CCM yakiri watumishi wa Umma kuvujisha siri nyeti

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]
Na Peter Mwenda

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekiri kuwa kuna baadhi ya watumishi wa umma ambao si waaminifu wanaovujisha siri za Serikali.Akizungumza katika mahafali ya
23 ya Chuo cha Biashara na Uhazili cha Splendid, Dar es Salaam juzi Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Kilumbe Ng'enda, alisema makatibu muhtasi ni wanataaluma na wenye maadili ya kutunza siri za ofisi, hivyo hakuna sababu ya kuwakumbatia wasiofuata maadili.

Alisema ni kweli risala ya wanachuo 98 waliohitimu katika chuo hicho wamesema kweli kuwa wafanyakazi wa serikali wengi wanavujisha siri, hivyo CCM inaahidi kuwaondoa na kuweka wenye maadili ya taaluma zao.

Bw. Ng'enda alisema wapinzani wamekuwa wakitumia visingizio vya maandamano kupinga Serikali ya CCM, lakini wajue kuwa hiyo si njia ya kutatua kero za wananchi.

Aliwataka wapinzani kutekeleza ahadi zao kwa wananchi badala ya kutafuta visingizio.

Alisema CCM imejipanga kushinda Jimbo la Igunga na lazima italichukua kwa sababu wananchi wanapenda chama hicho kwa sababu ndicho kinawakomboa katika matatizo mbalimbali ya elimu, uchumi na kuendelea kuwajengea amani.

Bw. Kilumbe aliahidi kuwatafutia ajira wahitimu hao katika ofisi za chama ngazi ya wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke na kutoa kompyuta mbili na mashine za kupiga chapa mbili kwa ajili ya chuo hicho.

Awali Mkuu wa Chuo hicho, Bw. Caasim Taalib, alisema chuo hicho kinatoa nafasi kumi kwa vijana wa CCM kusoma bure kozi ya uhazili katika chuo hicho na kati ya wahitimu hao 65, wamekubali kujiunga na CCM na kuacha vyama vyao vya upinzani.
 
sasa hawa magamba wanachomind nni sawa wamekiuka ethics za kazi lakini inapobidi bora kufanya hvo
 
walisema casa zicpelekwe vyuoni leo hii wanafanya nini.waungwana 2kumbuke mfa maji haishi kutapatapa mwishoe utackia nape mkuu wa chuo ili waweze kuwakontol wanafunzi vizuri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom