikwetu ni ngedere.
Angepokea tu, kwani haibadiri ukweli watanzania wameichoka CCMMamluki wamekodiwa kutoka vijijini, na kadi mpya za CDM zimesha kuwa printed ili mamluki wajidai wanazirejesha.
Malipo kwa mamluki hao ni sh. 10'000/=
Mdogo wangu alipewa kazi hiyo na amekataa kupokea hiyo hela.
Mimi Fuso zangu mbili ziko Booked tangu juzi, hivi saa hizi naeleka Bar kupata supu na Lager, i sold in cash.
View attachment 55865