Ccm yakubali ukweli wa watanzania

andrews

JF-Expert Member
Mar 28, 2012
1,679
152
[h=3]Neno Fupi La Usiku Huu; Na Mukama Naye Ameusema Ukweli Wake![/h]



Ndugu zangu,


Vijana wengi leo wanaikimbia CCM na hawataki kuhusishwa nayo. Tujiulize; ni kwa namna gani vijana hawa watakuwa na mapenzi na chama kinachohusianishwa mara kwa mara, na kashfa kubwa za kifisadi. Kashfa zinazoathiri maisha yao? Kwao wao, wanayaona ‘madudu’ kwenye vazi la chama. Hatuyaoni?


Ni sawa na kisa kile cha ‘ Mfalme aliyetembea uchi’. Watu wazima walijipanga barabarani kusifia vazi jipya la mfalme huku wakiifumbia macho kasoro kubwa ya vazi hilo, kuwa lilimwacha mfalme nusu uchi. Na hata pale mtoto alipotamka; “ Jamani, mfalme yuko uchi!” Kuna waliofunika nyuso zao kwa aibu. Maana, mtoto aliusema ukweli wake.


Na leo nimesoma kwenye moja ya magazeti yetu; kwamba Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Wilson Mukama ameweka bayana, kuwa kuna Wana- CCM wasaka madaraka. Kwamba CCM ina makundi ; kuna Nato, G8 na kadhalika. Wilson Mukama ameusema ukweli wake.


Na hakika, ukweli ni mzigo mzito. Mwanadamu hupaswi kuubeba na kutembea nao, bali kuutua na kila mmoja akauona. Naam, kuna wanaokimbilia CCM kusaka madaraka na si uongozi. Kiu ya madaraka ni kiu ya kutawala, wakati uongozi ni dhamana.


Iweje basi Wana- CCM leo wakatumia muda na fedha kushiriki semina ya ‘ Utawala Bora’ badala ya ‘ Uongozi Bora’? Maana kazi ya chama cha siasa ni kuongoza, si kutawala. Hata Mwalimu alitumwambia, kuwa ili tuendelee tunahitaji mambo manne; Watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi Bora, si ’ utawala bora’, Au?


Na hilo ni Neno Fupi la usiku huu.
Maggid Mjengwa,
 
Hakika hii itakuwa "A photo of the day" katika hii JF. Naamini kila mmoja atakubaliana nami.
 
Adui ni Hilo Jengo wanalolibomoa, Watu wa CCM au IDEA za CCM?
 
Back
Top Bottom