CCM yamteua Raza kugombea jimbo la Uzini

Na Bashir Nkoromo, Zanzibar

Mohamedd-Raza.jpg

Kamati Kuu ya CCM imemteua mwanachama wake, Mohammed Raza kuwa mgombea wa Uwakilishi jimbo la Uzini.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema kwamba kikao hicho kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kimempitisha Raza baada ya kuridhika na sifa zake.

Nape alisema, Kamati Kuu pia imemteua Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Aman Karume kufungua kampeni za CCM za kuwania jimbo hilo ambazo zitafanyika Januari 28, mwaka huu katika Uwanja wa mpira wa Ghana.

Alisema wakati kampeni zitafunguliwa na Dk. Karume, ufungaji kampeni hizo utafanywa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwenye Uwanja wa mpira wa Tunduni.

Uchaguzi mdogo wa uwakilishi jimbo la Uzini unafanyika kufuatia kufariki dunia aliyekuwa mwakilishi wake kwa tiketi ya CCM, Mussa Hamis Silima aliyefariki kwa ajali ya gari,Septemba 23, mwaka jana.

Kuhusu minong'ono kwamba Raza ana utata katika uraia wake, Nape alisema Kamati Kuu imelitaza jambo hilo kwa makini lakini haikuweza kulipa uzito wa kumyima Raza nafasi ya kugombea kwa kuwa hakuna ushahidi wowote uliowasilishwa kuthibitisha hilo.

"Bado tunao muda wa kutosha, kama yupo mwenye ushahidi wa kutosha kuhusu hili anaweza kuleta ushahidi, ukiwa na uzito hatutaupuuza", alisema Nape

Haya majina ya mdebwedo huniacha hoi......Mchambawima!
 
Haaahaaa! Kuna mtu alienda na photocopy za vyeti vya form four kuonyesha jinsi alivyokimbiza madarasa. Kumbe safari zenyewe mwisho wake ndo kule kule kwa mwajiri wetu mkubwa, lol!!
 
Mkuu ni UWAKILISHI sio Ubunge....unless uwe unamaanisha Mjengo wa Baraza la Wawakilishi!
Mbunge aliyefariki alikuwa Muwakilishi anayewakilishi kwenye bunge la Muungano kwahiyo nadhani pia Raza atagombea hivyo anapenda sana Ubara, majumba kariakoo na Yanga Jangwani...
 
Na Bashir Nkoromo, Zanzibar

Mohamedd-Raza.jpg

Kamati Kuu ya CCM imemteua mwanachama wake, Mohammed Raza kuwa mgombea wa Uwakilishi jimbo la Uzini.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema kwamba kikao hicho kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kimempitisha Raza baada ya kuridhika na sifa zake.

Nape alisema, Kamati Kuu pia imemteua Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Aman Karume kufungua kampeni za CCM za kuwania jimbo hilo ambazo zitafanyika Januari 28, mwaka huu katika Uwanja wa mpira wa Ghana.

Alisema wakati kampeni zitafunguliwa na Dk. Karume, ufungaji kampeni hizo utafanywa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwenye Uwanja wa mpira wa Tunduni.

Uchaguzi mdogo wa uwakilishi jimbo la Uzini unafanyika kufuatia kufariki dunia aliyekuwa mwakilishi wake kwa tiketi ya CCM, Mussa Hamis Silima aliyefariki kwa ajali ya gari,Septemba 23, mwaka jana.

Kuhusu minong’ono kwamba Raza ana utata katika uraia wake, Nape alisema Kamati Kuu imelitaza jambo hilo kwa makini lakini haikuweza kulipa uzito wa kumyima Raza nafasi ya kugombea kwa kuwa hakuna ushahidi wowote uliowasilishwa kuthibitisha hilo.

“Bado tunao muda wa kutosha, kama yupo mwenye ushahidi wa kutosha kuhusu hili anaweza kuleta ushahidi, ukiwa na uzito hatutaupuuza”, alisema Nape

Big Test kwa the so called serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar. Wanandoa hawa watasigana kwenye majukwaa au vipi? Cant imagine kumuona Maalim Seif na kaulli mbiu zake zile za SAWA SAWA!!!?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom