CCM Dar yamtaka Dr. Magufuli aombe radhi

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Haya tena kamati ya siasa ya mkoa wa DSM imemwomba Dr. Magufuli kuwaomba radhi wananchi wa DSM kuwa kauli yake ni ya kuwadharau wananchi.

=======
Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam kimemtaka Waziri wa Ujenzi, John Magufuli aache kufanya kazi kwa jazba, dharau na maneno ya kejeli.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, alisema jana kuwa hawakufurahishwa na lugha ya kibabe aliyotoa Magufuli alipozungumzia sakata la kupanda kwa nauli za kivuko cha Kigamboni.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Guninita alisema kuwa kauli aliyoitoa Magufuli kwa mbunge wa Kigamboni Faustine Ndungulile na wananchi ya kuwataka kupiga mbizi na kwamba mbunge wa Kigamboni kama anawaonea huruma wananchi anunue boti itakayoitwa kwa jina lake au chama chake ni kauli inayotia hofu na inaweza kupoteza wanachama, na chama hicho kimkoa kimemtaka awaombe radhi wananchi kutokana na kauli yake hiyo.

“Kuna haja viongozi wachague kauli ya kusema na sheria zimetungwa na kutengenezwa na watu na zinazungumzika, ukifananisha vivuko vya Ziwa Victoria na hiki cha Kigamboni ni tofauti kubwa na neno ‘marufuku’ si neno jema hivyo ni busara kuomba radhi,” alisema Guninita.

Guninita alisema kauli hiyo ya Magufuli haijengi mshikamno na ushirikiano kati ya viongozi wa CCM, serikali ya mkoa na wananchi, na kwamba kama malalamiko ya wananchi hao hawezi kuyasikiliza, asingetumia maneno aliyoyasema.

Aidha Guninita alisema kuwa CCM mkoa wa Dar es Salaam, imeipokea kwa masikitiko kauli hiyo na imewaomba wananchi kuwa na subira wakati uongozi wa chama ukiendelea na jitihada za kuzungumza na serikali ili kutatua tatizo hilo kwani umesikia kilio chao cha kupanda kwa nauli na unawathibitishia kutatua tatizo hilo.

via Tanzania Daima


==========

My Take:

Mimi ninavyoelewa kazi za kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya CCM ya mkoa ni hizi hapa
1. Kutoa uongozi wa siasa ktk mkoa
2. Kueneza itikadi na siasa ya CCM ktk mkoa
3. Kuandaa mikakati ya kampeni za uchaguzi na kampeni nyinginezo ktk mkoa
4. Kusimamia utekelezaji wa shughuli za kila siku za CCM na maamuzi yote ya CCM chini ya uongozi wa H/ KUU ya CCM MKOA
5. Kupanga mipango ya kukipatia chama mapato,kusimamia kwa dhati utekelezaji wa mipango hiyo,kudhibiti mapato na kusimamia matumizi bora ya fedha na mali za chama ktk mkoa

Sasa hili tamko lao la kumtaka Waziri wa Ujenzi aombe radhi mbona si moja ya kazi zilizopo hapo juu?

Kazi ipo jamani

Siasa ktk kazi hadi lini?
 
Hakuna haja ya kuomba radhi, Panton limeua watu wengi tangu enzi ya kina Mustafa Nyang'anyi na watu hawakuombwa radhi, ni mara ngapi yalikufa mapantoni ya Kigamboni watu wakakosa huduma leo watu wa Dsm hawataki kufikiri, likifa na hilo hao wabunge watachangia?
Kwa hilo bora magufuli ajiuzulu nauli hakuna kushuka na CCM haihusiki (Itenganisha Siasa na kazi) na usalama wa watu au majini watakapozama
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Ngoja tumwangalie magufuri hapo,but sioni haja ya kuomba msamaha ila vile ni wenyewe kwa wenyewe(ccm) lets wait and see
 
kamati ya siasa ndio ipi hiyo?

ktk hivi vyama vina kamati zao mbarimbari,moja ya kamati hizo ni kamati ya siasa ya mkoa,ambayo wajumbe wake ni
1.mwenyekiti wa CCM wa mkoa
2.katibu wa ccm wa mkoa
3.mkuu wa mkoa ambae ni mwanachama wa ccm
4.katibu wa siasa na uenezi wa mkoa
5.katibu wa uchumi na fedha wa mkoa
6.mjumbe au wajumbe wa H/ KUU
7.M/kiti wa kila jumuia wa mkoa
8.meya anayetokana na ccm
9.wajumbe waliochaguliwa na H/kuu kuingia ktk kamati ya siasa
 
ubabe umezidi!
Kwanini wasipandishe tarehe 1/7 kwenye bajeti ili kujua maisha ya mtz yamepangwa vipi ndani ya mwaka wa fedha!
 
ubabe umezidi!
Kwanini wasipandishe tarehe 1/7 kwenye bajeti ili kujua maisha ya mtz yamepangwa vipi ndani ya mwaka wa fedha!

Hizi ni siasa za kuumbuana
kwanini Kamati ya siasa ya mkoa isimwalike Mh Dr.Magufuli ktk kikao chao na kumweleza wazo lao,ili anavyokuja kuomba radhi basi tunaelewa kuwa si shinikizo la chama

lakini walicho kifanya ni kutaka kumshinikiza Mh Waziri kuomba radhi na kutueleza wananchi kuwa CCM haina mawasiliano na Wabunge wake

hizi siasa mimi sizielewi kabisa,ni kama kuna kuonyeshana ubabe vile
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Haya tena kamati ya siasa ya mkoa wa DSM imemwomba Dr. Magufuli kuwaomba radhi wananchi wa DSM ,kuwa kauli yake ni ya kuwadharau wananchi.

kazi ipo jamani

siasa ktk kazi hadi lini?

Hao jamaa wa CCM Mkoa wa D'salaam wazushi tu, hawana lolote. Akikataa kuwaomba radhi watafanya nini? Si watadhalilika tu mbele ya vilaza wenzao?

Inabidi watambue kuwa Dr Magufuli anahangaika kukusanya mapato kwa ajili ya kuendesha kivuko na kuwalipa posho Wabunge.
 
Viongozi wa Tanganyika kuomba radhi ni mwiko kwao hata kama amekutukania mama yako, wao mda wote wapo right
 
Haya tena kamati ya siasa ya mkoa wa DSM imemwomba Dr. Magufuli kuwaomba radhi wananchi wa DSM ,kuwa kauli yake ni ya kuwadharau wananchi.

kazi ipo jamani

siasa ktk kazi hadi lini?

Halina mshiko, labda cc iseme aombe radhi
 
Hakuna haja ya kuomba radhi, Panton limeua watu wengi tangu enzi ya kina Mustafa Nyang'anyi na watu hawakuombwa radhi, ni mara ngapi yalikufa mapantoni ya Kigamboni watu wakakosa huduma leo watu wa Dsm hawataki kufikiri, likifa na hilo hao wabunge watachangia?
Kwa hilo bora magufuli ajiuzulu nauli hakuna kushuka na CCM haihusiki (Itenganisha Siasa na kazi) na usalama wa watu au majini watakapozama

Kwanza ifahamike, kivuko si jambo la biashara, ni moja kati ya majukumu na wajibu wa serikali kuhakikisha kwamba raia wanafika sehemu moja kutoka ingine, na kivuko ni sawa na daraja. Kama serikali imeshindwa kujenga daraja kati ya magogoni na kigamboni, si haki kwao kutoza wananchi wanaovuka hapo, na ikiwa hivyo ndivyo basi hata yale madaraja makubwa wawe wanatoza nauli
 
Magufuli ni CCM na CCM imezoea kutenda hayo.Sasa amuombe radhi nani?Hiyo ni dalili za chama kufilisika kisiasa,sasa sakata la kuuza nyumba za serikali ndio linaibuka;Kama CCM ni wapenda haki kwanini waseme haya baada ya hili kutokea?Hili linaonesha kwamba kuna mengi mabaya yamejificha ila kila mmoja anasubili nani aseme.
 
Kwanza ifahamike, kivuko si jambo la biashara, ni moja kati ya majukumu na wajibu wa serikali kuhakikisha kwamba raia wanafika sehemu moja kutoka ingine, na kivuko ni sawa na daraja. Kama serikali imeshindwa kujenga daraja kati ya magogoni na kigamboni, si haki kwao kutoza wananchi wanaovuka hapo, na ikiwa hivyo ndivyo basi hata yale madaraja makubwa wawe wanatoza nauli

kivuko si sawa na daraja

kivuko kinahitaji
1.ukarabati wa kila wakati
2.mafuta kwa ajili ya kukiendesha
3.mishahara kwa watakao kihudumia

lakini daraja halina mahitaji hayo,unadhani bila pesa kivuko kitaendeshwa vipi?
 
Kajitakia mwenyewe. Hili Jiji tafsiri ya jina la lake ni Nyumba ya Amani na itabaki kuwa hivyo. Lazima uwe na busara kwa watu wa jiji hili. Ubabe kwa wananchi sio mahali pake hapa. Hivyo Rais wa awamu ya pili alikuwa akitoa amri kwa kauli laini si ya uwoga bali ndio ustaarabu. Kalikoroga mwenyewe analo.
 
Magufuli ni CCM na CCM imezoea kutenda hayo.Sasa amuombe radhi nani?Hiyo ni dalili za chama kufilisika kisiasa,sasa sakata la kuuza nyumba za serikali ndio linaibuka;Kama CCM ni wapenda haki kwanini waseme haya baada ya hili kutokea?Hili linaonesha kwamba kuna mengi mabaya yamejificha ila kila mmoja anasubili nani aseme.

"mtu ukiwa unaoga kichaa akapita akachukua nguo zako,na ukaanza kumfukuza wewe ndio utaonekana kichaa zaidi"
Kuna kauli moja tu ambayo ilipaswa watanzania tuombwe radhi nayo ni"ndege ya raisi lazima inunuliwe hata kama watz watakula nyasi"Lakini si hii ya kupiga mbizi,ambayo kwanza anawahamasisha wana kigamboni kufanya mazoezi,ambalo zoezi la kuogelea viungo vyote vya mwili vina fanya kazi.Hapa hakuna lolote zaidi ya mbio za uraisi.Hii wizara waliyompa jamaa na kwa utendaji wake wanajua atazidi kujiimarisha.ndio maana hata waliipungunguza.Watanzania tuache kutetea upuuzi na kupenda vitu vya bure.Linalonisikitisha ni kwamba kwa mara nyingine Magamba wameweza kutuhamisha kutoka kwenye mdahalo wa katiba na kuanza kuongelea kupiga mbizi.
Hao viongozi wa Dar wote wachumia tumbo waliishanunuliwa,na kwa kwa Magufuli nnayemjua hataomba msamaha,ndio tuone watasema nini.
 
...maneno yakisha-tamkwa hayarudishiki tena mdomoni eee...pembe la-ng'ombe...
 
"With friends like these who needs enemies?. CCM wanajimaliza wenyewe na adui yao mkubwa ni wao wenyewe wala sio upinzani.

Guninita amefanya nini la maana kwenye hili jiji la Dar? Mafuriko yametokea Dar, Magufuli bila kujali ni x'mas alikuwa barabarani akisimamia ukarabati wa madaraja, Guninita na wenzake walikuwa wapi? Kwa nini Guninita hakumtaka Waziri wa Ulinzi awaombe radhi wakazi wa Dar kutokana na milipuko ya mabomu licha za waziri ahadi kwamba hayatarudia? Watu wamepoteza maisha, kwanini Guninita hakujitokeza kwenye vyombo vya habari na kudai msahama wa waziri wa ulinzi?

Nahiisi wabunge wa Dar wamoena ngoma nzito wakaamua kujificha kwenye hii ngozi ya 'ccm-mkoa wa Dar' ili wamkomoe Magufuli. Juzi Magufuli amesema anataka kivuko kijitegemee lakini pia anataka kutumia kiasi cha fedha kitakachopatikana ili kujenga vifuko vingine ili kupunguza tatizo la usafiri Dar. Sasa Guninita analeta porojo gani hapa? Hili tatizo limekuzwa na hawa hawa wabunge wa ccm -Dar. Na ni aibu kubwa kuona hawa mufilisi wakiendeleza ngonjera kwenye vyombo vya habari kwa mambo yaliyo wazi kabisa. Mbali na Magufuli ccm wana waziri gani mwingine mchapa kazi? Wassira? Kawambwa? Ngeleja?

Magufuli usirudi nyuma wafanye wanalotaka lakini usirudi nyuma kabisa kabisa. Na kwa Guninita na wenzake, wahanga wa mafuriko bado hawana mahali pa kukaa, huko wanakopelekwa hakuna chochote ni viwanja vitupu sijui watalala wapi hadi watakapojenga nyumba! Je, mnaoliona hilo au kila kukicha mnawaza namna ya kushambuliana?

Mmeshindwa kusimamia maamuzi yenu ya siku tisini sasa mnataka pa kutokea!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom